SEHEMU YA 10
ILIPOISHIA
Hata alipopita kwenye chumba cha Jesca alisikia tu akimsifia mtu aliyekuwa anampa raha hizo. Aliishia kutabasamu tu mlinzi huyo baba Dula na kuendelea na safari yake.
SONGA NAYO
Baada ya mida kupita hali ilikuwa shwari. Wote walikuwa hoi kwa kile ambacho kimetendeka.
Jesca alijiangalia kwa bibi na kubaki kusikitika tu.
“Tangu niyajue mapenzi sijawahi kufanywa hivi aisee. We mkaka mbona unanifania kusudi hivi jamani!”aliongea Jesca akimpa sifa hizo Badu aliyekuwa anainuka akivaa nguo zake.
“Nadhani soda itakuwa imepoa sasa kutoka kwenye kuganda.”aliongea Badu na kimfanya Jesca acheke huku akitazama chini kwa aibu, maana janja aliyotumia haikuwa na kichwa wala miguu.
“Halafu sijalijua jina lako hadi sasa eti.”
“Doh yani unanipa utamu hata hunijui jamani!”
“Unajua hata sijielewi imekuwaje mwenzio.”
“Hahaha haya bwana miye naitwa Badu”
“Oh sawa Badu. Ila kwa ulichonifanyia leo hapa wacha nikuite Badboy. We mwanaume mbaya kitandani sijapata ona. Na sidhani kama nitaishia hapa tu kwa leo, hii huduma nitaitaka tena Badu nikubalie uwe unanihudumia basi mpenzi please!”aliongea kwa sauti ya upole Jesca alidhamiria kweli kulihitaji penzi la kijana huyo.
Aliachia tu tabasamu akiwa anamalizia kuvaa nguo zake.
“Wacha nikapumzike kwanza. Kesho tutaongea.”aliongea Badu na kutaka kusogea mlangoni.
“Hee wewe subiri!”alinyanyuka Jesca akiwa hana nguo kabisa.
“Nini tena?”aliuliza Badu akiwa anamtazama mwanamke huyo. Alisogea hadi pale mlangoni akafungua kidogo kuchungulia kwa nje. Alitazama kila pande hakuweza kumuona mtu yeyote pale kisha akarudisha kichwa ndani.
“Haya toka haraka uingie kwako. Sitaki uonekane umetoka humu.”alisema Jesca akiwa anamtazama Badu, alitabasamu kisha akamchapa Jesca kofi la huba kwenye makao yake kisha akatoka zake nje kuingia chumbani kwake.
Jesca alirudi pale kwenye sofa na kujilaza. Alitabasamu tu kuona leo amepatikana.
” Anajua kunikuna huyu kijana jamani. Sijui alikuwa wapi kipindi chote hicho.”alijisemea Jesca akiwa anaitazama feni ya juu ikiwa inazunguka.
Muda huohuo uliingia ujumbe kwenye simu yake ilokuwa kitandani. Alinyanyuka kwenda kuichukua kutazama. Aliona jina la BABA DULA ambalo alikuwa amelisave, ilibidi afungue kuisoma meseji ile.
“We mwanamke leo umeninyima mimi ukidai Simba wanachezi kumbe watu wanapiga kama kawaida. Sijapenda ulichonifanyia Jesca.”ilikuwa ni meseji ya yule mlinzi wa mnara baba Dula akiwa analala kwa Jesca.
“We mjinga nini kukupa siku moja tu ndio umenogewa. Mkeo sio yupo!”alijisemea mwenyewe Jesca kisha ile meseji akaisave kwenye simu yake zikionekana kuna baadhi ya meseji kadhaa ambazo baba huyo alikuwa akizituma. Alitupa simu yake kitandani akachukua maji kwenda bafuni kujimwagia.
Badu alikuwa zake kwenye sofa amejilaza akitafakari penzi la Jesca ambalo muda mfupi ametoka kulifaidi. Alijikuta anacheka tu maana njama aliyotumia mwanamke huyo hadi kufanikiwa hakuweza kuijua kirahisi. Alinyanyuka pale alipo baada ya dakika kadhaa na kuchungulia nje kuona Jesca akitoka bafuni akaingia zake ndani. Naye alitoka kwenda kujimwagia usiku huo kuondoa jasho.
Kesho yake baada ya Adhuhuri pilikapilika za hapa na pale zikiendelea, Mwajuma alikuwa anapiga simu kwa bwana’ke Roja lakini simu haikuwa yenye kupokelewa. Hadi alianza kukosa furaha baada ya kuona kama anafanyiwa kusudi na mwanaume huyo ambaye siku hiyo ndio walikuwa wamepanha wakutane baada ya Mwaju kumhitaji mwenzake. Alikuwa zake chumbani kwake tu anachezea simu yake kwa dakika kadhaa huku akijaribu mara kwa mara kumpigia Roja, simu iliita tu na mwishowe kukata.
“Huyu sijui yuko wapi jamani hadi hapokei simu zangu.”aliongea Mwaju akionesha kufura kwa hasira sana.
Muda huo Roja mwenyewe alikuwa zake chini ya gari akifanya service ya kumwaga oil kwenye gari moja aina ya Harrier. Kazi yake ya ufundi magari ndio humpatia kipato kuweza kusongesha maisha yake.
Alifanya kazi hiyo kwa umakini wa hali ya juu na alipomaliza aliweka oil safi kisha akaelekea kwenye mlango ambapo mhusika alikuwa ndani na mpenzi wake pembeni.
“Bosi hebu washa gari, nadhani nimeshamaliza upande wangu ” aliongea Roja akiwa kwenye ovalori lake la kazi akifuta mikono yake kwa kitambaa.
“Ahaa sawa.”
Gari liliwashwa pale likawa linaunguruma huku Roja akiimana chini kuhakikisha kama kuna rikeji yeyote imetokea. Alipoona huduma yake iko vizuri alimhakikishia bosi wake huo ambaye alishuka kwenye gari na kwenda kumalizana na Roja.
Yule mpenzi wake ndani ya gari alikuwa anamtazama tu bosi huyo akitoa waleti na kuanza kumuhesabia Roja. Alinyanyua simu yake na kutafuta namba moja kisha akaipiga, sekunde chache tu simu ikapokelewa.
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU