KIAPO CHA MASIKINI (19)

SEHEMU YA 19

ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA NANE: Lakini akufanikiwa ata kuzifikia ngazi zile, maana wakati anaendelea kujikongoja, ghafla akawaona vijana wawili wakiibuka kwenye korido, toka kwenye ngazi, wakija upande wake kwa speed kali huku macho yao wameyaelekeza kwake, vijana ambao mwanadada huyu, aliwakumbuka mala moja, kuwa ni vijana wa bwana Kalonga… Endelea……
ambao mala ya mwisho walimvamia muda mrefu uliopita, mbele ya eneo la ofisi yake, na kusaidiwa na mtu mgeni, ukweli Careen alihisi miguu nakosa nguvu, kwakujuwa kuwa leo hakuwa na ujanja, wa kuwaponyika watuawa ambao walikuwa mbali nayeye kwamuda mrefu kidogo, ni baada ya kupokea kipigo toka kwa kuyule kijana wa sikuile, Careen akapa wazo la kuingia kwenye moja ya vyumba vilivyokuwa vimejipanga kolidoni, na mlango uliokuwa karibu, ni mlango wa chumba na saba na itakuwa kama ata ingia nakukuta kuna watu au mtu mbaya zaidi, ambae ayafunga chumba na kumfanyia vitendo vibaya zaidi.
Lakini wakati anawaza hayo huku anawatazama wale vijana wawili waliokuwa wanamsogelea kwa mwendo wa haraka, mala akaona mlango wa chumba kile namba saba ukifunguliwa.**
Naam wakati haya yatokea huku MAKIMALUGA MOTEL, kumbe dakika chache zilizopita Sada alikuwa amesha fika Msogeze pub, ambako alitafuta meza iliyojificha kidogo, na kukaa huku akiagiza bia, na baada ya hapo akazima simu ya Peter, na kuanza kuchambua begi la Peter, akipekenyua nguo na viatu vya watu wake wawili yani, mzazi mwenzie Peter, na mwanae Michael, mpaka alipofikia kipochi flani chenye ukubwa wa wastani, kipochi ambacho nachoweza kusema, kuwa kilichukuwa sehemu ya robo nzima ya begi lile, akakitoa kabisa nje ya begi na kukifungua, akuwa na aja ya kumaliza kufungua begi lile kwa kile alicho kiona ndani ya bochi ile kubwa, japo alitarajia kukuta kile alicho kikuta, lakini alishtika sana, nazani akutegemea kukutana na mzigo mkubwa kama ule, ambao akuwai kuugusa katika maisha yake nifedha nyingi kuliko zile alizo ziiba wakati ule atoroka kijijini, “siamini macho jamani” alisema Sada huku anarudisha pochi lile kubwa kwenye begi, na kuchukuwa simu yake kisha na kumpigia mpenzi wake, yani Emmanuel, ambapo simu ilianza kuita mala moja.***
Naam Peter alikiwa mlangoni akilikodolea kolido refu, lenye vyumba pande zote mbili, alitazama kulia na kumwona mwanadada yule alie mwona kamasaa machache yaliyopita, akiingia humu ndani, akiwa anatembea kwa kujikongoja, kuja upande wake, alionekana kuwa amelewa vibaya sana, alikuwa mita chache sana toka pale alipokuwepo, yani kwenye mlango wa chumba namba saba, “mjini sijuwi kuna nini, yani mwanamke mzuri kama huyu analewa hovyo namna hii, siwanaweza kumbaka” alijisemea Peter, huku anageuka kutazama upende wa kushoto, ambako aliwaona vijana wawili wakija kwa haraka, kuelekea kule anakotokea yule mwanamke, akutumia ata dakika kuwatambua kuwa ni wale vijana wezi waliotaka kumpora mwanamke huyu huyu, miezi kadhaa iliyopita na yeye akamsaidia, akajuwa kile alichokiwaza ndio kinaenda kutokea tena, na wakati huo huo akasikia simu ya mmoja wa wale vijana ikiita.
Emmanuel Pengo na mwenzie Hussein yani Janja, walipoibukia kolidoni, walifanikiwa kumwona mtu waliekuwa wanamtafuta, yani mwana dada alie tapakaa vito vya dhahabu katika sehemu za mwili wake, kama vilee hear ring za masikioni, mikufu ya shingoni, ata hand ring, na pete vidoleni, ambavyo vilikuwa ni vya dhahabu harisi, “kama zari vile huyu hapa sasa tunaondoka nae kama tulimweka” alisema Emmanuel, huku wote wawili wanautazama mlango wa chumba komoja kati ya vyumba vingi pale kolidoni, ambao hawakuutazama, ni namba ngapi, na kumwona yule jamaa ambae muda flani walimwacha pale mtini Pub, “hii nuksi hipo huku inachukuwa chumba VIP” alisema Janja, na hapo nipo Pengo alipo itoa simu yake iliyokuwa inaita mfukoni, na kutazama, akizania kuwa pengine mpigaji atakuwa ni boss wake, yani Kalonga, lakini alipoitazama hakuwa boss wake, ila alikuwa ni Queen, kwanza alitaka kuikata ile simu, kwakuona niusumbufu, lakini akaona kuwa ile simu ndio kitu pekee cha kuzugia, ili huyu mtu aliesimama mlangoni.
Kwaupande wa Careen ambae mpaka sasa alikuwa amesimama mkono mmoja ameshikilia ukuta, akishindwa kupiga ata hatua moja, alimwona yule kijana alie simama pale mlangoni, na kumtambua kuwa ni kijana alie waikumsaidia miezi kadhaa iliyopita, hapo akajaribu kutanua midomo yake ilikuomba msaada, lakini mdomo wake ilikuwa mzito kutokana na kuzidiwa kwa kilevi, akaona njia nyepesi nikuonyesha ishala ya mkono, lakini kabla ajainua mkono, akamwona yule kijana mwenzie, akigeuka upande wa kutokea kwenye ngazi kuwa tazama wale vijana wawili wa Kalonga, ambao walikuwa wanazidi kumsogelea huku mmoja wao akipokea simu na kuiweka sikioni, “Queen nilishakuambia leo ninakazi muhimu ya kufanya, kwanini unapenda kunisumbua wewe” alisema Pengo, huku anaendelea kutembea, kuvuta usawa wa mlango wachumba namba saba, ambacho Peter alikuwa amesimama anawasindikiza kwa macho, akisubiri kuona kitakacho tokea, hakuna alie kuwa anasikia alichikuwa anaongea mpigaji wasimu hiyo, lakini ungeweza kuhisi kwa majibu ya Emmanuel, “haaaaa! Umesha mpiga huyo fala wako…. Basi wewe endelea nitakupigia baadae” alisema Emmanuel huku anakata simu, na wakati huo tayari walisha mfikia yile mwanamke, mrembo mwenye dhahabu nyingi mwili wake.
Careen alisha jikatia tamaa, jamaa walisha mfikia, na mmoja akaukamata ule mkoba na kuupola toka kwenye mikono yake, huku alikuwa ni pengo, na Janja yeye alaimshika yule dada mkono wake na kumpachika kwenye bega lake, kwamaana mfano wa mtu alie msaidia mgonjwa au rafiki alie lewa, Careen akiwa anajuwa kuwa licha ya kupolwa vitu muhimu kwake, lakini pia anaenda kufanyiwa kitu ambacho akupenda kukishuhudia akifanyiwa katika maisha yake, kwamba anaenda kubakwa, maana ni moja kati ya ndoto za bwana Kalonga.
Careen akiwa amekosa cha kufanya, aliona wale vijana wakimkokota, kuanza kuelekea upande wa ngazi za kushukia chini, alimtazama yule kijana kwa macho ya huruma, nakujaribuku kumweleza kuwa anaitaji msaada wake, ukweli alikuwa tayari mkoba uende maana kama nifedha ata tafuta nyingine, ila siyo kuingiliwa kimwili, maana isinge futika kichwani mwake, nikweli macho yake yalikutana na yule kijana, ambae alikuwa anamtazama kwa macho ya mshangao, lakini bado alikuwa amesimama mlangoni anamshangaa, “unashangaa niniwewe, ebu ingia ndani” alisema Janja ambae alikuwa anamkokota Careen, huku Pengo wakiwa nyuma yao, nikama yule kijana alikeleka nadharau za janja, “inamaana umenisahau, hen?” aliuliza Peter, na wote wawili wakageuka na kumtazama Peter, na hapo ndipo walipo mkumbuka kuwa alifanya hamna kule ofisini kwa Careen miezi kadhaa iliyopita, kumbu kumbu iliyo mjia ni jino lake ambalo limempatia jina la Pengo, ni ngumi nzito ya kijana huyi ambayo ilitua sehemu hiyo ya mdomo na kumpasua vibaya sana.
Wakatoa macho kwa mshangao, “washenzi nyie mbona mnamwonea sana huyu dada, ebu mwachieni haraka” alisema Peter huku ghafla na kwa haraka akimfyetua Emanuel mtama mmoja hatari wa kuto kutegemea ambao ulimzoa na kumrusha juu, kisha ukambwaga chini kama kifurushi, akijipiga kiuno na kuachia kelele ya maumivu, huku akiachia begi la Careen, kuona hivyo Janja akamwachia Careen, ambae alienda chini taratibu, yeye akamfwata Michael, ambae akusubiri Janja amfikie, pale alipo kuwepo, akamrukia teke, ambalo lilitua kifuani kwa Janja, ambatupwa hatua kadhaa nyuma na kwenda kujibamiza ukutani kisha kuanguka chini akifikia uso, na kujibamiza mdomo wake, wakati huo Emanuel pia aliinuka kwa lengo la kukimbia, akukumbuka tena ule mkoba, maana alikumbuka vyema shughuri ya kijana huyu, mwenye mwonekano wa kutoka shamba.
Lakini ile anaanza kukimbia tu, akajikwaa kwenye mguu wa Janja ambae alikuwa ambae pia alikuwa anajiandaa kuinuka, na wote wawili wakajibwaga chini tena nakubamiza nyoso zao sakafuni na kuinuka tena huku wameshikilia nyuso zao, zilizokuwa zinavuja damu, na kuanza kukimbia kuelekea kwenye ngazi za kueleka chini, wakati huo Careen akijaribu kutaa kuelekea ndani ya chumba namba saba, kitendo ambacho Peter alikishangaa na kukiogopa, maana aliofia angekosa cha kujieleza mbele ya mke wake, pale atakaporudi toka kutafuta chakula….

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata