
SEHEMU YA 66
ILIPOISHIA SEHEMU YA SITINI NA TANO: Bahati nzuri kwake, kila nguo na viatu alivyo vikuta mle ndani vilikuwa ni vipya kabisa, na avikuwai kuvaliwa ata mala moja, Sada akaachia tabsamu pana kweli kweli, “hapa nita jipatia ela ya kula” alisema Sada huku anarudisha vitu vile kwenye begi, na kujiandaa, tayari kuelekea mjini kuuza nguo alizo ziiba kwa mumewake wa zamani na mwanae wakumzaa…..Endelea…
Akiwa anamatumaini ya kupata chochote kitu, kutokana na upya nguo na viatu vile.****
Sasa naomba wahadithie kwa namna ya mjumisho, maana matukio mengi tanatokea sehemu moja.
Tayari mke wa Mlashani alikuwa amesha maliza kunywa chai, ilikuwa ni mala tu baada ya kutoka kanisani, na sasa walikuwa wanaingia ndani ya gari kuelekea NPF, kwenye viunga vya michezo ya watoto, ambavyo kwa siku za week end. wazazi uwaleta watoto eneo ilo, kwaajili ya kufurahi na michezo mbali mbali, huku wao wakikaa pembeni na kupata burudani mbali mbali, ikiwa ni pamoja na vinywaji mbali mbali, huku wakiwatazama watoto wao, wakibembea na kucheza michezo mingine ya kufurahisha,chini ya wasimamizi wa eneo lile.
bibi na mjukuu waliondoka nyumbani, wakimwacha mzee Mlashani anaanza kupitia baadhi ya nyaraka zilizo kuwa zinaelezea matukio mbali mbali ya kiuchunguzi namitego iliyoshindikana, au kuferi, kwa kusa ushaidi au kuwakosa watuhumiwa, katika msako wa wasafirishaji wan a waingizaji wa dawea za kulevya mkoani Ruvuma,
NPF ni sehemu ambayo inatumia mwendo wa dakika tano mpaka saba, tu kwa gari, tena kwa mwendo wakawaida toka kwa RCO Mlashani, endapo autopitia sehemu yoyote, hivyo mke wa RCO alisimamisha gari, kwenye maegesho yanayotazamana na lango la hospital ya mkoa, maana ndio upande wa kutokea nyumbani kwao.
Bibi yake Jasmin akashuka toka kwenye gari, akiwa na mjukuu wake Jasmin, na kwenda kumlipia kwaajili ya bembea namichezo mbali mbali, ili yeye arudi akatulie kwenye bar moja nzuri, karibu na pale kwenye maegesho ya NPF, ni pale ambapo Tina alitoa tairi la gari, la Jenssen (kiapo cha damu ya chui mchafu), hakika ni sehemu tulivu sana.
Masikini mke wa mlashani yani bibi yake Jasmin akujuwa kuwa, muda wote huo, kuna watu wanne, walikuwa wanamfwatilia kwa ukaribu sana, na sasa walikuwa wanasubiri mtego ukubari li waondoke na windo lao, ndio kwanza yeye akaagiza bia flani hivi nyepesi sana, inaradha nzuri sana, asa tena ata unapoinywa unywa laini kooni, na kuanza kuinywa taratibu, huku akitazama watu waliokuwa wanapita barabarani, kuelekea hospital na sehemu nyingine za mji, kaupepo mwanana kakimpepea.
Mita hamsini upande kushoto wa ile min pub, aliyokuwepo mke wa RCO Mlashani kulikuwa na gari aina ya Toyota Noah jeusi, lililokuwa limeegeshwa kwa kutazama upande wa ile pub, ndani yake kulikuwa na vijana wawili waliokuwa wanafwatilia kila hatua ya mama huyu, mita kama alobaini upande wakulia, jilani na mti moja mkubwa na mkongwe wa muembe, nyuma kidogo ya vibanda vya mama ntilie, (kama unakumbuka ndiyo eneo ambalo bi Celine, mama yake Jenssen alikuwa anauza chakula) lilionekana gari dogo aina ya Toyota IST, lililoegeshwa pasipo dalili ya mtu yoyote kushuka toka kwenye gari ilo, ambalo bila kuuliza tunalitambua kuwa ni gari wanalotumia wakina Emma, ambao mida hii walikuwa ndani yagari, macho yao yote wakiyaelekeza kwenye ile pub, kuhakikisha vijana wao wanafanya kazi waliyo watuma, “Janja ebu mpigie Dullah, mwambie wamfatwatilie huyo mtoto huko ndani” alisema Emma, huku akipekuwa dash board na kutoa msokoto wa bangi, kisha akaiwasha huku mwenzie Janja anatoa simu na kupiga kwa Dullah.
Mida hiyo hiyo hiyo, ndiyo mida ambayo gari aina ya BMW jeusi, lilikuwa linakatiza barabara kuu iendayo mikoa ya jilani, ndani ya gari ilo alikuwepo Jasmin, mlinzi kuu wa kampuni ya Careen, ambae alikuwa anaendesha gari ilo, pembeni ya Jasmin, yani upande wakushoto, alikuwepo Peter, ambae sasa alikuwa anatazama vyema mji wa songea akiwa ndani yagari, na wakati mwingine akitazama kwa umakini namna ya kuendesha gari ili, ambalo alina tofauti na gari lile analo tembelea Careen, pia kulikuwa na dada mmoja wa kazi ambae alikuwa amekaa seat ya nyuma, pamoja na mtoto Michael, wote walionekana kuwa nafuraha kubwa usoni mwao.
Lakini wakiwa wanakatiza eneo flani ambalo Peter akulijuwa kwa jina, wakawapita wazee wawili, yani mke na mume wakiwa wamevalia mavazi chakavu, na mfuko mkononi, wazee ambao ambao siyo tu kionekana kama wametokea kijijini, ila ni wazi walikuwa wametoka katika maisha duni.
Moyo wa Peter ulilipuka kwa mshtuko na mshangao, baada ya kuona sura ya mzee wa kiume, ambae aliambatana na mkewake, wakikatiza kwenye mchanganyiko wa watu, pembezoni mwa barabara, “mh! ebu kwanza, ni macho yangu au nikweli wenyewe” alsema Peter huku anagaeuza shingo yake kuwatazama wazee wale, ambao alihisi kuwafahamu, lakini kutokana na mchanganyiko wa watu akashindwa kuiona vyema sura ya mzee yule, ambae alimfananisha na baba wa mke wake wa zamani, yani mzee Nyoni, pengine nime mfananisha tu, sidhani kama anaweza kuwa amekuja huku” alijisema Peter moyoni, huku anatazama mbele, ambapo sasa aliona uzio wa NPF, ambao yeye hakuwa anafahamu kama wanaelekea hapo.
sekunde chache baadae akaona Jasmin anakata kona kulia kuinga, barabara moja ya upande wa kulia inayoelekea hospital ya mkoa, ambapo gari alikwenda ata mita ishilini, nalo likaingia na kuelekea upande wa hospital ya mkoa, huku Peter akisoma bango kubwa, lililo andikwa NPF KIDS CONER, jilani na hospital ya tumaini, (ambayo baba Tina, alikuwa anafanyia kazi, kabla ya kupata hajari),
“shemeji hapa ndiyo sehemu ambayo, Michael atacheza na watoto wenzake, wewe utatulia kwenye bar hipo hapo mbele, kuna vinywaji vya kila aina, na dada Careen atakukuta hapo” alisema Jasmin, huku anapunguza mwendo kukata kona kuingia kwenye njia panda ya kueleka mjini na ile ya kueleka upande wa magereza, na ndio upande wenye lango la kuingilia hospital lilipo, “hooo! sawa nipazuri sana, siku itaenda vizuri” alisema Peter huku anatazama upande wake wakushoto, ambako kulikuwa na gari dogo lililosimama pembeni kabisa ya barabara, chini ya mti mkubwa, wa muembe, jilani na vibanda vya mama ntilie, ambavyo pia vilimvutia Peter, ambae alivitazama mpaka walipovimaliza na kuingia eneo la wazi, lililotazama na lango la hospital na kuunganika na maegesho ya pili ya eneo la NPF, sambamba na bar ile ndogo, iliyowekwa katika mazingira tulivu.
Naam Jasmin alisimamisha gari, mbele ya ile bar, yani kwenye maegesho, na hapo Peter, Michael na dada wakazi wakashuka toka kwenye gari lao yani, BMW, Jasmin akaondoka kuelekea dukani, akiwaacha wakina Peter wakielekea sehemu ya kulipia ambayo walielekezwa baada ya kufika kwenye lango la kuingilia viungani, kiingilio kilikuwa ni kwaajili ya watoto pekee, nasiyo wasindikizaji.
Naam baada ya kulipia, dada wakazi akaingia ndani pamoja na Michael, huku mbele yao akitangulia kijana mmoja mwenye kuvalia kofia ya duara, na miwani ya giza, ambae pia alikuwa anaingia ndani ya viunga vile vya michezo ya watoto, huku Peter akirudi pale bar, ambapo palikuwa na watu kadhaa waliokuwa wamekaa wawili wali mpaka watatu au zaidi, wakipata vinywaji vyao, Peter akatazama sehemu ya kukaa ambayo ingekuwa nzuri kwake, ata Careen akija amwone kiulahisi, nae akaenda kukaa jilani na mama mmoja mtumzima, alie kuwa anakunywa bia yake taratibu, huku macho yake yakiwa barabarani, nauso wake ukionyesha wenye furaha,
Peter akutaka kuagiza pombe ya aina yoyote, maana aliona kuwa ni mapema sana, baada yake akaagiza soda na kuanza kuinywa taratibu, huku na yeye akitazama barabarani kuangalia wapiti njia, na magari ya aina mbali mbali, huku baadhi ya wadada waliokuwa wanakatiza maali pale wakiwa wanamtazama Peter kwa macho ya uitaji, unajuwa kwanini, ukweli Peter alikuwa amebadirika kimwonekano, yani alionekana hand some, kwa mavazi na sura pia.
Naam! mita chache toka pale alio kuwepo Peter, upande wa chini wa eneo lile, la NPF, baba na mama Sada walikuwa wanatembea taratibu pembezoni mwa barabara kuu, ya kutokea mjini kwenda nje ya mji, japo wao awakutambua kuwa ile ndio barabara ya kelekea kwao, maana wao ni wageni pale mjini, na bado walikuwa ndani ya mji.
Njaa ilikuwa ina wasokota wawili awa, ambao toka wamekula jana mchana, kule chakula ambacho walikichukuwa kwenye sherehe yam zee Mangolingoli, walitembea huku wakitazama kushoto na kulia, wakiwatazama watu wegi waliokuwa wanapisha nao, watu ambao, waliokuwa wanaelekea sehemu mbali mbali za mji, ikiwepo ni hii sehemu ya karibu ya NPF, karibu na eneo la michezo ya watoto, ambao ata wao waliweza kuona jinsi walivyo jaa kwa ndani, ya uzio mkubwa wa ukuta, wakiendelea na michezo yao.
Tayari wawili awa, walikuwa wamesha zunguka sana eneo la kati kati ya mji wa songea, wakiuliza sehemu anakoishi binti yao Sada, ambae walimuulizia kama mwanamke tajiri, mwenyeji wa kijiji cha Mwanamonga, majibu yalikuwa yamewachosha sana, maana akuna alie mtambua Sada Nyoni, “yani hapa mjini mwanamke tajiri ni mmoja tu anaitwa Careen, tena siyo wa hapa Tanzania, yeye ametokea #Mbogo_Land” ilo ni moja ya jibu ambalo walilipata mala nyingi sana, toka kwa watu waliokuwa wanawauliza,
“Imenichosha sana hii mama Sada, inakuwaje awamjuwi Sada” alisema mzee Nyoni, ambae alikuwa anatembea kichovu sana, “kweli ata mimi nimeshangaa sana kwanini awamjuwi, bora ata tungepajuwa anapokaa Kadara yule binti wa mzee Ndumbalo, angetupeleka anapokaa mwenzie” alisema mama Sada ambae pia alikuwa amechoka sana, huku wanatembea pembeni ya barabara, usawa wa uzio wa NPF, chini ya vimvuri vya miti mikubwa ya miembe, ya wakoroni, wakielekea wasiko kujuwa, “mama Sada ebu kwanza tutafute sehemu tupumzike kidogo, maana nahisi miguu inaniuma, alisema mzee Nyoni huku anatazama kushoto na kulia, “hapo umeongea neno, ebu tupumzike kidogo” mama Sada aliunga mkono wazo la mume wake.
Nikweli walikuwa wamechoka sana, maana licha ya uchovu wa kuto kulala vizuri usiku, wakitegemea muda wakuamka mapema kwaajili ya kuwai gari, pia walikunywa pombe nyingi sana jana usiku, na ukizingatia walikuwa mlo mmoja tu, mida ya mchana, “twende kwenye muembe ule kule, maana huku barabarani watu wengi sana” alishauri mzee Nyoni, akionyesha mti mkubwa wa muembe, ambao ulikuwa unaoneka upande wapili wa uzio. ….……….. itaendelea..
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU