
SEHEMU YA 42
ILIPOISHIA SEHEMU YA ALOBAINI NA MOJA: “huu ni msimu wa malipo ya fedha za tumbaku, hivyo watu ukaa mpaka usiku wakinywa pombe na kucheza music” alijibu Peter huku anafwatilia kila ambacho Careen alikuwa anakifanya kwenye simu yake, “Peter umesikia mama alivyosema, usikutane na mwenda wazimu?” aliuliza Careen, kwa sauti tulivu safari hii akiacha kubbofya simu na kumtazama Peter usoni.
Hapo Peter alitulia kidogo, kama anatafakari jambo, huku Careen akimtazama kwa jicho la wasi wasi, nazani alitaka kujuwa kama Peter bado alikuwa anampenda Sada ……..Endelea…
“Careen naomba unielewe, licha ya kwa Sada nilikaa nae kwa muda mrefu pia ni mzazi mwenzangu, lakini kwasasa, nimehesabu, kuwa Michael akuwa na mama, na wala sija wai kuwa na mwanamke, ni kutokana na maneno aliyo jiambia, na mambo aliyo nifanyia, hakika ninge kuwa na uwezo, ninge kumtafuta mwanamke wenye upendo wa wadhati kwa kwangu na kwa mwanangu Michael, niishi nae, lakini siyo Sada” alisema Peter kwa sauti iliyojaa hisia kali za kutoka moyoni, na kumfanya Creen atabasamu, “vipi kuhusu mimi ninaweza weza kuwa mama mzuri kwa Michael?” aliuliza Creen, swali ambalo lilikuwa nikama laghafla kwa Peter, ambae alimtazama Careen, kuona alikuwa anamaanisha nini kuongea vile, “hakika una faa kuwa mama, kama siyo utofauti tulionao, ningesafiri mpaka kwa wazazi wako, kokote waliko nikatoe barua ya uchumba” alisema Peter, huku anacheka kidogo, ambae sasa alijuwa wanaongea ya kawaida yenye utani.
Careen akaachia tabasamu afifu, “Peter unazani kazi zangu zinaweza kutuzuwia tusiwe mke na mume?” aliuliza Careen kwa sauti tulivu, sasa walisha sahau kuelekezana kuhusu matumizi ya simu, “ndiyo, sijapanga kuishi na mke wangu mbali mbali, yani mfano mke wangu ni mwalimu au sijuwi nani, anafanya kazi mpingi, mimi nipo namtumbo, sasa itakuwaje?” alijibu Peter, ambae akujuwa kama Careen alikuwa anaongea katika uharisia, na siyo utani kama yeye anavyo fanya, “kwani unamzungumzia mwanamke gani?” aliuliza Careen kwa sauti ile ile tulivu, safari hii bila kutabasamu, “hakuna mwanamke ninae mzungumzia, ila nina toa mfano” alijibu Peter, huku anageuza usowake kumtazama Careen ambae alikuwa anamtazama, “mimi naongelea kuhusu mimi na wewe, kitugani kitatufanya tushindwe kuishi pamoja?” ukweli ta kama ni wewe, kwa swali ilo sijuwi ungelielewaje, “hoooo! kwamfano ni mimi nawewe, bado ingekuwa ni ngumu, tu, kwanza watu watasema nimukupa dawa..” alisema Peter, na hapo Careen akamkaiza kwa haraka, achana na mambo ya watu, tuongelee mimi na wewe” alisema tena Careen safari kwa sauti ya msisitizo, kama vile analalamika, “kazi zako, za hapa mjini na mimi nitatakiwa kwenda kulima kijijini” alisema Peter, na hapo Careen akacheka kidogo, nikicheko cha furaha, na raha, “kumbe tatizo ni ilo tu, lakini siunanipenda hen!?” aliuliza Careen huku anapeleka mkono begani kwa Peter, ambae alihisi msisimko wa ajabu, nusu autoe mkono wa Careen kwa uoga lakini kwa raha aliyo ipata akauacha uendelee kumtekenya, kwa joto lake tamu, “nakupenda… nakuupenda sana, kwanini nisikupende…” aljibu Michael lakini katika hali ya kutokuelewa anachomaanisha Careen, katika ile hali ya unywaji wa wine.
Jibu la Peter lili mfanya Careen aachie tabasamu moja matata sana, lenye kulemewa na mchanganyiko wa furaha na raha, “ilo ndilo la msingi, zaidi ya hapo tuutajuwa baadae kama ni kukodi mashine za kulimia, au watu” alisema Careen, huku anajiegemeza kwenye bega la Peter, ambae alitoa alihisi hali flani ya msisimko ulio penye mpaka chini kabisa kwenye jinsia, Peter akatoa macho kwa mshangao, akuelewa kama anacho kisikia ni kweli au utani, na kama ni utani, iweje sasa mschana huyu mrembo amwegemee kwa mtindo huu wa kutiana majaribuni, “Careen unaitaji kwenda kulala, naona tumekunywa pombe nyingi sana” alisema Peter, ambae sasa dudu ilikuwa inajitutumua kwenye bukta yake nyepesi, na kusimama kama cobra alieona panya.***
Naam mita mia nne toka nyumbani kwa Careen, ikiwa ni mita mia mbili toka shule ya msingi Maji maji, ikiwa imetenganishwa na barabara ya lami itokayo mjini, usawa wa idara ya mahakama, kwenye eneo la makazi ya maafisa wa ulinzi na usalama, palikuwa na nyumba anayo ishi afisa mkuu wajeshi la polisi, katika kitengo cha mpelelezi wa makosa ya jinai, RCO, bwana SP Cletus Mlashani, mzee wa makamo, mida hii alikuwa kitandani, hakuwa peke yake, juu ya kitanda, alikuwa pamoja na mke wake na mjukuu wao wakike mwenye miaka miwili na nusu, ambae alikuwa amesha lala, tofauti na wanandoa awa ambo walikuwa macho, nikama walikuwa wanasaka usingizi, “baba Sophy, hivi jumapili utakuwa na safari yoyote ya mbali?” aliuliza mke wa mzee Mlashani, “mhhhhhh juma piliiiii, hapana nikisha toka kanisani, nitakuwa nyumbani, vipi unainshu yoyote?” aliuliza mzee Cletus, huku anageukia upande aliokuwepo mke wake na mjukuu wao alie lala katikati yao, “niliitaji dereva wako atupeleke NPF, kwenye bembea za watoto, nimpeleke Jasmin akabembee kidogo” alisema mke wa bwana Mlashani, “hooo! nakumbuka ulimuahidi toka week ileeee, hakuna shida, tkutoka kanisani, utampeleka, nazani itakuwa ni mida ya mchana” alisema mzee Mlashani, ambae pia aliongeza, “ila nakushauri mgetumia gari binafsi, maana ninaweza kupata dharula, alafu mkakatiza atarehe zenu” alisema RCO, “kwani wewe uendi na sisi, mimi nilisema hivyo nikiwa na maana ya kwamba utatupeleka” alisema mke wa RCO, na hapo mzee Mlashani akatulia kidogo kama anawaza jambo, alitumia sekunde kadhaa kuwaza, kisha akasema, “ok! basi tutaenda wote, maana sitokuwa na chakufanya” alisema RCO ambae ni vyema kama tukimfahamu kwa undani kidogo.
Bwana Mlashani ni baba wa watoto wawili, Sophia ambae ni mkubwa, na Johnson ambae ni mdogo kwa Sophia, Sophia ambae anamiaka therasini na moja, amemzidi John kwa miaka minne, wakati Sophia sasa yupo mwaka wapili, katika chuo cha sanyansi na tiba ana somea degeree yake ya utabibu, mwenzie Johnson alikuwa anamaliza mafunzo ya uafisa mwanafunzi, wa jeshi la ulinzi, huko #mbogo_land, wenyewe wanakuita, wanaita kwa king Elvis wa kwanza, niutaratibu wa kawaida kwa askari kuchangia mafunzo ya kijeshi, na nchi nyingine, Jasmin ni mtoto wa Johnson, ambae alimzaa na mschana mmoja alie dahamika kwa jina la Joanitha.
Labda unaweza kujiuliza kwanini Jasmin awe na waazazi wa Johnson baada ya kukaa umamani, ukweli nikwamba, wakati Johnson alimpatia ujauzito Joanitha, Joanitha alikuwa mwanafunzi wa kidato cha sita, ulitokea ugomvi mkubwa sana, kati ya wazazi wa Joanitha, ambao ni walikwa waishi kwa kutegema jembe la mkono, zidi ya familia ya bwana Mlashani, wakati wazi wa joanitha, ambao walikuwa wamemsomesha binti yao kwa shida, wakidai kuwa Johnson alifanya hivyo makusudi, akijivunia baba yake ambae ni mkubwa nadi ya jeshi la polisi, dhana ambayo ilipingwa vibaya na mlashani, ambae anasifika kwa kutnda haki katika utumishi wake, ndani ya jeshi la polisi, na alicho kifanya nikujaribu kutafuta suluhisho, kwakukaa naochini kumaliza swala ili.
lakini licha ya bwana Mlashani kusema kuwa, ata hakikisha natoa huduma kwa mama mjamzito, na mala atakapo jifungua atahakikisha anampeleka shule tena kumalizia elimu ya juu ya sekondari, huku waliopeana mimba wakisema kuwa, wanampngo wa kuowana hapo baadae, lakini wazazi wa Johanitha awakukubariana na ilo, mwisho wazazi wa Johantha wakapanga kuipeleka kesi mahakamini, kitu ambacho Johanitha mwenyewe alikipinga vilivyo, kitu ambacho kiliwapelekea wazazi wake wamfukuze nyumbani, na yeye kwenda kukaa na wazazi wa Johnson, yani kwa mzee Mlashani, ambao walimpokea na na kumlea mpaka alipo jifungua salama, na kulea mtoto kwa mwaka mmoja, kabla ya kumpeleka shule kwa mala nyingine, wakati huo tayari Johnson alikuwa amesha jiunga na jeshi, na sasa Johanitha anasoma chuo cha uhasibu, na tayari wazazi wake walisha tuliza hasira zao, na kupatana na mzee Mlashani, ambae aliwakomboa kutoka kwenye jembe la mkono kwa kuwanunulia vifaa vya kisasa vya kilimo.
Mlashani na mke wake wanampenda sana mkujuu wao, ambae wamempatia mfanyakazi wakumwangalia mala kwa mala, japo bibi yake muda wote yupo makini kumtunza mtoto huyo, ambae anakuwa akiwa na afya nje, akipatiwa kila kitu, kwa upendo wa hali ya juu, Johnson na Johanitha bado wanatunza ahadi ya kuoana mala Johnson akirudi toka mfunzoni.***
Naam saa nne kamili ndiyo muda ambao, bwana Pitus Kalonga alipo achana na na ASP Alphonce Clemnt Mwanauta, na kuelekea nyumbani kwake, huku kichwani mwake akiwaza na kupania, jinsia atakavyo mshugurikia mwanadada Careen siku akimtia mkononi, “huyo fala anae ingilia anga zangu ninani, mbona sijawai kushindwa ata siku moja, yeye ni nani mpaka nifanye nishindwe?” aliwaza Kalonga, hukuakizidi kupandwa na hasira na chuki, zidi ya kijana huyo, anaesemekana ni mtu kutoka kijijini, “Emma nae ni bule kabisa yani toka mwaka jana, mpaka leo bado ajafanikiwa kumliza huyu Malaya, mpaka huyu bwege anaingilia mipango yetu” alijisemea kwa sauti Kalonga, “ila safari hii, Careen aandike ameumia, hakika awezi kuchomoka kwenye mtego wangu” alisema Kalonga, huku anakanyaga mafuta kuelekea round about ya songea girls, “hapa nita dili na mipango yote miwili, lazima nifanikishe mpango wa huko Linjumbwi, huku Careen hna huyo chawa wake wanaisoma namba” alisema Kalonga wakati huo anapunguza mwendo kuingia Round about, kisha akakata kushoto alafu akakanyaga mafuta kwa nguvu, kushuka mtelemko wa mateka, “mpuuzi sana, nita mgonga Careen mbele yake” ukweli ata mimi sijuwi ni kujiamini kwa aina gani alikokuwa nako Kalonga, au ni ile pombe kali toka #mbogo_land, aliyo ifakamia pale Angon Arms, na viji tako vilivyokaa vizuri nitahakikisha nime fukua fukua” yani kwa mwonekano wa mzee Kalonga, usingezania kama anamawazo ya ajabu kama aya, “ukweli kijana umejiingiza kwenye ugomvi usio kuhusu” alisema Kalonga ambae aliamini kuwa, lazima OCD Mwanauta atampatia kijana huyo mikononi mwake.**
Careen alitazama muda, akaona kuwa inakaribia saa nne na nusu za usiku, kisha akainua uso wake kumtazama Peter, “mume akisema basi mke hana chaguo” alisema Careen huku anainuka na kumpa mkono Peter, kwa maana ya kumtaka aushike, Peter akaushika mkono wa Careen huku kichwani mwake akijadiri swala zito, “inabidi niwe makini sana, nisije kufanya jambo la kipumbavu alafu nikaishia jela” aliwaza Peter, huku anainuka toka kwenye kiti, hapo kwa bahati mbaya Careen akatazama sehemu zambele za Peter, usawa wa bukta, alicho kiona kilimfanya atabasamu, “nimeelewa kwanini unasema tuende kulala, lakini mbona hivyo alafu bado mapema sana” alisema Careen kwa sauti iliyoambatana na kicheko flani hivi cha aibu, huku anatazama chini………..
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU