SEHEMU YA 30
Baada ya muda Mwajuma aliweka kufika karibu na chumba cha Roja. Alimlipa bodaboda ili apate kuanza kusogea kwenye chumba hicho. Sauti za watu ndani wakichombezana zilisikia huku muziki ukipoza sauti hizo kuweza kusikika vizuri. Mwajuma alipata tahaluki baada ya kusikia hivyo na kujua ndani kuna mwanamke. Ilimbidi asogee karibu kabisa na dirisha kuwexa kusikiliza sauti hizo. Hawakuwa wenye kuongea mazungumzo zaidi ya kutekenyana tu huku mwanamke akisikika kutoa mideko. Dakika chache mbele muziki uliongezea sauti kidogo na kusikika mwanamke akilalama kwa sauti za mahaba. Mwajuma aliumia moyo tu pale nje baada ya kujua Roja ameingiza mwanamke ndani.
Alisikia tu mwanamke huyo akimtaja Roja kwa vile anavyomfanya, akimsifia kwa ufundi wake kitandani. Sauti hizo zilimkera Mwajuma kutaka kugonga mlango lakini alisita baada ya kujua yeye na Roja wamechuniana. Alijikuta anakunja ngumi kwa hasira tu, hakutaka kuendelea kukaa tena hapo aligeuka na kuondoka zake.
Njiani alijikuta anajilaumu tu mwenyewe kwa kujipeleka kwa Roja na kujionea mambo ambayo muda huyo yanamuumiza moyo. Alijuta kwanini alienda kwake, lakini upande wa pili aliona bora amepata kujua ukweli kuwa Roja anamwanamke mwengine. Alinyanyua simu yake na kuweza kumpigia shoga yake Mayasa, simu ikikuwa inaita tu bila kupokelewa.
Alikata na kuiweka simu yake kwenye mkoba akiwa amenuna sana, aliamua kurudi zake tu nyumbani apate kutuliza akili.
Roja alikuwa anaendelea kupeleka moto kwa Mayasa. Mwanamke ambaye alijitoa kimasomaso kumgeuka rafiki yake Mwajuma iki tu apate kuliteka penzi la Roja. Na uthubutu wake ulifanikiwa baada ya kujirahisisha kwa Roja na kumjali zaidi hadi kuamua kulala kwake usiku wa jana
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU