KIAPO CHA MASIKINI (22)

SEHEMU YA 22

ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHILINI NA MOJA: “kumbe wewe ndie ulie mpeleka yule mjinga pale Makimakuluga, ametuaribia kila kitu yule mbwa” alisema Emmanule ambae nusu ampige tena Sada, kwa kosa alilo lifanya, “kwahiyo yule fala ndio Peter?” aliuliza Emma kwa mshangao, wa kuto kuamini, Sada akaitikia kwa kichwa, ungesema anajuwa kilicho mtokea Emma, “yani mjinga mmoja toka kijijini anakuja kuaribu inshu za watu” alisema Emma kwa hasira huku anachukuwa simu yake na kumpiga kwa Hussen…..Endelea……
Simu ambayo iliita sana pasipo kupokelewa, akarudia tena na tena, lakini mambo ni yale yale, simu aikupokelwa, muda wote Sada aliekuwa anajiuliza upotevu wa mamilioni, aliyo yaiba toka kwa Peter, akimtazama mpenzi wake Emma pasipo kuelewa alichokuwa anamaanaisha kuhudu mzazi mwenzie, ya ni baba Michael, “huyu mjinga anawezaje kulala namna hii, wakati mambo yame haribika?” aliongea Emmanuel Msengi, mwenye mapengo mawili ya kufwatana, na kuwa tobo, na siyo pengo kama tunavyo fahamu, “samahani Emma, kwani Peter amefanyaje?” aliuliza Queen kwa sauti iliyojaa uoga na tahadhari kubwa.
Kwanza kabisa Emmanule Pengo mbili, alimkata jicho kali sana Sada yani Queen kisha akaitazama simu yake na ambayo sasa alikuwa anaandika ujumbe, kwenda kwa Hussein, “kumbe yule jamaa ni boya tu, chukuwa vijana wawili mkamvizie pale hotelini, akitoka tu semeni nae, mkiwa watatu awawezi” kisha akautuma na kurushia simu kitandani, “yule mjinga wako, amevuluga mpango tulio kuwa tuna ufukuzia, ya ni mpango wa ela nyingi sana, mpaka sasa boss ametununia” alisema Emma huku na yeye anapanda kitandani, na kujilaza, “msheng..sana yule kumbe ndio amewaaribia, hivyo, bora ata ninge mpa sumu afilie mbali” alisema Sada ambae akufikilia mwanae Michael ataishije, “mh! unajifanya tu hapo, utashangaa baadae hapo unajipeleka kwake, unataka mrudiane” alisema Emma kwa sauti iliyojaa hasirda na chuki, “haa wapi, mimi nikarudiane na yule nyani, nita muweka wapi, yani ata hiyo mwanzo ilikuwa sababu ya utoto tu!” alisema Queen kwa sauti ya kujinasib, nikweli alionekana anamaanisha alichosema, lakini Emma akujibu kitu, aliendelea kutulia pale kitandani, kama vile anasaka usingizi, maana akuwa amelala usiku kucha mpaka sasa kunakaribia kukucha.***
Aya sasa turudi MAKIMAKULUGA Motel, kule ambako kijana Peter alikuwa amelala na mwanae Michael, ndani ya chummba namba saba, chumba walichopelekwa na mke wake, yani mama Michael chumba ambacho awakujuwa ata bei yake, Peter alipoamka akumkuta yule mwanamke, alie msaidia jana, yani yule mwanamke mrembo sana, niwazi alisha ondoka, aikumshangaza sana, kwa kuondoka bila kuaga, maana ukiuachilia kuwa mschana yule mrembo alikuwa na mwonekano wa kitajiri sana, pia nikama akuwa mwongeaji sana, na hawakuwa wanafahamiana.
Ilisha timia saa moja na robo, Peter akiwa ana nawa uso bahati nzuri mswaki na dawa ya mswaki vilikuwa ndani ya chumba hiki, tayari yeye na mwanae walikuwa wamesha oga, maji waliyo yafurahia sana, maji ya juu, maji ya mvua, lakini sasa mambo mawili yakaanza kusumbua kichwa cha Peter, moja ni madai ya mwanae Michael, kwamba anaitaji chakula maana njaa ilishaanza kumchonyota, na jambo la pili ni kwamba, hakuwa amemwona Sada toka alipoondoka ile jana usiku, “inamaana atakuwa amepatwa na tatizo au?” aliwaza Peter ambae akuwa na uwezo wa kupiga simu kwa Sada maana hakuwa na simu, na simu yake aliondoka nayo mke wake huyo, alie aga anaenda kuifadhi fedha na mizigo yao pale mapokezi, “ngoja kwanza nijiandae, nika chukue begi langu pale mapokezi, kisha nitafute njia ya kumpigia, lakini sijuwi wata nikubaria kuchukuwa bego langu, maana mjini wanamambo mengi sana” aliwaza Peter, ambae pia alianza kujihisi njaa, kutokana na kwamba siku mbili hizi hakuwa amekula vizuri, kutokana na hamu ya kumwona mke wake, alie tengana nae siku nyingi zilizo pita.
Peter alijiweka sawa, kisha yeye na mwanae wakatoka kuelekea chini, kule mapokezi, ambako ile anafika tu pale mapokezi, aka kutana na mwanamke mhudumu wa pale mapokezi, ambae ni yule ambae alikuwa anaongea na Sada ile jana usiku, “vipi kaka ndio ulikuwa unaondoka?” aliuliza yule dada kwa sauti ya uchangamfu mkubwa, “ndiyo maana nime ona mama Michael ajarudi, na muda unzidi kwenda, nikaona bora nije mwenyewe” alisema Peter kwa sauti ya uchangamfu, huku moyoni akishukuru kukumbukwa na yule mwanamke mhudumu, “tena umefanya vizuri kuja mapema ilibakia kidogo nikufwate, maana muda wangu umeisha, nataka kukabidhi mahesabu, aya nibasi nipatie fedha niandike hapa” alisema yule mwanamke huku anachukuwa kitabu kikubwa cha mahesabu, na karamu ya wino, “hooo! kumbe akukulipa ile jana, basi nipe begi, ilinikupe fedha yako” alisema Peter pasipo kuwa na wasi wasi, au mashaka yoyote, “begi, unazungumzia begi gani?” aliuliza mwanamke wa mapokezi, huku akimtazama Peter kwa macho ya mshangao.
Hapo Peter alihisi kuwa amekosea sehemu usika, “kwani mizigo yenye fedha uwa wanaifadhi wapi?” aliuliza Peter, ambae aikuwa amemshika mkono mwanae Michael, ambae muda wote alikuwa anasikilizia sehemu ambayo wataenda kupata chai nzito, ikiwa ni mja ya vitu ambayo vilimvutia Michael katika safari hii ya mjini, “mizigo gani unayozungumzia kaka, au niujanja wako wa kukwepa kulipa” alisema yule dada kwa sauti ya kumtilia shaka kijana Peter, ambae sasa nikama alianza kuhisi kilicho mkuta, “samahani dada wala sina lengo ilo, niwamba kwenye maelekezo yenu mlisema kuwa, kama mteja anakitu chenye thamani ya kuanzia laki mbili kiletwe kuifadhiwa hapa” alifafanua Peter, “ndiyo na imeeleza kuwa endapo itapotea kama ujaleta hapa, hotel aitousika, sasa wewe ulileta hapa?” aliuliza mwana dada mhudumu wa vyumba, wa pale mapokezi, “ndiyo mke wangu alileta begi hapa” alijibu Peter kwa kujiamini, “we! kaka unasema alileta mkeo, mkeo yupi, wewe siuliletwa na yule mwanamke jana usiku, akaondoka zake akasema utakuja kulipia mwenyewe, au lile begi alilotoka nalo ndilo ilo unalo semea?” aliuliza yule mwanamke, kwa sauti ya kusuta, na kumfanya Peter amtazame Michael, kwamacho flani hivi, kama vile anataka amwulize jambo, lakini alipokutana na macho ya kiulizo ya Michael, ambae nikama alikuwa na hamu ya kujuwa jambo, Peter akakumbuka madai ya mwanae usiku, ni kuhusu viatu vyake, ambayo mwanzo alihisi kuwa mama yake anaondoka navyo na havitorudi tena, na yeye akampuuzia na kumwita bwege, na sasa alitambua kuwa bwege amekuwa yeye, na siyo Michael, kwakifupi Peter alisha fahamu kuwa Sada amesha mwibia kwa mala ya pili, tena safari hii ni fedha nyingi kuliko zile za kwanza, ata simu yake pia ilisha ibiwa na huyo huyo mzazi mwenzie.
Hapo Peter akajikuta anashikwa na uchungu mkubwa sana, alitamani kulia kwa sauti kubwa, kutokana na uchungu aliokuwa nao, “Sada kumbe nia yako ilikuwa ni kuniibia tena, nimekukosea nini lakini?” alisema Peter na kwa sauti iliyojaa uchungu mkubwa, na baada ya kuangua kilio kwa sauri baada yake akajikuta anaachia kicheko afifu, huku macho yake yaki bubujisha machozi, “we kaka acha usanii wako, ebu toa fedha za watu, nikabidhi nikapumzike bwana” alisema yule mwanamke, kwa sauti kavu ambayo aikuwa na chembe ata moja ya huruma, Peter hakuwa na jibu lolote, zaidi ya kutulia kimya, akifikilia jinsi atakavyo ingia kijijini Mwanammonga katika hali ya kukabiliana na macho ya wanakijiji wenzake, pamoja na wazazi wake, ambao waliomuonya swala la yeye kuwasiliana na Sada, asa watakapo fahamu kuwa ameibiwa fedha zote, alizo ziangaikia kwa jasho na ugumu, aking’oa visiki na kuchimbua ardhi kwa jembe la mkono, huku mikono ikipata malengelnge, kabla aija pata sugu, na mipasuko kama njayo za mwenda peku, “we anko, lete fedha ya watu, usijifanye umebung’aa hapa” alisema yule mhudumu kwa sauti ya kupayuka, kiasi cha kuwafanya wahumu wenzake na vijana ambao wanafanya kazi pale hotelini kama walinzi na waangalizi wa usalama, wakasogea ilikujuwa kinachoendelea, “vipi hapa kuna nini, au anajaribu kukutaperi?” aliuliza mmoja kati ya walinzi waliosogea pale mapokezi, “anasema ameibiwa na mwanamkea liekuja nae jana, na amelala namba saba ya VIP, anadaiwa laki moja” alisema yule mhudumu, na hapo ukazuka mjadara mkubwa huku wafanyakazi wa pale wakiongezeka, pale mapokezi, “basi tupige simu polisi, vinginevyo nani atalipia laki moja” alisema mmoja wa wahudumu, mmoja mwenye kimbele mbele huku anatia simu yake na kupiga kwa mtu flani ambae ni wazi alikuwa ni askari wa jeshi la polisi, na hapo ndipo Peter alipozinduka toka kwenye mawazo yake, ambayo yalikuwa ni afadhari kuliko kile ambacho kinaenda kumtokea sasa, na kingine ambacho kilimshtua zaidi ni kwamba, Sada licha ya kujuwa anataka kumtaperi, lakini bado akampeleka kwenye hoteli ambayo inakodisha vyumba kwa bei ya ghari sana.
Hapo Peter akaona kuwa ni wazi sasa anapelekwa kituo cha polisi kwa mala ya kwanza, na mbaya zaidi yupo na mwanae “sahamani jamani naomba msinipeleke polisi, nisaidieni mawasilino niwapigie simu nyumbani, wanisaidie hizo laki moja” alisema Peter, na hapo mhudumu mmoja akajitolea simu yake.
Kwanza Peteralianza kuipiga namba yake, maana namba ya Sada hakuwa ameishika kichwani, lakini simu yake aikuwa inapatikana, na bahati nzuri kwake, alikuwa anaikumbuka namba ya baba yake, akaiandika kwenye simu na kuipiga, nayo ikaanza kuita, aikuchelewa kupokelewa, “hallow nani mwenzangu” ilisikika sauti ya mzee Jacob, upande wapili wasimu, “ni mimi baba ni mimi Peter, shikamoo” alisamilia Peter, kwa sauti iliyojawa na haraka, “hoooo! kumbe umenunua simu mpya, mama yako alikupigia jana huku patikana, vipi lakini mnaendeleaje huko?” aliuliza mzee Jacob yani baba yake Peter, ambae alionekana kuwa bado alikuwa kitandani, “simu imeibiwa baba, na hapo nipokwenye matatizo makubwa naomba unisaidie” alisema Peter, na kuanza kumweleza baba yake kwakifupi kuhusu mkasa uliomkuta, lakini kabla aja maliza kueleza simu ikakatika, na alipojaribu kupiga tena simu aikupatikana, “unaona sasa atahuyo baba yako sijuwi nani amekuzimia simu, bwana ee sisi hatuna la kufanya inabidi uende kituoni, ukae huko mpaka ndugu zako watakavyokuja kukulipia” alisema mmoja, ambae alionekana ndie kimbele mbele “lakini tungempa muda iliafanye mawasiliano na ndugu zake” alisema mwingine na yule mwenye kmbele mbele, ambae alikuwa ni mfanyakazi wa hotel mwenye jinsia ya kiume akadakia, “bwana ee mimi nimesha piga simu polisi, wapo njiani wanakuja” alisema yule jamaa na akati huo huo wakasikia ngurumo ya gari likiingia kwa kasi ya hajabu pale Hotelini, na kufunga brake za ghafla, kusotesha tairi zake kwafujo, “tena haoooo! wamesha ingia”……

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!