SEHEMU YA 21
TULIPOISHIA
Udhaifu huo ndio aliutumia Mama J kuhakikisha anapata kumtumia kimwili baba Dula ambaye hakuwa na chaguo zaidi ya kukubali alichoambiwa.
SONGA NAYO
Jesca alikuwa nyumanyuma hadi mahala ambapo aliweza kufika mama J.
“Looh huyu mama ndio anapofanyia ufuska hapa. Muone yuulee anataka kuingia gesti. Kavizia kigiza kimeingia ndio afanye mambo yake looh!”alijisemea Jesca na kubaki kucheka tu mwenyewe. Aliamua kuondoka zake baada ya kutambua siku hiyo mama J ameenda gest japo hakujua mtu ambaye anakwenda kukutana naye.
Mama J alipata kuzama kwenye nyumba hiyo ilikuwa na geti, humo alipata kuelekezwa na baba Dula hadi kwenyw chukba ambacho yupo anamsubiri. Moja kwa moja alielekea huko na kumkuta baba huyo akiwa amekaa kitadani anamtazama Mama J anavyoingia.
“Mbona kinyonge hivyo we mwanaume? Unaumwa au!”aliuliza mama huyo akiweka pochi yake kwenye meza kisha akamsogelea karibu baba Dula.
“Hivi mama Mwajuma hiki unachotaka kufanya umeridhika kabisa kutoka moyoni?”aliuliza Baba Dula akiwa anamtazama mama huyo aliyeonekana hajali kabisa akianza kuvua nguo zake na kubakia na nguo ya ndani tu. Alichukua taulo la hapo gesti akajifunga na kurejea kitandani alipo baba Dula.
“Kwani we shida yako iko wapi? Hiki tunachofanya ni kwa matakwa yangu na kwa faida yako pia.”aliongea mama J akianza kumfungua vifungo vya shati baba huyo.
“Kwani huwezi kunisaidia tu hivi bila ya sisi kufanya haya? Maana hii ni hatari nikijulikana na mzee Chombo itakuwaje? Si ndio nitasambaziwa mtaa mzima hata mkewangu atajua kuwa nimetoka nje ya ndoa.”
“Acha ufala wewe kwani nani hapa hajaolewa? We unanipa burudani halafu unakaa bure miezi miwili unataka nikusaidie nini tena hapo? Au kama hutaki basi narudi nyumbani na jioni nataka kodi yangu sitaki maneno.”aliongea mama huyo na kushuka kitandani. Alichukua nguo zake akionesha kuchukia, baba Dula alitafakari na kuona leo ataumbuka endapo akidaiwa pesa ya kodi maana hana ela. Alijikuta anapata nguvu ya kunyanyuka pale kitandani na kumkumbatia mama huyo ambaye ndio alikuwa akivaa sidiria yake.
“Nakutania bwana jamani, hata mimi nilikuwa natamani niutumie mwili wake.”alisema baba Dula akipeleka mikono kifuani mwa mama huyo na kuanza kuchekea maziwa.
Kama maji vile, Mama J alipoa baada ya kushikwa tu. Alikuwa ameshika dela lake akitaka kuvaa, alishindwa kuendelea akajikuta analitupa chini huku akipapaswa na kushikwa kiuno na baba Dula. Aligeuka na kuanza kupena mabusu tela, walisukumana kitandani na kuanza kufanya kile kilichowaleta humo gesti.
Baada ya muda kupita Badu na Mwajuma waliweza kurejea nyumbani baada ya kutoka kufanya mazoezi ya aina mbili. Mwajuma alionekana kuchoka sana hata tembea yake tu ilidhihirisha hilo. Na muda huo ndio Jesca alikuwa naye akiwasili hapo wakapata kukutana wote getini wakiingia ndani. Mwajuma alitoa salamu kwa Jesca ambaye hakuitika salamu hiyo, hakujali hilo Mwajuma aliingia zake ndani baada ya kifungua geti moja kwa moja akaenda zake ndani. Tembea yake ilimtia mashaka sana Jesca ambaye moyoni alianza kuingiwa na wivu akihisi ukaribu huo wa wawili hao.
“Mbona unashangaa hivyo Jesca? Kwema?”aliuliza Badu akitaka kuingia ndani kwake.
Jesca alimtazama Badu kwa muda na wala hakusema kitu zaidi ya kuingia moja kwa moja hadi chumbani kwake akajifungia.
Alitupa mkoba wake kwenye sofa naye akaenda kukaa kitandani kuvua viatu vyake huku mawazo yakimzonga.
“Hawa wamekuwaje mbona wanaukaribu vile. Wameanza lini kufanya hayo mazoezi pamoja hadi usiku huu? Hapana huyu malaya anataka kumchukua Badu , sitakubali hili jambo litokee. Mfyuuuu!”aliishia kwa kutoa sonyo likiwa kama moja ya chuki kwa Mwajuma ambaye amemuhisi kumtamani Badu.
Alikaa dakika kadhaa akitafakari juu ya kile alichokiona lakini moyo wake haukutulia kabisa, hata yeye mwenyewe alijishangaa kuona amekuwa na wivu mno kwaajili ya Badu. Ilibidi anyanyue simu yake kumpigia Badu, muda huo alikuwa anajiandaa kwenda bafuni kuoga alipata kuona simu yake inaita. Alitazama na kuona ni Jesca akapokea.
“Nambie J.”
“Haya tangu lini wewe na Mwajuma mkafanya mazoezi pamoja?”aliuliza Jesca akionesha kuwa na shauku ya kujua.
“Ah Jesca ndo maswali gani hayo? Mbona tuna kama wiki hivi tunafanya pamoja! Kwani kuna tatizo?”
“Mimi siamini kama hakuna kinachoendelea tofauti na mazoezi haya. Labda nikwambie tu Mwajuma ni kicheche yule anatembea na wanaume kibao hapa mtaani na nasikia taarifa zake. Sasa kama ndio anakunyemelea kaa ulijue hilo.”
“Ah Jesca bwana mbona unafika mbali huko? Mwaju ametaka tu kampani ya kukimbia hata wewe ukitaka pia fresh tunajiunga.”
“Ah niache miye unikimbize kwa matatizo gani? Ila moyo wangu hauna amani kabisa leo siamini haya usemayo. Na huenda ikawa ndio gia ya mazoezi kumbe mnafanya mambo yenu kisiri. Maana tembea ya Mwajuma sijaielewa kabisa leo.”
“Acha hizo bwana Jesca.”
“Hapana Badu, nakuja sasahivi navua nguo hapa fungua mlango wako.” alisema Jesca na kukata simu baada ya kutoridhishwa kabisa na maneno ya Badu.
Alishangaa mwanaume kuona Jesca amekuwa na wivu wa waziwazi kabisa juu yake.
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU