
SEHEMU YA 36
ILIPOISHIA SEHEMU YA THERATINI NA TANO: “umekutana na mke wako Peter” aliuliza Careen kwa sauti tulivu ya upole, “ndiyo nimekutana nae” alijibu Peter kwasauti tulivu, huku akiwa kama amekumbushwa machungu, “umesha msamehe?” aliuliza Careen ambae jibu la Peter liliushtua moyo wake, “yes nimesha msamehe” alijibu Peter, huku akijaribu kujiweka katika hali ya kawaida na siyo ya udhuni, lakini aikuwezekana, Careen alijikuta akipunguza mwendo, sijuwi kwanini jibu lile lilimkosesha amani kiasi kile.…. Endelea…
Na kabla ajauliza lolote, akamsikia Peter akiendelea kuongea kwa sauti ya udhuni, “nime msaheme, maana sina la kumfanya, na yeye anaitaji mwanaume mwenye fedha nyingi na tajiri” alisema Peter kwa sauti iliyo jaa uzuni, “kwahiyo… kwahiyo mmesha achana, “aliuliza Careen kwa sauti ambayo ilikuwa inaficha furaha yake, “ndiyo, na ninachosikitika zaidi, sidhani kama nitakuwa na ujasiri wa kumweleza Michael kiapo cha mama yake” alisema Peter, kwa akionyesha kusikitishwa na kile kilicho tokea, “ametoa kipao gani?” aliuliza Careen ambae alionyesha kuitaji kusikia kilichotokea, kwa mgeni wake, ambae akusita kusimulia kilichotokea, na jinsi maongezi yake na Sada yalivyokuwa.****
Naam mzee Jacob, akiwa na simu sikioni, akisibiri kuongea na Michael, alie ambiwa kuwa alikuwa ghorofani, aliwatazama wenzake huku amaeachia tabasamu pana kweli kweli, “anampelekea simu Michael yupo ghorofani” nikama alinongona, lakini ukweli ni kwamba sauti ile ilipenya upande wapili wasimu, maana aliongea kwa sauti iliyosikika wazi kabisa, “aya mzee huyu hapa ongea nae, ilisikika sauti ya mwanamke mtu mzima, na aikuishia hapo akasikika akimsemesha Michael pia, “Michael, njoo uongee na babu” ilisikika ile sauti, wakati huo mzee Ngongi akimpola simu mzee Jacob, na kubofya kitufe cha kuwekea speeker za wazi, loud speeker, na wote wakaanza kusikia sauti za upande wapili, “babu wa Mwanamonga?” ilikuwa ni sauti ya ya kitoto ya Michael, hapo mama Piter akadakia, “nipo na mimi bibi yako” nazani upande wapili pia walikuwa wameweka loud, maana Mchael akadakia, “shikamoo bibi” kabla ata bibi, yani mama Peter ajaitikia mzee Jacob akaingilia kati, “niamkie na mimi Michael” alisema mzee Jacob, babu wenzio viatu vyangu vile alivyo ninunulia baba, vimeenda” alisema Michael kwa sauti ya kusemelea, “vimeenda wapi?” aliuliza mama Peter, “baba amempa yule mwanamke” alisema Michael, na hapo yakafwatia maongezi machache, huku Michae akisifia kuwa alikuwa kwenye nyumba nzuri, anafaidi kuangalia video, na kubembea, “hoooo mpo kwa nani hapo?” aliuliza mzee Ngongi, “tupo kwa shangazi mzuri mzuri” alisema Michael, na wazee awa wakajikuta waicheka kwa furaha, “sasa mnakuja lini?” aliuliza mzee Jacob, “mi sijuwi” ilikuwa ni sauti ya kitoto, ya Michael iliyojibu.**
Hakiwa amesha sahau kilicho tokea Mtini Pub, Sada au Queen alifika nyumbani kwa Emma kule Mahenge, akiwa na fuko la bia, na chakula alicho nunua pale mtini pub, alimkuta mpenzi wake, Emma akiwa anamsubiri kwa hamu, “bora ume fika maana hiibaridi ilisha aanza kuniletea maumivu” alisema Emma huku anachomoa chupa moja ya bia na kuifungua kwa kutumia kingo ya kitanda, alafu akaipelekea mdomoni, na kupiga funda moja dogo la majaribio, nazani jaribio lilienda vibaya, ni baada ya bia kukaa kwenye pengo jipya, maana ghafla Emma akakunja uso kwa maumivu, “huuuu haaaaa” alilalamika Emma, huku akiaminishia maji ya bia upande wa kushoto, ambako akuna pengo, na kumeza lile funda, kwa fujo, “dah! afadhari, nitanywea upande huu” alisema Emma, akionyesha upande wa kushoto wa mdomo wake, “ukinywa mbili tu, tayari maumivu yamekata” alisema Sada, huku ana fungua bia yake kwa mtindo ule ule ambao Emma aliutumia, yani kufungulia kwenye kingo ya kitanda, na upiga funda moja la nguvu, “Janja alikuacha na kuondoka?” aliuliza Emma, hku wakiuendelea kunywa bia zao, “ndiyo alisema anakazi ya kufanya” alisema Queen, ambae nikama alikumbuka kitu, “alafu kuna kitu nimekumbuka Emma, nimekutana na yule mjinga, nimemtukana kama simjuwi” alisema Sada, akiwa na lengo la kumfurahisha mpenzi wake Emma, huku akijitengenezea uaminifu na kuonekana kumwonyesha Emma amempa nafasi kubwa kiasi gani, “umekutana na nani, yule bwana wako wakijijini?” aliuliza Emma kwa sauti iliyo jaa dharau, na chukji, “huyo huyo mshamba, eti hooooo namba turudiane, tukalee mtoto, nikamwambia weeee! unikome, tena utajijuwa na mwanao” alisema Sada kwa sauti iliyo jaa uzani wa majivuno na sifa, “kumbe bado yupo hapa mjini, unge nipigia kunijulisha” alisema Emma kwa sauti ya kulahumu, “simu nimeibiwa jana, nitanunua line niweke kwenye simu ya ya Peter” alisema Sada, huku sauti ikipoa kidogo, “yani ukimwona tena niambie mala moja, huyu mshenzi lazima alipie alicho kifanya” alisema Emma kwa sauti iliyojaa machungu na hasira, “usijiri Emma, tutampata tu, tena ukizingatia hapa mjini awezi kuwa na sehemu ya kukaa, atakuwa anatanga tanga tu” alisema Sada, akiwa anaamini anacho kiongea.**
Naam maelezo ya Peter, japo yalikuwa ni yakuudhunisha, lakini kiukweli ilimfurahisha sana Careen moyoni mwake, japokuwa usoni, alionekana kama amenyongea, “pole sana Peter, unaitaji kumsahau kwa sasa, siyo mtu sahihi kwako” alisema Careen wakiwa wanashuka toka kwenye gari, ni baada ya kufika nyumbani kwa mama wadhahabu, huku wakipokelewa na wafanyakazi wa Careen, “siwezi kumsahau kwa kile alicho nifanyia, ila nimesha mtoa moyoni mwangu” alisema Peter kwa sauti yenye kumaanisha, hapo Careen akachia tabasamu pana, huku wanaingia ndani na kupandisha ngazi kuelekea ghorofani, “ambako walikutana na yaya Groly, alie kuwa anashuka ngazi, “yaya tuandalie bustani, chakula cha jioni mimi na Peter tuta kula huko” alisema Careen, ambae baada ya kufika kule juu akaagiza Peter na Michael wapewe zile nguo alizokuja nazo, “Peter utavaa bukta na tishet zipo huko ndani” alisema Careen huku anaelekea chumbani kwake, “asante sana” alisema Peter huku akimsindikiza kwa macho mwana dada huyu mrembo ajapata kuona mfano wake…..
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU