UTAMU WA JAMILA (19)

SEHEMU YA 19

“Basi sawa nitaifanya kazi hiyo mzee wala usijali.”aliongea Jesca na kumfanya mzee huyo afurahi. Waliendelea kushushia na juisi huku maongezi yakiendelea.

TUENDELEE

Alasiri ya siku hiyo Mwajuma aliamua kwenda kumtembelea rafiki yake Mayasa. Ni masiku kadhaa yamepita bila wawili hao kuonana, hivyo siku hiyo ilikuwa kwao ni furaha. Lakini kwa Mayasa haikuwa zaidi ya mwenzie. Ni baada ya kuujua utamu wa Roja ambaye ni mchumba wa Mwajuma na alilijua hilo kabla. Hivyo alimfurahia siku hiyo na kuongea mengi.

“Sikuhizi Roja simuelewi kabisa shosti. Naona amebadilika kabisa sijui tayari kashapata malaya kambadilisha akili jamani!”aliongea Mwaju wakiwa wamejilaza kitandani chumbani kwa Mayasa.

“We mpumbavu mi malaya?” Moyoni aliyasema hayo Mayasa baada ya kutafsiri kauli ya rafiki yake.

“Mh mbona unamuhisi vibaya shemeji? Sio vizuri.”

“Hapana Maya, saivi Roja sio yule kabisa. We angalia jana hadi kwenda kwake nimefanya kufosi mimi yani. Na tumefika anaanza kunidengulia hadi namlazimisha tusex hivi kweli Roja wa kubembelezwa vile? Na tukiduu kidogo tu amechoka nakwambia yaani jana sikumuelewa kabisa.”

“Jamani Mwaju, sasa unajua kazi za shemeji ni za kutumia nguvu kishindana na mavyuma huko. Wewe unaanza kumfikiria vingine tena jamani hebu acha zako bwana.”

“We hujui tu Maya kilichonitokea jana. Unajua sijasex muda mrefu sana nilitegemea jana angeninyoosha ile roho inapenda. Kwakweli alinipaka tu shombo na niliondoka kwake kwa hasira sana. Nahisi tu ananizunguka anademu mwengine yule.”

“Mh pole mwaya, ndio wanaume hao mwaya japo sina hakika kama anakucheat.”alisema Mayasa akimtazama Mwajuma kwa dharau maana anaona kama anampigia makelele.

Huku upande wa pili Jesca alikuwa anarejea zake kwake mara baada ya kuachana na Mzee Chombo kisha akapitia sehemu zengine kwenye mihangaiko yake. Katika kutembea akiwa anakaribia na maeneo ya mtaa wao alipata kuonana na baba Dula mpangaji mwenzake.

“Dah afadhari nimekuona we mwanamke.”aliongea baba huyo mlinzi wa mnara.

“Unashida gani na mimi we baba?”

“Hebu acha hizo Jesca, hebu sogea huku tuongee vizuri.”

“Bwana mi ninaharaka zangu nimechoka nataka nikapumzike.”

“Sikia basi, mimi leo nataka nilale na wewe aisee. Nimekumbuka lile penzi ulonipa usiku ule Jesca, nakuomba sana leo.”

“Hii wewe unawazimu? Umuache mkeo ndani uje kuniparamia miye huoni haya?”

“Hebu acha hizo bwana Jesca, unajua napatwa na wivu nikisikia miguno ikitokea chumbani kwako nikijua kuna mwanaume anakufaidi kama nilivyofaidi mimi. Naomba aisee leo nitakupa mzigo mkubwa Jesca.”alisema baba Dula kwa sauti ya chini huku jua likianza kuzama kuashiria jioni imeingia.

“We mlinzi nisikilize, ile siku nilikubali kukuvulia bikini yangu ni kwasababu nilikuwa natafuta chumba cha kukaa na wewe ndio ukanipokea. Sasa kukupa siku moja ndio umeifanya yako? Yako ipo ndani kwako nenda kafaidi utakavyo. Isitoshe, unakipi cha kunipa saivi baba dula? Tafuta ela kwanza siku ukitaka mechi na mimi ujipange haswa sio kitoto. Kwaheri naenda kulala.”aliongea Jesca kwa kujiamini kisha akaondoka zake kumuacha mwanaume huyo akiwa amesimama tu. Alimtazama hadi alipotokomea na kushusha pumzi kuona amechemka leo kumshawishi Jesca ambaye ni wazi hang’atuki bila ya pochi.

“Mtoto mtamu sana huyu, kama shida hela nitazitafuta. Na siku akinipa nitamuonesha jinsi gani nilivyompania, naamini atanilegezea tu siku nyengine.”alijisemea mwenyewe pale aliposimama kisha akaingia mkono mfukoni na kutoa noti mbili za elfu kumikumi, alizitazama kisha akazirudisha mfukoni na kuondoka zake.

Muda huo Badu alikuwa zake nje ya chumba chake akifuta viatu vya mazoezi. Muda huohuo alitokea Mwajuma na kumkuta Badu akiwa amesimama pale mlangoni akifutafuta viatu.

” Vipi ndio kumekucha au?”aliuliza Mwajuma.

“Yah kama kawaida nataka nikapashe kidogo mwili.”alisema Badu akionesha kujiandaa kwa mazoezi ya jioni.

“Ah basi ningoje, usiondoke ningoje.”aliongea Mwajuma na haraka kwa kukimbia akaingia zake ndani kwao kwenda kubadilisha nguo. Badu alimtazama huku akitabasamu kisha akaendelea na kazi yake.

Dakika kadhaa geti lilifunguliwa na kuingia Jesca. Alipiga hatua kadhaa na baada ya kutazama mbele alipata kumuona Badu pale mlangoni. Alisogea na kumsalimia kwa tabasamu.

” Haya wapi tena mbona umesimama?”

“Ah muda wangu wa kufanya tizi umefika. Nikimbie kidogo hadi saa mbili saa tatu narudi.”

“Oh sawa, mi nipo tu ndani napumzika. Unajua kiuno kinaniuma kwa mbali bado.”aliongea Jesca kwa sauti ile ya madeko.

“Oh pole sana dear.”

“Ukirudi uje unichue kidogo huenda kikaa sawa.”aliongea Jesca akiwa anamtazama Badu kwa kumtega.

“Acha basi uchokozi huo Jesca. Unaniangaliaje hivyo?”alisema Badu na kumfanya Jesca acheke kwa sauti. Hata yeye alijishtukia na kuziba mdomo.
Haraka akapiga hatua za mwendo hadi kwake. Alifungua mlango na kuingia zake ndani huku Badu akiwa anatabasamu baada ya kumuona mwanamke huyo.

Muda mfupi alikuja Mwaju akiwa fiti, walitoka wawili hao na kuanza mazoezi ya kukimbia.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!