UTAMU WA JAMILA (02)

SEHEMU YA 04

Siku hiyo chumba cha Roja kilisikika muziki tu kuanzia walipoingia ili kupunguza ukakasi wa sauti zinazotoka pindi wanapofanya yao.

Upande wa pili Mwajuma baada ya kujihakikishia mpenzi wake yupo kwenye utafutaji alielekea zake jikoni kupakua chakua apate kula. Muda huo ndio akaweza kumkumbuka yule mpangaji mgeni ambaye mchana wa siku hiyo alikuwa bize na kuhamisha vitu vyake.

“Maskini yule mkaka sijui amekula! Hebu wacha nikamuangalie sijui atakuwa amelala?”aliongea Mwajuma na kutoka zake nje. Aliongoza moja kwa moja kwenye chumba cha Badu akaanza kubisha hodi mara kadhaa bila kujibiwa. Punde tu geti lilifunguliwa na kuingia kijana Badu. Mwajuma aligeuga na kuweza kumuona kijana huyo taratibu alisogea hadi pale kwake.

“Ah kumbe ulitoka! Nikajua utakuwa umelala.”aliongea Mwajuma kwa ukarimu.

“Hapana nilitoka sasahivi kwenda kuangalia msosi ila nimekosa kila sehemu hola.”

“Oh pole, hata hivyo nilikuja hapa kwaajili hiyo, nilikuja nikuulize kama nikuwekee chakula maana kipo kingi tu kimebaki cha sherehe.”

“Dah itakuwa poa sana. Wewe niletee nile maana ninanjaa.”aliongea Badu na kumfanya Mwajuma akubali. Alielekea zake ndani kuchukua chakula apate kuleta.

“Anaonekana mkarimu sana. Napaswa nimheshimu tu kwakweli anajali sana watu binti wa watu.”aliongea mwenyewe Badu akimfikiria Mwajuma.

Muda mfupi alirejea Mwaju akiwa na hotpot, alimkabidhi mwanaume alibaki kushangaa.
“Jamani si ungenipakulia tu kwenye sahani!”

“Ah nimekuwekea humo ujipimie mwenyewe. Kuwa na amani tu kakangu wewe kula kesho nitakuja kufuata vyombo.”

“Aisee nashkuru sana leo umeniokoa maana nimezunguka huko hakuna chakula zaidi ya chipsi tu. Nami niliapa kutokula hizo si unajua wanaume sisi.”alisema Badu na kumfanya hata Mwajuma acheke kwa kile alichomaanisha kijana huyo.

“Haya basi wacha nikale miye, nikutakie usiku mwema.”aliaga Badu.

” Haya, ndio unaitwa nani vile?”aliuliza Mwajuma.

“Oh nimesahau kujitambulisha kumbe! Naitwa Badu.”

“Ahaa sawa, basi usiku mwema Badu.”

“Haya nawe pia Mwajuma.” aliongea Badu na kushuhudia tabasamu la msichana huyo aliyegeuka na kuondoka zake. Naye akaingia chumbani kwake kupata kula.
Kwa Mwajuma baada kuingia tu ndani alipata kumuona mama yake akitoka zake chumbani kwake na kuonana uso kwa uso.

“Haya kulikoni saizi umetoka wapi?”aliuliza mama mtu akiwa anajifunga kanga yake vizuri.

“Nimetoka hapo nje.”

“Nje wapi sasa!”

“Hapo nje kwa huyo mpangaji mgeni.”

“Mpangaji mgeni? Imekuwaje mpaka uende kwake? Alikuita?”

“Hapana mama. Unajua toka ile mchana nilimkaribisha chakula akasema yupo bize na kuhamisha vitu. Sasa nikaona si vibaya nikampelekea chakula kaka wa watu na ilikuwa kama Mungu naye alikuwa hajala hivyo ndio nikampa nami ndio nimerudi. Au kuna ubaya?” aliongea Mwajuma kwa kujiamini akimtazama mama yake.

“Mh haya we nenda kalale huko. Ila usijitie kimbelembele kwa watu wageni unamjua tabia yake yule hadi unamzoea hivyo! Shauri yako.”alisema mama huyo na kutoka zake nje kwenda chooni kujisaidia.
Mwajuma alibaki kushangaa tu akijua mama yake anamfikiria vibaya. Hakujali sana aliingia chumbani kwake kulala.

Asubuhi ya siku inayofuata mapema Badu aliamka na kuvaa suruali yake ya track na raba huku juu akiwa tshirt yake aliyoikata mikono na kuwa kama singrendi. Alifungua geti kukiwa bado ni Alfajiri na taratibu akaanza kukimbia kama moja ya mazoezi ya kujiweka imara. Ilikuwa ndio desturi yake kila asubuhi hufanya mazoezi na hasa kuenda kwenye viwanya vya mipra na kuanza kuzunguka uwanja kwa raundi kadhaa kisha hunyoosha viungo na kurudi zake.

Ratiba hiyo aliiendeleza kama kawaida takribani wiki nzima hali iliyowafanya baadhi ya majirani humo ndani wajue ndio kawaida yake kwa kijana huyo. Kwa upande wa Mwajuma yeye alijikuta anashawishika katika jambo hilo, hivyo hakusita kumfuata Badu na kumueleza kile ambacho anatamani.

” Hivi unadamkaga asubuhi sana kifanya mazoezi eh!”alihoji Mwajuma.

“Ndio mapema sana kama saa 11 kasoro hivi.”

“Mh natamani sana kufanya mazoezi namimi ya kukimbia ila sasa huo muda mimi nakuwa nakoroma. Sidhani kama nitaweza.”

“Hamna kila kitu ni kuamua. Kama kweli unayoniya basi nipo tayari kukuamsha nikitaka kutoka ili tuongozane.”

“Ahaa hapo sawa, basi naomba kesho tuanze hivyo.”

“Ila uwataarifu kabisa na wazee wasije kunijia juu inakuwaje tena.”

“Ah wala usijali kwani mimi mtoto bwana, hata hivyo hatunaga mambo ya kufatiliana mi naweza kutoka muda wowote ule wala usijali.”aliongea Mwaju akimuaminisha Badu.
Walikubaliana juu ya swala hilo kuwa watakuwa pamoja.

Mchana wa siku hiyo Badu akiwa zake chumbani kwake anaangalia movi alipata kusikia mlango unagongwa. Ilimlazimu kunyanyuka kwenda kuufungua mlango ambapo alishtuka pale alipomuona mdada mmoja akiwa amevalia bukta na jezi ya Simba. Hakika aliumbwa haswa, shepu yake ilidhihirisha wazi kwamba anamilikiwa na watu wenye pesa zao.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!