UTAMU WA JAMILA (32)

UTAMU WA JAMILA 32

Mama J alibaki pale ameinamisha kichwa tu akitafakari kile kitendo ambacho alikuwa anataka kukifanya. Mazoea yalimlevya na kujikuta kuwa aliletwa na mumewe kwaajili ya kuanza maisha mapya na kuachana na tabia ambazo si rafiki kwa rika lake na utu wake. Kwa zoezi hilo alijitahidi kumshinda shetani aliyekuwa anataka kumtawala tena. Baada ya muda alirejea mumewe wakaendelea kula raha ndani ya hoteli hiyo.

Hata kuanza kuingia jioni Roja ndio alipata kumuachia Mayasa aweze kurejea kwao. Alimsindikiza lengo ni kuhakikisha anapata usafiri wa kumfikisha mwanamke huyo kwako bila wasiwasi.

“Roja.”aliita Mayasa wakiwa wanatembea jioni hiyo.

” Naam..”

“Hivi hadi sasa bado unampenda Mwajuma tu? Pamoja na yote aliyokufanyia kutokukujali hadi siku ya leo.”alisema Mayasa akilala.

” Maya, hebu achana na hayo mambo yatakupa presha bure. Wewe shida iko wapi sasavi kama kukupa kila kitu nakupa na mapenzi unainjoy. Sasa tatizo lako lipo wapi mpenzi, asiyekuwepo na lake halipo.”alisema Roja akimpa moyo Mayasa. Na kwa kauli yake ua mwisho ya Roja ikamtia ufahari wa kujihisi yeye ndio mwanake halali kwa Roja.

“Mimi nakuhakikishia nitakupenda hadi pumzi yangu ya mwisho. Sitokubali Mwajuma akuchukue tena. Nakupenda Roja.”

“Usijali Mayasa. Nami nakupenda sana.”alisema Roja na kuendelea kutembea. Walifika mbele kidogo wakasimamisha bodaboda. Mwayasa alipanda na kuanza safari ya kurejea kwao huku Roja naye akirudi kwake.

“Namsahau Mwajuma sasahivi! Maana huyu demu amekuja na moto na hata hajali kuhusu rafiki yake. Sijui siku akijua Mwaju itakuwaje aisee.” aliongea Roja akitafakari swala hilo. Aliona wazi Mayasa ameshajihalalishia kabisa kuwa naye.

Hadi kufika saa mbili usiku mama J pamoja na mumewe waliweza kurejea zao nyumbani mara baada ya kushinda kutwa nzima hotelini. Walifika na kukuta Mwajuma ndio anataka kupika chqkula. Walimuamuru apike kiasi chake tu maana wao wameshakula huko walipotoka.

“Mnaroho mbaya nyie mmeniacha hapa mmeenda kula makuku huko na machipsi mnatudi kunidolishia. Sawa bwana ngoja nisonge ugali wangu.”aliongea Mwajuma huku akipunguza maji ya ugali aliyoanza kuyabandika jikoni.
Mzee Chombo aliachia tu tabasamu na kuelekea zake chumbani.

“Wala hatujala hayo makuku mwanangu, tumeshiba wali tu usije kupasuka kwa kudhani tumekula hayo manyama.”aliongea mama J akiwa anavua viatu vyake.

“Haya bwana.”

“Vipi hakuna mtu yeyote aliyekuja kuniulizia?”aliuliza mama J.

“Mh hapana sijaona mtu hapa kuja. Ila amekuja yule mpangaji wa chumba cha tatu amenipa ela yake ya kodi nimekuwekea kwenye kabati lako.

“Na bora ameileta mwenyewe maana nilitaka nimfuate usiku huu. Haya siye twaingia kulala tena kesho.”aliongea mama huyo.

“Haya usiku mwema kwenu ” aliaga Mwajuma na kushuhudia mama yake akiingia zake chumbani.

“Yesss! Leo nipo free sasa, ngoja nimalize kupika nile niende kupewa raha na Badu.”aliongea Mwajuma akiwa mwenye uchangamfu wa hali ya juu.

Baada ya muda kupita Badu aliwweza kurejea kutoka kazini huku akiwa amebeba mfuko wa chakula kutoka kazini kwao. Kwa uchovu wa kuzunguka siku hiyo aliamua kwenda kuoga mapema kabisa, aliwasha sabufa lake na kuweka muziki kisha akaelekea zake bafuni.
Mwajuma alipata kusikia kelele zile na kutambua tayari Badu amerejea. Alinyanyua simu yake na kumtumia ujumbe mwanaume huyo kisha akaiweka simu kwenye kochi. Aliachia tabasamu muda huo akiwa ndio anatoa zake vyombo baada ya kumaliza kula. Aliviweka sehemu husika kisha akaelekea zake chumbani kwake, akawa amesimama tu akiangalia kabati lake.

“Leo nimvalie nini sijui cha tofauti!”alijisemea mwenyewe Mwaju akiwa mwenye kutafakari.
Ilimbidi asogee mpaka pale na kuangalia nguo ya kuvaa. Alikuja kutabasamu baada ya kukamata bikini nyekundu akiwa na sidiria yake. Aliona ndio nzuri hizo kuvaa kwa usiku huo.

Badu aliweza kurejea zake chumbani akiwa amechangamka. Alijifuta maji kwa taulo kisha akatulia kwenye kochi akiinyanyua simu yake. Alipata kuona ujumbe umeingia kutoka kwa Mwajuma ikbidi ausome.
“Ndo natoka ndani hapa, zima taa ya hapo nje na uache mlango wazi.”ulikuwa ni ujumbe wa Mwaju akimtumia Badu.
Alitabasamu tu mwenye na kukumbuka kumbe muda ule akiwa kazini Mwajuma alimpigia simu kutaka waonane. Akajua lengo la Mwajuma ni kutaka kupata ile kitu roho inapenda.
ITAENDELEA 

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!