UTAMU WA JAMILA (29)

UTAMU WA JAMILA 29

Upande wa pili Mwajuma siku hiyo aliamua kumpitia Mayasa ili kusudi amsindikize kwenda kumuona Roja. Alipanga kumfanyia suprise Roja kule kazini kwake. Maana yapata wiki na masiku kadhaa sasa hawaongei, moyo wake ulimkumbuka mwanaume huyo na kuona wacha akamsalimie.
Alipofika nyumbani kwa akina Mayasa hakuweza kumkuta mwenyewe zaidi ya kuambiwa na mama yake kuwa ametoka hapo tangia jana usiku akidai kwenda kwenye sherehe ya rafiki yake.
Ilibidi Mwajuma akubaliane na maelezo hayo kisha akaamua zake kuondoka mwenyewe huku akitabasamu tu kuhisi huenda Mayasa amemdanganya mama yake na kupitia kwa bwanake.

Alifika hadi pale gereji na kuweza kumuuliza Roja.
“Hayupo, tokea jana aliondoka hapa jioni hajaonekana tena.”aliongea kijana mmoja aliyechafuka ovaroli lake huku akijifuta oil mikononi.

“Na hajasema kuwa leo anakuja ama laa?”aliuliza Mwajuma.

“Mh sidhani kama anaweza kuja, hadi muda huu hajafika hiyo kesho tena.”alisema kijana yule.

“Haya poa nashkuru.”aligeuka zake Mwajuma baada ya kutambua Roja hakuweza kutokea siku hiyo. Aliamua kutafuta zake usafiri kuweza kurudi nyumbani, lakini moyo wake unakuwa mzito kukubali jambo hilo kirahisi. Alijikuta anaoatwa na hofu tu ya gafla.

“Mh au amepatwa na tatizo Roja mimi sijui. Mungu wangu mbina kama nakuwa na wasiwasi hivi leo! Hapana inabidi niende kumuona kwake.”alisema Mwajuma na kuamua kuelekea nyumbani kwa Roja aweze kujiridhisha kama yupo salama tu.

Huku hoteli baada ya kufaidi upendo wao mpya siku hiyo Mzee Chombo alinyanyuka kutoka kitansani akiwa amejifunika taulo. Alisogea hadi kwenye ile simu ya mezani kisha akakamata kitabu kidogo kilichopo palepale. Alisoma kwa aekunde kadaa na kuona namba mule zimeorodhesha, alichagua namba iloandikwa chakula kisha akapiga. Alitoa oda yeye na mkewe wakapata kuambiwa wanaletewa muda mfupi.

“Wacha nikaoge najua nikirejea chakula tayari.” alisema mama J akishuka zake kitandani akiwa mtupu.
Mumewe alimtazmaa na kuachia tu tabasamu huku moyoni akijisifu kwa kuchagua. Hakika mama J aliumbwa haswa ingawa umri umemtupa mkono lakini hakuonesha dalili zozote za kupoteza uzuri na umbo lake murua.
Mzee Chombo alichukua rimoti na kuwasha televisheni akawa anaangalia.

Msosi uliandaliwa na meneja akampa kazi Badu ya kuhudumia wateja hao kuhakikisha wanapata huduma mzuri. Alipatiwa chakula Badu kikiwa kwenye mahotpot na kupangwa na kikokoteni kidogo. Akawa anakisukuma kuelekea kwenye chumba ambacho amepewa kazi ya kuhudumia. Alipofika mlangoni alingonga mlango apate kufunguliwa, punde tu aliona ukifunguliwa huku akiwa mwenye tabasamu bashasha. Alishangaa kumuona mzee Chombo akifungua mlango ule wakawa wanatazamana.

“Hee Badu! Kumbe ndio unafanya kazi hapa?”alishangaa mzee huyo kumuona kijana wake.
Jina la Badu lilimshtua Mama J akiwa zake amekaa kitandani akichezea simu. Akawa anaangalia kile mlangoni ambapo mimewe amesimama.

“Mzee shikamoo, nipo hapa ndio napofanyia kazi mzee.”

“Marahaba aisee, kumbe ndipo unafanyia kazi hapa. Safi sana Badu, haya karibu, karibu lete chakula.”aliongea mzee huyo na kumpisha Badu aweze kuingiza kile kitololi kilichobeba chakula. Alishangaa kumuona mama J akiwa amekaa kitandani anamtazama.

“Oh Badu kumbe upo hapa?”alistaajabu Mama huyo akimuona Badu akiwa kwenye sare za kazi ndani ya hoteli hiyo.

“Ndio mama nipo hapa, shikamoo.”alisalimia Badu na kimuona mama yule akimtazama kisha akapotezea salamu ile bila kuijibu.

“Hongera mwaya. Leo tumekuja na babako hapa kupumzika. Na kama bahati leo unatuhudumia.”

“Wala usijali mama yangu nipo hapa kwa miaka mingi kidogo hivyo nitawahudumia mfurahie huduma zetu.”alisema Badu huku akitenga chakula kwenye meza iliyo pembeni.
Alikuwa mshapu sana kwenye kazi yake na dakika chache alimaliza kila kitu na kuwakaribisha wapate kula wateja wake.

“Haya miye wacha niwaache niendelee na kazi zengine.”

“Sio ungekuja na wewe kupata chakula hapa!”aliongea mzee Chombo akiwa ananawishwa mikono na mkewe.

“Hahaha hapana mzee hapa nipo kazini, ondoa shaka kabisa.”

“Haya kijana wangu, kazi njema.”

“Haya mzee baadae.”alisema Badu na kumuona mama J akimtazama. Alimkonyeza huku akiendelea kumnawisha mumewe, Badu alitabasamu tu na kugeuka kuondoka zake.

“Yaani nyumba yote ipo hapa, na sijui kama wanajua kama Jesca naye yumo humu. Ah kazi kwelikweli.”aliojisemea Badu akielekea zake kwenye lifti kushuka chini akiwa na kitololi chake.
ITAENDELEA

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!