SEASON 2: KIAPO CHA MASIKINI (41)

SEHEMU YA 41

ILIPOISHIA SEHEMU YA ALOBAINI: Naam hapo Careen akaanza kuziandika namba zile kwenye simu, huku akiwa ameisogeza simu karibu na Peter, ambae pia alikuwa ana chungulia kwa karibu ile simu, ilikona jinsi Careen alivyo kuwa anapyatila (gusa) kioo cha simu yake, kwa vidole vyake vizuri, akiandika namba alizokuwa anazitaja, na alipomaliza akabofya kialama cha kijani chenye mchoro wa mkonga wa simu…..………..Endelea…
Huku akiweka sauti ya wazi, nahapo wote wakasikia simu inaanza kuita.**
Yap, mama na baba Sada, waalienda moja kwa moja mpaka nyumbani kwao, ambapo walikaribishwa na giza nene, akukuwa na dalili yoyote ya kuwepo mtu nyumbani, walilitarajia swala ilo, maana pale nyumbani walikuwa wanaishi wao peke yao, waliusukuma mlango mbovu wa nyumba yao mbovu, iliyo choka na kutengeneza nyufa kwenye kuta zake, wabatizaji wa majina, nyumba kama hii uita mbavu za mbwa, na kuingia ndani kimya kimya, huku wakitembea kwa bashiri sehemu za kukanyaga, kutokana na giza ambalo, nikama lilizidi mala dufu mle ndani, na kuwa kama ndani ya shimo, walipapasa huku wakiendelea kutembea, na kupishana na viumbe wanavyo ishi navyo mle ndani kama vile, panya na mende, mpaka walipoufikia mlango wa chumba chao.
Amini usi amini, akuna mmoja kati yao ambae alikumbuka kuoga au kunawa miguu na sehemu ambazo, zina itaji kufanyiwa usafi mala kwa mala, awakujari kuwa toka asubuhi ya siku ile walikuwa ni wazurulaji, na kwamba walizurula toka asubuhi mpaka usiku ule wa saa tatu, hawakujari vumbi jasho ppengine na mabaki ya mikojo waliyo kuwa wanakojoa wakiwa njiani, wakapanda kitandani, kila mmoja kwenye sehemu yake nazani wanao lala wawili wawili wananielewa, mke uwa anaijuwa sehemu yake ya kulala kila siku, yani kama ni ukutani basi ni ukutani siku zote, na pia anaifahamu sehemu ambayo mume wake analala kila siku.
Kimya kilitawara mle chumbani, hakuna aliesikika akiongea lolote kati yao, zaidi zilisikika sauti za mihemo yao na vikoozi vya hapa na pale, sambamba, na pulukushani za panya kwenye milingoti ya na nguzo zinazo shikilia paa la bati chakavu, la nyumba hiyo, na michato ya mende, ungesema wamesha lala, waliokuwa wanaangaika kwenye vyombo vichafu, toka upande wa pili wa ukuta wenye nyufa wa jikoni, chumba ambacho siku za nyuma kilitumiwa na Sada, kama chumba cha kulala.
Ukimya wa wawili awa aukuwa bule, kila mmoja alikuwa anawaza la kwake, juu ya kile walicho kisikia kwa mzee Jacob, walichokuwa wanawaza ni maswali yaliyokuwa yanatawala vichwa cha wawili awa, yalikuwa yana fanana, kwa kiasi flani, “inawezekanaje mtu aende mjini jana tu, leo tuambiwe anakaa kwenye ghorofa, au wamefikia kwa Sada, ila anaona wivu sisi tukifahamu” alijiuliza mzee Nyoni, alie kuwa amelala chali, ana angalia nyota, za angani upitia matundu makubwa yaliyo jaa kwenye paa la nyumba ile, chakavu, wakati huo mama Sada yani mke wa Mzee Nyoni, “huyu alisema anaenda kukutana na Sada, na ata kama ajakutana na Sada, sasa mbona wanasema anakaa kwenye ghorofa?” alijiuliza mama Sada.***
Naam mida hii kwa mzee Jacob, ndio kama kulikuwa kuna kucha, maana watu walikuwa wanazidi kuongezeka, na kuwa wengi zaidi, ni watu wale wale walio kuwa wanakuja kupata habari waliokuwa wana pitia kwa mzee Jacob kupata utibitisho wa habari zilizokuwa zina tawanywa na mzee Nyoni na mke wake, ya kwamba Peter na mwanae Michael wamekutwa na matatizo huko mjini, kila mmoja alitafuta uthibitisho akiwa na lengo lake, wapo walio uzunishwa na habari zile kama ilivyokuwa kwa mzee Ponera, kutokana na jinsi kijana Peter alivyo mchapakazi mwenye nidhamu, na heshima, pia wapo waliofurahia habari zile kutokana na chuki binafsi juu ya utendaji wakijana huyo, ambae kila kijana mwenye kujitambua alitamani kufanana na nae, wapo walio mchukia sababu ya kutamkwa vizuri na watu wengi, wapo waliomchukia kutokana na mafanikio yake kwenye kazi za mikono yake, japo azikuwai kumnufaisha yeye mwenyewe Peter, maana ni mala ya pili sasa mavuno yote yanaishia kwa Sada.
Lakini watu wale walipofika nyumbani kwa Jacob, ambako walitegemea kumkuta akiwa amenyongea wanashangaa kukuta watu wanaendelea kulewa na kupiga kelele, huku sasa kukiwa na sauti za music toka kwenye speeker kubwa za redio za mmoja wawana kijiji alie kuja nayo, nazani nilisha kudokeza kuwa hii moja ya tabia ya watu wa kabira ili la wandendeule, ya kutembea na redio ata kama nikubwa kiasi gani ilimladi wenzake waone au kujuwa kuwa anamiliki redio kubwa, nikama walikuwa wanasherehekea wasicho kijuwa.
Wapo waliokuja na madumu yao ya ulanzi, na wapo waliokuja na bia zao, japo kwa sasa wengi walisha ishiwa bia na kuendelea na ulanzi, wakidiriki kuagiza ulanzi mwingine, ilimladi waendelee kuunywa mpaka muda watakao ona sasa pombe basi, “baba Peter Simu inaita” alisema mama Peter akimwonyesha simu yake mzee Jacob, ambae alitazama ile namba na kuona kuwa ailikuwa ngeni, kwamaana akuwai kisave, akaipokea na kuiweka sikioni, “hallow nani mwenzangu?” aliuliza mzee Jacob, huku akiwa amekaa kwenye kundi la wenzeke, waliokuwa wanaendelea kupombeka, “mimi Peter baba, shikamooo” ilisikika sauti ya Peter toka upande wapili wa simu, hapo mzee Jacob ali inuka gahfla, na kupiga ukelele wa shangwe, “jamani Peter amepiga simu” hapo wenzake wakaacha walichokuwa wanafanya ikiwa pamoja na kucheza music, “weka loud” alisisitiza mama Peter, huku anamsogelea mume wake, ambae libonyeza sehemu ya kuluhusu sauti ya wazi, huku bwana Ngongi, akionyesha ishala ya kuzimwa mwa music, ambao ulizimwa mala moja, “we mtoto, mbona umetutisha wenzako ebu tueleze huko mjini hupo kwanani na ime kuwaje ukatuambia kuwa umepatwa na matatizo?” safari hii aliongea mama Peter, “usiwe na wasi wasi mama nipo salama kabisa, rafiki yangu anataka kukusalimia” alisema Peter, huku kila mtu akiwa kimya anasikiliza maongezi yale, “aya nimsalimie” alisema mama Peter kisha ukimya ukatawara, kila mmoja akaisubiri kusikia salamu ya rafiki yake Peter, “hallo mama mpendwa salamu ya heshima kwako” ilisikika sauti tamu ya kike iliyojaa utulivu wa hali ya juu, “ujambo mama” alisema mama Peter, ambae alikuwa anasubiria salamu ya shikamoo, “sijambo, mimi ni rafiki yake Peter, jumamosi nitakuja kuwatembelea huko nyumbani na Peter nita wabebea zawadi” ilisikika ile sauti tulivu ya kike, ambayo kwakuisikia tu, ungetambua kuwa unaongea na mtu wa aina gani, “karibu mama, karibu sana, ila muangalie magari huko mjini, tulikuja leo tuliona yapo mengi sana, alafu mzshauri asikutane na huyo mwendawazimu” alisema mama Peter na hapo nikama alimshtua kidogo Peter, “mama acha uongo, wewe umekuja saa ngapi mjini?” aliuliza Peter kwa namna ya kumshushua, “tulikuja leo, tukakutana na Sada pale stend” alisema mzee Jacob, na hapo nikama Peter alizidisha mshtuko, “weeee! mlitoka salama kweli, aku….” kabla ajamalizia kuongea simu ikakatika, na kuzima kabisa, “haaa chaji imekata” walipiga kelele karibu wote waliokuwepo pale, ni kweli mzee wakati ule, Jacob alikuwa ameamlisha simu iletwe kabla aija jaa, ili aweze kuwasilina na kijana wake.
Music uliwashwa na shuguri ikaendelea, “mzee Jacob, unazani huyo mwanamke ni yupi?” aliuliza mzee Ponera, ambae kiukweli anachofahamu yeye Peter akuwa na rafiki mjini, “ata mimi najiuliza swali kama lako, maana Peter siyo mwendaji sana wa mjini” alisema mzee Jacob, na kuamua kuachana na maswali hayo ambayo, ambayo waliamini uwa majibu yake watayapata siku ambayo Peter atarudi kijijini kama yule mwanamke alivyosema, kuwawa juma mosi wanatarajia kuja kuwatembea, na ukizingatia kulikuwa na siku moja tu ya ijumaa mbele yao ili ifike jumamosi.****
Naam turudi nyumbani kwa mzee Nyoni, ya ni kwa wazazi wa Sada, au Queen, ambako wawili hao walitumia masaa kadhaa kuwadha jambo lile pasipo kupata jibu, zaidi walijikuta wakiumia mioyo yao, kwa kiwango kikubwa cha wivu, juu ya kile walicho kisikia kuhusu Peter na Michael, ambae na wao pia ni mjukuu wao, wakati mwingine walijikuta wakianza kuwaza juu ya binti yao Sada, na ndio wakati ukimya ulipovunjika baina yao, “mama Sada mama Sada” aliita mzee Nyoni, huku anamtikisa, mke wake, akizania amelala muda mrefu uliopita, “nakusikia bwana” alisema mama Sada, kwa sauti ya ukali, nikama alikuwa amechukizwa na jambo flani, au akutaka usumbufu, “sasa unanikasirikia nini bwana, baada ya kusikia ninachotaka kukuambia” alsema mzee Nyoni, kwa sauti ya ukali pia, “aya sema sasa nakusikiliza” alisema mama Sada, ambae pia alikuwa amelala chali, “hivi kwanini Sada toka aende mjini, ajawai kuja kutusalimia?” aliuliza mzee Nyoni, kwa sauti ya mamshaka, “sasa baba Sada mimi nitajuwaje na wakati wote tupo hapa kijijini” alijibu mama Sada, kwa sauti yenye mtindo wa kukwepa lawama, “yani toka ameenda hakuna cha simu wala nini, ata kusema vijisenti hivyo hapo kwaajili ya dagaa” alisema mzee Nyoni, kwa sauti ya kulalamika na kunyongea, wakati huo nikama pombe zote zilisha wakauka vichwani mwao, “ile kweli yani mhuyu mtoto anashindwa ata ana kadara, alie enda juzi juzi tu, aliwatumia wazazi wake fedha za mbolea ya tumbaku, si unaona walivyo vuna, wala hawa nashida” alisema mama Sada safari hii akiwa mwenye uchangamfu mkubwa, “shida hipo kwa mwanao Sada, yeye siyo wa chumvi wala sukari” alisema mzee Nyoni, “lakini mimi naona atakuwa na maisha mazuri tu, kama angekuwa na tatizo lazima angerudi au kututafuta” alisema mama Sada, na hapo wakaongea mawili matatu, kabla awajapata wazo la itimisho, “mimi naona tutafute elfu tano, twende mjini tuka mwone” alisema wazo ilo alilitoa mzee Nyoni mwenyewe, “hapo umeongea jambo la msingi, twende mjini tukamwone Sada, najuwa lazima atakuwa tajiri, hao unao waona wanakuja kudondea (kudowea) vijiela” alisema mama Sada, kwa kujiamini, “umeona hen, we ngoja tupate nauri, siku tukirudi kila mmoja ata tushangaa” alisema mzee Nyoni akiunga mkono maneno ya mke wake, “sasa tutajuwaje sehemu anayo kaa?” aliuliza mama Sada, yani mke wa mzee Nyoni, na hapo kika pita kimya kifupi, nikama walikuwa wanatafakari, swali ilo gumu kwao, maana ukweli licha ya kufahamu kuwa binti yao alikuwa mjini, awakujuwa anaishi vipi, wapi, na anaishi na nani kama nani, “hivi unakumbuka Kadara alisema uwa anaonana na Sada huko mjini?” aliuliza mzee Nyoni, “ndiyo alisema uwa anakutana nae kila siku” alisema mama Sada, na hapo wawili awa wakapata wazo la kuwa wataenda nyumbani kwa wazazi wa Kadara, ili wakachue namba ya simu ya Kadara, ili wawasiliane na Kadara ambae ndie anaweza kuwapeleka anapoishi Sada.****
Naam baada ya simu kukata ghafla na kujaribu kupiga mala kadhaa na kuambiwa simu aipatikani, Peter na Careen wakiwa wamekaa karibu karibu, kupata kinywaji huku Careen akianza kumfundisha Peter namna ya kuitumia ile simu, “inaonyesha kijijini kwenu pazuri sana, watu wanafuraha muda wote?” alisema huku anafungua simu upande wa mipangilio, (proglam) “huu ni msimu wa malipo ya fedha za tumbaku, hivyo watu ukaa mpaka usiku wakinywa pombe na kucheza music” alijibu Peter huku anafwatilia kila ambacho Careen alikuwa anakifanya kwenye simu yake, “Peter umesikia mama alivyosema, usikutane na mwenda wazimu?” aliuliza Careen, kwa sauti tulivu safari hii akiacha kubbofya simu na kumtazama Peter usoni.
Hapo Peter alitulia kidogo, kama anatafakari jambo, huku Careen akimtazama kwa jicho la wasi wasi, nazani alitaka kujuwa kama Peter bado alikuwa anampenda Sada ……..

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!