KIAPO CHA MASIKINI (12)

SEHEMU YA 12

ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA MOJA: Kadara akaelekea stendi ya bus, akimwacha Peter pamoja na mwanae Michael, wakisimama huku wakimsindikiza kwa macho Kadara, huku Peter moyoni mwake akiwa mwenye furaha kubwa, kusikia kuwa Sada anawakumbuka yeye na Michael, walimtazama mpaka alipotokomea zake, kisha Peter akamtazama mwanae Michael, “mwanangu sasa tunaenda kumrudisha mama yako, ametambua makosa yake, na sasa anatukumbuka sana” alisema Peter huku anamnyayua mwanae, na kuchukuwa mfuko wa vitu alivyonunua wakaanza safari ya manunuzi, Michael ambae akuwa anatambua kuhusu mtu anae itwa mama, alikodoa macho yake akimtazama baba yake, ambakiukweli hakujuwa kuwa kinachofwata mbele nizaidi ya burudani kwake. ………Endelea……..
Maana ata alicho ambiwa na Kadara ni uongo mtupu, hakukuwa na ukweli wowote kuhusu Sada kumkumbuka yeye na mwanae.***
Naam akiwa katika maisha ambayo alitegemea kuwa yange kuwa ni mazuri, kama vile alivyokuwa anaota kuishi kula siku, Sada au mama Michael ambae ndie Queen, maisha ambayo sasa alikuwa anayaishi, yani kula vinono, kunywa bia kila siku, na kuvaa vizuri, na sasa alikuwa anatembezwa kwenye gari la pengo, yani Toyota Ist, ni maisha ambayo ameshindwa kujinasua, ata baada ya kugundua kuwa mpenzi wake huyu, ni mtu hatari anae jiusisha na matukio mabaya na uuzaji wa dawa za kulevya, biashara haramu ya boss wa mpenzi wake huyo, yani bwana Kalo.
Siku moja saa nne za asubuhi, akiwa anatembea kwa miguu kukatiza mitaa ya soko kuu, akielekea majengo nyumbani kwa rafiki zake wakina Rose, mala akamwona Kadara anapakiza mizigo kwenye gari dogo, la mizigo, maarufu kama kilikou, lililosimama pembeni ya yamduka ya jumla ya vifaa vya urembo, na nguo za kike na watoto, likiwa ni tawi la mwana dada mrembo Careen, ukweli moyo wa Sada ulilipuka sana, siyo kwa mshangao au furaha, ya kuona mwenzie ananunua vitu vingi vya thamani, kwamba amefanikiwa kimaisha, hapana, ukweli moyo wa Sada ulilipuka kwa wivu wa ghafla, “mh! hapana siyo vyake” aliwaza Sada au Queen kama wanavyo mwita wenzake, huku mjini, akiamini kuwa vile vitu siyo vya Kadara, ila ata kuwa anamsaidia mtu flani mwenye fedha zake, alie mwomba Kadara kumsaidia kununua vitu hivyo, pengine anataka kumwajili kwenye duka au tayari amesha mwajili, Sada alitazama vizuri kama angemwona mtu mwingine ambae ndie muhusika wa mizigo ile, lakini hakukuwa na mtu yoyote ambae angekuwa mmilikiwa mizigo ile, Sada alizidi kushikwa na wivu na akutaka kuamini kuwa Kadara mwanamke anae fanya kazi ya kuhudumu kwenye jiko la Msogeze Pub, eti ananunua vitu vingi kama vile, ambavyo kwa haraka haraka, vingezidi zaidi ya million tatu mpaka tatu na nusu, “hapana wacha nikamwulize” alijisemea Sada huku anachepuka na kusogelea kilikuu, huku anatazama kwa makini vile vitu ambavyo vilikuwa vinapakizwa kwenye gari, ambavyo vilionekana wazi kuwa vya thamani na vinaenda kuwekwa dukani, tena duka jipya, “jamani taratibu, msije kunivunjia hicho kioo” alisikika Kadara, akiongea kwa namna ambayo ungejuwa tu kuwa yeye ndie tajiri wa ule mzigo, “mambo kadara” alisalimia Sada, mala baada ya kumfikia Kadara, ambae mwanzo hakuwa amemwona, maana aligeuka kwa haraka, na kumtazama, “mambo Queen hupo my” alisema Kadara kwa sauti flani iliyojaa pose, za ela ela, kitu kilicho mshangaza Sada, ambae yeye alijionaga kuwa ndie ni mmoja kati ya nwanawake wenye bahati ya kuwa na mwanaume wenye fedha na gari, na aliamini kuwa yeye ndie mwanamke ambae anamafanikio makubwa sana kati ya wanawake te toka kijijini, pia aliamini kuwa yeye ndie mtoto au kijana wenye mafanikio makubwa kati ya vijana wote waliopo kule kijijini kwao Mwanamonga, ila leo ndio aligundua kuwa ukiachilia bia chips na kupewa dudu, hakuwa na mafanikio yoyote, na pengine angefaa kujiliwa na Kadara, “hongera mwenzangu, ebu niambie umemwotea mwanaume gani huyo, ambae amekupa ela ndefu kama hiyo?” aliuliza Sada kwa sauti ya chini na yamshangao.
Kwa Kadara alianza kwa kucheka, “nimepewa na baba yangu baba yangu, kuna buzi la kukupa million nne?” aliuliza Kadara, ambae alimkumbusha Sada kuwa msimu ule ulikuwa ni wamalipo ya tumbaku, msimu ambao kule kijijini kwao kuna kuwa na fedha nyingi sana, msimu ambao mwaka jana aliondoka kijijini akiwa ameiba fedha za mzazi mwenzie yani kijana Peter au baba Michael, “jamani, amekupa zote hizo?” aliuliza ka mshangao Sada ambae siku zote amekuwa akiambulia kupewa bia, na vyakula, pasipo ata sent tano, inafikia hatua anatembea kwa miguu akikosa ata elfu moja ya pikipiki, “ndiyo uwa namsaidia kumtumia fedha za matumizi, asa wakati wa kilimo, ndio maana unaona ananipa ela nyingi” kauri hiyo ilifanya Sada aishiwe nguvu, maana akuwa na uwezo wa kuomba fedha kwa wazazi wake, ambao awakuwa na shamba la tumbaku, zaidi ya shamba dogo la maindi, na wakati ule walikuwa wanategemea kupata fedha toka kwa Michael, ambae alikuwa kama mkombozi katika familia yao, “jamani na mimi ningejuwa si ninge wasaidia katika kilimo ilinijipatie fedha, kama wewe” aliongea kwa sauti ya nyinge Sada, wakati huo dereva wa Kilicou alikuwa anavunga vyema mizigo kwenye bodi la gari.
Kadara akatabasamu kidogo, “una juwa nini Queen, wenzio Peter atakuwa amesha lipwa fedha nyingi sana za tumbaku, maana nimemkuta anafedha kama zote” alisema Kadara, na hapo ndio kama alizidi kumtia untinge Sada, “sasa fedha za Peter zina niusu nini, unazani ata nipa ata sent yake baada ya kumfanyia yote hayo niliyo mfanyia?” aliuliza Sada kwa sauti ya kinyonge huku roho ikizidi kumchonyota, Kadara akatabasamu tena, “anashindwaje kukupa fedha kwa jinsi anavyo kupenda?” aliuliza Kadara na hapo Sada aka tabasamu kwa furaha na mshangao, “weweeeee! Acha utani, ananipenda kivipi wakati nilimfanyia ubaya?” aliuliza Sada kwa sauti ya kuto kuamini, na hapo Kadara akaanza kumsimulia jinsi alivyo kutana na Peter na kumdanganya kuwa yeye anamkumbuka sana pamoja na mtoto wao, na kwamba yupo tayari kurudiana nae, “tena namba yake hii hapa” alisema Kadara na kumpatia namba ya simu Queen yani Sada, kabla awaja achana akimwachia elfu ishilini, ambayo ilikuwa ni fedha kubwa sana, ambayo akuwai kuishika kwa miezi zaidi ya sita sasa, lazima nile fedha ya huyu mshenzi” alijisemea Sada huku anageuka nakurudi alikotoka akighairi safari ya majengo.***
Naaam mida hiyo eneo la uwanja wa ndege, wa luhuwiko, alionekana mwana dada mrembo Careen, akiwa amesimama ubavuni mwa gari lake, aina ya range rover, akitazama gari moja aia land rover puma, lililokuwa lina pakiza mzigo toka kwenye ndege yenye nembo ya nchi ya kifalme, ya #mbogo_land, huku magari mawili ya polisi, yenye polisi wenye salaha zao, yakiwa yanasubiri, kutoa ulinzi katika msafara utakao kuwa unaelekea mjini, kwenye jengo la Mbogo land Sonara, muda wote wa upakizani wa vifurushi hivyo, Careen alionekana kuwa kimya akitazama shughuri ya upakizaji wa.
Upakizaji huo aukutumia muda mrefu sana, wote wakaingia kwenye magari usika, na safari ya kuelekea mjini ikaanza, gari moja la polisi mbele moja nyuma moja, huku askari wakining’inia kwenye magari hayo, ambayo yalionyesha kuwa yapo kwenye ulinzi wa kitu kikubwa chenye thamani kubwa, magari mawili yalikuwa kati kat, ya magari ya polisi, Range rover la Careen lilikuwa nyuma ya gari la kifahari lililo beba mzigo ulioshushwa toka kwenye ndege, yeye alikuwa peke yake, huku magari mengine yakiwa na watu wasiopungua wanne, ebu turudi kwenye gari la mbele kabisa, ambako pembeni ya seat ya dereva wa gari ilo la polisi, alikuwa amekaa askari polisi mwenye cheo cha koplo, ambae alionekana akitoa simu yake na kuandika ujumbe, “tayari ameshapokea mzigo, tunaupeleka ofisini kwake” kisha akautuma ujumbe huo kwenye namba iliyoandikwa Mr Kalo, baada ya hapo aikuchukuwa ata dakika jibu likaja, “poa kaka, wacha nitengeneze mazingira, cha msingi naomba uandae ulinzi kwaajili yetu, endapo chochote kitatokea” ndivyo ulivyosomeka ujumbe huo.
Naam kwenye gari aina ya Range rover, Careen ambae mala zote uwa anaendesha gari mwenyewe, alikuwa ana tafakari mambo mengi kichwani, asa ni usumbufu ambao aliwai kuupata, kwa kuandamwa na bwana Kalonga, ukizingatia nimuda mrefu sana ulikuwa umepita, toka tukio la mwisho la yeye kuvamiwa na vijana wa Kalonga, na kusaidiwa na yule kijana ambae akuitaji chochote toka kwake,nikijana jasiri, ambae kiukweli alijitolea kupambana kwaajili yake, niwazi akuwa anamfahamu yeye ni nani, ni kijana ambae mala kadhaa alisha mjia katika kumbu kumbu zake, kutokana na kijana yule alicho kifanya kwake, akimzidi ata mlinzi wake alikuwa na bunduki, lakini malazote Careen akijitaidi kuondoa kumbu kumbu zile, sababu akutaka kumweka kichwani kijana yule, ambae licha ya hivyo alitamani siku moja akutana nae ili ampatie zawadi kwa kile alicho mfanyia, maana Careen alimini kuwa, kijana yule ndio sababu ya kukoma kwa usumbufu wa Kalonga na vijana wake.
Leo Careen alikuwa amepokea mzigo mkubwa wa vitu vya thamani, toka nchi kwao, ukiwa ni mzigo toka kwenye kiwanda cha dhahabu cha mfalme wanchi hiyo mfalme Elvis Mbogo wa kwanza, ikiwa ni sehemu ya kuonyesha nikiasi gani anaitaji Careen amchukulie kama rafiki na urafiki wao udumu, kuonyesha kuwa amesha msamehe kwa kile alichokifanya kwa kuowa mwanamke mwingine akimwacha yeye Careen, rafiki wa utotoni, mizigo ambayi ilitoka mbogo land likuwa ni vito vya dhahabu harisi toka mbogo land, dhahabu ambayo inasakwa katika masoko yote makubwa ya madini duniani.***
Naam mida ya saa saba mchana pembezoni kabisa, mwa mtaa mkubwa wa Mateka, nje ya jumba moja kubwa la kifahari, lililopakana na ifadhi ya msitu wa matogoro, mita mia nne toka kwenye barabara ya vumbi, iendayo Ndilima, tungeweza kuona magari manne ya kifahari, na moja la tano dogo aina ya Toyota IST, ndani ya uzio mkubwa wa ukuta uliozunguka jengo ilo, eneo la mbele la jengo ilo ambalo pilika za kila siku zilikuwa ziendelea kama kawaida, lilipambwa na vijibustani vizuri vya mauwa mazuri yaliyo pendeza pembezoini mwa vijinjia vilivyo sakafiwa na vitofari vya semeni.
Tuachane na sifa za jumba ili la kifahari, nazani itakuwa vyema kama tukiingia ndani ya jengo ilo la kifahari, tuna ibukia ndani ya sebule kubwa sana, ambapo tuna kutana na mama mmoja mtu mzima, alie kuwa amejilaza kwenye kochi, anatazama television, huku anapata soda yake ya baridi, huyu anaonekana kuwa ni mama mwenye nyumba, hakika sebule inavitu vingi vya kifahari, lakini wakati tunashangaa pale sebuleni, mala watu wawili wanaibukia pale sebuleni, huku wanasisitizana jambo, “hakikisha kila kitu kinaenda sawa, msakeni, msije mkaukosea mpango nimesha weka kila kitu sawa” alisema jamaa ambae alionekana amevalia kaptulah, na singland, “aina tatizo boss, safari hii naamini tuta fanikiwa, asa baada ya kukaa muda mrefu pasipo kumsumbua, ata zania kuwa tumesha msahau” alisema yule kijana alie valia tisht na jinsi, mkononi akiwa amebeba box moja dogo, lililofungwa vizuri sana.
Wawili awa waliendelea kuongea mpaka walipotoka nje kabisa ya je nyumba ile, “Emma tunaitaji tupate zile funguo, na kuingia ndani ya office za yule mwanamke mshenzi, tafadhari kosa lolote lita sababisha madhara makubwa sana” alisema yule mzee kwa sauti ya chini, iliyojaa msisitizo, wakiwa wamesimama mita kadhaa toka mlangoni, “safari hii boss hakuna kitakacho aribika” alijibu yule kijana alie itwa Emma, kwa sauti ya kujiamini, “ok! we nenda kumbuka kikao ni kesho kutwa, na mzigo umesha ingia ofisini kwa yule mpuuzi” alisema yule alie vaa kaptulah,a mbae kimwonekano, alikuwa ni mtu mzima, waliagana na yule mtu mzima aliingia ndani huku kijana akielekea kwenye gari, aina ya Toyota ist, na kutoka zake nje ya geti la uzio wa jumba lile, la kifahari.
Awa wawili ni Bwana Kalonga na kijana Emanuel, ambao walionekana kuwa walitoka kwenye kikao kukubwa na kikali cha siri, ambacho kilikuwa kina lengo la kuweka maazimio ya kutekeleza mpango wa uvamizi na wizi wa vitu vya thamani.**
Saa tatu usiku, bwana Peter alikuwa chumbani kwake ana maliza kuweka fedha zake kwenye begi ambalo alipanga kusafiri nalo siku tatu zijazo, kuelekea mjini, ambako angeenda kununua vaa muhimu kwaajili ya ujenzi wa yumba kubwa na vifaa vya umeme wa nguvu za jua, ambavyo vingeambatana set ya TV na redio kubwa, ambayo inge mliwaza kwa kusikiliza music na kuona wazungu, aliamini kuwa safari hii ata mke wake Sada akirudi basi atoweza kuondoka, kwa hali ambayo angemkutanayo pale kijijini, na kitu ambacho Peter alipanga kununua mala tu akapoingia mjini, nisimu ya kisasa.
Naam baada ya kumaliza kuweka kiasi cha million kumi na moja na laki kadhaa, ndani ya begi, Peter alichukuwa simu yake ambayo toka alipoichukuwa dukani kwa kwenye kuchaji, akuwa ameiwasha, aka panda kitandani, ambako mwanae Michael alikuwa amesha lala muda mrefu uliopita, akaiwasha simu yake hiyo na kusubiri kwa dakika kama mbili, kabla ajasikia jumbe mbili zikiingia kwa kufwatana, akuchelewa kuzifungua jumbe zile, ambazo zilikuja kwa namba ngeni, ya kwanza kabisa ambayo ndiyo ya mwisho kutumwa, iliandikwa hivi, “basi ukiwasha simu nitafute, nimewamiss sana wewe na Michael, ujumbe ambau ulimshtua sana Peter, ambae alitazama ile sms nyingine ambayo ndiyo ilikuwa yakanza kutumwa, “mambo za kunisusa mume wangu, mimi mama Michael” hapo Peter alijikuta anaachia tabasamu pana la furaha….

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!