UTAMU WA JAMILA (39)

UTAMU WA JAMILA 39

“Karibu kipenzi changu.” alisema Jesca na kusogea kwenye mlango akapata kuufunga kabisa kwa funguo.

“Jesca unataka kufanya nini? Inamaana hujui nipo kazini hapa?”

“Nafahamu sana, na ndio maana nimekuja hapa kazini kwako ili unihudumie.” Maneno hayo yamlichosha Badu na kuona ilikuwa ni janja tu ya Jesca kuja hapo hotelini.

“Yaani Jesca mechukua chumba hapa kwaajili ya uchafu unaotaka kufanya?”

“Uchafu unaujua wewe ila kwangu ndio starehe. Nimekufuata wewe maana umenichanganya kwa kauli zako ulizoniambia. Hivi Badu unamiona mimi malaya sana eh! Kukupa uchi wangu uuchezee ndio unanifanya kama usukani unanizungusha utakavyo. Kwanini lakini unanifanyia hivi?”

“Nisikilize kwa makini Jesca, tambua kwamba mimi na wewe sio wapenzi. Hilo ukilijua tu basi hiyo roho yako ya wivu utaiacha. Mimi na wewe tumekutana, tumetamaniana, tumepeana na kunasaidia tu na sio kuwa ndio tunadumu kila siku. Unapokuwa na hamu zako mimi ndio nakumaliza namimi hivyohivyo. Wewe una mabwana sijui bwana wako na mimi ninampenzi wangu. Hivyo ifike mahala tusitishe hii vita maana naona mwenzangu umenipania kuniua sasa.” alisema Badu na kumfanya Jesca atabasamu.

“Haijalishi unampenzi au wapenzi. Mimi nachotaka kwako ni kunirizisha tu. Usione jana nimefanywa na leo nataka kwako, ninataka kurizishwa nadhani umeshapata jibu kama mtu mzima.”aliongea Jesca akiwa anajiamini sana.

“Jesca, natembea na Mwajuma. Yule binti wa mzee Chombo.”aliamua kuanika wazi Badu mahusiano hayo baada ya kuona sasa anapoelekea Jesca ni kwenda kummiliki Badu.
Kauli ile ilimshtua mrembo huyo akabaki ameshikwa na butwaa.

“Mwajuma ndio mpenzi wangu, na ndio nilikuwa naye jana usiku kucha. Hadi nakwambia sina hamu ni yeye ndiye amenifanya hivyo. Kwahiyo nimeona nikwambie tu ukweli ujue mapema ili hata siku ukinikuta naye ulijue hilo.”

“Yaani Badu ndio umeamua kunidanganya! Siku ile nilikuwa ninamashaka na ukaribu wenu kumbe ni kweli nilikuwa sahihi!”

“Sikutaka ujue mapema maana ndio kipindi kile ulikuwa unakuja moto kwangu. Lakini nimeona hili litaniweka sehemu mbaya hapo baadae, bora wewe ujue najua ni muelewa.”alisema Badu na kushuhudia kofi zito likitua shavuni kwake.

“Badu wewe ni malaya, kauli zako tu zinaonesha umeyazoea haya mambo.”

“Sawa mimi malaya ila wewe umenizidi vyeo vitatu. Kwahiyo wewe ni mkubwa wangu kwenye fani hiyo.”alisema Badu na kumfanya Jesca acheke tu maana yanayoongelewa hapo yamemgusa. Hata Badu mwenyewe aliamua kicheka, maneno yake yanaukweli ndani yake na alikuwa anajua mapema kuwa Jesca ni mdangaji ila naye akajiweka ili tu kumfaidi dada huyo.
Jesca alimkamata shati Badu na kumvutia kitandani.

“Haijalishi Mwajuma ni nani kwako ila nitakufuata popote pale unikune. Umeshaniharibu Badu haipiti siku mbili bila kunifanya wewe sijisikii kabisa hata nifanywe na wanaume 20. Kwahiyo usifikirie kuniambia kuwa upo na yule msichana ukadhani utaniumiza nikuache. Wewe na yeye, mimi na wewe sipoi hata kidogo.”aliongea Jesca bila kupepesa macho. Alianza kumvua Badu suruali pale kitandani bila kujali.

“Jesca lakini nipo kazini mbona unafosi hivyo?”

“Nimeshamwambia meneja wako kuwa nataka huduma yako. Kama ameelewa tofauti na nilivyofikiria mimi badi.”aliongea Jesca akionesha kama kuchanganyikiwa.
Hali ile alipata kuiona Badu, na ili kumtuliza Jesca alikubaliana naye. Waliingia kwenye huba zito Badu akimpa raha Jesca vile anavyotaka.

Hadi jioni inafika Mayasa ndio alikuwa anaagana na Roja kuweza kurejea kwao. Alipanda bodaboda na kurejea kwao huku usoni akiwa na ngeu kwa lile virumai lililotokea.
Roja alirudi ndani na kupata kutulia akifikiria lile tukio.

“Dah siamini kama ndio nakata mahusiano na Mwajuma siku ya leo. Mayasa ananipenda kwa moyo wake wote kabisa lakini Mwajuma ndio kiboko yangu. Mwanamke anajua sana mapenzo yule basi tu siku za mwizi zikitimia huna budi kunyanyua mikono juu kusalimu amri.”aliongea Roja akionesha kujutia kile kilichotokea.

Mzee Chombo alikuwa zake ndani amepumzika, alikuwa anaitazama simu yake kuitafakari ile video ya mkewe aliyotumiwa na Jesca. Alisema na moyo wake ukaamua kufuta kabisa ile video asipate kuona tendo lile. Aliamini mkewe amebadilika tangu siku ile walipotoka kule hotelini kuanza maisha mapya.
ITAENDELEA 

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!