SEHEMU YA 38
ILIPOISHIA
“Haya mumewangu.”alisema mama J na mumewe akainuka pale alipo akaelekea zake chumbani.
SONGA NAYO
Mama Dula alifika kwake moja kwa moja akaingia chumbani ambako alimkuta mumewe amelala bado, kwa hasira alizonazo alichota maji kwenye jagi na kumwagia mumewe ambaye alikurupuka pale kitandani.
“Wewe vipi unakichaa?”aliongea kwa jazba na kuonekana mwenye hasira.
“Wewe ndo mwenye kichaa, unajifanya unausingizi hapa ulilala wapi jana? Na sio jana tu ulilala wapi siku hizi mbili?”aliuliza mama Dula akiwa ameshika jagi.
“Unaniuliza nililala wapi kwani hujui kazi yangu? Na tangu lini unaniuliza maswali hayo?”
“Kazi yako? We unakazi ngapi unazofanya labda tuanzie hapo. Kama ni ulinzi ninayoijua mimi basi leo utanieleza ulipolala siku hizi mbili.”aliongea mama Dula akionekana kufura kwa hasisa.
Mwanaume alimtazama mkewe na kutambua kuna jambo amefahamu mkewe na huenda akajiingiza kwenye matatizo endapo hatakuwa makini.
“Nilikuwa kazini jana.”
“Kazi gani hiyo mbona unakuwa muongo wewe! Hapa nimetoka kazini kwenu nimemkuta mwenzio nikamuuliza. Amenieleza kila kitu na sikutaka ajue kabisa.”alisema mama huyo akimfanya mumewe apoe, alibaki kupangusa maji yalokuwa yanatiririka usoni.
“Mwanahizaya mkubwa wewe kumbe ndio unavyofanyaga hivi siku zote. Nakaa na wenzangu wananikanya niwe makini na wewe, mimi najitetea kuwa huna uhuni huo kumbe ndio walewale. Hapana siwezi vumilia hili, huenda umeshazoea sana kosa langu ni kukuamini na kukupa uhuru wa kutokukufuatilia, hapana siwezi naenda kwetu.”aliongea mama huyo na mwishowe machozi yakaanza kumtoka.
“Aaah mkewangu usifanye hivyo, naomba tukae kwanza tuongee unisikilize.”
“Niache! Usinishike.”alipandisha hasira mama huyo akielekea kwenye kabati na kuanza kuchukua nguo zake kuweka kwenye begi.
Baba Dula alikuwa na kazi ya kuomba samahani hadi kwa kupiga magoti lakini hakuweza kusikilizwa.
Mwanamke alinyanyua begi lake na kutoka huku baba Dula akijitahidi kumzuia kwa kumshika mkono. Mama Dula alitumia hadi meno kung’ata ili apate kuachiwa. Kwa hilo alifanikiwa baada ya mumewe kuugulia maumivu akafungua mlango kuondoka kabisa.
Alibaki ndani anautazama mkono wake ukiwa unatokwa na damu, haraka alienda kujisafisha na kukifunga kidonda hicho.
“Dah nimefanya makosa kweli yani hadi waifu kajua, kesi hiyo tena kwa wakwe.”alisema baba Dula akiwa ameegamia kochi akitafakari ukubwa wa jambo hilo.
“Sijui shetani gani amenifanya jana nisifike chumbani kwangu niishie kwa yule mtoto malaya, najuta miye aibu hii.”alijisemea baba huyo akijutia kile alichofanya jana kwa Jesca.
Baada ya masa kadhaa kupita Jesca alifanikiwa kufika kwenye hoteli ambayo Badu anafanya kazi hapo. Alichukua chumba siku hiyo na alipata mtu wa kumhudumia tofauti kabisa na Badu. Alipewa maelekezo na mhudumu yule namna ya kupata huduma yeyote anayoitaka.
“Samahani kama nitakuwa nimekusea, kuna mhudumu aliwahi kunihudumia hapa kuna kipindi, anaitwa Badu sijui unamfahamu!”
“Ndio namfahamu.”
“Yupo kazini leo?”
“Yeah yupo ndio.”
“Ahaa sawa, nashkuru unaweza kwenda.” alisema Jesca akiwa mwenye tabasamu zito.
Yuke mhudumu alipotoka tu Jesca alielekea kwenye ile simu pale na kuweza kuangalia kitabu cha namba pale pembeni. Alishusha kidole hadi kwenye namba iliyoandokwa MENEJA. Akaanza kuzikopi zile namba kisha akapiga simu muda huohuo ikapokelewa.
“Hallow habari mpendwa.”ilisikika sauti ya meneja akiongea kwa unyenyekevu.
“Salama tu Meneja, nilikuwa ninaombi moja kama itawezekana.”
“Sawa hakuna shida nakusikiliza.”
“Asante, nilikuja juzi hapa na nikiweza kuhudumiwa vizuri na kijana mmoja niyemfahamu kwa jina la Badu. Natamani sana leo anihudumie, aniandalie chakula siku ya leo, nitafurahi kama nitasikilizwa.”alisema Jesca akiwa anavua viatu vyake.
“Ahaa sawa hilo halina tatizo kabisa. Nitamuagiza aweze kukuhudumia. Kuwa na amani kabisa. Nipate tu oda yako ya chakula.”
“Asante.”alisema Jesca na kuagiza chakula anachotaka kisha akakata simu baada ya kuhakikishiwa hilo. Aliinuka sasa na kuvua nguo zake kisha akaelekea zake bafuni kujimwagia.
Baada ya muda kupita Badu alipata kuelekea kwa Meneja wake ambaye alikuwa akimsubiria.
“Okay Badu, kuna mteja ametaka umhudumie wewe leo. Amepiga simu hapa anahitaji chakula umpelekee chipsi kuku na juisi ya embe. Naomba umoatie huduma bora na umuoneshe uaminifu kama alivyokuamini wewe. Yupo chumba namba 39 nenda jikoni kachukue msosi umpelekee.”alisema Meneja huyo na muda huohuo simu yake ikaita. Ilibidi apokee haraka huku akimuoneshea Badu mkono wa kwenda alikomtuma, aligeuka Badu na kuondoka zake.
“Mh nani huyo amepiga simu kwa Meneja kutaka nimhudumie mimi?”alijiuliza Badu asipate kujua.
Ilibidi afanya kama alivyoambiwa, alielekea jikoni na kuchukua chakula hicho moja kwa moja kwenye lifti ilomfikisha kwenye floo yenye vyumba hivyo. Akaanza kutembea hadi kufika kwenye mlango wa chumba namba 39, alibisha hodi na kusikia sauti ya kike ikimuamuru kuingia ndani. Alifungua mlango na kuingia na kitololi cha chakula, alipotazama mbele alipata kumuona Jesca akiwa kwenye vazi la chupi tu huku chuchu zake zikiwa wazi sura ilojaa tabasamu ikimtazama Badu. Alibaki kushangaa tu kumuona Jesca ndiye aliyekuwa mteja, ndio mtu aliyetaka ahudumiwe na Badu siku hiyo.
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU