
SEHEMU YA 24
ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHILINI NA TATU: aliuliza Jasmini ambae aliona kama vile kunajambo wanajaribu kuwaficha, polisi manager na wenzake wakatazamana, kwa macho ya mashaka, na mshangao, “we dada una uhakika kama yeye ndie mgeni wa yule mama wa dhahabu, au mmemfananisha, kwani alilala chumb anamba ngapi?” aliuliza Bakari ambae alionyesha kuto kuami, na kumdharau sana Peter, “ndiyo kaka yangu, boss wangu anamgeni hapa, alilala chumba namba saba ghorofa ya tatu, yupo na mtoto mdogo” alifafanua Jasmin, kwa sauti ya upole, Bakari akatoa macho kwa mshangao,”aiwezekanani, lazima mtakuwa mme changanya, kama vipi wakamtoe huko huko kituoni” alisema Bakari, ungesema alikuwa na ugomvi mkubwa na Michael……… Endelea…
ambae sasa alikuwa ameshikiliwa na polisi pale mlangoni, “sahamani jamani tunaweza kukutana nae au kuna tatizo limetokea?” aliuliza Jasmin kwa sauti ya upole, huku yeye na wenzake wakionekana kuingiwa na wasi wasi juu ya ile kinachoendelea maali pale.**
Naam baba na mama Peter sasa walikuwa njiani wanatembea kuelekea sehemu ambayo wangepata boda boda, za kuwapeleka wilani namtumbo ambako wangepata usafiri wa kwenda songea mjini, lakini kabla ya kufika popoye walipanga kwanza kupitia nyumbani kwa mzee Nyoni, kueleza hisia zao juu ya kile ambach binti yao amekifanya kwa kijana wao, pengine walizania inaweza kuwa njia ya wao kumpata Peter kilahisi.
Nikweli walifanikiwa kuwakuta wazazi wa Sada, ambao ndio kwanza walikuwa wanajiandaa kupata kifungua kinywa cha chai na mihogo, “karibuni jamani, inapendeza kwakweli, vijana kurudiana jana tu, leo mnatutembelea mapema mapema” alisema mama Nyoni wakati mzee Nyoni mwenyewe akiwa anatoka nje na kikombe mkonononi, “karibuni jamani, karibuni sana, sasa nayaona matunda ya watoto kupatana” alisema mzee Nyoni, au baba Sada, kama tunavyo mfahamu, “bwana Nyoni, nazani juhudi za Peter kumrudisha Sada katika familia yake ili walee mtoto, zime kwama na kuleta matatizo zaidi” alisema mama Peter, hapo bwana Nyoni na mke wake wakatazamana, kwa mshangao, “mh! kivipi tena, Peter alifika hapa na kutueleza kuwa, anaenda kukutana na Sada, kwani unasema imeleta matatizo?” aliuliza mzee Nyoni kwa mshangao na mshtuko, “Peter ameibiwa kila kitu, mpaka simu, na ameazima simu kutupigia, anasema yupo kwenye matatizo na anaitaji msaada wetu” alisema mzee Jacob na hapo mzee Nyoni na mke wake wakatazamana kwa sekunde kadhaa, kisha wote kwa pamoja wakaangua kicheko kikubwa sana, cha kebehi na dharau, “nilijuwa tu, mshamba akienda mjini lazima wamkaribishe” alisema mzee Nyoni, huku yeye na mke wake, wanaangua kicheko kikubwa cha kuudhi, “niushamba, anamwingiza Sada, mwenzie ni mtoto wa mjini, na amesomea” alisema mke wa mzee Nyoni, yani mama Sada, “sawa naona mnafurai kwakilicho mkuta Peter, lakini naomba isije kuwa, huyo mtoto wenu wa mjini, ndie anaeusika na kilicho mpata mwanangu na mjukuu wangu, hakika nita mpeleka jela mchana kweupeee” alisema mama Peter, kisha akamshika mkono mume wake, na kumvuta ili waondoke kuelekea barabarani kuchukuwa boda boda, huku wakiwaacha mzee Nyoni na mke wake wakiendelea kucheka, “kwani Sada ndie alie mfunga kamba mtoto wao mjinga, yeye mwenyewe na upumbavu wake, eti hooo! mama! mimi naenda mjini, nitakutana na Sada” alisema mke wa mzee Nyino, huku akigiza sauti ya Peter kwa kubana pua, na aliongea ilo kwa sauti ya juu, ili mzee Jacob nana mke wake wasikie****
Hapo koplo wa polisi na akamtazama manager, kama vile anamwuliza kuna aja ya kukaa kimya, na kama vile manager hakuwa na jibu, polisi akawatazama wale polisi wengine waliokuwepo pale mlangoni, wamemshikilia Peter, ambae tayari alikuwa amevishwa pingu, na mwanae Michael alikuwa amemshikilia mguu, pasipo kumwachia baba yake, huku kilio cha nguvu kikimchomoka mdomoni, “mleteni huyo jamaa hapa” alisema yule polisi koplo, na wale polisi wengine wenye cheo cha constable, wakamsogeza Peter pala mapokezi, “je anaweza kuwa ndie huyu?” aliuliza yule polisi koplo mala baada ya Peter kusogezwa mbele yao, “sina hakika, ila kama mna hakika ndie alie kodi chumba namba saba, na alikuwa na mtoto mdogo, basi ndie yeye” alisema Jasmini, huku ana mtazama Peter, ambae kiukweli kwamwonekano wake japo alikuwa na umbo lakuvutia la kume lakini hali yake ilionekana wazi kuwa ni ya hali ya chini na duni sana, pia mshamba asie juwa lolote juu ya maisha ya sasa, ata mtoto wake ambae pia alikuwa anaanza kufwata umbo na sura ya baba yake, alionekana kuwa mfano wa mtoto alie kulia kwenye mazingira ya kijijini kabisa, tena kijiji cha mbali sana.
Mpaka hapo Peter alishagundua kuwa, watu awa watatu wenye kuvalia na kupendeza walikuwa wanamuulizia yeye, je watumwa na nani, “nyie ni wakinani, au mme tumwa na Sada vipi fedha, simu na nguo zetu zipo wapi?” aliuliza Peter ambae alikuwa amefungwa pingu kwa nyuma, “naviatu vyangu vipya?” alikumbusha Michael ambae sasa alikuwa anapunguza kilio chake, wakati huo wakina Janja walikuwa wanashuhudia kinachoendelea, “hapana sisi tume tokea #mbogo_land sonara, tume agizwa kukufwata, na kukupeleka nyumbani kwa Madam Careen” alisema Jasmini, kwa sauti iliyojaa nidhamu ya hali ya juu, watu wote wakashangaa sana kuliko walivyo shangaa mwanzo, ata Peter nae alishangaa kwakuona watu wote wanashangaa hivyo, tena huku wakitazamana usoni, siyo wale wahudumu peke yao ni ata wale polisi pia, walikuwa wameshikwa na mshangao.
Ukweli mni kwamba, kwa watu ambao ni wenyeji wamkos huu, na wanao fahamu kuhusu Careen, au mama wa dhahabu, apakuwai ukaribishwa mtu mwingine asa mwanaume ambae siyo wa jamii yake, yani toka #mbogo_land king dom, pia ata wafanyakazi wakiume wa nyumba ile, ambao nao ni wenyeji toka mbogo land, walikuwa luhusiwa kuishia flow ya chini tu, kama wangelazimika kupanda ghorofani, basi ni lazima wange pewa luksa maalumu, ya kuvuka ngazi za kupandia huko, kwahiyo Peter ndie mwanaume mtu wa kwanza kusikika kuwa anakaribishwa nyumbani kwa mwanamke huyo, ambae siyo upole pekee, ila ni kwamba akuwa na muda waongea na mtu mwingine, zaidi ya mambo ya kikazi pekee, “hapana siyo mimi, mtakuwa mme kosea, sina mtu mwingine ninae mfahamu zaidi ya Sada, alie kumbia na begi langu lenye fedha, na nguo zetu” alisema Peter, ambae bado alikuwa na pingu mkononi, “sahamani muungwana pengine unaitaji kukumbuka kidogo, ukumbuki kuwa jana ulikutana na mschana mmoja mrembo, wenye kuvaa vito vingi vya..” alisema Jasmin na kabla aja malizia, Peter akadakia, “hoooo! unasema yule dada mzuri, ambae awezi kuongea, nikweli nilimsaidia jana na ali…” nazani Jasmini alijuwa kuwa Peter anataka kusema kilichotokea, ndio maana akamkatisha, “ndiyo huyo huyo, je unatatizo lolote, maana naona hupo chini ya ulinzi wa polisi?” aliuliza Jasmin, na hapo Peter akajieleza jinsi ilivyo kuwa, mpaka akatapeliwa na Sada, ambae ni mzazi mwenzie, “leo asubuhi nagundua kuwa hakulipia chumba nilicholala, ameondoka nasimu na pia ameondoka na fedha zangu na vitu vyote, vilivyokuwepo ndani ya begi” alieleza Michael, huku watu wote wakisikiliza, pamoja na Bakari ambae alionekana kutopendezwa na matokeo yanayotaka kutokea, “ok! ilo siyo tatizo, wacha tuwasiliane na ofisi, ili malipo yafanyike kwa njia ya benk, si itakuwa sawa?” aliuliza Jasmini, huku anatoa simu na kupiga ofisini kwao, kwenye kitengo cha dharula, huku polisi wakimfungua pingu Peter.
Husein na wenzake wawili, wakishuhudia kinachoendelea, “kumbe huyu fala ata akuwa anamfahamu yule demu?” aliuliza kwa mshangao na chuki ya hali ya juu, unajuwa kwanini, ukiachilia kuwa yeye Janja na Emma walikuwa wanamfwatilia sana Careen ili kumwibia na pengine kumteka wampeleke kwa boss wao akambake, lakini pia wote wawili walikuwa wanamfahamu vyema mschana huyu, kuwa ni mrembo na tajiri wanguvu, na hakuna kijana wa ambae, akuwa anatamani japo kuwa kumfungulia mlango wa gari Careen akachukuwa simu yake na kumpigia Emmanuel.***
Mida hii ndiyo mida ambayo bwana Kalonga alikuwa anamfulia mlango mschana mmoja ambae akumjuwa atajina, ni yule alie letewa jana usiku, baada ya kumkosa Careen, ukweli licha ya kukesha na mwanamke huyu usiku kucha, akila kitumbua kwa vitu alivyo tumia, ikiwa ni maandalizi ya kukomoa Careen, lalini bado roho ilimuuma kwa kuona kwamba anashindwa kumthibiti mwanamke huyo, ikiwa yeye ni mtu ambae anasifika kwa kufanikisha mipango ya hatari, “ujinga nime kosa fedha nime kisa dhahabu, na mwanamke pia nimemkosa” alisema Kalonga kwa sauti ya juu, iliyojaa hasira, “hapana lazima lifanike jambo, huu sasa ni upuuzi, inakuwaje awa kijana mmoja mpuuzi awashinde majemedari wangu, anauwezo gani huyo mpuuzi?” aljiuliza Kalonga, ambae toka lile tukio la kwanza alitamani sana kumwona huyo kijana alie mwingilia kwenye mambo yake, na pengine amtia mikononi na kumwadabisha, “ila dawa ni ndogo tu, ngoja ni mpigie huyu malaya, nimchimbe mkwala” alijisema Kalonga, ambae licha uharifu wake wote, lakini akuwai kutia hatiani, kutokana nakukosekana kwa ushaidi, nah ii nisababu kuna mtu alikuwa anamsaidia, kufanya anayo yafanya.***
Naam mtaa wa Zanzibar mbele ya jengo kubwa la biashara la #mbogo_land, sonara, palionekana kujaliwa na watu wengi sana waliokuwa wanaingia na kutoka ndani ya jengo ilo kubwa la ghorofa mbili, kufanya manunuzi yao, ndani ya jengo ili kulikuwa na watu wengi sana, toka sehemu mbali mbali, wakifanya manunuzi yao, wapo waliokuwa na familia zao, yani baba mama na watoto, au mke na mume, wachumba au marafiki, pia wapo waliokuwepo mama mtoto, baba na kijana wake, ikiachilia hao, pia walikuwepo waliokuja hapa wakiwa mmoja mmoja. ………
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU