UTAMU WA JAMILA (25)

SEHEMU YA 25

ILIPOISHIA
“Pole shoga yangu nilikuwa kwa bwanako namhudumia. Wewe si umesusa kumpa mapenzi. Wacha nikusaidie mwaya.”aliongea Mayasa kisha akanyanyuka kuandaa maji kwenda kuoga.

SONGA NAYO

Siku hiyo Badu alikuwa zake amekaa zake nje ya chumba chake akiwa anafua nguo zake. Alikuja mwanamama mmoja ambaye ni mpangaji mwenzake.

“Za saahizi kaka.”alisalimia mama huyo kwa ustararabu.

“Ah salama dada tu kwema!”

“Kwema, samahani nadhani ulipokuja uliambiwa swala la usafi ndani hapa. Sasa tunakukumbusha tu kama huna muda wa kufanya usafi unampatia mwenye zamu ela anakusaidia zamu yako ikifika. Nasema hivyo kwakuwa kesho ndio zamu yako hapa kwahiyo nakupa taarifa hii mapema, na mimi ndio namalizia leo hii. Hivyo kama utataka nishikilie zamu yako unitafutie elfu tatu nikufanyie usafi wiki nzima.”alisema mama huyo.

“Aha sawa dada nimekuelewa. Wacha nitakujulisha basi baadae maana leo ninausafi hapa bado nipo.”

“Haya sawa.”
Aligeuka yule mama na kurejea zake kwake huku Badu akiendelea kufua.

Baada ya muda aliweza kumaliza na kuandaa maji kuanza usafi kwanza uwani. Muda huo Mwajuma ndio alikuwa anarejea kwao na kumkuta Badu akiwa ameshika ndoo ya chooni na ufagio.

“Haa Badu?”alishangaa Mwajuma. Kauli yake hiyo ilimgeuza Badu nyuma kupata kumuona msichana huyo akimsogelea.

“Haya vipi tena na ufagio wa chooni?”

“Safi tu, leo zamu yangu ya usafi ndio nakwenda kufanya mambo chap.”

“Ah hebu acha bwana kazi za kike hizo. Usijali mimi nitafanya leo na hizo siku zengine.”

“Mh Mwaju mama yako si atauliza kulikoni!”

“Si nitamwambia umenipa tenda ya kufagia. Umenipa hela nikushikie zamu yako sasa tabu iko wapi hapo.”alisema Mwajuma kwa kujiamini kabisa.
Maneno yake yalimpa faraja Badu. Aliamuliwa kiwrka maji na fagio pale chini ili Mwajuma aifanye kazi hiyo.

Walielewana Mwajuma akaelekea zake ndani kubadilisha nguo kisha Badu akarudi zake chumbani kwake kijilaza kwenye kochi. Alibaki kutabasamu tu kuona amepata mterezo kwa Mwajuma baada ya kujitolea kufanya kazi. Hakuwa na wasi tena, alinyanyuka kwenda kuwasha muziki sabufa likaanza kusikika chumbani.

Jioni ya siku hiyo kama kawaida mazoezi yaliendelea kwa Badu pamoja na Mwajuma. Jesca alikuwa zake pia nje anapika akapata kushuhudia wawili hao wakitoka kuanza mwendo pamoja. Wala hakuwa na wivu ule wa awali tena maana ameridhika na maneno ya Badu akajua ni mazoezi tu wanayofanya na wala hakuna kingine kinachoendelea. Alipokuwa anaendelea na mapishi yake alipata kumwona Mama J akiwa dirishani anachungulia huku akiwa anaongea na simu. Hakuweza kumuelewa dhumuni lake akawa anaendelea kupika huku anaibia kutazama kule dirishani na kuona Mama J ametoweka.

Alikuja kufungua mlango Mama huyo huku akitazama pale nje ambapo hapakuwa na mtu zaidi ya Jesca tu kisha akairudi zake ndani. Jesca alikuwa anatazama pembeni asije kuonekana kama anafuatilia kile anachofanya mama huyo.
Dakika tatu mbele geti lilifunguliwa na kupata kuonekana kijana mmoja makamu ya Badu akiwa anaingia, moja kwa moja alinyoosha kuelekea ndani kwa mwenye nyumba. Na hapo ndipo alipojua sababu ya mama J kuchungulia dirishani na kuuacha wazi mlango wake. Kumbe alikuwa anamuingiza kijana huyo kijanja asipate kujulikana.

“Kaaah! Hii sasa kiboko huyu mama amehamisha uchafu wake ndani? Hapana hili silifumbii macho.”aliongea Jesca na kuepua sufuria yake ya mboga ilikuwa inachemka akaiweka pembeni.

Aliingia ndani haraka na kwenda kuchuka simu yake kisha akaongoza njia kuelekea kwenye mlango wa mwenye nyumba. Muda eote alikuwa akitazama kila chumba cha wapangaji hakuna ambaye aliyeweza kuona linaloendelea. Alifika pale na kuufungua mlango taratibu kisha akaingia ndani. Kitendo cha kuingiza tu mguu sauti za mahaba alipata kuzosikia pale mlangoni zikitoka chumbani. Alinyanyua simu yake na kuanza kurekodi video huju akitembea kwa kunyata kabisa asipate kusikika.
Mama J alikuwa chumba cha ziada ambacho kilikuwa kwaajili ya wageni tu wakija kuwatembelea. Huko ndio aliona kuna uhuru wa kufanya uchafu wake na kijana mdogo ambaye amemuingiza muda huo.
Kibaya zaidi walikuwa wanafanya kwa haraka tu hata kuufunga mlango wa chumba hicho walisahau kabisa. Nafasi hiyo ndio akaitumia Jesca kuanza kurekodi tukio hilo vizuri kabisa huku akibaki kusikitika tu.

Video ya dakika nne ilimtosha kabisa Jesca kuupata ushahidi ambao aliamini ataweza kuupeleka kwa mzee Chombo aliyemtuma kazi hiyo. Taratibu kama alivyoingia ndivyo aliweza kutoka hadi kurudi zake kwake akiwaacha wakiendelea kufanya mambo yao ndani.

“Huyu mama hatokuja kusikia salamu yangu tena, ni kujidhalilisha tu yaani vijana wadogo kabisa anawavulia chupi tena ndani kwake kabisa! Hana woga wala haya jamani wamama wengine kumbe akili zao fyatu eh!”aliongea kwa hisia kali Jesca akilaani kile anachofanya mama yule mtu mzima kabisa mwenye rika la mama yake. Alibandika tena sufuria yake jikoni na kuendelea kupika. Akanyanyua simu yake tena kuiangalia video ile, ni sauti tu za mahabu mama huyo anazotoa akiwa ameshikilia kitandani kijana akipeleka moto haswa bila kujali.
Jesca alibaki kutikisa kichwa tu kusikitika kwa yale anayoyaona.
Alitamani kumpigia simu mzee Chomo ili aje haraka kushuhudia uchafu wa mkewe ndani lakini aliona huenda akachelewa. Alitulia tu kusubiri kumuonesha video hiyo ili ajione mwenyewe. 

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!