SEASON 2: KIAPO CHA MASIKINI (49)

SEHEMU YA 49

ILIPOISHIA SEHEMU YA ALOBAINI NA NANE: huku anachukuwa simu na kupiga kwa yaya Glory, ambapo aikuita sana ikapokelewa, “yaya vipi ameshaamka?” aliuliza Careen wakati huo Solo alishatoka ofisini, “ameshaamka, lakini bado alikuwa ajatoka chumbani nimemtuma Cerine akamtazame” alijibu yaya Glory, huku akicheka kidogo, hapo nikama Careen alishtuka kidogo, “yaya kwajinsi nilivyo mwacha Peter kutakuwa na usalama kweli” aliuiza kwa sauti ya mshtuko Careen. ………..Endelea…
huku akionekana kutaka kusimama toka kwenye kiti alicho kalia, “wala usiwe na hofu, nipo hapa mlangoni akiwezi kutokea kitu chochote, kwa ni umwamini Peter?” aliuliza yaya Glory, huku akiachia kicheko cha utani, akimtoa wasi wasi, Careen, “lakini yaya, nilimwona Peter akiwa anatamani sana, usimwachie mfanyakazi peke yake aingie chumbani kwangu, kama Peter yupo ndani” alisisitiza Careen, “wala usiwe na shaka, amempelekea nguo kama ulivyoagiza, ila ondoa hofu, Peter ni kijana mwema” alisema tena yaya Glory, akizidi kumtuliza Careen, ambae sasa akaa vizuri kwenye kiti chake na kutua kama anajikumbuha jambo, “vipi kuhusu Michael nae ameamka?” aliuliza tena Careen, kwa sauti tulivu “yeye ameamka mapema sana, akalilia tuwashe TV, tuka mwashia, ila sasa amesha maliza kuoga, anaendelea kutazama TV huku anamsubiri baba yake waelekee kwenye chai, lakini aliuliza kuhusu wewe na baba yake mpowapi” alisema yaya Glory, “aliulizaje, na wewe ukamwambiaje?” aliuliza Careen akionyesha mwenye shahuku, na kijifuraha kwambali “alisema eti bibi, baba na shangazi, wapo wapi?” alisema yaya Glory, kwa mtindo wa kusimulia akijaribu kuingiza sauti ya kitoto, “enhe na wewe ukamjibu nini?” aiuliza Careen kwa sauti yenye shahuku zaidi, “nikamjibu shangazi ameenda kazini, na baba yako amelala, hapo akuonyesha wasi wasi tena” alieleza yaya Glory, “hivi yaya, kwani uwezi kumfanya Michael aniite mama?” aliuliza Careen, huku anaachia tabasamu afifu, “inawezekana Careen, mpaka hapo yeye ni mwanao” alisema yaya Glory, na hapo Careen akaachia tabasamu pana la furaha, “aya yaya sasa hivi nipo njiani, nakuja kunywa chai pamoja nao” alisema Careen, na kukata simu, pasipo kusubiri pengine Glory alikuwa na kitu cha kusema, akachukuwa begi lake jeusi, huku anainuka toka kwenye kiti cha ofisi, na kuanza kutembea kutoka nje, akimptia msaidi wake pale mlangoni, “mpigie fundi mkuu, aniletee BMW, alafu lile Range lover alifanyie service kesho nasafari ya kijijini” alisema Careen kisha akaendelea kutembea kuelekea kwenye ngazi za kushikia chini, huku macho yake yaki shuhudia watu wengi sana, waliokuwa wananunua maitaji yao ndani ya maduka yake.***
RCO Mlashan, akiwa ofisini kwake anaendelea kulikagua jarida la uchunguzi wa mdawa ya kulevya, ambalo lilikuwa linaelekeza sehemu yapo uzwa, sehemu ambazo kila walipoenda kushtukiza kwa lengo la kuwakamata, wamekuwa wakosa ushaidi, huku jarida lile likielekeza majina ya washukiwa, wa usambazaji wa dawa hizo, ambao mala kadhaa walisha kamtwa na kukosekana kwa ushaidi zidi yao, hivyo kuachiwa huru.
Mala SP Cletus Mlashani, akaletewa ujumbe kuwa anaitwa na RPC haraka sana, hivyo akainuka mala moja, na kutoka ofisini kwake, akaelekea ofisini kwa kamanda wapolisi mkoa wa huu wa Ruvuma, iliyopo ghorofa ya tatu, ambako aliwakuta RPC na staff officer, akasalimia kwa mujibu na taratibu za kijeshi, “kaa hapo RCO” alisema RPC na kikawaida asingekaa ata kama ni lisaa lizima, kama RPC asingesema, “aya tuambie umefikia wapi katika uchunguzi, wa uingizaji na usambazaji wa dawa zakulevya” aliuliza RPC, ambae aliongeza kuwa, “dawa na matumizi yake, yameongezeka kwa kiasi kikubwa sana, mkoani na mikoa ya jirani, tunashutumiwa sana kuwa mkoa wetu ndiyo njia kuu ya kupitisha dawa hizo, ebu tuambie, umefikiawapi bwana Mlashani” alimaliza RPC na kusubiri maelezo ya RCO, “afande tulicho gundua ni kwamba, Dawa za kulevya, uingilia bahari ya hindi, kwenye nomans land ya msumbiji na Tanzania, kisha kusafirishwa pembezoni mwa mto ruvuma wakiikwepa mbogo land, ambayo imefanikiwa kuthibiti dawa hizo kuingia nchini mwao, kisha kuingia nchini mwetu kupitia mkoa wetu wa Ruvuma, na kusambazwa mikoa ya jirani, huku kiasi kikubwa kikiuzwa hapa mkoani, tumesha tuma doria na mitego ya mala kwa mala, lakini waingizaji wa dawa hizo uonekana kusitisha kazi zao, kwa muda mpaka tunapo jilizisha kuwa hakuna usafirishaji, nakuondoka ndipo wao, uanza tena kazi zao, kitu cha kushangaza, aya tunapoweka mitego ya siri, bado wanagundua mapema na kutukwepa” alieleza SP Mlashani, kamanda wa upelelezi wa makosa ya jinai mkoa Ruvuma, “vipi kuhusu washukiwa, mliwai kuwapata, nakujaribu kuwahoji?” safari hii aliuliza Staff officer, “tume wapata wengi, ambao kila tukijaribu kuwa shtukiza na kuwakamata, atupati ushidi wenye nguvu, hivyo tunalazimika kuwaachia, tunashindwa kuelewa inatokea vipi, maana vyanzo vyetu uwa vinauhakika na kile wanachosema, mmoja wa washukiwa ni bwana Pitus Kalonga, ambae alishawai kuhusishwa na matukio mengi sana, ya kiarifu, ukiachia yale ya madawa ya kulevya, lakini akuna alie wai kumpata na ushidi” alisema RCO, na hapo RPC akatulia kidogo, kama vile anafikilia cha kufanya, kabla ajainua uso wake na kumtazama RCO, “huyo mtu nilisha wai kusikia habari zake siku zanyuma, nikiwa staff officer Iringa, hivi bado tu anaendeleza uharifu, inabidi atafutiwe dawa haraka sana” alisema RPC, na kumluhusu RCO aondoke huku akimsisitiza kuwa anaitaji kesi ile iishe haraka sana, kwa kupatiwa ufumbuzi, ambao ni kwakamata wasafirishaji na kuwatolea mfano kwa wengine.***
Habari za maisha mazuri na kumiliki ghorofa, ambalo Peter na mwanae Michael walilala, wakiwa wamesaidiwa na Sada, alie waokota baada ya kuibiwa kila kitu, na undokaji wao wakutoroka, kitendo ambacho kilisemwa kuwa ni wivu, zilizidi kusambaa kwa haraka sana kijijini Mwanamonga, huku zikizidi kuwekewa chumvi na vionjo vya kunogesha, maana kuna wakati wakina mama Sada walisema kuwa binti yao anamiliki gari, “ni jambo la kujivunia sana, hivi Sada sasa anakazi gani awasaidie na ndugu zake huku kijijini?” aliuliza mzee Lupogo, ambae sikuzite utimia busara nyingi sana katika mambo yake, japo ni kama wazee wengine wa pale kijijini, asa msimu huu wa mavuno, tumia muda mwingi kunywa pombe, “kaziiii…umesema kazi?” aliuliza mzee Nyoni huku mke wake, yani mama Sada akidakia, “anamiduka mikubwa kubwa mikubwa” alisema mama Sada, wakati huo tayari walikuwa wamesha changamka kwa lita kadhaa za ulanzi, ulio pokelewa na ugari maharage, waliokula kwa mama Njogopa.
Habari hizo zilimfikia mzee Jacob na mke wake, na kuzidi kuwaweka njia panda, maana ukiachilia maongezi ya Peter mwenyewe kuwa yupo salama, na atarajia kuwa tembelea hapo kijijini na rafiki yake, na walisikia pia kwa Michael mtoto mdogo, kuwa wapo sehemu nzuri kwa shangazi mzuri mzuri, huku akisema kuwa, aliibiwa viatu vyake na mwanamke, lakini kuhusu Sada, licha ya kumwona akiwa na yule kijina wote wakiwa wampondeka usoni, lakini ni kweli walikuwa na gari, lakini sasa mchanganyiko unakuja pale walipokumbuka kuwa Sada walikutana nae jana mchana, akiwa ajuwi maali Peter alipo, na akionyesha dalili ya kuwa fanyia vibaya, huku wao wakiongea na Michel na baadae Peter jioni ya siku hiyo hiyo, tena akiwa na rafiki yake wakike, sasa hiyo nyumba ya Sada waliyo lala ni hipi, na lini, wakati alisema walikutana juzi na alimpiga, “sikia baba Peter, ebu mtume mtu akachukuwe simu kule dukani, ili tupimgie Sada atueleze ukweli, maana aya mambo yanavyokwenda ata mimi sielewi elewi” alisema mama Peter, na mzee Jacob akaunga mkono swala ilo, “tena pate hiyo namba kwa mama Kachiki, yule jilani ya mzee Nyoni, ili tuongee na Sada atueleze ukweli maana Peter simwelewi huko mjini” alisema mama Peter, huku anatazama upande wa barabarani ilikuona kama atampata mtu ambae ataenda kumchukulia simu na kupitia namba ya simu kwa mama Kachiki, lakini akumwona mtu yoyote, “inachanganya kwakweli, lakini kwanini Peter amekuwa hivi huyu mjinga?” aliuliza mzee Jacob kwa sauti iliyojaa hasira, huku anaanza kutembea kuelekea upande wa madukani, “unaenda wapi sasa, wakati supu hipo tayari?” aliuliza mama Peter huku anamtazama mume wake, alie kuwa anaendelea kutembea, “naenda kuchukuwa simu, ningee na huyu mpuuzi, siwezi kusubiri zaidi” alisema mzee Jacob, na wakati huo huo, wakasikia msagano wa pendri za baiskeri…..……….

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata