SEHEMU YA 45
ILIPOISHIA
Alijikuta anaifungua zipu ya Badu na kutoka kilichopo humo kuanza kukinyonya vema. Badu akitabasamu tu kuona mama huyo amepoa sasa, wacha ampe huduma.
SONGA NAYO
Mzee Chombo siku hiyo alipata kukutana tena na Jesca, na lengo kibwa hasa ni kumuuliza kuhusu Badu kutokana ma malalamiko ambayo ameyapata kutoka mkewe.
“Hivi haya maneno ni ya kweli umewahi kuyasikia ama ni uvumi tu? Maana huyu kijana sikuwahi kusikia skendo zake hivyo nashangazwa!” alihoji mzee huyo.
“Mh hapana kwakweli mimi mwenyewe hilo swala ni geni sikuwahi kumkuta akiwa na mwanamke wala kusikia taani uchafu huo anaofanya.” alisema Jesca akiwa anamtetea Badu.
“Mkewangu unajua amenionya sana kuhusu yule kijana. Sasa nahofia asije kuhamia mule ndani akatembea na nyie wote mule ikawa ni aibu kwenye nyumba ile.”
“Ah hapana mzee wala usijali. Kila kitu kipo sawa kabisa na hizo taarifa mimi sikuzisikia. Ila nitakaposikia basi haraka nitakujuliza.”
“Hapo sawa mimi nitakuwa nasubiria niupate ukweli maana kama ni kweli inanibidi nimtimue tu nitafute mpangaji mwengine. Mimi vijana wahuni sipendi kabisa, basi tunawapisha kwa hizi shida.”alisema mzee huyo na kuamua kusubiria Jesca ampe mrejesho wa kazi hiyo.
Kesho yake Badu aliamua kuifanya kazi ya Mwajuma rasmi. Alimpigia Mayasa na kuanza kumpanga juu ya kazi ambayo alimdanganya kumpatia.
“Kesho ninasafari ya kuelekea Zanzibar nitakaa kwa wiki moja huko. Sasa sijui unaweza kuja nilipo sasa na vyeti vyako?”aliukiza Badu akiwa makini na maelezo yake.
“Hakuna shida wewe wapi?”
“Am ninakaa hotelini ndiko nimefikia hapa.”
“Ahaa sawa, basi unielekeze wapi pa kifika.”
“Sawa nakutumia sms hapa utaona.”
“Okay.”alikata simu Mayasa akionesha kufurahi sana.
Dakika chache tu iliingia mesegi na kuweza kuifungua. Alipata kuona ni ujumbe unaomuelekeza wapi pa kufika ili apate kuonana na mtu aliyemuahidi kazi.
Kwa upande wa Jesca jambo la kumfuatilia Badu kwake hakuliona zito kwake, maana anavyojua ni yeye pamoja na Mwajuma ndio wanamfaidi Badu. Hakuwa na shaka juu ya hilo hivyo alitafuta njia tofauti ya kumjibu mzee Chombo ili amtetee Badu.
Huku kwa Badu siku hiyo alikuwa hivyo alienda kwenye hoteli moja na kuchukua chumba. Alimpa taarifa hiyo mapema Mwajuma kuwa aje haraka.
“Ah sasa nije kufanya nini wakati ndio siku ya kwanza mnaonana?”aliuliza Mwajuma kwenye simu.
“Wewe njoo tena hakikisha kamera yako ya simu ipo vizuri uchukue matukio. Huyu leo hiihii namla mzigo nawe ndo utapata ushahidi mzuri wa kuchukua.”alisema Badu akiwa mwenye kujiamini. Alisikia kicheko tu cha Mwajuma na simu ikakatwa.
“Ah huyu vipi amekata simu?”alishangaa badu na kuamua kuiweka simu yake mezani.
Meza aliyoweka baadhi ya makaratasi yaliyobandikwa picha za watu, huku pembeni akiwa na kibegi kidogo. Alitabasamu mwenye baada ya kuona ameandaa vema mazingira ili apate kuonekana ni mtu wa mishe hiyo za kuwatafutia watu kazi.
Kwa mama J muda huo alikuwa zake kwenye bajaji akiwa anaelekea kwenye mihangaiko yake. Muda wote alikuwa kwenye wimbi la mawazo hasa kwa kile kitendo alichofanya na Badu pale sebuleni. Alijikuta anaulaumu moyo wake wa tamaa na kuona amevunja ahadi na mumewe mara baada ya kuamua kuanza maisha mapya yenye amani.
“Tatizo yule mtoto anajua kucheza na hisia zangu sana najikuta tu nakuwa mtumwa wa mapenzi kwake. Utanisamehe tu mumewangu, itanibidi nikusaliti bila wewe kujua. Na nakuahidi sitatoka kwa mwanaume mwengine zaidi ya Badu.”alijisemea mwenyewe Mama J akiwa zake kwenye bajaji.
“Anti samahani naingia hapa kujaza upepo mara moja kisha tunaendelea na safari yetu.”aliongea dereva wa bajaji.
“Si nitachelewa jamani!”
“Hapana ni dakika mbili tu wala hutachelewa.”aliongea dereva huyo na mama J akamuelewa.
Waliingia kwenye gereji moja iliyo pembeni na barabara, yule dereva alishuka baada ya kufika sehemu husika na kuongea na mhudumu ambaye alianza kufanya kazi hiyo. Katika kutazama huku na kule mama J alipatwa na mshtuko mara baada ya kumuona Roja akiwa pembeni ya gari moja ameshika spana analitengeneza. Lilikuwa ni gari la bwanake Jesca ambaye naye alikuwa humo ndani amekaa akisubiria gari hilo kutengenezwa wapate kuondoka.
” Ahaa huyu kumbe ndio anapofanyia kazi hapa!”aliongea mama huyo na kumuita Roja kwa sauti. Kijana huyo aligeuka kuangalia anayemuita na alipotazama alimuona ni mama J. Aliachia tabasamu Roja huku akimsogelea mama huyo hadi pale alipo. Jesca alipotazama pembeni alipata kumuona Roja akitembea kuelekea kwenye ile bajaji. Alishangaa kumuona mama J akiwa anamtazama Roja hadi alipomsogelea.
“Hee! Huyu mama vipi tena?”alijisemea Jesca akiwa anatazama kinachoendelea.
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU