SEHEMU YA 23
ILIPOISHIA
Hakutaka maongezi yawe marefu kwenye simu, alisogea mbele zaidi akasimamisha bodaboda safari ikaanza kuelekea kwa Roja.
SONGA NAYO
Hakutaka maongezi yawe marefu kwenye simu, alisogea mbele zaidi akasimamisha bodaboda safari ikaanza kuelekea kwa Roja.
Baada ya masaa kadhaa kupita Badu aliufungua mlango wake na kutazama huku na kule kama kuna mpangaji yeyote yupo nje. Alihakikisha kupo shwari aliingia ndani, muda mfupi Jesca alitoka zake akiwa kwenye vazi lake la kanga akionesha kuchoka. Moja kwa moja akaongia zake chumbani kwake na kijitupa kitandani.
Kile ambacho kimempeleka kwa Badu alikisahau kabisa baada ya kuzidiwa na hisia za mapenzi akajikuta anasahau kwamba amekuja kupata uhakika juu ya Badu na Mwajuma kama kuna kitu kinaendelea kati yao. Alibaki kufurahi tu na kusikitika jinsi alivyomhusudu Badu hadi kuwa na wivu naye.
Aliamua kuinuka kuteka maji kwenye ndoo akaondoe jasho mwilini.
Roja alikuwa ametulia ndani kwake akiendelea kutazama muvi kwenye Tv. Alikuwa bado hajaelewa msimamo wa Mwajuma baada ya kuonesha hana shida tena ya kuonana naye angali awali ndio aligoma kuondoka akitaka kupewa mapenzi na Roja aliyeondoka siku ile.
“Huyu mwanamke ndio ameninunia kiasi hiki jamani! Siku ile alokuwa aking’ang’ana kutaka tuendelee tu leo hii hataki kabisa kuniona! Au tayari kashapa mtu wa kumtoa hamu yake ndio maana ananidengulia leo!” alibaki kuhisi tu bila ya kuwa na uhakika wa kile anachofikiria.
Baada ya dakika chache mlango ulifunguliwa bila hata ya kubisha hodi. Mayasa alipata kuonekana akiwa mwenye tabasamu la aina yake. Alimfanya hata Roja afurahi baada ya kumuona na taratibu wakaogeleana na kukumbatiana.
“Nilikumisi mpenzi wangu.”alisikika Mayasa akiongea kwa sauti laini.
“Hata mimi pia nilikuwa nakuwaza, ila nikawa bize kuwasiliana na Mwajuma maana ameamua kunichunia kabisa.”
“Pole sana my, nikijisikia vibaya mwenzio Mwajuma alichokuwa anakisema. Ni wazi ameamua kukufanyia kusudi ili kukukomoa na sijui ulimfanya nini. Yaani anasema utatua sabuni jamani hahaha angejua!”aliongea Mayasa na kumfanya hata Roja acheke kusikia hivyo.
“Ah atajua mwenyewe bwana.”
“Kama amesusa siye twala, wanasema hainaga ushemeji.”aliongea Mayasa na kuzidi kumpa ujeuri Roja ajione hajapoteza kitu.
“Nawe umekuja muda mbaya sana saahizi utarudi kwenu saangapi.”
“Nipo njiani nimempigia mama kuwa sitarudi nalala kwa Mwajuma amenielewa. Hivyo leo tunalala wote hapa umalize haja zako mpenzi wangu nami unipe ile kitu roho inapenda.”aliongea Mayasa kwa kujiamini kabisa.
Kauli hiyo ilimpa amani Roja na kuona leo analala na mtoto mzuri bila wasiwasi. Hakufikiria tena swala la Mwajuma kumtosa.
Hadi kufika saa nne za usiku mama J ndio alikuwa anarejea nyumbani kwake. Muda wote huo alikuwa gesti na baba Dula wakifanya mambo yao bila bugudha ya aina yeyote ile. Hata alipoingia ndani alimkuta mumewe mzee Chombo akiwa mezani baada ya kumaliza kula amekaa na mwanaye Mwajuma.
“Haya bibiwee za huko utokako?”alianza kuongea mzee Chombo akiwa anamtazama mkewe.
“Salama tu kwema hapa ndani?”alijibu Mama J akionekana kuchoka mwili hata akili pia.
“Saa nne hii mke wa mtu umetoka wapi?”aliuliza baba huyo akionekana kuchukizwa na jambo hilo.
Mwajuma hakutaka kuendelea kukaa sehemu hiyo alinyanyuka na kuelekea zake chumbani kwake kujifungia.
“Ah nilikuwa na mihangaiko yangu tu leo. Nilienda kwa mama Siwema kumjulia hali kisha nikapitia kwenye vikoba huko ndipo nilipochelewa.”
“Muogope Mungu wewe mwanamke ujue! Hivi ni kikoba gani hicho cha saa 4 usiku? Au wewe ndio muweka hazina mlikuwa mnahesabu hela?”
“Sasa nikudanganye kwa kipi mmewangu? Nimetoka huko ndiko nimechelewa kuna mambo tulikuwa tunajadili. Na unajua mkeo sina kazi moja nikawa narudi mdogomdgo nikipitia madeni yangu ya kanga za watu waliokopa.”
“Ah haya sawa, ila nitajua tu ukweli kama unanidanganya pia itajulikana.”
“Jamani baba J unataka kuniambia umekosa uaminifu kwangu, na umri huu jamani saivi nitoke wapi mimi. Hebu niamini kama ninavyokuamini mumewangu siwezi fanya kitu tofauti.”
“Sawa nimekuelewa.”aliongea Mzee Chombo japo moyoni hakuwa na imani na kile kisemwacho na mkewe.
Kwa utashi wa maneno hayo mama J alimsogelea mumewe na kumbusu shavuni, alishuhudia mzee huyo akitabasamu kumuaminisha mkewe kuwa yupo sawa.
“Ngoja nikaoge tuje kula mumewangu.”
“We nenda kaoge uje ule mimi nishakula muda mrefu njaa ilikuwa inauma sana.”
“Ahaa sawa basi.”aliongea mama J na kuendelea zake chumbani.
Aliweka mkoba wake sehemu husika na kuanza kuvua nguo zake. Alivaa kanga kisha akajifunika na mtandio, taratibu alitoka zake na kwenda kuchukua maji kuelekea bafuni.
Hata alipokaribia mlango alipata kumuona Badu akitoka naye bafuni akiwa amevalia taulo lake. Waliangaliana tu huku kila mtu akitembea zake. Hakuna ambaye alikuwa na hamu ya mwenzake muda huo maana kila mtu muda mfupi tu wametoka kutumika haswa, si Badu aliyefanya mapenzi na Mwajuma pamoja na Jesca siku hiyo wala Mama J ambaye ndio anarejea kutoka gesti akiwa na baba Dula.
Aliingia zake bafuni kuoga na baada ya muda akarudi zake ndani……NINI KITAENDELEA
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU