SEASON 2: KIAPO CHA MASIKINI (33)

SEHEMU YA 33

ILIPOISHIA SEHEMU YA THERATINI NA MBILI: kule kijijini kuna mashamba yangu, na msimu wa kuandaa unakaribia, nita mwachia nani, labda ningekuwa nimesha maliza kilimo” alisema Peter, lakini aikuwa jibu sahihi, “ilo siyo tatizo, kwani kule kijijini akuna watu ambao unaweza kuwalipa waka lima shamba lote, au kutumia tractor kulima?” aliuliza yaya, na hapo Peter alicheka kidogo, “mama usinichekeshe, mimi mwenyewe ndie ninae lima kwenye mashamba yawatu, sasa nitawezaje kukodi mkulima” alisema Peter, kwa sauti ya mshangao. Endelea…
Na kujidharau, “kwani kigumu nini, kama uamini we tulia hapa mjini, utaona, ujuwe upaswi kuwa na wasi wasi kwanini tunaitaji ubakie hapa mjini, nikwamba Careen anakuamini kuwa unaweza kumlinda kwa wale vijana walio mvamia jana” alisema yaya Groly na hapo nikama alimfumbua masikio Peter, “hoooo! kumbe, basi akuna shida mama, ila ninaomba uniazime simu yako niongee na baba, maana toka asubuhi simu ilipokatika sijaongea nae tena, pia nitaomba nitoke kidogo, nikashangae shangae, maana sijawai kutembea kabisa huku mjini” alisema Peter, na kabla ajamalaiza kuongea tayai yaya Groly alishatoa simu yake, na kumpatia, “nazani utakuwa unaikumbuka namba yake” alisema yaya Groly wakati anampatia simu Peter, “ndiyo namba ya pili kuikalili ukiachilia namba yangu” alisema Peter, huku anapokea simu, ambayo aliitumulia macho, asijuwe la kufanya, maana licha ya kuwa ni ya kugusa, yani tachi, kama ya mkewake, lakini hii ilikuwa ni ya kisasa zaidi, akuwaikufikilia kama kuna matokeleo zaidi yamesha toka ya simu kama hizi, ambazo kuna watu wanaita za kupyatila, au za kupapasa, “naomba uniandikie namba” alisema Peter, huku anarudisha simu kwa yaya Groly, ambae aliipokea na Peter akamtajia namba, ambazo aliziandika na kupiga zile namba, lakini kwa bahati ambaya simu ilikuwa aipatikani, “basi ata kuwa bado anaichaji” alisema Peter, “kwanini usimwachie ujumbe iliakichaji, aukute” alishauri yaya Groly, na Peter akaelekezwa namna ya kuandika ujumbe, na yeye akaandika ujumbe mrefu sana, kama barua, kisha akautuma kwenda kwa baba yake, na kurudisha simu kwa yaya Groly, “Peter ukiwa tayari kwenda kutembea nijulishe” alisema yaya Groly, kabla ajaenda kumwonyesha chumba chake, ni kingine tofauti na kile cha mwanzo, maana chumba kile kiliandaliwa kwaajili ya Michael, kitu ambacho kilimshangaza sana Peter, “lakini Michael ataaribu godoro kwa mikojo” alisema Peter, akimweleza yaya Groly, ambae aliishia kucheka, “wala usijari kuna vifaa vya kuzuwia mkojo usifike kwenye godoro” ndivyo yaya Groly alivyo mweleza Peter, ambae licha ya kuonyeshwa chumba kizuri chenye kila kitu, tena vitu ambavyo akuwai kuvifikilia, lakini akupata ata muda wa kupumzika, maana alikaa kwa muda wa nusu saa, kabla ajafwatwa kwaajili ya chakula cha mchana, ambacho alisema atoweza kula, sababu alikuwa bado ameshiba, mwanae Michael alikula vizuri tu, kisha akaogeshwa na kupelekwa chumbani kwake kulala, wakati huo bwana Peter, anaenda kwa yaya Groly kuaga, kwamba anaenda kushangaa mji huu, ambao kila alipoingia, alikutana na majanga.***
Naam mida hii ya saa saba za mchana, mwana dada Careen alikuwa ofisini, ametulia kama vile akuwa na kazi yoyote ya kufanya, lakini ukweli alikuwa na lundo la kazi mezani kwake, maana ukiahilia kufanya majumuisho ya mzigo ulio uzika mpaka muda ule, na makusanyo ya fedha zilizo kuwa mezani kwake, pia alikuwa na nyaraka nyingi za mapendekezo na maitajio ya vitu ambavyo, wateja wake walikuwa wanaviulizia mala kwa mala, vitu ambavyo aliitajika kuviagiza toka nchini kwao #mbogo_land.
Usowake ulionekana kujawa na mawazo flani, ambayo kwa haraka ungeshindwa kuyatabiri, kama ni ya uzuni na wasi wasi, au yafuraha, maana kuna wakati ungemwona akiwa amenyongea, na kuna kwati ungemwona anatabasamu peke yake, na kuichukuwa simu kutazama kama kuna ujumbe au chochote ambacho kimeingia bila yeye kukisikia, akini hakukuwa na lolote, hivyo angegusa karatasi mbili tatu, akisoma maitajio ya vitu ambayo wateja wake walikuwa wanaviitaji kwa wingi na pengine pale dukani kwake havipo, “najuwa yaya Groly ata mshawishi abakie” aliwaza Careen huku anaachatena karatasi mezani, “akibakia nitafanya nini, ili niombe kuwa mchumba wake?” aliujiuliza Careen, huku uso wake ukivaa unyonge, na vipi kama ajavutiwa na mimi, nab ado anampenda huyo mke wake alie mfanyia ukatili?” alijiuliza tena Careen, ambae sasa akuweza tena kuendelea na kile alichokuwa ankifanya, “lakini ni mwanaume mmoja tu, ambae akuona uzuri wangu, nae ni kwavile alinichukulia kama dada, naamini ata yeye wakati ukifika ata naimbia ananipenda” aliwaza hiyo mwana mama wa dhahabu, huku anaachia tabasamu zito, na akiwa katika hali hiyo simu yake ikaita, alipoitazama alikuwa ni yaya Groly, akaipokea simu yake kwa haraka, tofauti na utaratibu wake wasiku zote, maana uwa antumia ata sekinde therathini mpaka kupokea simu, “niambie yaya, vipi Peter amekubari?” aliuliza kwa pupa yenye wasi wasi mwingi, hapo kikasikika kicheko toka kwa upande wapili wa simu, “mwanangu weee, mgeni wako yupo na ataendelea kuwepo, amesha tuma ujumbe kwa wazazi wake kuwajulisha kuwa yupo mjini, hapo ni sisi kuendelea kumshawishi aendelee kuwepo hapa mjini” alisema yaya Groly, na hapo Careen akaachia tabasamu pana usoni mwake, “sawa yaya, basi jitaidi wapate vitu vingi sana mpaka watamani kuendelea kukaa hapa mjini, mimi nitakuja na nguo zao, na vitu vya kuchezea mtoto” alisema Careen kwa saharaka haraka, huku anatoka na kuelekea kwenye store ya nguo na viatu, simu ikiwa sikioni, “sawa sisi tunawaandalia chakula kizuri kwaajili ya jioni, itapendeza mkila tena pamoja” alisema yaya kabla awaja agana na kukata simu, huku Careen akiwa nauso wa furaha, akiwaacha wafanyakazi wake wakijiuliza kuna nini leo kwa boss wao.**
Naam saa kumi na robo, za jioni, wakiwa na uchovu wa safari na mawazo, juu ya kilichoendelea watokea Peter na Michael huko mjini, mzee Jacob na mke wake, walifika nyumbani kwao na kuanza pilika pilika za kuwasha moto, na kubanika nyama ambayo waliinunua mjini, ikiwa ni kishushio cha bia walizo zinunua pia, huku wakiwa wameacha simu dukani kwaajili ya kuichaji, “yani mama Peter, mi mwenzio ata sielewei elewi, nahisi kama yule binti ametudanganya tu” alisema mzee Jacob, ambae alikuwa amekaa juu ya sturi ndogo, huku ameshikilia chupa ya bia akimtazama mke wake alie kuwa anaweka pande la nyama juu ya jiko, lililokolea moto wawastani, “yani baba Peter, mimwenyewe ata sielewi, nahisi kabisa yule binti ametudanganya, na nilivyo mwona na yale makovu, kama jambazi, tayari atakuwa amesha muibia Peter, alisema mama Peter, kwa msisitizo huku ana maliza kuweka nyama jikoni, kisha aka vuta kigoda karibu na mume wake, kisha akachukuwa chupa moja ya bia na kumpa mume wake amfunulie kwa meno, “tatizo huyo mwanao nae, sijuwi amelishwa nini, yani mechanganyikiwa na lile linunga yembe” alisema mzee Jacob, kwa sauti iliyojaa hasira, ila kama lime mpata jambo, lazima ata kuwa amejifunza kitu” alima mzee Jacob, huku anampatia mkewake chupa ya bia iliyofunguliwa ‘ila tunge zubaa tu, ingetupata kitu” alisema mama Peter, na wote wakacheka.****
Naam saa kumi na robo, ilimkuta Peter, akiwa mita chache toka kwenye gate la nyumba ya Careen, akiwa anaelekea upande wa mjini, huku mfukoni akiwa na elfu hamsini fedha ya kitanzania, ambayo alipewa na yaya Groly wakati alipokuwa ana muaga, kwamba anaenda kutembea, ukweli alikuwa ametoka kuwaza juu ya Sada, kwahiyo aliitafuta namba yake ili amuibie, na kama ndiyo hivyo, kwanini alimwibia kila kitu pasipo kufikilia juu ya mtoto wao, “inamaana Sada ndio amekuwa mwizi kiasi hiki, anaiba aya nguo na viatu vya mwanae” aliwaza Peter ambae mwanzo akujuwa aingilie wapi atokee wapi, huku kichwani mwake, akiilenga ile sehemu ambayo alifikia jana, na kupata bia, kala ajakutana na Sada, pengine anaweza kuutana na mke wake huyo wa zamani, nikimwona boda boda nita mwambia anipelee huko” aliwaza Peter.**
Wakati huo huo, Sada na Janja nao, walikuwa wanatoka nyumbani kwa Emma, yani kule Mahenge, na kuelekea mjini wakipanga kuelekea mtini pub wakanunue bia, ili Queen akanywe nyumbani na mpenzi wake Emma, “yani ata sielewi wale vikongwe wali shtuka vipi” alisema Sada kwa sauti ya kujilahumu, “tatizo huku niambia mapema, ningeenda kuwapora lile begi live live” alisema Janja, alie kuwa anaendesha gari, “mimi nilitaka niwazungushe kidogo alafu tukawalewe viaya sana, na wengelewa tu, wangeamka asubuhi awana kitu” alisema Sada ambae janja ana mfahamu kama Queen, na wote wakacheka kama malofa, huku safari ikiendelea, kuelekea mjini, ila shem umepoteza fedha nyingi sana, ilikuwaje ukalewa mpaka ukazima gari?” aliuliza Janja, kwa namna ya kulahumu, “yani we shem acha tu, yani roho inaniuma” alijibu Sada, akionyesha ni mwenye machungu mengi sana.**
Naam saa kumi na nusu, ndio muda ambao mwana dada wa dhahau yani Careen alikuwa anaingia ndani ya gate lake kubwa lenye rangi ya dhahabu, na kusimamisha gari, akashuka huku akipokelewa na wafanyakazi wake kama ilivyo kawaida, walipokea mabegi mawili makubwa ya nguo, na mabox ya vifaa vya kuchezea mtoto, huku Careen mwenyewe akitangulia ndani kwa mwendo wa haraka akitegemea kumwona Peter, lakini hakumwona na baada yake akamwona yaya Groly alie kuwa anamsubiri kwa hamu sebuleni, “yupo wapi?” aliuliza Careen kwa sauti ya kunong’ona huku akiachia tabasamu, “ametoka mala moja ameenda kutembea, nimempa elfu hamsini akanunue vitu vyake muhimu” alisema yaya Groly, kwa sauti ya chini pia.
Kwakusikia hivyo Careen akashtuka na kubarika sura kwa ghafla, “ameenda wapi, na nani, yani ….. yani….. amepelekwa nani?” aliuliza Careen kwa mshtuko, “yeye ni mwenyeji huku, ameenda peke yake, ila mwanae yupo juu” alisema yaya Groly, kwa sauti iliyopoa kidogo, maana aliona mabadiliko ya Careen, “namaanisha ameenda na gari gani?” aliuliza tena Careen, sasa kwa sauti ambayo ilikuwa kama inawasi wasi, “ameenda kwa mguu” alijibu yaya Groly kwa sauti ambayo ilizidi kupoa, “hapana yaya atakiwi kutembea kwa mguu, amesema anaenda wapi, niambie yaya, nimfwate” alisema Careen huku anageuka na kuanza kutembea kutoka nje….

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata