SEHEMU YA 28
ILIPOISHIA
Kitendi hicho kikamfanya mama J apeleke hisia mbali na zikapolekewa na vichocheo. Aligeuka kuanza kumpa mabusu tele mumewe na kujikuta wakiangukia kwenye huba zito.
SONGA NAYO
Siku hiyo Jesca alipata kukutana na yule bwana wake ambaye alimkwepa siku moja na kumdanganya kuwa mama yake anaumwa. Walikaa na kupanga waende kupumzika kwenye hoteli moja wakiongea mambo yao.
“APEX HOTEL iko poa sana itakuwa vizuri tukaenda pale.”aliongea Jesca na kumfanya yule mwanaume atabasamu.
“We mjanja sana aisee, ulijuaje kama namimi nilitaka kukwambia twende hapo. Okay wacha tufikie hapo ” alisema mwanaume yule wote wakiwa kwenye tabasamu. Waliongozana pamoja wakiwa ndani ya gari la huyo mwanaume ambaye kidogo alikuwa mwenye uwezo wake. Walichagua kwenda kwenye hoteli hiyo ambayo hata mzee Chombo na mkewe mama J wapo humo pia.
Walipofika kwenye hoteli hiyo waliyochagua moja kwa moja waliingia na gari kulipaki sehemu husika. Kwa pamoja walishuka na kuanza kuongozana kuingia ndani. Walifika mapokezi pale na kukutana na mhudumu wakaanza kusalimiana.
“Tunahitaji chumba tafadhari.” Aliongea mwanaume huyo akiwa amemshika kiuno Jesca aliyekuwa anatafuna big G.
“Okay sawa.”alijibu yule mhudumu na kuanza kubofya keyboard ya computer kujaza taarifa za wateja hao. Kisha akampigia mhudumu mmoja aweze kufika hapo mara moja apate kuongozana na wateja hao kuwafikisha kwenye chumba walichohitaji.
Dakika kadhaa tu aliwasili mhudumu huyo.
” Wapeke hawa room namba 27 wakapumzike.”alisema yule mhudumu akimwelekeza mwenzake.
Jesca aligeuka kumtazama huyo ambaye anawaongoza, alishtuka kumuona ni Badu. Hata yeye mwenyewe alishangaa kumuona Jesca pale yupo na yule mwanaume akiwa amekamatia kiuno.
Hakutaka kuonesha utofauti wowote Badu aliachia tabasamu kwa wateja wake na kuongoza njia kwenda kwenye Lift. Jesca alibaki kushangaa tu huku akitembea na mtu wake, hakutegemea kama Badu ndipo anapofanyia kazi hapo.
Waliingia kwenye lifti wote watatu na kuanza kwenda juu hadi kwenye floo husika. Walitoka humo na kupiga hatua kwenda kwenye chumba namba 27 ambacho ndio wanafikia Jesca na yule mwanaume.
Badu aliwafungulia mlango kisha akawakaribisha.
“Karibuni sana EPEX HOTEL, hapa mtapata kila kitu mnachohitahi ikiwa ni pamoja na chakula. Huduma ya choo na kila kitu kipo humu ndani kwa uhakika wa asilimia zote. Na kama mtahitaji chochote basi kuna simu ya mezani pale na maelekezo ya huduma unayotaka ili uletewe haraka.”alisema Badu akiwa mwenye tabasamu kwa wateja wake.
“Asante sana. Kwanza ningependa kujua chakula gani kipo hapa.”alisema yule mwanaume akiwa anatazama kile chumba jinsi kilivyokuwa vizuri.
“Hapa kila chakula kipo bosi wangu. Ni wewe tu kutoa oda pale kwenye simu kuna kila namba ya sehemu unayotaka kupata huduma.”
“Ah safi sana, basi wacha tupumzike kidogo, kama namba zipo pale tutawapigia tukihitaji chakula.”
“Sawa bosi karibuni sana, dada karibu sana.”alisema Badu akimtazama Jesca aliyeachia tu tabasamu baada ya kusemeshwa na Badu kwa makusudi.
“Haya asante mwaya.”alisema Jesca na kumuona Badu akitoka zake.
” Oh sorry!”alisikika yule mwanaume na kumfanya Badu asimame, aligeuka kumsikiliza.
“Vipi zana mmeweka wapi?”aliuliza mwanaume yule akimaanisha condom.
“Bila shaka zipo pale pembeni ya taulo.”alisema Badu.
“Ahaa sawa shukrani.”aliongea mwanaume yule na kuufunga mlango wa chumba hicho.
Badu alibaki kutazama tu mlango ule huku akitabasamu.
“Dah leo Jesca analiwa kazini kwangu na mimi ndio nimewapokea! Noma sana hii hahaha.”aliongea Badu na kuamua kugeuka zake kuondoka. Aliingia kwenye lifti na kuanza kushuka chini, punde tu ujumbe ukiingia kwenye simu yake. Aliitoa mfukoni kuweza kusoma.
“Badu kumbe unafanya kazi hapa? Dah umenishtua hata sikutegemea kabisa.”ulikuwa ni ujumbe kutoka kwa Jesca akiwa mule chumbani. Naye ikabidi amjibu kwa kumtumia ujumbe wakawa wanachati.
” We hebu fanyeni huko kilichowaleta unachati na mimi wakati upo na mwanaume ndani humo!”
“Ah huyu si ndio yule aliyetaka twende Bagamoyo nikakwambia unitumie msg kuwa mama anaumwa! Leo kanibana inabidi nimridhishe.”
“Hahaha haya ngoja akunyooshe.”
“Ah wapi hana lolote huyu kimoja chali.”
“Mmmh!”
“Mi si ndio namjua, hapa kaenda bafuni kuoga akirudi anapiga kimoja analala.”
“Mh sasa kama hivyo yanini kuja kuchukua chumba kwenye hoteli kubwa hivi?”
“Huyu ni classic mtu na pesa zake. Wacha nimlie hela leo najua tu hatoniridhisha. Jioni nitakutafuta mpenzi wangu. Baadae naona anataka kutoka bafuni.”alituma ujumbe huo Jesca na kumfanya Badu asikitike tu huku akitabasamu.
Ni wazi Jesca anadanga! Kazi yake ni kujiuza tena kwa watu wenye pesa zao ili apate pesa za kuendeleza maisha yake. Ila kote anakoenda amezama kwenye penzi zito la Badu mpangaji mwenzake.
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU