SEHEMU YA 22
Bila kuongea chochote, Nurat alitoka mbio kuelekea chumbani huku moyo ukimdunda sana.
βMungu wangu!!! Ndo nimefanya nini?β aliongea kwa hasira na aibu βMimi nilijua yupo Ommy jamani kaaah!β alizidi kusema huku akiwa ameweka viganja vyake mdomoni kwa aibu βSasa atanionaje?β aliwaza
Wakati anawaza hayo, pia Baba Denis naye alikuwa akiwaza yake βHuyu ntoto ni shetani au?β alijisemea huku akiwa emeshika tama βKwanini anafanya hivi huku ndani? Au anampenda Omary? Hapa lazima kuna siriβ alitafakari kisha akainuka ili aende chumbani kukaa na mkewe
Ghafla kabla hajaondoka alisikia hatua zikija sebuleni, akageuka na kukuta Winnie. Alipomaliza aligeuza shingo na kuendelea na safari yake lakini hakufika mbali akapata wazo na kumuita
βWinifridaβ alisema mzee huyo
βAbeeβ Binti alisema huku akiibinya midomo kwa ndani na kufanya mashavu yabonyee βShikamoo babaβ
βMarahaba, samahani kwanini huendagi ibadani?β
βAam….mh aahβ alianza kupata kigugumizi ndipo mzee akajikoholesha.
βAnyway, unaonekana hauna sababu ya msingi ila jitahidi uwe unahudhuriaβ alisema mzee huyo
βSawa babaβ
βSamahani kuna kitu nataka unieleze kwa kinaβ alisema Mzee
βKitu gani baba?β aliuliza
Mzee alishusha sauti na kuweza kuongea bila mtu mwingine kusikia
βHivi Nurat na Omary wana mahusiano gani?β aliuliza
βHeeehβ Winnie alishangaa na kushika kiuno halafu akacheka kwa nguvu
βSssshβ mzee alimzima βTumia sauti ndogoβ
Sasa kumbuka Winnie ana bifu na Nurat hivyo aliitumia ile fursa vizuri
βSawa, acha nikueleze…..huyu Nurat muda mrefu yuko katika Mahusiano na Ommy…..mbaya zaidi pia yuko na Denis, anawachanganyaβ aliamua kumwaga mchele
βJesus!!!β Mzee alishtuka
βNdio hivyo, hapa hatoweza kufaulu kwani kwanza ana simu kubwa nimekuta akiwatumia picha za uchi wanaume mtandaoni?β
βWinifrida……are you serious?β
βYesβ
βKwanini hukusema?β
βSikupata nafasi ya kusemaβ alisema na kuondoka zake, lakini alimuacha mzee mdomo wazi anashangaa
Mzee alipagawa ikabidi aende chumbani kujadili na mkewe…..JE ITAKUWAJE? WATAMNYANGβANYA SIMU?
USIKOSE
All Rights Reserved Β© | Simulizi TAMU