UTAMU WA JAMILA (02)

ILIPOISHIA
Badu alibaki kumtazama mama huyo ambaye sekunde chache tu ametoka kusikia wanawake pembeni kuhusu taarifa za mama huyo.

SONGA NAYO
“Asante sana mama, shikamoo.” alisalimia Badu.

“Haya, pole mwaya naskia umekuja na gari uhamie leo.”

“Ndio mama yangu, nimekuja na dereva hapo yupo nje anasubiri. Sijui tunafanyaje hapa.”

“Usijali mwanangu. Hapo mbele kuna fremu yangu haina mtu bado. Utashusha vitu vyako kwenye gari utaviweka humo kwanza. Sherehe imeshaisha hapa ni bibi harusi tu kuweza kuchukuliwa hapa basi watu wataondoka. Nisamehe sana babangu sijakutaarifu mapema kama kuna sherehe. Pole kwa usumbufu huu ulojitokeza.”aliongea Mama J akimueleza Badu.

“Usijali mamangu wala hakuna shida. Wacha basi tuongozane ukanielekeze sehemu ya kuweka vitu ili mwenye gari arudi zake.”

“Sawa hakuna shida. Mwaju shika funguo hii kafungue ile frem pale aweke vitu vyake. Ongozana na huyu baba atakuonesha.”

“Sawa mama. Aliongea Badu na kuondoka zake akiwa sambamba na Mwajuma.

Walifika hadi kwenye gari na Badu akamuelekeza dereva yule ageuze gari na kusogea jirani na eneo hilo ambapo ipo fremu ya mama mwenye nyumba. Zoezi lilifanyika kwa takribani nusu saa nzima kuweza kukamilisha kumaliza vitu vyote kuvishusha na kuviweka ndani fremu. Alitoa waleti yake Badu na kuweza kumlipa pesa yule dereva baada ya kukamilisha jambo hilo. Aliwasha gari lake na kuweza kuondoka zake huku Mwajuma akiwa anafunga geti la fremu ile.

” Nimekusumbua sana besti nisamehe bure maana ulipaswa kuwa kwenye sherehe ya dada yako kule.”aliongea Badu baada ya kuona muda wote huo walikuwa sambamba na Mwajuma kuingiza vitu.

“Wala usijali kakangi, hata hivyo sherehe yenyewe ilishaisha waende tu kwa huyo mumewe.”aliongea Mwaju na kauli yake hiyo ilimshtua kidogo Badu. Hakutaka kulidadavua sana jambo hilo akikung’uta tu mikono yake iliyokuwa na vumbihuku akitazama kule sherehe inavyoendelea.

“Sasa mimi wacha niingia hivi kati kuna mambo naenda kuyaweka sawa. Huenda nikirudi kutakuwa kumetulia nitakuwa na kazi ya kuingiza vitu chumbani kwangu.”

“Sawa hakuna shida, utakaporudi ukihitaji msaada utanijulisha tu.”

“Haya nashkuru, baadae.” aliongea Badu akigeuka kuondoka zake huku Mwaju naye akirudi zake ndani kwao.

Shuhuli iliendelea huku mzee Chombo akihakikisha kila kitu kinaenda sawa hadi binti yake alipokuja kuchukuliwa na mumewe wakapanda kwenye gari kuondoka, huku magari kadhaa nyuma yakifuata kutoka upande wa mwanaume waliokuja kumchukua mkewao. Watu walicheza hapo kwa muda na jioni ilipoanza kuingia vitu vikaanza kurudishwa vilipokuwa huku maturubai na mikeka ikikunjwa kuonesha shuhuli imekwisha.
Mzee Chombo alipata habari kuhusu kijana Badu kufika toka mchana wa sherehe akiwa na vyombo vyake, alielezwa kile kilichitokea hadi vitu vyake kustoriwa kwenye fremu. Jambo lile lilimsikitisha kuona hawakumpa taarifa kijana huyo. Alichofanya ni kuwachukua vijana watatu anaowaamini wakaenda kwenye ile flemu na kuanza kutoa vitu vyote kuvileta ndani karibu na chumba cha mwenyewe. Walifanya hivyo kumrahisishia kazi hiyo huku vikiwa salama vitu hivyo hasa vikiwa kwa ndani. Kila moangaji alirudi kwenye chumba chake baada ya sherehe kwisha maisha yakaendelea.

Hadi kufika mishale ya saa mbili na nusu usiku Badu alipata kuwasili nyumbani hapo baada kufungua geti na kuingia ndani alipata kushangaa kuona vitu vyake vikiwa pale nje. Alikuja mama J na kumuelewesha kijana huyo aliyekuwa mwelewa wa haraka. Taratibu akaanza mwenyewe kuviingiza vitu vyake. Mama J alibaki kumtazama kijana huyo kwa jicho la aina yake. Alijikuta tu anashawishika kummiliki kijana huyo kingono kama ilivyo tabia yake ambayo baadhi ya wapangaji wameijua.

“Wacha nikuchezee michezo ya hatari utalainika tu mwenyewe. Nyie vijana dawa yenu ninayo.”alijiseme mwenyewe moyoni mama J akiwa amevalia dera lake lenye mpasuo mkubwa tu kisha akageuka na kuingia zake ndani huku Badu akiwa vize na kupangilia vitu vyake kuingiza ndani.

Mama J alifika kwake na kumkuta mumewe amejilaza zake kitandabi kwa uchovu wa kutwa nzima. Alibaki kutabadamu tu mama huyo na taratibu akaanza kuvua nguo zake na kubaki kama alivyoletwa duniani. Alijitazama kwenye kioo mashallah si haba alijaaliwa japo umri umekwenda lakini alikuwa na ushawishi. Bila kupepesa macho alichukua bikini yake nyekundu akaivaa kisha akavuta kanga yake nyepesi na kujifunika mwili. Alijitazama kwenye kioo na kubaki kutabasamu tu.

” Hapa atatoka kweli? Hapana huchomoki hapa. Mimi ndio mama mwenye nyimba bwana lazima nikukaribishe.”aliongea mama J akidhamiria kweli jambo lake. Alichukua majina kujaza nusu kwenye ndoo ya kuogea, akachukua kopo la sabuni na kutoka zake nje.

Badu akiwa anaendelea na kazi yake mama J alipita kuelekea bafuni akijifanya hana habari kabisa. Alitembea kwa kuburuza malapa kusudi na kweli alifanikiwa kunyanyua macho ya kijana Badu kutazama anayetembea.
Moyo ulishtuka kumuona mama huyo akiwa kwenye vazi lile la hasara kabisa. Alikuwa anatembea kwa kutingisha makalio yake haswaa, kwa mitetemo ile ilimfanya kijana hiyo ameze funda moja la mate akiwa ameshikilia mito ya kitandani pake nje.

“Mh haya majaribu gani tena siku ya kwanza tu hii!”alishindwa hata kufanya kazi yake vizuri usiku huo akimtazama tu mama mwenye nyumba akielekea zake bafuni.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!