UTAMU WA JAMILA (27)

SEHEMU YA 27

ILIPOISHIA
Alitoa shati jeupe la mikono mirefu lililokuwa na nembo ya hoteli moja mashuhuri pamoja na suruali nyeusi. Aliziweka sawa akijua kesho anarudi zake kazi baada ya muda mrefu kukaa nyumbani bila kazi.

TUENDELEE

Siku ilofuata mishale ya saa saba mchana Jesca alipata kupanga miadi ya kukutana na mzee Chombo. Alikuwa mwenye kujiamini sana mara baada ya kuwa na ile video ambao aliweza kumrekodi mama J akiwa ndani na kijana wa mtaani wakifanya yao.

Mzee Chombo alikuwa wa kwanza kufika sehemu husika akiwa na shauku ya kujua alichoitwa na mpangaji wake Jesca ambaye ndio muda huo alikuwa akitoka zake chumbani kwake kenda kutafuta bodaboda ya kumfikisha sehemu husika.
Mama J alikuwa anamchungulia kupitia dirisha lake la sebuleni kumuona Jesca akiyokomea. Aliachia sonyo baada ya kuanza kumhisi mwanamke huyo kuwa si mwema kwa upande wake.
Pia alishukuru kuona ameondoka hivyo atakaa kwa amani kwa muda huo.

Chumbani kwa baba Dulla mambo yalizidi kuwa moto. Tangu alivyopata taarifa ya mumewe kuweza kutembea na mama mwenye nyumba, mama Dulla hakutaka kabisa kuonesha dalili yeyote kama ameanza kumhisi mumewe. Alifanya kila kitu ambacho mumewe alikuwa akihitaji kufanyiwa lakini alipanga jambo lake moyoni.

Siku hiyo kama kawaida kwa mzee Chombo huwa anamfanyia vitu vya upendo mkewe ili walau abadilike. Siku hiyo alimtoa mkewe kumpeleka kwenye hoteli moja yenye hadhi yake. Walifika mapokezi na kuweza kuchukua chumba iki wapate kushinda wote siku hiyo pamoja. Baada ya kupewa funguo waliongozana na mhudumu mmoja wakielekea kwenye Lifti kupanda juu kwenda kwenye chumba husika.
Hata walipofika waliweza kukaribishwa na kuona jinsi chumba hicho kilivyokuwa kizuri kwa kupambwa.

“Waooh pazuri sana jamani.”aliongea mama J akiangaza macho yake huku na kule.

“Karibuni sana EPIX HOTEL, hapa mtapata kila kitu mnachohitahi ikiwa ni pamoja na chakula. Huduma ya choo na kila kitu kipo humu ndani kwa uhakika wa asilimia zote. Na kama mtahitaji chochote basi kuna simu ya mezani pale na maelekezo ya huduma unayotaka ili uletewe haraka.”aliongea yule mhudumu wa kiume akionesha tabasamu.

“Asante sana kijana, tumekuelewa.”aliongea Mzee Chombo.

“Basi sawa niwatakie mapumziko mema wazee wangu.”aliongea yule kijana kisha akaondoka zake.
Mzee Chombo alisogea mlangoni na kuufunga kwa ndani kisha akamgeukia mkewe. Alijisogeza mama J kwa mumewe na kuanza kumpa mabusu tele.

“Leo umenisuprise mumewangu na hata dikutegemea kama utafikiria kunileta hapa.”

“Usijali mkewangu. Yote haya nafanya kwakuwa nakupenda sana. Na nimekuleta hapa kwamaana kubwa sana.”

“Maana gani hiyo mumewangu?”aliuliza mama huyo na kumfanya mumewe ashushe pumzi kwanza kabla ya kusema, kisha akamkamata kiuno mkewe kwa mikono yake miwili.

“Haijalishi mangapi mabaya umeyafanya ukijua sitoyajua. Nasikiaga tu maneno ya watu kuhusu wewe mkewangu. Hivyo nimekuleta ili uyafikirie mabaya hayo kisha uyafute kabisa akilini mwako. Hebu achana na vishawishi vya kijinga ambavyo vinakuharibia jina lako mtaani na kwa watu wanaokuheshimu. Nimekuja hapa kukuomba ubadikike mama Jamila. Mimi nimekusamehe yote hayo ulonikosea. Tuanze kuwa wapya sasa mkewangu.”aliongea kwa upole mzee Chombo akiwa anamtazama usoni mkewe.

Maneno yake yalimfanya mama J aone aibu, alitazama chini ashindwe kuwa na ujasiri wa kumuangalia mumewe usoni. Mzee Chombo alinyanyua sura ya mkewe ili watazamane.
“Nataka nisikie kauli yako leo uniahidi kubadilika mkewangu.” alisema Mzee huyo kwa kujiamini sana.

“Baba Jamila, naona aibu hata kukuangalia. Naomba sana unisamehe mumewangu.”

“Wala usijali mkewangu mimi nimeshakusamehe, na ndio maana nimekuleta hapa ili tusahau ya nyuma. Pindi tunapotoka humu ndani tuwe wapya sasa.”

“Ni kweli nimekukosea sana mmewangu. Sijui nilimbwa na pepo gani hata sielewi. Ila kama kweli umenisamehe leo basi nakuahidi hutosikia tena maneno kutoka kwa watu kuwa nimefanya ujinga. Nakuahidi hili mumewangu.”alisema mama huyo akionesha huruma ilotawala usoni mwake.
Mzee Chombo alimvuta mkewe kumkumbatia wote wakionesha kuguswa na jambo hilo.
Mama J alijikuta anatokwa na machozi akifikiria yale alofanya. Ni jana tu ametoka kumuingiza kijana ndani kwake kabisa na kufanya naye mapenzi bila woga kabisa. Alitikisa kichwa tu baada ya kuona kweli amekuwa mkosaji sana.
Mzee Chombo alianza kushusha mikono yake na kushika makalio ya mkewe akianza kuyaminya kwa hamu huku akiyapapasa. Kitendi hicho kikamfanya mama J apeleke hisia mbali na zikapolekewa na vichocheo. Aligeuka kuanza kumpa mabusu tele mumewe na kujikuta wakiangukia kwenye huba zito.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!