
SEHEMU YA 14
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA TATU: Emma alimsikia Sada akiongea kwa sauti ya kubembeleza ambayo yeye aliisikiaga miezi mingi iliyopita, ukweli moyo wake ulilipuka vibaya sana, akajwa na wivu mkali sana, “inamaana huyu Malaya ananisaliti, na anamwanaume mwingine, tena anambembeleza namna hii” aliwaza Emma au pengo huku moyo wake ukipatwa na machungu ya kiwango cha juu sana, “ila baby, wala usijari, ngoja nipige mswaki, nioge, alafu nitakupigia sawa mume wangu?” alisema Sada na hapo nazani, alikata simu, “atanitambua huyu mshenzi” alisema hivyo Emma, huku ana usukuma ule mlango na kuingia ndani, na kumkuta Sada akiwa ametoa macho kwa mshangao………. Endelea…….
Akimtazama Emanuel aliekuwa anamjia pale kitandani kwa kasi ya ajabu, huku sura ameikunja kwa hasira kali, “Ima tafadhari tulia kwanza nitakueleza kila kitu aipo kama unavyozania..” labla Sada ajamaliza kuongea, tayari Emma, alikuwa amesha mfikia, “mjinga wewe auna cha kuniambia nimekusikia mwenyewe ukiongea na hawara yako mshenzi wewe” maneno hayo ya Emanuel, yaliyojaa hasira kali yaliambatana kofi kali lililovutwa na kushushwa usoni kwa Sada, “paaah! Kibao kilichotoa mlio, kama puto limepasuka, “mamaaaa nakufaaaaa” ilimtoka Sada au Queen, kwa sauti ya juu sana, huku anajaribu kuinuka lakini akapelekewa kofi jingine lililotuwa pale pale usoni, na kumrudisha kitandani, na kumfanya Sada azidi kuongeza sauti kwa kilio, lakini aikusaidia, aliweza kuona vipigo mchanganyiko vikimshukia, mala ngumi ya tumbo, mala kofi la musoni mala teke la kwenye makalio, sambamba na kilio cha paka jizi, “Emma mume wangu utaniuwa bule baba, mwenzio sikusaliti, nisikilize kidogo” alipiga kelele za kuomboleza Sada huku anapiga magoti mbele ya Emanuel Pengo, pasipo kujali makofi na mangumi yaliyokuwa yana mshukia mwilini mwake, “uniambie nini?, uniambie nini wakati nime kusikia mimi mwenyewe?” alisema Emma huku anaendela kushusha kipigo kwa Sada au Queen kama ambavyo alikuwa anamfahamu, ungesema ni mpiga ngoma wa band ya the sky way ya hayati Lucky Philipo Dube, akiwa amesha pata kile kivuto cha kuweusha, “subiri kwanza nikueleza, naomba usinipige kwanza” aliomba Sada, na safari hii ombi lake lilisikilizwa, kwa Emma kuacha kumdunda, “dakika moja unieleze, na ole wako unidanganye” alisema Emma, na hapo Sada akatumia nafasi hiyo kuongea kwa haraka, “huyo siyo mpenzi wangu, nilisha achana nae, anaitwa Peter, yeye yupo kijijini, anafedha nyingi nataka fedha zake, lakini sitofanyanae chochote” alisema Sada kama mashine ya kushoea nguo, yani ilikuwa ni kwa haraka haraka sana, “una uhakika anafedha nyingi, kwanini sasa hukuniambia” alisema Emma kwa sauti ambayo ilianza kuipooza, “nilitaka kwanza niongee nae, nikipata uhakika ndiyo nikupigie” alisema Sada kwa sauti ambayo iliambatana na kilio cha chini chini, “ok! ebu ongea nae mbele yangu na mpange kila kitu, weka loud speeker” alisema Emma huku ana chukuwa simu ya Sada na kumpatia, nae akaipokea na kujiweka sawa, ili kuondoa ile hali ya kutoka kwenye kilio, “jitaidi sasa hasijuwe kama ulikuwa unalia” alisisitiza Emmanuel, alikuwa amesimama pembeni ya Sada.***
Naam watu walikuwa wengi ndani ya duka kubwa la vito vya thamani ambayo ni urembo kwa wanawake na wanaume pia nguo zuri zakike, la #mbogo_land Sonara, waliokuwa wananunua bidhaa nzuri toka nchini Mbogo land, ya mfalme Elvis, mwana dada Careen akiwa amesimama kwenye kibaradha cha ghorofa ya pili, akitazama chini kuona jinsi wafanyakazi wake walivyokuwa wanawahudumia wateja wao, kwa ukarimu mkubwa, ambao ni utamaduni wa nchi yao, nchi yenye sifa ya kipekee kama lilivyo kabira la samalia, huko Israel.
Careen mschana mrembo na mkimya sana, alikuwa amesima pale juu, akiendelea kutazama, japo usingeweza kuona wazi usoni mwake, ila moyoni mwake alifurahi sana, kuona mauzo yana ongezeka, ni kawaida kwa msimu huu wa mavuno na malipo mbali mbali yanayofanyika kwa wakulima, maana ukiachilia malipo ya wakulima wa tumbaku, pia kulikuwa na malipo ya wakulima wa korosho, na toka tunduru, na wakulima wa zao la kahawa toka mbinga, nikipindi ambacho watu upendeza sana, watu ununua nguo nzuri, watu ununua nguo za kufungia ndoa, maana ndio kipindi ambacho watu ufunga ndoa kwa wingi, licha ya aya yote lakini usingeweza kuliona japo tabasamu la mwana dada huyu, ambae ata wafanyakazi wake uwa wanakaa mwezi mzima pasipo kuliona tabasamu lake, achilia kicheko ambacho ata yeye uwa anasahau mala ya mwisho alicheka lini.
Biachara ilikuwa yenye mafanikio, mauzo yalikuwa juu, ilifikia wakati kila baada ya msaa mawili alikuwa anaingia kwenye chumba cha uifadhi ni baada ya kuletewa makusanyo ya fedha ofisini kwake, kwenda kuzifungua kwenye makabati ya chuma, ambayo mala zote utumia kama benk yake, ya muda, kabla aja safirisha kwa ndege kupeka nchini kwao kwenye account yake, au kulipia mzigo mwingine wa biashara, ma wakati akiwa anaendelea kuwatazama wateja na wafanyakazi wake, mala akamwona mfanyakazi wake mmoja wakike ambae tunaweza kumwita kuwa ni karani au msaidizi wake, akija na simu mkononi, “samahani dada simu yake inaita” alisema yule msaidizi huku anamkabidhi simu ambayo nikweli ilikuwa inaita, akaichukuwa na kuitazama, akaona jina limeandikwa mkurugenzi JJ Campany, akaipokea mala moja, “hallow mkurugenzi habari za kazi” alisalimia Careen kwa sauti tulivu, iliyojaa nidhamu, “nzuri dada Careen habari ya wewe” ilikuwa ni sauti ya kiume iliyochangamka toka upande wapili wasimu, “salama tu naam nikusikilize tafadhari” alisema Careen ambae ni wazi akuitaji maongezi mengi, “yah! nilitaka nikupa mabadiriko madogo ya ratiba, tunaomba tukutane saa mbili usiku, pale Makimakuluga motel” ndivyo ilioongea ile sauti ya kiume yenye kuchangamka, hapo Careen aka kunja usowake kama vile aja kubariana na swala ilo, “mh! nazani tughairishe kikao, muda huo ni muda wangu wa kupumzika, sipendi watu ambao hawana uhakika na ratiba zao, muda ni sa saa kumi na moja zaidi yahapo hakuna kikao siyo kesho tu, ila hakuna biashara kabisa” alisema Careen kwa sauti kavu kabisa, sauti ambayo aikuwa na dalili ya utani, “ok! sawa sawa, tutafanya muda huo huo, saa kumu na moja, na nusu, tutakuwepo hapo” alisema yule jamaa kwa sauti ya kuomboleza, “tafadhari, wakati mingine ukupiga uwe na vitu vya msingi vya kuongea” alisema Careen na kukata simu, kisha akampatia yule mfanyakazi wake, kisha yeye akaendelea kutazama wateja na wahudumu wake.****
Naam baada ya kutoka yumbani kwa wazazi wake akiwa amekatiwa simu ghafla na Sada akiwambiwa kuwa wataongea baadae, kijana Peter Jacob, alitembea taratibu kuelekea nyumbani kwake, huku akifanyiaa utani na michezo ya furaha a mwanae Michael, kila alie mwona Peter wakati ule niwazi angegundua furaha ya wazi aliyokuwa nayo kijana huyu, “tuka jiandae kesho ukakutae na mama yako” alisema Peter, ambae akiwa a habari ya kile kinachoadaliwa kwaajili yake huko mjini…… Endelea……
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU