SEHEMU YA 40
ILIPOISHIA
Aliamini mkewe amebadilika tangi siku ile walipotoka kule hotelini kuanza maisha mapya.
SONGA NAYO
Muda wote Mwajuma alikuwa anatafuta kitu ambacho atakifanya ili tu kumkomoa Mayasa. Ni wazi kuwa sasa ameshakuwa adui yake mara baada ya kutambua alikuwa anashea naye bwana siku zote. Aliangalia saa yake ya simu na kuona inaelekea saa 1 jioni, alitamani Badu aweze kurudi mapema ili wapate kuongea jambo. Alishapanga jambo la kufanya na Badu lengo ni kumkomesha Mayasa.
Muda huo Badu alikuwa zake anabadilisha nguo zake kwenye stoo ya kubadilishia nguo mara baada ya kutimia muda wa kuondoka. Alikumbuka yale ambayo walikuwa wanafanya na Jesca kwenye kile chumba alichokodi Jesca lengo tu ni kumpata Badu. Alitabasamu mwenyewe baada kuona ingawa na umalaya anaofanya Jesca lakini kwake hapondui kabisa.
“Huyu mwanamke atanigombanisha na Mwajuma, nimeshaamua kuwa na mtoto wa Mzee Chombo lakini huyu Malaya ameganda kama ruba. Lakini ananiburudisha sana yupo moto na hana garama kama anavyowafanyia watu zake.”alisema Badu akivimba kuona amemshika masikio Jesca.
Hadi kufika saa mbili kasoro Jesca aliweza kukaribia geti kupata kuingia kwake apate kupumzika. Alipata kuona anashikwa mkono alipotaka kufungua geti, alipogeuka sura ya baba Dula ilipata kuonekana ikiwa na usiriasi ndani yake. Alianza kumvuta kwanza pembeni akionesha anajambo la kuongea.
“We baba vipi mbona tunavutana usiku huu?”alihoji Jesca baada ya kuona anapelekwa pembeni na nyumba hiyo.
Walifika sehemu ambayo ilikuwa na giza wakapata kusimama hapo.
“Nimekuleta hapa kwa ishu moja tu, naomba kuanzia leo tuheshimiane tu kawaida. Maswala ya kukutana kimwili tena yaishie siku ile ya jana, nahisi mkewangu ameshajua kuhusu ile jana nilipolala kwako hadi kuondoka alfajiri. Imepelekea hadi kuondoka nyumbani kurudi kwao, yaani kiufupi hili swapa limeshakuwa kubwa kwa upande wangu.”alisema baba Dula akionesha kuvurugwa.
” Akhhh! Hivi we unakichaa? Sasa kuondoka kwa mkeo mimi inanihusu nini? Unataka nikamrudishe au? Halafu, we ulikuwa unadhani nilikuwa nakuta saana hadi useme kuanzia leo tusiwasiliane! Yaani kati ya watu ambao sijawahi kuwawazia ni wewe baba Dula. Yaani nikae nianze kukufikiria wewe, hapana kwakweli we kuwa na amani tu sitakutafuta wala kukusimamisha sehemu.”
“Unasemaje? Kwahiyo mimi sina umuhimu kwako?”
“Babuwee elewa mara moja bwana. Wewe unamkeo wa ndoa ukija kwangu najua unapunguza mawazo tu mimi sina umuhimu wowote kwako. Na ndivyo ilivyo kwangu, jana ile nilikuwa na upiru umenikamata na sikuwa na jinsi ndio maana niakuita unifanye, usije kujiona saaana ukapata bichwa. We fanya mambo yako bwana kwa amani.”alisema Jesca kwa kujiamini kabisa. Baba Dula alimtazama msichana huyo aliyejawa na kiburi dhahiri, alishusha pumzi tu na kuamua kuondoka zake mara baada ya kufikisha taarifa hiyo kwa mlengwa.
” Hovyoo! Sasa mkeo akiondoka mi inanihusu nini? Ulitumwa unifuate!”aliongea Jesca akiwa anamtazama baba J aliyekuwa mbali kuondoka, aligeuka kuelekea zake ndani.
Alipofika mlangoni mwake alipata kumuona Mwajuma akitoka bafuni kuoga akiwa ametota maji mwilini. Alibaki kumtazama kwa kuobia tu huku akiingia zake chumbani kwake.
“Yaani yule mtoto ndio ananipiku mimi kwa Badu! Hivi anakitu gani hasa hadi kumchanganya Badu adiriki kunikataa mimi. Kweli Mwajuma wa kunizidi mimi kwa kipi hasa alichonacho? Au ndio hiyo shepu tu!”alijisemea mwenyewe Jesca akimsindikiza Mwaju kwa macho hadi alipoingia kwao.
“Hapana sikubali, nitafanya juu chini kuhakikisha nawagombanisha ili tu nimmiliki mimi Badu.”aliongea Jesca na kuweka dhamira yake kwa hilo.
Saa sita kasoro za usiku Badu alipata kumpigia simu Mwajuma.
” Oya umelala.”
“Haoana nipo macho. Vipi umeshamaliza mambo yako.”
“Yeah tayari njoo basi.”
“Haya poa zima hiyo taa hapo nje.”
“Okay.”alisema Badu kisha akainuka kutoka kitandani na kutoka nje. Alizima taa ile ya nje pale ambayo ipo karibu na ukuta wake ikimulika nje kote.
Mama J alikuwa kitandani anachezea simu yake huku pembeni mzee Chombo akiwa anakoroma. Alipata kuona nje kumekuwa na giza gafla. Ilimbidi ainuke kutazama dirishani. Alipata kumuona Badu akiwa amesimama mlangoni akiwa na boxer yake huku akiangalia huku na kule. Gafla akapata kusikia mlango wa nyumba yake unafunguliwa. Alishtuka na hakuweza kujua nini kinaendelea. Ilibidi akae palepale kutazama dirishani na sekunde chache tu alipata kumuona binti yake Mwajuma akiingia chumbani kwa Badu kwa kunyata kama mwizi. Jambo hilo lilimshangaza sana mama J na kubaki kushika tu mdomo.
“Mungu wangu! Huyu mtoto amepata ujasiri gani wa kutoka nje saahizi kwenda kwa Badu! Mh halafu anaonekana amezoea hana wasi kabisa.
Mpumbavu huyu kijana amehamishia dudu lake kwa mwanangu! Subiri sasa niwakomeshe.”alisema mama J na taratibu akaanza kushuka pale kitandani bila kumsumbua mumewe. Alianza kupiga hatua za taratibu kutoka nje kuelekea akipoenda binti yake.
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU