UTAMU WA JAMILA (12)

SEHEMU YA 12

ILIPOISHIA
“Badu, naomba tukutane Deluxe Bar hapa Magomeni. Chukua boda nitalipia.”alisema Jesca na kukata simu.
Alimuamuru dereva taksi aelekee Magomeni Mapipa kwenye Bar hiyo.

SONGA NAYO
Baada ya muda kupita Mwajuma alishindwa kuvumilia kuteseka vile kitandani. Alikuwa alibiringita mwenyewe kwa ile hamu aliyonayo ya kukutana na mpenzi wake.
Alijiandaa vizuri ili apte kuondoka kuelekea ofisini kwa Roja apate uhakika kama kweli yupo na anamfanyia kusudi kutopokea simu yake muda wote.

Alipotoka tu nje alipata kumuona Badu naye akiwa anaufunga mlango wake kuweza kutoka. Alimtazama kijana huyo na kujikuta anashusha pumzi.
“Yaani leo Roja akinizingua tu nachepuka kwakweli. Sitaweza kuvumilia kuumia kiasi hiki kama sina mpenzi bwana.”alijisemea mwenyewe pale huku akiwa anamtazama Badu ambaye baada ya kuhakikisha mlango wake ameufunga imara aligeuka kuondoka zake. Mwajuma naye akafuata nyumanyuma naye akitoka kuelekea safari yake.

Muda huo Roja ndio alipata kuchukua simu yake kwenye chaji baada ya kuona simu yake inaita. Alipotazama alipata kuona ni Mayasa ndiye anapiga, ikabidi apokee.

” Yes Mrembo wangu.”

“Mambo Roja.”

“Safi tu mzima wewe.”

“Mimi mzima niambie uko wapi?”

“Nipo job ila ndio nimemaliza kazi hapa nataka kurudi geto nikapumzike leo sina mood ya kazi.”

“Okay basi sawa my dear. Nitakuja basi kukuona maana nipo mitaa ya kwenu nimekuja kumcheki mamamkubwa hapa.”

“Ahaa sawa, ila ukija usianze uchokozi wako leo sina mzuka.”

“Ah we nawe acha hizo. Haya nitatulia tu.”alisema Mayasa na simi ikakatwa akionesha kufurahi .

Roja naye akipokata simu ndio akapata kuona missed call zaidi ya 10 tena ni mtu mmoja tu, Mwajuma.
“Oh huyu mwanamke kumbe alinipigia, wacha nimpigie.”

Alinyanyua simu na kumpigia Mwajuma ambaye haraka alipokea.
“We ndio umeamua unipigie muda unaotaka wewe si ndio? Umenichunia muda wote ushamaliza mambo yako ndio unanitafuta saivi Roja.”
Hakutaka hata salamu akaanza kuporomosha lawama kwa mwanaume huyo.

“Basi basi my usiendelee kulalama hivyo haipendezi. Naomba nisamehe kwanza mpenzi wangu maana sikuwa na simu karibu. Niliiweka chaji namimi nikawa nafanya kazi huku nje na hapa nimemaliza ndio nashika simu.”

“Roja! Roja ujue mi sipendi uniumize kichwa changu kukaa kukufikiria wewe kama mtoto bwana.”

“Basi mamaa nisamehe .”

“Uko wapi saivi.”

“Nipo kazini hapa nataka kutoka saivi niende geto.”

“Nisubiri hapohapo.”

“Eh, nini? We uko wapi?”

“Nakaribiria hapo nipo kwenye bodaboda nisubiri twende wote.”aliongea Mwajuma na kumfanya Roja ashtuke kusikia hivyo. Ilimbidi akate simu kwanza.

“Ebwana eeh ukisikia Both team to score ndio hii sasa. Nimkatae nani sasa hapa aiseee. Mwajuuuuuu hapana nimemchenga sana leo wacha nikamalizane naye. Mayasa utanisamehe mpenzi wangu.”aliongea Roja na kunyanyua simu tena kumpigia Mayasa.

“Yes hubby.”

“Mayasa niskilize. Mwajuma yupo karibu anakuja hapa amelazimisha niondoke naye geto. Tangu siku ile hadi leo sijakutana naye nadhani leo ameamua. Nakuomba mpenzi usije home yasije kuzuka mengine. Please!”

“Ah hayo mambo ndio siyatakagi bwana.”

“Sawa lakini hakuna jinsi my. Kumbuka tumeduu siku mbili mzima hadi leo Mwaju sijaonana naye. Sasa usitake anishtukie miye akaja kuanza kuchunguza ukajulikana. Wewe leo tulia tu ukitoka kwa mamako nenda kwako katulie tutawasiliana.”aliongea Roja akitaka kuyaweka mambo sana.

“Halafu Roja isije kuwa ni mwanamke mwengine huko unanistopisha kumbe sio Mwajuma!”

“Aaaaaa Mayasa naanzaje kuchukua mwengine. Ni Mwajuma sio utani, na tena huyu hapa amefika baadae baadae Mayasa.”aliongea Roja na kukata simu yake baada ya kumwona Mwajuma akishuka kwenye bodaboda akimlipa. Taratibu akaanza kumsogelea kijana huyo ambaye alionesha tabasamu baada ya kumwona Mwajuma.

“Waoh my wife. Nambie.”

“Safi tu vipi.”

“Poa, naona leo umewaka.”

“Ah acha zako bwana. Roja hebu tuondoke haraka tukaongee kwako.”aliongea Mwaju kwa sauti ya uchovu.

“Mh mbona wanitisha kuna tatizo.”

“Bwana Rojaa! Nini ambacho huelewi bwana twende uko!”aliongea Mwajuma na kumsogelea Roja pale aliposimama.
Kwa macho ya watu pale gereji alijitoa pale na kumkamata mkono Mwajuma akamuingiza kwenye gari dogo lililopaki pembeni. Aliona kweli mwanamke huyo hali ni tete upande wake na huenda angefanya jambo pale watu wanamuona.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!