UTAMU WA JAMILA (43)

SEHEMU YA 43

“Basi sawa, sitaweza kumfukuza mapema hivyo hadi nipate kumchunguza na endapo nikibaini haya unayosema basi nitamtoa humu. Wacha nilifanyie kazi hilo nimepokea malalamiko yako.”alisema Mzee huyo akimjibu mkewe wa busara.

“Utachunguza hadi lini sasa? Au huniamini haya niyasemayo?”

“Mama J si nimeshakwambia nitafuatilia swala hilo! Umekazania sana kuhusu huyu kijana? Au kitu gani kinaendelea hapa?”alicharuka mzee huyu kimfanya hata mkewe kushtuka kuona mumewe amebadilika.
Aliona akiendelea kumzonga huenda yakazuka mengine.

“Hapana mmewangu hakuna zaidi ya hilo tu nilokwambia. Kama unachunguza sawa mimi nipo pamoja na wewe.”alisema mama J akionesha kupoa gafla.
Mzee Chombo alimtazama mkewe kisha akaamua kujilalia zake.
Mama J alibaki kumtazama tu mumewe aliyeonekana anaanza kuutafuta usingizi usiku huo.

“Huyu mwanaume kwa kuchunguza mambo ananikera! Sasa anataka kuchunguza akija kujua na mimi alinila yule kijana itakuwaje! Si ndio kuabika kwenyewe huku sasa. Mh.”alitafakari mama J juu ya swala hilo na kuona kuna kazi ya ziada kuifanya.

Kesho yake ilikuwa ni wikiendi nzuri kwa Badu, maana aliitwa na bosi wake kwenda kuchukua mshahara wake wa mwisho wa mwezi. Alielekea kwa bosi huyo na kupewa bahasha ya kaki iliyokuwa na pesa ndani yake. Alifurahi sana na baada ya kuagana alishika njia kurejea zake kwake.
Akiwa njiani alikumbuka ile kazi ambayo alipewa na Mwajuma kuhusu Mayasa. Aliamua kutoa simu yake kumpigia Mayasa na simu ikapokelewa.

“Habari yako!”

“Salama.”

“Aah samahani nimepewa namba yako na bosi Hemedi amesema unatafuta kazi. Wewe si ndio Fatuma?”

“Mh hapana mimi sio Fatuma.”

“Mh au nimekosea namba!”alisikika Badu kwenye simu ya Mayasa.

“Yeah itakuwa, ilaa…”alikata simu Badu baada ya kuona Mayasa anataka kujieleza. Alitabasamu kuona njia hiyo huenda ikawa sahihi kwayeye kumpata Mayasa kirahisi.
Akiwa kwenye kusubiri simu yake ilipata kuita na alipotazama aliona ni Mayasa, alitabasamu kisha akapokea.

” Halow!”

“Ah samahani kaka yangu, najua ulikosea namba ila nilikuwa ninashida hata mimi. Ni kuhusu kazi maana nipo tu mtaani sina kazi, sasa nimesikia unaongeleakuhusu kazi hapa, ni kazi gani hiyo maana hata mimi ninahitaji kaka.”

“Ah ni kazi tu ya hotelini. Unacheti cha Form Four?”

“Ndio kipo nyumbani, ninacho.”
Haraka akajibu Mayasa kuonesha anashinda kweli na kazi.

“Aha basi sawa, wacha kwanza nitafute tena namba ya huyu Fatuma kisha nikufanyia mpango na wewe.”

“Sawa kaka naomba usinisahau, mimi naitwa Mayasa save tu namba yangu nitakuwa nakukumbushia kila wakati.”alisikika Mayasa akiongea kwa unyenyekevu wa hali ya juu.

” Sawa Mayasa hakuna shida.”alisema Badu na kukata simu yake.

“Huyu kashaingia kwenye mtego.”alisema Badu na kuendelea na safari yake.

Mayasa alikuwa zake njiani muda huo akienda kwa Roja, ilimbidi arudi kwanza kwao kwenda kutafuta cheti chake cha shule kukiweka karibu ili asije kupata tabu siku akitafutwa.
Moyo wake siku hiyo ulilipuka kwa furaha na kuona huenda Mungu ndio amemfungulia milango ya riziki kwa njia hiyo ya mtu kumpigia simu akiwa amekosea namba.

Huku Badu aliweza kumpa taarifa hiyo Mwajuma kupita simu. Alifurahi kuona njia aliyotumia Badu inaweza kumvuta Mayasa wakakutana.

“Na alivyokuwa na hamu ya kazi walahi utampata kirahisi sana, na sijui ulifikiria nini hadi kutumia njama hiyo. Nakupigia saluti.”alisema Mwajuma akiwa zake chumbani anajipaka losheni kutaka kutoka.

“Usijali nitakuwa nakujuza kila hatua niliyofikia.”

“Poa mida.”alisema Mwajuma na kukata simu.
Alijitazama kwenye kioo cha dressing table yake akijiona jinsi aliyo na tabasamu mwanana.

“Mayasa, siwezi kukuacha uwe na mtu niliyekuwa nadate naye, bora wote tukose kuliko kukuachia Roja muanze kunisema kila mkikutana.”alisema Mwajuma akiwa anajitazama kwenye kioo.
Punde tu mlango ulifunguliwa na kupata kumuona mama yake anaingia humo chumbani.

“Mh mama ndio hata kubisha hodi jamani!”

“Nibishe hodi kwenye nyumba yangu, hebu usinipangie miye kwani wewe mwanaume?”

“Mh mama!”

“Nimekuja hapa kuna maswali nataka kukuuliza hapa.”aliongea mama huyo na kukaa kwenye kitanda akiwa anamtazama binti yake akiwa bize na kujipodoa.

“Mambo gani tena hayo mama yangu?”

“Hebu geuka kwanza huku usinipe mgongo wakati naongea na wewe.”aliongea mama huyo na kufanya Mwajuma ageuke kumtazama mama yake, sura yake ilionekana kuwa na jambo.

“Haya nakusikiliza mama.” 

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!