UTAMU WA JAMILA (11)

UTAMU WA JAMILA 11

“Yes hallow!”

“Hallow mambo.”

“Safi tu nani?”

“Mmh wee naye kwani namba yangu hii…! Oh sorry kumbe nimepiga kwa voda. Ni mimi Jesca nambie Badu.”

“Ah safi tu Jesca vipi uko powa? Mi nikajua upo ndani kwako maana nasikia mziki tu chumbani kwako.”

“Ah wewee nimetoka tangu asubuhi hapo nimeacha hivyo ninamaana yangu. Kuna kitu nataka nikwambie Badu.”

“Ehe kitu gani hicho?”

“Kwanza leo utakuwa free au utatoka?”

“Aaam leo niko free ila jioni kama kawaida naenda mazoezi si unajua kutoa jasho kidogo.”

“Ah Badu bwana, sasa sikia mimi leo nataka tushinde wote. Tukatafute chumba tofauti na hapo ndani. Ile shoo ya jana nimeielewa ila sijapata tu muda mzuri wa kufaidi. Nataka ukanipe zaidi ya pale hayo mazoezi ya kutoa jasho utatoa kwenye mwili wangu Badu.”

“Aaah Jesca mambo gani tena hayo, hebu acha hizo bwana.”

“Kweli Badu sio utani ujue. Im sirious!”

“Nikwambie tu sina ela kwasasa ya kukupeleka huko bwana. Na isitoshe tumeduu kwa kutamaniana tu isiwe ndio mazoea.”

“Acha ufala huo Badu, wewe mtu mzima na mimi pia. Leo tunaendelea tulipoishia jana na sisemi kuwa ndio tumeanza kuwa wapenzi. Tunafanya kisha kila mtu na maisha yake, na swala la kulipia huko we ondoa shaka kila kitu nasimamia mimi. Okay!”aliongea Jesca akiwama kweli anamaanisha. Huku macho yake yakitaza kwa nje na kuona yule boss akigeuka kurejea kwenye gari.

” Okay sawa. Wapi sasa?”alisikika Badu kwenye simu.

“Nitakutumia sms sasahivi naomba unifowadie mimi tena hiyo sms haraka sana, fanya hivyo.”alisema Jesca na kukata simu yake. Akaanza kuandika ujumbe kwa haraka kisha akamtumia Badu.
Na muda huo ndio yule boss aliweza kufika ndani ya gari na kumkuta Jesca akiwa anachezea simu yake.

“Oh my love nimekuacha pekeyako sorry.”

“Usijali mpenzi.”

“Okay kila kitu kipo fresh. Leo tunaenda kulala Bagamoyoo, siku mbili tutakuwa huko jila kitu kipo fresh. Au unasemaje!”alisema mwanaume huyo aliyeonekana kutabasamu.

“Hakuna shida my. Leo utanitumia utakavyo dear.”aliongea Jesca na gari likawashwa safari ikaanza huku Jesca akiweka simu yake pembeni karibu na mwanaume huyo. Yeye akaanza kutoa lipstick kujipodoa, alimfanya yule mwanaume afurahi tu kuona yupo naye siku hiyo.

Waliingia kwenye lami gia zikaanza kupanguliwa. Hata dakika chache zilipita ujumbe ukapata kuingia kwa Jesca.
“Simu yako inaita baby, nahisi ni sms.”alisema yule mwanaume akiwa anaendesha gari.

“Ah ifungue my mi najiweka sawa hapa.”aliongea Jesca akimruhusu mwanaume huyo kushika simu yake. Aliona ndio anapendwa haswa kuona mpaka anaaminika kufungua simu ya mwabamke huyo. Alipoitazama ile meseji alishtuka kidogo yule mwanaume.

” Baby, Mmh!”

“What! Mbona umeguna?”

“Nahisi kwenu kunatatizo.”

“Tatizo? Kuna nini? Hebu nipe hiyo simu.”aliongea Jesca na kuacha kazi yake ya kujipodoa akiichukua simu mikononi kwa mwanaume huyo ambaye alitafuta sehemu nzuri kulipaki gari lile kwanza pembeni.

Kule alipo Badu alikuwa anashangaa sana kwa kile ambacho ameambiwa na Jesca muda ule.
“Huyu mwanamke kuna mtu yupo naye anamchezea mchezo sio bure.”aliongea Badu mara baada ya kuujua ukweli.
Ni muda ule baada ya kuongea na Jesca kisha kumwambia airudishe sms ambayo atamtumia muda huo. Hata ulipoingia ujumbe huo Badu aliusoma.

” DADA NJOO HARAKA NYUMBANI MAMA AMEZIDIWA NA PRESHA TUNATAKA KUMPELEKA HOSPITALI.”

Ujumbe ambao ulimfanya Badu astaajabu sana, lakini ilimbidi amrudishie Jesca tena kama alivyoagizwa.

Kule Jesca alibadili jina la Badu na kuandika MARIA na kuiweka simu pembeni. Na zoezi lake lilitimia baada ya boss yule kuona jina la MARIA likituma ujumbe ule akijua fika ni familia yao.
Jesca alizuga kuchanganiyika huku akitulizwa na boss huyo ambaye hakuwa na chaguo zaidi ya kushuka kwenye gari na kusimamisha Taxi. Alimshika Jesca kumuingiza humo ili apate kuwahi kwao waweze kumuwahisha huyo mama anayesadikika kuzidiwa.

“Kila kitu kitakuwa sawa my wala usijali. Wahi nyumbani kwanza kacheki hali ya mama tutawasiliana. Pole sana mpenzi.”aliongea yule boss huku akimpatia pesa Jesca zaidi ya laki na hamsini.

“Sawa my, wacha niwahi tutawasiliana.”aliongea Jesca na kuagana safari ikaanza.

Yule boss alibaki kusikitika tu maana alishapanga siku hiyo kwenda kuponda raha na mwanamke huyo Bagamoyo. Bila kujua yote hayo ameigiziwa tu, aligeuka nyuma Jesca na kutabasamu tu kuona janja yake imetiki. Alinyanyua simu yake na kumpigia Badu haraka ikapokelewa.
“Badu, naomba tukutane Deluxe Bar hapa Magomeni. Chukua boda nitalipia.”alisema Jesca na kukata simu.
Alimuamuru dereva taksi aelekee Magomeni Mapipa kwenye Bar hiyo.
ITAENDELEA 

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!