UTAMU WA JAMILA (18)

SEHEMU YA 18

HAKIKISHA KABLA YA KUSOMA UNALIKE KWANZA KISHA UENDELEE KUSOMA

ILIPOISHIA
kuona siku moja tu ya kukutana na Badu ndio amejihakikishia kupata penzi lake muda wote.

TUENDELEE

Saa sita mchana Mwajuma alikuja kuamshwa na muito wa simu yake. Aliinyanyua kwa uvivu na kutazama aliyempigia, jina la ROJA lilipata kuonekana kwenye screen ya simu yake.
Alipindisha mdomo wake na kuikata simu hiyo kisha akaitupa pembeni ya kitanda na kuendelea kulala.
Haikupita hata dakika moja ilisikika simu ikiita tena hali hiyo ilimkera Mwajuma na kuamua kupokea kwa hasira.
“We unataka nini watu wamelala?” alifoka kwa ukali Mwajuma.

“Haaa my unaongeaje hivyo? Na hadi saa sita hii unalala kweli!”

“Ndio nimechoka.”

“Umechoka! Umechokeshwa na nini mpenzi wangu.”

“Wee shuhuli ya jana niliyoifanya sio ya kitoto. Hapa kiuno chote kinauma!”alisema Mwajuma na kumfanya Roja kule alipo acheke kwa kile alichosikia.

“Wala jana hatujafanya sana ilikuwa ni kawaida tu round moja unasema umechoka kweli jamani!”aliongea Roja akijua vile walivyofanya na Mwaju ikapelekea mrembo huyo kuchoka.

“Ah we hujui tu. Ila elewa tu kuwa nimechoka kiuno kinauma hatari, naomba nipumzike.”

“No no no Mwajuma hebu ngoja basi, leo nipo free my njoo geto leo tutashinda wo..”

“Wee kumbe hunielewi unazani nakutania. Hapa sina hata muwasho mmoja yani zote zimekwanguliwa jana. Nipo mwepesi kabisa na sihitaji kukutana na mtu. Kwaheri.”

“Nini? Hallo! We Mwajuma mbona sikuelewi!”

Alitazama simu yake na kuona alikuwa tayari Mwajuma amekata simu.
Akibaki njiapanda kwa kauli za msichana huyo.
“Mbona simuelewi huyu? Au ndio hasira za kumuacha jana geto. Dah!”alisema Roja akiwa amekaa nje ya chumba chake. Alitazama beseni mbele yake lililokuwa na nguo zilizomo ndani ya maji.
Ni zile ambazo Mwajuma alizitia humo kwa hasira kisha akaondoka zake. Hakuwa na ujanja ilibidi aanze kuzikamua mojamoja na kuzianika zote, huku akiamini baada ya muda ataongea na mpenzi wake watakutana tu.

Muda huo Jesca alikuwa zake anatoka ndani ya nyumba aliyopanga. Alifika nje na kuchukua bodaboda akionekana kuelekea sehemu. Simu yake ilipata kuita na alipotazama aliona ni jina la baba mwenye nyumba mzee Chombo. Alipokea.

” Ndio mzee, shikamoo.”

“Marhaba, haya umeshaanza kutoka?”

“Ndio nipo kwenye bodaboda.”

“Sawa, ukifika tu nijulishe nipo nakusubiri.”

“Sawa.”alikata simu baada ya kuwasiliana na safari ikaanza.

Mama J alikuwa zake anafanya usafi ndani na kuandaa chakula cha mchana. Mara kadhaa alikuwa anatazama tu mlango wa binti yake huku akiendelea na kazi.
“Huyu mtoto mpaka sahizi hajaamka kweli jamani! Au anaumwa?” Taratibu akainuka pale alipo na kuanza kumuita mwanaye Mwajuma, aligonga mlango mara kadhaa na punde tu ukafunguliwa.

“Mwenzetu haya! Kulikoni kutulalia mpaka saa sita hii inakwenda saa saba mtoto wa kike umelala tu.”

“Ah sijisikii vizuri tu kichwa kinauma.”

“Mh kimeanza saa ngapi?”

“Tangu jana ila naona ndio kinazidi.”

“Umeze dawa sasa sio kulala unadhani ndio utapona. Amka umeze dawa bwana unakaa ndani unatutisha tunajua umekufa bwana. Hebu amka!”aliongea mama huyo akigeuka kuondoka zake pale.
Mwaju alibaki kutabasamu tu baada ya kumdanganya mama yake. Akirudi zake chumbani na kujitupa tena kitandani.

“Kwakweli sijapata kutumika kiasi hiki hadi nalala mpaka saahizi! Huyu mkaka jamani khaaa! Amejua kuninyoosha kwakweli.” alisema Mwajuma akiwa anatabasamu akiwa anakumbuka shuhuli ya jana usiku chumbani kwa Badu. Alikamata simu yake na kumtuma meseji Badu ya kumjulia hali.
Punde alijibiwa na kuanza kuchati muda huo.

Baada ya muda kupita Jesca aliweza kukutana na Mzee Chombo kwenye mgahawa mmoja wakiwa wamekaa huku mezani kila mmoja akiwa ameagiza juisi.

“Haya nimeitika wito wako mzee hadi kufika hapa sielewi unataka kuzungumza nini na mimi.”alisema Jesca.

” Ni kweli nimekuita hapa na sikutaka kukwambia lolote lile hadi ufike. Na sitaki tupoteze muda uwe tu na amani. Kuna kazi nataka unifanyie ya upelelezi kidogo nadhani mara kwa mara nakuonaga tu upo mule ndani. Napata taarifa zako kuwa unaingiza wanaume sana. Ila kwa kipindi hiki sijasikia tena hayo mambo naamini umeacha si ndio!”alisema Mzee huyo na kumfanya Jesca acheke kidogo.

“Okay hilo sio lililotuleta achana nalo. Ishu iko hivi, nimekuchagua wewe kwakuwa nimeona huna mazoea na mtu yeyote mule ndani. Nikaona unaweza kuifanya kazi yangu hii. Nataka umchunguze mkewangu mimi yaani Mama J nasikia taarifa mbaya kwake kuwa anatembea na vijana wadogo na wanaume wengine pia mtaani pale. Na hasa nasikia ameanzisha tabia yake ya kutembea na wapangaji mule ndani. Sasa nataka unihakikishie hili nijue kama ni kweli au laa. Na ushahidi ukiupata hata kwa vitendo naomba nijuze mapema kama nitakuwa karibu nije kuhakiki. Je utaiweza hiyo kazi?”aliuliza mzee huyo akionesha kweli kutaka msaada juu ya jambo hilo. Taarifa za mkewe zilimfikia pia yeye hivyo lengo lake ni kuupata ukweli ili afanye maamuzi.

“Mh mzee wangu hilo swala naona kama gumu kwangu!”

“Wala usijali binti. Naomba tumia njia yeyote ile unithibitishie hilo. Na nakuahidi kama nitaujua ukweli utakaa pale miezi 6 Bure kabisa.”aliongea mzee Chombo akiwa anamaamisha.

Jesca alipekecha akili na kuona kazi hiyo si ngumu sana kwake. Kodi ya elfu 50 kila mwezi akipewa uhuru wa mieI 6 bila kulipa si jambo dogo kwake.

“Basi sawa nitaifanya kazi hiyo mzee wala usijali.”aliongea Jesca na kumfanya mzee huyo afurahi. Waliendelea kushushia na juisi huku maongezi yakiendelea.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!