
SEHEMU YA 39
ILIPOISHIA SEHEMU YA THERATINI NA NANE: “kwani mzigo wenyewe hupo wapi?” aliuliza yule jamaa, mzigo bado hupo Linjumbwi, ndio unavinwa” alisema Kalonga, “akuna shida cha msingi waandae magunia kama kumi ya mkaa, ili yakae mwanzoni, na ukiwa tayari utanishtua” alisema yule jamaa, huku wakiendelea kupata kinywaji. Huyu jamaa anaitwa Alphonce Clemnt Mwanauta, ni OCD wa songea mjini, akiwa na cheo cha ASP, kilicho tambulishwa na nyota zake tatu mabegani…..Endelea…
japo hapo alikuwa amevalia nguo nadhifu za kiraia, Alphonce Mwanauta ni rafiki mkubwa sana wa bwana Kalonga, ni mmoja wawatu ambao unufaika sana na shughuri za bwana Kalonga, kwa kifupi alikuwa anafahamu michezo yote michafu anayoifanya Kalonga, na yeye ndie aliekuwa anamkingia kifua na wakati wingine kusaidia kutenda uovu.***
Naam kule nyumbani kwa Careen mambo yalikuwa yanaendelea, na sasa wale wanawake wawili walishamaliza maandalizi ya chakula na kusimama pembeni kwa pamoja, kisha wote wakainamisha vichwa chini, na kummoja wao akasema, “ewe dada mkubwa Careen, chakula kwaajili yako na wageni wako kipo tayari” ukweli ukiachilia upole na ustaarabu wa watu wakwenye nyumba hii, lakini sasa Peter aliekuwa ajuwi lolote kuhusu mwanadada Careen akaona lazima ifike pahala apate majibu yakinifu, “ok! nyie mnaweza kwenda, mtakuja kumchukuwa Michael saa tatu kamili” alisema Careen kwa sauti tulivu yenye upole na wakuvutia.
Hapo wale waschana waliondoka zao kuelekea ndani, wakimwacha Careen ana anza kuweka chakula kwenye sahani, za kila mmoja, maana aikuwa sahani moja, siunajuwa vyakula vilikuwa vingi na vya aina mbali mbali, huku muda wote Peter akimtazama mwanamke huyu, kuanzia usoni yani kwenye macho yake, mashavu, pua masikio yaliyo baba hear ring za dhahabu, midomo mizuri ya mschana huyu, na kushuka shingoni ambapo likuwa na mkufu wa dhahabu, na pia kifuani ambapo palikuwa na matiti mazuri yaliyo funikwa na iki kigauni chepesi, Peter akuishia hapo, alimtazama mpaka mikono, yenye vidole vizuri, vilivyo vishwa pete za dhahabu, ungesema anamkagua, au anataka kumchora, “hooo! alafu Peter, nilisahau kukuambia kuwa, nime mtuma mtu akaangalie shule kwaajili ya Michael, hivyo jumatatu ataanza shule” alisema Careen wakati wanakula, huku anamtazama Peter, ambae alishangaa kidogo, na kushindwa kuelewa inakuwaje maana niwazi alitakiwa kurudi kijijini, pengine baada ya week au week mbili, saa inakuwaje Michael aanze shule, “lakini ulisema nitakaa week muda mfupi hapa kwako” alisema Peter huku akimtazama Careen ambae alikwepesha macho, huku moyo wake ukianza kunyongea, “lakini Peter, nakumbuka tulisha ongea mchana, nakuitaji ubakie na mimi” alisema Careen kwa sauti ya kuomba, “lakini ulisema ni kwa week moja” alisema Peter, ambae kiukweli alionyesha zamila yake ya kurudi kijijini, “sawa sikatai wewe kurudi kijijini ukasimamie mashamba yako kama ulivyo sema, na vipikama nitakupatia fedha ya kukodi wakulima unaweza kubakia na mimi?” aliuliza Careen na hapo Peter akatulia kwa sende kadhaa akiwaza, na kisha akatoa jibu, “lakini kwanini nikupe mzigo, wa kunifanyia hayo yote, uoni kama nitakiwa nime kuibia nguvu yako ya utafutafuji?” aliuliza Peter na kumfanya Careen acheke kidogo, “sito jari Peter, cha msingi wewe hupo hapa na isitoshe najihisi nipo salama nikiwa na wewe” alisema Careen na hapo Peter akatulia tena, huku wakiendelea kula na kunywa, “sawa nita bakia hapa, lakini naomba niende mala moja kijijini nikawaeleze wazee juu ya uamuzi huu” alisema Peter na hapo Careen akaachia tababasamu pana kweli kweli, lililoachilia ushindi, “usijari tutaenda week end, ninatamani sana kukuona kijijini kwenu, pia nikawaone wazazi wako” alisema Careen, na hapo Peter akatoa macho kwa mshangao, “haaa! we Careen unayajuwa magari ya kwetu jinsi yalivyo mabovu, sidhani kama unaweza kusafiri nayo, na pia uwa yanaenda mala moja, ayarudi mpaka kesho” alisema Peter, kwa msisitizo na mshangao, na hapo Careen akatabasamu, kidogo, kumbuka tabasamu lake uwa anachezesha mdomo kidogo, pasipo kuonyesha meno yake meupe kama seruji, “Peter umesahau kama ninagari?” aliuliza Careen huku tabasamu likiwa bado usoni mwake, “hoooo! sasa wewe unataka nipigwe kipapai, yani tuende mwanamonga na gari zuri hivi, alafu wanakijiji wanakuona hivi” alisema Peter kwa namna flani hivi ambayo, ilimfanya Careen akaangua kicheko cha sekunde kama saba hivi, kikiwa ni kicheko chake kirefu kwa muda wa miaka menne iliyopita, “yani Peter kwajinsi navyokuamini alafu unakuwa muoga hivyo” alisema Careen huku anamalizia kicheko chake, “siyo hivyo lakini kule kijijini sana, alafu hivyo ulivyo uende kule kunavumbi, yani mimi nakushauri usiende” alisema Peter, ambae kiukweli alishaona kuwa huyu dada akuwa anatania, “kwani mimi nipoje?” aliuliza Careen, kwa sauti tulivu huku akimtazama Peter, ambae kiukweli alisita kutoa jibu, akiofia kama linaweza lisimpendeze mwanadada huyu, lakini sasa kwa bahati nzuri au mbaya, Michael aliekuwa anafwatilia maongezi yao huku anakandamiza nyama ya bata iliyochomwa vizuri, akatoa jibu, “mzuri mzuri” alisema Michael na wote wawili wakamtazama mtoto huyo alie kuwa busy na sahani zake, kisha wakatazamana wenyewe kwa sekunde kadhaa, kisha wakatabasamu, “mbona ata wewe nimzuri Peter, na unakaa huko, na bado unatamani kurudi huko?” aliuliza Careen, huku anainamia sahani yake ya chakula, na kuendelea kula.
Unajuwa kuna kitu ukiambiwa lazima ata wewe mwenyewe, utajuwa kama unautaniwa au unaambiwa ukweli, ata Peter aliachia tabasamu flani, la kujicheka, maana niwazi aliona kuwa Careen ana msanifu, “acha utani dada Careen, mimi nakuambia ukweli, kule kijijini akukufai, alafu kuna mapanya mengi na mende, pia kuna mmbu wengi sana utaumwa malaria” alisema Peter kwa sauti ya msisitizo akidhamilia kumtishia Careen asiende kijijini kwao, hofu yake kubwa ikiwa ni hali ya sehemu ambayo Careen angefikia, na vyakula ambavyo angekula kwa muda atakao kuwepo atakama ni dakika moja, lakini mazingira ya nyumba yake, ata kwa wazi wake, akukuwa na sifa ya kufikia mwanamke mzuri kama Careen, ambae siyo tu uzuri na mwonekano wake, pia nni tajiri na mwenye kumiliki wafanyakazi wengi sana.
Nitofauti na Peter alivyo tegemea kuwa, angemwona Careen akishtuka na kusisimkwa na mwili, lakini akamwona anainua usowake na kumtazama peter usoni kwa macho changamfu, huku tabasamu la furaha likiwa limetawala usoni mwake, niwazi kuna jambo lilimfurahisha, “hooo! kumbe huko kuna panya na mende wengi, bila shaka itakuwa siku nzuri kwangu, nitaona panya wanavyo fukuzana na kula mende, namini utawazuwia wasije kwangu” alisema Careen kwa sauti iliyo changamka, akionyesha kufurahia habari ile.
Hapo Peter akashusha pumzi mzito, kama vile amechoka, huku akisahau kama alikuwa anakula mapocho pocho, “baba namimi nitaenda kumwona babu, alafu nitarudi huku kwa shangazi mzuri mzuri” huyo alikuwa Michael, ambae alimfanya Careen acheke kwa furaha, nasiyo kutabasamu kama ilivyo kawaida yake, Peter akamtazama Michael, ambae akuwa na habari, yeye alikuwa anendelea kukandamiza paja la kuku, akaishushia kwa juice yake, “lakini dada Careen mimi naona kama utakuwa unajisumbua tu! hakuna aja yawewe kwenda huko, nitaenda mala moja asubuhi na kurudi jioni” alisema Peter kwa sauti ya upole iliyojaribu kushawishi, “usijari Peter, tutaenda wote, ata kama ukitaka tulale, itakuwa sawa tu!” yani kwajinsi alivyokuwa anaongea Careen, niwazi kabisa, akukuwa na dalili ya kubadiri mawazo yake, “lakini dada Careen, nivyema nikinda kwanza nikawajulishe wazee kuwa utawatembelea, ili wajiandae, alafu tutapanga siku nyingine” alishauri Peter, lakini nikama ushauri wake ulikataliwa, “Peter hakuna sababu ya kuwasumbua wazee, sisi ndio tunapaswa kuwabebea zawadi, wao tuta wajulisha kwasimu” alijibu Careen, ambae ulaji wake utazania wakwenye video, yani ana tafuna bila ata kufungua mdomo, na akifungua mdomo uoni meno, siunajuwa ule ulaji wa wanyilamba, anafunua mdomo mpaka unaona kidaka tonge (natania) pasipo kusaha kumwongea chakula Michael mala kwa mala, kama wafanyavyo wazungu.
Hapo Peter alibakia ametulia anawaza chakufanya, ilikuweza kumshawishi Careen afute wazo la kwenda Mwanamonga, na baada ya sekunde kadhaa akaanza kuongea, kwa sauti tulivu yenye dalili za kubembeleza, “Dada Careen nambao unisikilize kidogo…” lakini kabla Peter ajamaliza Careen akamkatiza, kwa kumtazama usoni kwa macho mkali sana, ambayo aya kuwa na dalili yoyote ya urafiki wala tabasamu, ungesema kuna neno baya aliliongea kiajana huyu toka shamba, ambae ukweli alishtuka na kubaki akimtazama Careen kwa macho yaliyojaa viulizo, “mh! nime kosea wapi tena?” ndivyo alivyiuliza Peter, wakati huo Michael alikuwa anaenda kula, pasipo kuzingatia kinachoendelea, “Peter, nikuambia usiniite dada, niite Careen au jina lolote litakalo tufaa” alisema Careen kwa sauti tulivu ambayo usingeweza kuiweka upende wowote, kama niya hasira, au ya kawaida, “hooo samahani nilisahau” alisema Peter, huku anajichekesha kidogo, “napenda wewe ni mwelewa sana, alafu unasikia kile unachoambiwa” alisema Careen huku anachukuwa kijiko banio, na kupeleka kwenye bakuli kubwa la kioo, lenye nyama za kuku, “Peter hiki chakula ni kwa kwaajili yetu, tendelee kula, naona umesahau kula” alisema Careen huku anachukuwa kipande cha nyama ya kuku na kukiweka kwenye sahani ya Peter, kisha akabana kipande cha keki na kukiweka tena kwenye sahani ya Peter, huku akimalizia kwa kuchukuwa chupa ya wine na kuimimina kwenye garass ya Peter, akifanya hivyo kwa kumimina juice kwenye grass ya Michael, “inatosha hiyo dad.. Careen, huyo dogo huyo ata jikolea kitandani” alisema Peter huku kipeleka mkono wake kwenye mkono wa Careen na kuushika ilikumziwia.
Naam ile kumshika tu Peter alijikuta akikutana na mkono line wenye ngozi nyororo, kiasi cha kuhisi pengine angeuchubua, huku joto flani tamu toka kwenye mkono wa mwanamke huyu, likipenya wenye viganja vya mikono yake na kumsisimua, na kujikuta akiachia kwa haraka sana, kama vile amegusa umeme au kitu chochote kwa bahati mbaya, huku akimtazama Careen usoni, akamwona nae akimtazama kwa macho tulivu yaliyojaa aibu, na tabasamu laini la kupendeza likichanua usoni mwake, “Usijari Peter, ulisha niambia kuwa anaweza kukojoa kitandani, hivyo nimesha leta vifaa vya kuzuwia mkojo” alisema Careen huku anakwepesha macho kwa aibu, na kumtazama Michael, ambae alikuwa anaitazama grass yake ambayo sasa ilikuwa inakaribia kujaa mpaka, kisha akamtazama tena Peter, huku analaza kinja chake cha mkono pale alipoguswa na Peter, na kufanya kama anaupapasa taratibu, mkono wake huo ambao ndio alioshikia ile juice, huku Peter nae aliekuwa anafinyanga kinganja chake kile cha mkono mfano wa mtu anae viliga chakula, akimtazama mschana huyu, na kufanya macho yao yakutane tena, wote waka tabasamuliana, “shangazi inamwagikaaa” alipiga kelele Michael, na hapo ndipo Careen na Peter, kwa pamoja waka tazama ile grass ya Michael………..
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU