SEASON 2: KIAPO CHA MASIKINI (50)

SEHEMU YA 50

ILIPOISHIA SEHEMU YA ALOBAINI NA TISA: “inachanganya kwakweli, lakini kwanini Peter amekuwa hivi huyu mjinga?” aliuliza mzee Jacob kwa sauti iliyojaa hasira, huku anaanza kutembea kuelekea upande wa madukani, “unaenda wapi sasa, wakati supu hipo tayari?” aliuliza mama Peter huku anamtazama mume wake, alie kuwa anaendelea kutembea, “naenda kuchukuwa simu, ningee na huyu mpuuzi, siwezi kusubiri zaidi” alisema mzee Jacob, na wakati huo huo, wakasikia msagano wa pendri za baiskeri…..………..Endelea…
Zikija upande wao kutokea mashambani, na kuelekea upande wa madukani, “baiskeri hiyoooo tunaweza kuagiza mtu” alisema mama Peter na mzee Jacob akatulia kuangalia zinakotokea kelele za baskeri, yani upande wa mashambani, ambako pia ni upande anakoishi jikana wao Peter, ambako aliweza kumwona kijana mmoja wanae mfahamu akija na baskeri yake, ni yule walie mwagiza simu siku iliyopita, hivyo akasogea barabarani akamwagize awaletee simu hiyo, japo kwa sasa ilikuwa na lisaa limoja tu, toka imepelekwa chaji, safari hii tununue Solar yetu, sasa hii ni aibu” alisema mama Peter, huku akimtazama mumewe alie kuwa anamuwai yule kijana ambae ata kama asinge mfwata lazima angepita kuwasalimia.**
Peter alimaliza kuoga, na kama siyo kuogelea, kisha akavaa vyema kabisa nguo zake, na kutulia kidogo, akiwaza namna ya kuituliza njaa iliyokuwa ina msumbua tumboni mwake, wakati huo huo akiwaza juu ya mwanae Michael, juu ya hali ambayo yeye anajisikia, ile ya njaa, wakati huo huo akawaza juu ya kile kinachotokea juu ya kula na mwanamke huyu mrembo kitanda kimoja, mwanamke ambae jana alivua nguo mbele yake, “mbona anaonekana kuwa ni boss sana” aliwaza Peter, ambae alishangaa sana, Careen kufanya vile mbele ya kijana kama yeye ambae akuwa na mbele wala nyuma, maana alisha poteza kila kitu, na kilicho mfanya abakie kwenye viulizo, ni kwamba, mwanamke yule ambae ni Boss, alionyesha wazi kuwa anampenda kiukweli ukweli.
Wakati anawaza hayo, mala mlango wa chumba kile ukagongwa, na yeye akainuka haraka kwenda kuufungua, akakutana na yaya Glory, alie ambatana na Michael, shikamoo baba” alisalimia Michael, huku anaachia mkono wa yaya Glory, na kumshika baba yake yani Peter, marahaba Michael” aliitikia Peter, ambae alimtazama yaya Glory, na kumsalimia, “shikamoo mama” alisalimia Peter, huku uso wake ukishikwa na kijiaibu, kwa kile kilichotokea, “marahaba bwana Peter, naamini usikuwako wakwanza hapa nyumbani ulikuwa mzuri sana” alisema yaya Glory, kwa sauti tulivu iliyojaa furaha, kwa heshima ya shikamoo aliyopewa na bwana Peter, “nashukuru sana, lakini naamini sijafanya baya lolote, ata baada ya kulewa” alisema Peter, ambae nikama aliona lahisi kuongea na yaya Glory, kuliko kuongea na Careen mwenyewe, ambae wakati huo huo alisikika akiitikia salam kwenye kolido la ghorofa hii ya pili, sambamba na mlio wa visigino vya viatu, vilivyokuwa vinakanyaga kwa haraka kuja upande ule wa chumbani, “bila shaka Peter, kwani unawasi wasi na lolote?” aliuliza yaya na wakati huo tayari Careen alikuwa amesha fika, mbele yua mlango wa chumba, na kuchungulia ndani, macho yao yakakutana na macho ya Peter, wakajikuta wanatabasamulia, huku wanakwepesha macho yao, “salaam mume kipenzi, umeamkaje?” alisalimia Careen, huku anainamisha kichwake kidogo, “salama tu, sijuwi wewe” alisema Peter ambae bado akuwa anaelewa utaratibu wao wakusalimia ndani ya nyumba hii, “kwamaana ya kwamba akuwa anafahamu hasiri ya wakina Careen kuwa ni watu toka #mbogo_land, “mimi nipo salama, hofu ilikuwa juu yako maana nilikuacha….” alisema Careen, ambae alisita kidogo, na kumtazama Michael, alie kuwa anamtazama kwa macho ya tabasamu, kisha akamtazama yaya Glory, “basi twendeni tukanywe chai, alafu tuka nunue vitu ambavyo unaona ni muimu sana kwa safari ya kesho” alisema Careen huku anaukamata mkono wa Michael, “shikamoo shangazi” alisalimia Michael, na hapo hapo yaya akamdaka, “Michael niliakuambia huyu ni nani?” aliuliza kwa sauti ya upole na unyenyekevu, hapo Michael akalipuka kwa shangwe, “shikamoo mama” ilikuwa ni sauti ya juu iliyo changamka.
Ukweli kama kuna siku Careen alitabasamu basi kama hivi, basi ilikuwa zamani sana, kabla mfalme Elvis wa kwanza wa nchini kwao, Mbogo Land ajaipoteza furaha yake, kwa kuowa mwnamke wingine wakati yeye alizania kuwa urafiki wao watokea utotoni utageukia kwenye mapenzi, “marahaba Michael” aliitikia Careen alie kuwa ametangulia mbele, kifwatiwa na yaya Glory, nyuma kabisa akiwa Peter, ambae alikuwa amtoa macho yakuto kuamini kile kinachoendelea, huku wakielekea sebuleni.***
RCO Cletus Mlashan, alipotoka ofisini kwa RPC, alienda moja kwa moja ofisini kwake, huku uso wake ukiwa umesawajika, kwa mawazo yaliyo mletea hasira, maana licha ya kwamba mtuhumiwa anafahamika, lakini inakuwaje kila wanapo karibia kumkamata wanamkosa, au wanamkamata lakini wanakosa ushaidi, niwazi anakuwa anafahamu ujio wa polisi, swali linakuja ni vipi anapata taarifa za ujio wao, siyo mtuhumiwa mmoja tu, ni karibu wote, kila wanapoelekea kukamatwa tayari wanakuwa wamesha ondoa ushahidi wote, “kama huyu Kalonga, huyu ni wazi kabisa kuwa ni mwarifu, na habari zake zinafahamika, sasa inakuwaje tunakosa ushaidi?” alwaza Mlashani, akiwa ametulia kwenye kiti chake ofisini, “any way kama kuna mtu ndani ya jeshi anae tumiwa na huyu mtu, basi nita mpata tu” alisema hivyo huku anachukuwa simu yake na kupiga ofisini kwa OCd wa songea mjini, simu iliita kidogo na kupokelewa, “jambo afande” alisalimia OCD Mwanauta, ambae alionekana wazi kuwa ndani ya gari linalotembea, “jambo OCD, hupo wapi sasa hivi?” aliuliza RCO ambae alionekana kuwa alikuwa anaitaji kumpatia jukumu flani Mwanauta, “afande nipo njiani naelekea Hanga, kukagua vituo vya huko” alisema OCD Mwanauta, “ok! endelea na jukumu lako” alisema RCO nakukata simu, alafu akaipiga kwa OC CID, yani mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai, wilaya ya songea mjini, ambae ofisi yake hipo kule kule kwa OCD, yani kituo cha polisi cha wilaya, simu ambayo aikuita sana ikapokelewa, na CID mwenyewe, “shikamoo afande” alisalimia OC CID, marahaba, saa kunakazi nataka uifanye, piga simu kwa raia mmoja anaeitwa Pitus Kalonga, mwambie aje hapo kituoni haraka, mmpe masaa mawili, na akija nijulishe ninaitaji kuja kuonana nae” alisema RCO Mlashani, kwa sauti ya kaida tu, usingesema kwamba ni kamanda anatoa amri ya kuitwa kwa mwarifu mkubwa sana wa madawa ya kulevya, “ndiyo afande nampigia sasa hivi” alisema OC CID, na hapo RCO akatoa tahadhari, “kumbuka huo wito ni wakwako, siyo mimi” alisema Malashani, kisha akakata simu.**
Naam mzee Jacob aliletewa simu yake pamoja na namba ambayo ilipigwa na Sada kwenye simu ya mama Kachiki, hapo Mzee Jacob ambae alikuwa anamaliza kunawa ili aanze kupata supu ya kuku, apokea simu yakuku akapokea simu yake na kuanza kuandika namba ya simu aliyopewa na yule kijana, mwendesha baskeri.
Mwanzo alipoanza kuandika zile namba zilitokea namba nyingi kwekioo cha simu yake, nikawaida kutokea hivi, lakini kila alipokuwa anazidi kuziandika ndivyo namba zilivyokuwa zinapungua, na kubakia chache, na kitukilicho mshangaza ni kwamba, kila alipo zidi kuziandika namba zile, nambazote za simu ziliondoka na kubakia moja tu, ambayo ni nama ya kijana wake Peter, akaitazama mala mbili mbili kuahakikisha kama ajakosea, lakini aliona kuwa namba zile zinafanana kwa kila kitu, “au amekosea huyu, itakuwaje namba hii litokee jina la Peter, aliwaza mzee Jacob, huku anabofya simu yake na kuipiga, akia na uhakika kuwa kama nikweli namba ile alipiiga Sada, basi lazima watakuwa wote au nikweli alikutana nao, na anajiuwa sehemu walipo, wakati huo kijana mwendesha baskeri alikuwa amesha ondoka zake.****
Simu toka OC CID ilimkuta Kalonga akiwa nyumbani kwake, Mateka, ndio kwanza anaamka, ni baada ya jana kulewa sana pombe kali, “kuna tatizo lolote?” aliuliza Kalonga, ambae kiukweli licha ya kuitwa sana kituoni, na kuondoka akiwa ameonekana hakuwa na hatia, lakini mala nyingi uwa alikuwa anaitwa huku anafahamu kuwa lazima ata itwa, sasa leo mbona ajajulishwa chochote, “utakuja kujuwa ukifika kituoni, unachotakiwa kufanya report mala moja hapa kituoni, ndani ya masaa mawili uwe umefika kituo cha polisi wilaya” alisema OC CID, na kukata simu, hapo haraka sana Kalonga akapiga simu kwa OCD Mwanauta, ambae akuchelewa kupokea, “ndiyo bwana Kalonga umesha mpata mtu wako tuka mfanyie kazi?” aliuliza Mwanauta, ambae alonekana kuwa alikuwa ndani ya gari anaelekea sehemu, “kwanini ujaniambia kwamba ninaitajika kituoni asubuhi?” aliuliza Kalonga kwa namna ya kushutumu, “tuliabwana Kalonga, we nani kakuambia unaitajika kituoni?” aliuliza ASP Alfonce Mwanauta, ambae ndie mkuu wa polisi wilaya, nimepigiwa simu CID kwamba nireport kituoni ndani ya masaa mawili” alisema Kalonga, ambae naka zote Mwanauta amekuwa ndie msaada wake mkubwa, kumweleza mipango yote inayopangwa juu yake, “kwanini awa CID wanajiamulia mambo namna hii?” alifoka Mwanauta, kisha akamweleza Kalonga kuwa, atulie kwanza, yani asiende kule kituoni, mpaka yeye Mwanauta arudi, maana sasa alikuwa safarini kuelekea Hanga monastery, ikiwa ni safari ya kikazi, “niamini Kalonga hakuna kitu kitakacho aribika” alisema Mwanauta, kabla ya kukata simu, na hapo Kalonga alikuwa amesha tulia na kidogo, na kuondoa wasi wasi wake.***
Upande wa Sada mwenyewe tayari alikuwa amesha fika nyumbani kwa Emma, yani kwa mpenzi wake, kama ambavyo tunaweza kusema alikuwa ameshafika nyumbani kwake, maana ndiyo sehemu pekee ambayo alikuwa anaweza kuishi, akiwa amesha pitia sokoni kununua vitu vya kupika, akiwa ameongozana na Janja, “vipi ulisha wasiliana na huko nyumbani kwa kina huyu fala wako?” aliuliza Emma ambae alikuwa amejilaza kitandani, huku Janja akiwa amekaa pembeni yake, “nimesha ongea na mama, muda wowote tunapata jibu, alisema Queen, huku anatoa vitu kwenye mfuko, kwaajili ya kuanza mapishi, kwakutumia jiko la gas la mtungi mdogo, “ndio maana na kupenda sana Queen ujuwe hupo faster sana” alisema Emma huku anainuka kitandani na kuchukuwa kopo la sabuni, na ndoo tayari kuelekea bafuni, “chezea mimi wewe” alisema Sada, na wakati huo huo, dogo Janja nae akaaga, sasa bro, mimi wacha niende kwenye mishe mishe, si unajuwa bado sijapitia makusanyo ya boss” alisema Janja, akikumbusha jukumu lake, ambalo kwa sasa anamsaidia Emma, la kupita kwenye vijiwe vidogo vidogo vya kuuzia madawa yao, “ok! poa, ila kuna kitu nimekumbuka, mtafute dogo mmoja amfwatilie, Careen siunajuwa boss awezi kuacha kumfanyizia yule demu” alisisitiza Emma, kabla Janja ajaondoka zake,
Naam ile Janja anafunga mlango akiwa amesha toka tu, mala simu ikaanza kuita mle ndani, kwanza wote wawili wakatazamana, yani Emma na Sada, kila mmoja akizania ni simu ya mwenzie ndiyo inaita, kabla Sada ajakumbuka kuwa ni ile simu ailiyoiiba kwa Peter ndiyo ilikuwa inaita, “atakuwa mama huyo, sijuwi wamesha pata jibu” alisema Sada huku anatoa simu mfukoni na kuipokea mala moja, bila kuangalia jina la mpigaji wala namba yake, akizania kuwa ni simu ya mama Kachiki, “hallow niambie” alisema Sada, kwa kujiachia kweli kweli, “habari za leo Sada amjambo huko” ilisikika sauti ya kiume iliyo changamka kiasi, hapo kidogo Sada alishtuka maana sauti aikuwa ya baba yake, “nani wewe?” aliuliza Sada kwa ukali, mimi baba Peter, naomba kuongea na Peter” nikweli ile sauti ilikuwa ni yam zee Jacob, yani baba kwe wake wazamani…..…..………..

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata