SEHEMU YA 35
Hadi kufika saa nane usiku Mwajuma alitosheka na kile alichokuwa anakihitaji kutoka kwa Badu.
“Hapa Badu inatosha sitaki tena kuongezewa raha maana nitapitiliza kujikuta nalala kabisa humo asubuhi iwe aibu kuonekana nikitoka humu.”alisema Mwajuma na kumfanya Badu acheke. Alimpiga busu kwenye chuchu na kumfanya Mwajuma atabasamu.
“Haya my, nenda ukapumzike sasa nami wacha nikaoge nilale.”
“Haya Badu. Nakupenda sana we mwanaume.”
“Nakupenda Mwaju.”alisema Badu na kuweza kuagana na Mwajuma. Alinyanyuka na kufungua mlango huku akiwa makini kutazama nje kukiwa shwari. Alitoka mule na moja kwa moja akaingiabzake kwao bila yeyote kujua.
Badu alichungulia na kuhakikisha Mwajuma ameingia ndani kwao, alishusha pumzi sasa baada ya kujua ana ahadi na Jesca aliyemwambia amsubirie. Alipumzika dakika kadhaa kisha akatoka nje akitazama mlango wa mwenye nyumba asije Mwajuma kutoka tena. Alifika kwenye mlango wa Jesca alishangaa kusikia kelel za chinichini ndani ya chumba. Alipotega sikio vema alipata kutambua Jesca ameingiza mwanaume ndani na ni wazi wapo wanajivinjari muda huo.
“Huyu malaya kaamua anikomoe! Dah haya sio kesi hata hivyo sina hamu ya uchi tena.”aliongea Badu baada ya kuona amefeli kuonana na Jesca usiku huo. Aliingia kwake kuchukua maji kwenda kuoga kisha akarejea kulala.
Alfajiri ya saa 11 mzee Chombo alitoka kuelekea zake bafuni kuoga. Alipotaka kutoka tu alipata kushuhudia baba Dulla akitoka chumbani kwa Jesca aondoke zake kurudi kwanza kazini kwake apate kuvuta muda ili kupambazuke arudi kwake bila kujulikana. Jambo hilo lilimshangaza mzee Chombo ambaye alikuwa anatazama tu hadi alipotokomea mpangaji huyo.
Alibaki kusikitika tu baada ya kuona kumbe kuna mambo makubwa yanayoendelea ndani ya nyumba yake hiyo. Alifungua mlango na kuelekea zake bafuni kuoga.
Hadi kufika saa sita za mchana Roja alikuwa amepumzika baada ya kumaliza kazi yake. Alitulia sehemu akiwa anajifuta oil kwenye mikono. Alinyanyua simu yake kumpigia Mayasa ambaye alipokea muda mfupi tu baada ya kupigiwa.
“Oya vipi tayari?”
“Ndio namalizia kusoga ugali haya mpenzi wangu nitakushtua nikimalizia.”
“Haya mi nishamaliza kazi ndio najiandaa kurudi hapa.”
“Sawa my we njoo tu nitakuwa nishamaliza kupika.”
“Sawa.”alisema Roja na kukata simu yake. Alitabasamu huku akinyanyuka kwenda kunawa apate kirudi kwake ambako amemuacha Mayasa ampikie mchana.
Muda huo Mwajuma alikuwa anawasili nyumbani kwa akina Mayasa shoga yake. Alimkuta mama yake amepumzika zake sebuleni akiangalia televisheni. Alimsalimia mama huyo na kukaribishwa akapata kukaa.
“Hivi sikuhizi mnanifanyia kusudi nyie watoto eh!”alihoji mama huyo na kumfanya Mwajuma ageuke kumtazama huku akitabasamu.
“Kwanini mama?”
“Sasa mwenzako kaja kwako asubuhi anasema unaenda kumsuka. Saivi unakuja wewe mwenyewe hapa au ndio kapata giya ametoka kwako kapitia kuzulula huko.”alisema mama na kumshangaza Mwajuma kwa maneno yake hayo.
Alibaki kuonesha tabasamu tu Mwajuma huku moyoni akitafakari maneno ya mama huyo.
“Haya nyiye jifanyeni wajanja tu.”alisema mama huyo akiendelea zake kuangalia runinga.
“Nipo ndani mara moja mama.”
“Haya mwanangu.”
Mwajuma alinyanyuka na kuelekea chumbani kwa Mayasa akapata kukaa kitandani akiwa mwenye kutafakari sana.
“Hivi huyu kwanini ananificha sikuhizi? Yaani kwao anaaga kuja kwangu kumbe anadanganya, sasa kwanini haniambii?”alibaki kulitafakari hilo na kuamua kumpigia simu kwanza apate kumueleza ukweli shoga yake kwa tabia yake. Simu ilipata kuita tu bila kupokelewa hadi akaamua kuacha Mwajuma.
Alishindwa kuelewa kabisa, aliamua kuweka simu yake pembeni na kuamua
kujilaza kwa muda kutafakari. Kitendo cha kujilaza pale alihisi amelalia nguo, alipeleka mkono kuweza kuitoa huku akiitazama.
“Haaa! Hii nguo si ya Roja? Na imefikaje humu chumbani?”alishangazwa Mwajuma kwa kile anachokiona. Alijikuta anakuwa na wasiwasi juu ya jambo hilo. Haraka akainuka pale kitandani akianza kuvuta matukio mawili ya Mayasa. kutopokea simu akiwa hayupo kwao. Alivuta kumbukumbu siku ile akiwa na ambayo alimkatia simu Roja mbele ya Mayasa, na ndio muda ambao shogayake huyo aliaga kuondoka. Ajabu kesho yake Mwajuma anakuja kwa akina Mayasa na kuambiwa hajarudi tangu jana na amedanganya kuwa yupo kwao.
“Hapana hapa kuna mchezo unaendelea sio bure.”aliongea Mwajuma haraka akatoka zake mule chumbani kutaka kuondoka.
“Mama nitakuja baadae kuna sehemu nawahi mara moja.”
“Hee mbona gafla mwanangu?”aliuliza mama huyo bila kujibiwa alipata kumuona Mwajuma anafungua mlango kuondoka zake.
Njiani alianza kuhisi kuvurugwa Mwajuma akiwa kwenye bodaboda, alitamani wafike haraka akapate kuona kile ambacho anakihisi muda huo.
Huku upande wa pili Roja alifika kwake na kumkuta Mayasa ameshapika chakula anamsubiri yeye.
“Dah unatumia fursa we mwanamke sio siri.”alisema Roja akivua nguo kuvaa taulo.
“Yaani nahakikisha nampiku mwenye mali yake, na siku atakapojua sijui itakuwaje.”alisema Mayasa akinyanyuka kwenda kuchota maji kuyaweka kwenye ndoo ili Roja akaoge.
“Aisee na alivyo mkali kwa maneno Mwajuma.”
“Ah atajua mwenyewe bwana, kama amekuchunia sisi tunamsaidia. Ngoja nikupelekee maji bafuni mumewangu. Au wataka tuoge wote?”aliongea Mayasa kwa sauti ya ushawishi akimtazama Roja.
“Mh hapana my ntaoga mwenyewe. Najua tukioga wote hutaniacha salama huko bafuni.”aliongea Roja na kusikia kicheko kikitoka kwa Mayasa.
“Haya bwana kaoge uje ule, tupeane tena. Hapa kurudi nyumbani hadi jioni.”
“Hilo usijali kipenzi. Narudi unipe ile tamu yangu.”aliongea Roja akachukua ile ndoo ya maji kuelekea zake bafuni.
Siku hiyo Jesca katika mihangaiko yake alipata kuonana na mzee Chombo. Alikuwa na shauku kubwa sana ya kumpata mzee huyo na ni kwasababu ya ile kazi alompa.
Walitafuta sehemu wakakaa ili wapate kuongea.
“Mimi sio mkaaji sana mzee Chombo, ile kazi uliyonipa nimeikamilisha na nimefanikiwa kupata ushahidi. Sitaki niseme mengi uangalie mwenyewe kwa makini kisha utapata kuchukua maamuzi.”aliongea Jesca akimpatia mzee huyo simu yake kisha akamuonesha ile video aliyomrekodi mama J akiliwa uroda ndani kwake na kijana wa mtaani hapo.
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU