
SEHEMU YA 52
ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA MOJA: “eti amepokea mwanamke, anasema yeye nifanyakazi kwa Careen, eti Peter yupo mezani anakula atapiga baada ya kumaliza kula” alisema mama Peter, “siunaona huuni huo, usinge mpigia simu yangu singe haribika” alilalamika mzee Jacob, huku anafunua kizibo cha simu na kutoa betri, “lakini baba Peter, nimesikia sauti ya mwanamke mwingine anasema lete hiyo simu, aongee, tena ameongea kwa ukali sana, nazani ni yule mwanamke wajana usiku” alisema mama Jacob, ambae nikama alishikwa na sinto fahamu…..Endelea…
Ukweli mzee Jacob akuitaji tena kuendelea kuzungumzia swala lile, “bwana eee, maliza kunywa supu, uandae ugari wanguvu, baadae tujinywee ulanzi wetu, huyo mjinga atajijuwa mwenyewe na ujinga wake” alisema mzee Jacob, kwa sauti iiyo jaa mapuuza, huku anaweka ile simu pamoja na betri lake juu ya kigoda, ni wazi akutaka kumiza kichwa chake kwa swala lile, japo moyoni mwake alikuwa na maswali mengi juu ya mabadiliko yam wane Michael, “lakini baba Peter, ni kweli Peter amelala kwenye ghorofa la Sada?” aliuliza mama Peter, yani mke wa mzee Jacob, huku anachukuwa bakuri ililo jaa supu ya na paja la kuku, “mh! uliona dalili ya kukaa kwenye ghorofa pale” alijibu mzee Jacob kwa mtindo wa swali, kwa sauti ile ile iliyojawa na kupuuzia.**
Yap! baada ya kumaliza kula Careen Peter Michael, walitoka nyumbani wakiwa na mschana mmoja wa kazi walitoka pale nyumbani wakitumia gari dogo aina ya BMW la kifahari kweli kweli, kuelekea mjini mjini kufanya manunuzi, ikiwa ni maandalizi ya safari ya kesho kijijini, safari ilianza kwa namna ya kipekee, maana ukiachilia Michael ambae alikuwa anaongea sana kumsemesha maschana wakazi, aliekaa nae seat za nyuma, akiuliza na kuonyesha kila alichokiona, ila kwa upande wa Peter na Careen ilikuwa kimya kimya, huku wakichake mala moja moja, kwa vituko vya Michael, na wakati mwingine wakijikuta wanatazamana na kutabasamuliana wakioneana aibu.
Naam licha ya manunuzi kuya fanyia kwenye maduka ya Careen mwenyewe, lakini pia walienda kwenye kampuni ya kuuza vifaa vya umeme wa jua, ambako waliweka oder ya vifaa vya umeme huo, kwa kiwango cha umeme wa nyumba kubwa, ambapo kwa utaratibu wao ukichukuwa vifaa kwa kiasi hicho, unapewa na mafundi wa kwenda kufunga, huku vifaa vikibebwa na gari la kampuni.
Ukweli ilikuwa ni siku nzuri yenye furaha kwa wote watatu, yani Peter Careen na Michael, ambao walizunguka sehemu mbali mbali wakiwa ndani ya gari, ni baada ya kumaliza kufanya manunuzi, tayari walisha nunua nguo na vitu vingi sana kama zawadi kijijini, upande wanguo na viatu, Careen alikuwa anamwuliza Peter, kwamba “hii inamfaa mama?, hii vipi nah ii” hapo kama kina mtosha mama au baba yeye angekubari na kama aikufaa basi angesema kuwa aimtoshi, japo hakuna kilicho kuwa kibaya vyote vilikuwa ni vizuri na vya gharama.
Licha ya wanafamilia awa kuwa wenye furaha, na wakina Peter na Michael kuvaa vizuri, lakini bado utofauti wao ulionekana wazi kabisa, na saa saba za mchana ndio moda ambayo Careen aliwaacha wakina Peter nyumbani, akiwaa amesha kula nao chakula cha mchana, na kuwaacha Peter na Michael wakianza kunyolewa na nywele zao, na vinyozi maalumu wa pale nyumbani kwa Careen, maana kulikuwa na saloon ya kike na kiume kwaajili yake na wafanyakazi wake,***
Yap! mida hii ya saa saba, ndio mida ambayo RCO alipopiga simu kwa OC CID nakumwuliza kama bwana Pisut Kalonga amesha fika kituoni kama alivyoagizwa, “afande bado ajafika, na tumesha mwachia masaa mengine mawili ya ziada, na ameshindwa kutii wito” alisema OC CID, “sasa umechukuwa uamuzi gani OC?” aliuliza RCO Mlashani, ambae mida hii alikuwa anajiandaa kwenda nyumbani kwake, ukichukulia kuwa leo ni siku ya ijumaa, ambayo baadhi ya askari wale wahumini wa dini ya kiislam wanakuwa wamesha toka mapema kwenda ibadani, “afande kwa sasa nitaka nitume askari wakamchukue, kama ulivyoagiza” alisema OC CID, “sawa sawa, na sasa uta mkamata kwa kosa la kuto kutii wito?” alisema RCO Mlashani, kabla ya kukata simu.***
Naam!! mida ya saa nane na robo, kijijini mwanamonga, kijiji kilicho changamka kupita maelezo, burudani zilikuwa zinaendelea, huku habari zilizo tamba ni zile za Sada kuwa na nyumba kubwa ya ghorofa, ambayo mzee Jacob na mke wake wanatamba kuwa kijana wao alilala jana usiku, na mbaua zaidi ni kwamba, kijana huyo yani Peter, ametoroka mwenyewe bila kuaga kwa Sada, kitu ambacho kilitafthiriwa kuwa ni wivu, habari hizo zilikuwa ni chukizo kwa mama Peter, ukimwachilia mzee Jacob, ambae alijitaidi kunywa ulanzi akichanganya na bia, ilialewe, na kuto kuyawaza mambo ya Peter, japo kila lilipo mjia wazo la Michael mjukuu wake, hakika roho ilimuuma, lakini alijitaidi kuyafukua mawazo hayo, “huyu mtoto akija kesho, yani ata nitambua, kwanza ata tutia aibu kubwa, akija na huyo mwanamke wake wa kuokota” alisema mama Peter, ambao sasa walianza kupokea wageni, mmoja baada ya mwingine, ambao baadhi yao walikuwa ni marafiki, na wengine walikuwa ni wambea waliokuja kuwa sanifu, kutokana na habari zilizo wafikia asubuhi ile, toka kwa mzee Nyoni na mke wake, ambao walijitaidi kusambaza zile habari kwauwezo wao wote, “yani zile mbwe mbwe zote za jana, “kumbe Peter amefikia kwa Sada?” nduvyo baadhi ya watu walivyo sema, huku wakimalzia kwa kicheko cha dharau, “yani inasikitisha sana, mzee nyoni ambae mwao amefanikiwa wamekaa kimya wala awajisifu, lakini wao mtoto wao amekaa sikumoja tu ghorofani tumejuwa kijiji kizima” ayo ni baadhi ya malalamiko ya wanakijiji, ambao awakuwai kujiuliza Sada amepata wapi mafanikio.***
Huku nako OCD Mwanauta, akiwa njiani anarudi mjini, akitokea anga monastel, alipigiwa simu na mmoja askari wake, anae fahamika kwa jina la Ezekiel Panga, “afande nime sikia OC CID anawatuma askari kwenda kumkata Kalonga, kwa kosa la kuto kutii wito” alisema Panga, na hapo OCD alishtuka kidogo, “eti! ni kwanini huyu mpuuzi ameamua kufanya ilo jukumu ghafla hivi, na kwanini ajaniambia kama kuna tuhuma mpya juu ya Kalonga?” aliuliza OCD kwa sauti ya kufoka, huku simu ikiwa sikuoni, “afande ninahisi kuwa ayo nimaagizo toka ngazi zajuu, hivyo inabidi ufanya jambo juu ya ilo” alisema Panga, na hapo sikapita sekunde kama tano ukimya ukitawara, “sikia Panga, mimi nipo njiani, nampigia simu Kalonga aje hapo kituoni haraka, na wewe wewe jitaidi, usiondoke hapo kituoi mpaka nitakapo kuja, uwe unanipa taarifa zote” alisema Mwanauta kabla ajakata simu, na kupiga kwa Kalonga, ambae bahati nzuri kwake akuchelewa kupokea simu, “ndiyo Mwana niambie” alisema Mwanauta ambae alionyesha kuwa alikuwa amelewa kidogo, “sikia kaka, acha kila unachokifanya nenda haraka kituoni kariport kama ulivyo ambiwa, sema ulikuwa nje ya mji, na ujitaidi uwe na mwanasheria wako, vinginevyo utazuiliwa mpaka jumatatu” alisema Mwanauta kwa sauti iliyojaa msisitizo, kabla ajakata simu, kisha akamtazama Dereva, “ebu endesha gari kadiri unavyoweza tunatakiwa kuwai kituoni haraka” ndivyo alivyosema Mwanauta, “yani awa washenzi, wakisha ona mtu anaviela tu, wanaanza kumwandama ili awaonge onge” alisema Mwanauta, kwa sauti iliyojaa hasira na lawama.****
Nusu saa baadae RCO Mlashani, akiwa nyumbani kwake, akiwa anajiandaa kupata chakula, mala akapigiwa simu na OC CID, kwamba Kalonga amesha fika kituoni, kwamadai kuwa, amechalewa kufika [ale kituoni, sababu alikuwa mbali na mji, “na amekuja na mwanasheria wake” alisema OC CID, na hapo Mlashani akatabasamu kidogo, “ok! mwache aende zake” alisema RCO na kukata simu, kisha akatulia na kumtazama mjuu kuu wake Jasmne, alie kaa kiti cha mbele kinachotazama na kiti chake, pale kwenye meza kubwa ya chakula.
Siyo mwamba Mlashani, alikuwa anamshangaa mjukuu wake, ila alikuwa anajaribu, kuipata picha ya mtu anae mwongoza Kalonga, aliepo ndani ya jeshi la polisi, aliwaza kuhusu OC CID mwenyewe, lakini akaona kuwa aiwezekani, akawaza kuhusu askari wachini wapale wilayani, lakini akawakosa, akawaza juu ya OCD mwenyewe, ambae ndie mkuu wakituo kile, na hapo pia akakosa usahihi wa mawazo yake, kwamaana alikosa wakumtilia shaka, “aiwezekani akawa mtu wanje ya pale, lazima atakuwa yupo pale pale, sasa ni nani huyo” aliwaza Mlashani ambae kiukweli aliitaji sana kupata ufumbuzi juu ya swala ili, la kiuchunguzi, ili aweze kumaliza kesi ya kuchunguza biashara hii ya madawa ya kulevya.***
Naam msaa matatu kwa Careen ndani ya ofisi yake, yalikuwa mengi sana, mala kwa mala alikuwa anapiga simu nyumbani, kuulizia juu ya wageni wake, “wanafanya nini sasa hivi” angeuliza Careen kwa sauti tulivu ya chini, na yaya angejibu, kuwa wapo saloon” hapo Careen ange tabasamu kidogo, na kusema, wakimaliza kunyoa nitumia picha zao” na maongezi yangfe ishia hapo, kisha yeye kuendelea na kazi zake, kwa muda wa dakika kama kumi au kumi na tano, kisha angeshika tena simu yake, na kupiga simu kwa yaya Glory, akiuliza kama wamemaliza, pengine angejibiwa kuwa bado wananyoa, nayeye angesisitiza kuhusu picha, ya wakina Peter, kisha ange kata simu na kuendelea na kazi zake, huku mala akwa mala anatazama simu yake kama kuna ujumbe wa Picha umeingia, akitazama mala kadhaa bila kuona basi ange piga simu kuulizia, na angepewa jibu la kwamba wamesha malizia na sasa ndio anawapiga picha, na sekunde kadhaa baadae angetumiwa picha ya wawili hao, wakiwa wamebadirika sura zao, na kuonekana katika mwonekano mzuri zaidi, ambae unamfanya Careen atabasamu, huku anabofya namba kwenye simu yake, na safari hii anampigia Peter mwenyewe, ambae anachelewa kidogo kuipokea, “mbona ume chelewa kupokea ulikuwa unafanya nini” angeuliza Careen kwa sauti ya chini na tulivu, “nilikuwa naangaika kupokea, amenisaidia huyu mama” pita alijibu huku anajicheka, na hapo Careen ange tabasamu, na kuongea kwa sauti iliyo changamka kidogo, “umependeza sana” na hapo wangeongea mawili matatu, kisha wangeagana kwa Careen kumsisitiza Peter kupumzika kidogo, kwa maana ya kulala.
Naam baada ya hapo, Careen ange tulia kwa muda akitafakari juu ya maisha mapya mausiano aliyo yaanza jana, huku akiwa amesihika simu yake yenye picha ya Peter juu ya kioo, ni kama alijiona mwenye furaha katika siku mbili hizi, yani jana na leo, hivyo anaona nivyema kama akiwajulisha wazazi wake juu ya mpenzi wake Peter, hapo anapekuwa namba za simu na kupiga kwa mama yake, ambae akuchelewa kuipokea, “salaam mama yangu mpendwa” alisalimia Careen kwa sauti tulivu iliyojaa nidhamu, “salaam mwanangu mpendwa, nikipi cha kupendeza kilicho kupigisha simu mchana huu?” aliuliza mama Careen ya ambae ni waziri wa mama watoto na jinsia, wa nchini #mbogo_land, katika serikali ya mfalme Elvis Mbogo kwanza.
kwanza Careen anaanza kwa kucheka kidogo, kicheko ambacho ata mama yake ukisikia mala moja moja sana, katika Maisha ya Careen toka alipovunjwa moyo na Mwenye Elvis, miaka miwili iliyopita, “nimepata mchumba mama” alisema Careen huku anacheka cheka, hapo ukafwata mshangao wa hali ya juu toka kwa mama Careen mke wa mzee Martin, “weee unahakika unacho kisema, ni nani huyo mchumba, ni mmoja wawafanyakazi wako, au ni mtazanzania?” aliuliza mama Careen kwa mshangao wa hali ya juu.……..
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU