UTAMU WA JAMILA (37)

SEHEMU YA 37

Kelele zilizagaa hapo hadi kuwafanya baafhi ya majirani watoke makwao kuja karibu ba chumba hicho kujua kimetokea nini.
Mwajuma alikuwa na hasira sana na Mayasa kwa kuona amejirahisisha kwa bwana wa mwenzake. Hata Mayasa naye hakuwa haba kwenye kujitetea, alijaribu maye kurusha makofi kadhaa hata kumvua wigi mwenzake aliyekuwa amesuka mabutu kichwani.
Mwisho wa siku Roja alifanikiwa kumtoa Mwajuma nje ambaye hakutaka tena kukaa eneo hilo anaondoka zake. Watu walijaa nje wakishangaa tu wasipate kujua ukweli, waliamua kusambaratika na baada ya muda hali ikawa shwari nje.
“Yule fala kumbe hanijui eh. Nitampasua yule demu wako!”alipaza sauti Mayasa baada ya kushambuliwa sana na Mwajua hadi kuchanika kidogo usoni kwa kucha za Mwajuma.
“Basi my yameshaisha “
“Wee koma, hayajaisha yaani ndio kwanza amechokoza huu mziki. We subiri ataona.”
“Sasa yanini ugomvi. Hivi hata ungekuwa wewe ndio Mwajuma halafau umuone mwenzio amepitia njia ulizopita wewe kunipata mimi si lazima atakuwa na hasira kama hizi.”
“Kwahiyo unamtetea yule malaya! Niache!”
“Hapana, Mayasa hebu acha hasira basi.”alimshika mkono mwanamje huyo aliyetaka kuondoka.
“Hebu nisikilize mimi kwanza Mayasa. Hivi unamjua Mwajuma alivyo jambo lake akiliamua harudi nyuma. Hapa ndio mwisho wa mahusiano yangu mimi na yeye. Hivyo hii ndio nafasi ya wewe kuwa na mimi kwa uhuru Mayasa, hujaliwazia hilo kabisa mpenzi! Hebu tulia sasa hii ilikuwa kama unatetea penzi lako, umeshapata ulichotaka sasa hupaswi kuwa na hasira naye tena. Tulia mpenzi wangum” alisema Roja na kumtuliza Mayasa.
Maneno yake yalikuwa kama dawa kwa Mayasa akapata kupoa hasira zake. Ilibidi Roja atoke hapo kwenda dukani kuchukua plasta na kurejea kumfunika Mayasa pale alipochanika. Walibaki wanafarijiana kwa kile ambacho kimetokea.

Kwa Mwajuma jambo lile lilimkera sana. Hakuwa na wivu juu ya Roja kabisa ila kitendo cha Mayasa kumdanganya kuwa na ushoga naye kumbe wanachangia bwana hicho ndio kilimfanya ajione amedharaulika sana.
“Huyu subiri nitamfanyia tukio ambalo hatalisahau maishani mwake.”aliongea Mwajuma moyoni mwake akidhamiria kumfanyia kitu Mayasa.
Alinyanyua simu kumtumia ujumbe Badu kisha akaongoza njia kuelekea zake kwao. Alishika kichwa chake na jubaki kusonya tu kuona wigi lake halipo na huenda muda ule akiwa anarumbana na Mayasa.

Siku hiyo mama Dula akiamua kufanya uchunguzi juu ya mumewe. Mchana wa siku hiyo alimuacha mumewe akiwa amelala ndani akijua anaingia shifti ya usiku kama kawaida yake. Aliobgoza njia hadi kufika eneo analofanyia kqzi mumewe na kumkuta mwenzake mmoja ndio aliyekuwa zamu ya mchana.
“Oh shemu karibu bwana.” alisalimia yule mwanaume akiwa kwenye mavazi ya ulinzi.
“Asante shemu naona upo kwenye majukumu.”
“Ndio hivyo shemeji si unajua mwanaume hasifiwi kula.”
“Ni kweli kabisa, kazi iendelee.”aliongea mama Dula na kumfanya shemeji yake huyo afurahi.
“Haya nambie shemeji yangu naona leo umenikumbuka kuja kunisalimia.”
“Ah mara moja moja bwsna nikikuwa napita naelekea hivi juu nikasema nipite kukupa hai shemeji yangu. We si hutaki kuja kutuona.”
“Ah usijali shemeji, hata hivyo nikipanga ndani ya wiki hii nije ila saivi naingia usiku toka juzi hivyo kuondoka hapa hadi mwenzangu akija. Hivyo nakuwa nimechoka sana nikirudi nalala tu.”alisema mwanaume huyo na kumfanya mama Dula afahamu jambo.

“Oh nilisahai aisee kumbe tangu juzi unaingia usiku?”

“Ndio, si ndio maana saivi unajidai jamaa anarudi mapema mnalala wote na baridi hili sasa ah!”alisema yule mwanaume na kumfanya Mama Dula atambue kumbe mumewe siku hizi hurudi mapema jioni.

“Kawaida tu shemeji.”

“Haya bwana siye tupo.”

“Basi sawa shemeji wacha nikuache. Siku njema.”

“Haya mama watoto.”

Mama Dula aliondoka zake bila kutazama nyuma tena.

Alipatwa na jazba sana baada ya kuujua ukweli ambao hakuwa anafahamu hapo awali.
“Huyu mwanaume jana alilala wapi hadi kunirudia alfajiri najua mtu katoka kazini? Ngoja atanikoma leo hadi nijue alipokiwa jana.”alisema mama Dula akiwa anakazana mwendo kurejea zake kwake.

Mzee Chombo aliwasili kwake, alimkuta mkewe akiwa anapiga muda huo na alipomuona mumewe alinyanyuka kumkaribisha na kupokea kifurushi alichoshika mkononi akaenda kukiweka. Mzee Chombo alienda sebuleni kukaa kwanza akitafakari jambo ambalo limemuingia moyoni mara baada ya kuona ile video ya ngono alilofanya mkewe. Alifkiria kuwa tayari wameshasameheana na mkewe na kuamua kuanza maisha mapya. Lakini kuna hasira bado anazo nabni kutokana na ile video aliyooneshwa. Aliitoa simu yake na kuamua kuwasha data kwanza kuangalia kilichojiri mitandaoni walau apoteze mawazo hayo.
Zilianza kuingia meseji kwenye whatsapp na kupata kuona Jesca akiwa amemtumia ile video. Alibaki kuitazama tubasiifungue video ile kuona huenda ikazidi kumtia hasira akachukua maamuzi yasokuwa ya heri.
Alifika mama J pale na kumoiga busu mumewe huyo aliyeanza kutengeneza tabasamu.

“Haya vipi huko ulipotoka?”

“Ah safi tu nimerudi mapema nipate kupumzika kichwa kinagonga.”

“Oh pole mumewangu, ni jua hilo inakupasa unywe dawa upumzike kwanza. Mimi naivisha chakula nikuandalie ule.”

“Sawa wacha niingie chumbani.”

“Haya mumewangu.”alisema mama J na mumewe akainuka pale alipo akaelekea zake chumbani.

ITAENDELEA 

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!