KIAPO CHA MASIKINI (68)

SEHEMU YA 68

ILIPOISHIA SEHEMU YA SITINI NA SABA: aliwaza Sada, huku anamtazama yule mtoto wakiume ambae alikuwa amegeuzia mgongo, “ngoja nika wwauzie wale, nazani watakuwa na fedha, nitamshawishi niuze ata kwa bei ya hasara, kwani nguo zenyewe nimenunua mimi” aliwaza Sada, huku anapiga hatua kuwasolea wale watoto wawili, ambao walikuwa kwenye bembea ya uzani, mwadada alie valia vizuri akiwa pmbeni yao anawasimia, wakati huo jamaa mmoja alie valia kofia ya duara, akiwa pembeni ana watazama kwa umakini wale watu watatu. ….………..Endelea…
RCO Mlashani akiwa mezani anaendelea na kazi zake mala akasikia simu yake inaita, alipoitazama ilikuwa ni namba ya kificho, ambayo ilikuja kwa jina la Privaate number, kwanza alitaka kuiuudhia, maana uwa aendi ujinga mdogo mdogo, lakini akajitafakari na kujikuta yeye ni mtu muhimu katika maswala ya kipelelezi, pengine kuna raia mwema anaitaji kutoa taarifa muhimu, maana mala nyingi watu kama hao uwa wanaficha utamburisho wao pamoja na namba zao, “hallow na nakusaidie nini?” aliuliza Mlashani kwasauti tulivu yenye umakini mkubwa, mala baada ya kupokea simu na kiweka sikioni.

Hapo kwanza Mlashani akakutana na kicheko cha taratibu, kilicho jaa kebehi na dharau, “hoooo! bwana RCO, umefanya jambo jema sana kupokea simu yangu, lengo langu ni kukupa hongera ka ufanisi wako wakazi, ila kuna jambo umelisahau, kwamba hapa songea pana wenyewe, na wenyewe ndio sisi” ilisikika sauti nzito na tulivu, ambayo ilikuwa sawa na kile kicheko, ni kwamba huyu jamaa alikuwa na dharau nyingi sana, “tafahdari eleza shida yako, ninakazi nyingi za kufanya” alisema Mlashani kwa sauti kali, “kumbe una kazi za kufanya, basi tulia kunakazi nyingine inakuja muda mfu ujao” ilisema il sauti na simu ikakatwa.

Hapo RCO Mlashani akatulia kidogo akitafakari maneno ya mipigaji wa simu, “nani huyu na anamaana gani?” alijiuliza Mlashani, huku anaitazama ile namba iliyo mipgia, ambayo kiukweli, akuweza kuiona namba wala jina la mpigaji, maana namba ilikuja kwa kificho.

RCO alijaribu kufikiri kwa haraka, huyu jamaa anamaanisha nini, jibu alilolipata nikwamba, kuna tukio la makusudi amepanga kulifanya kama kitisho, sasa je ni wapi na saa ngapi, hapo ndipo pagumu, “lazima nifanye ambo la haraka” alisema Mlashani, huku anatoa simu yake na kuanza kupiga kwa wakuu waidara, pamoja na wakuu wavituo kuwa julisha juu ya kile kilicho tokea, huku wakiwataka wawe makini sana, kuanzia muda ule, na kwamba wavijulishe vikundi vya doria kuwa makini zaidi, na babaada ya hapo Mlashani akampigia simu dereva wake, akimtaka kuja pale nyumbani haraka, ili na yeye aanze kutembea mitaani, ikiwa ni kama doria binafsi.**

Julius Tindwa alitoka pale min pub, akiendesha pikipiki yake taratibu, huku anakichwani mwake , akiwa mwenye mawazo mengi sana, siyo kwamba akupenda mabadiriko ya Peter ambayo yalionyesha wazi kufanikiwa katika maisha, ila kilicho muumiza kichwa ni kwamba Peter amefanikiwa vipi kwa muda mfui kama ule, wakati yeye anamwaka mzima hapa mjini na kila siku anaingiza fedha isiyopungua elfu ishilini akitoa mafuta ya elfu saba, anabakia anabakia na na elfu kumi na tatu ambayo angegawa chakula na faida ya siku, lakini mpaka leo ajafikia ata robo ya mwonekano wa Peter ambae anamwambia kuwa anasiku chache sana hapa mjini.

Wakati Tindwa anakaribia kumaliza eneo la vibanda vya mama ntilie, ilibakia kidogo awasukume, watu wawili waliokuwa wanakuja mbele yake, akakanyaga brake kwanguvu, na kuwa tazama watu wale ambao ni wazi walionekana kukata taamaa ya kupona toka kwenye ile ajari, ya pikipiki, na kutaka kuwa fokea.

lakini ile kuwa tazama vizuri watu wale ambao umri wao ulionekana kuenda kidogo, asa kwa mavazi waluvyo vaa natembea yao ya kichovu, Tindwa akajikuta anatoa macho ya mshangao, “mzee Nyoni, imekuwaje ni wewe” alisema Tindwa, huku ana tazama sehemu ya kusogeza pikipiki, ili aweze kusalimiana vizuri na wazee, ambao siyo tu kwamba ajawaona muda mrefu, lakini pia, mwonekano wao ulikuwa wakutilia shaka, nikama vile walikuwa wamekuja kutazama mgonjwa pale hospital, au wao wenyewe mmoja wao alikiwa anaumwa, “nipo bwana Tindwa, ume tusahau kabisa kijijini” alisema mzee Nyoni, huku ambae muda wote alikuwa amejishika kwenye mkono, ile sehemu aliyo chomwa na bangi ya bwana Emma, amba kila siku analala na kuamka na binti, tusimame hapo tuongee vizuri” alisema Tindwa, huku anasogeza pikipiki pembeni ya barabara, na mwishoni mwa vibanda vya mama ntilie, yani kule walikotokea wakina mzee Nyoni.***

Naam Sada aliwasogelea wale watoto waliokuwa wanachezea bembea ya mzani, (nazani mnaelewa naposema bembea ya mzani, kwamaana ni bembea ya kukaa huku na huku) pamoja na yule mwanamke alie valia vizuri akiwa pembeni yao kuakikisha watoto wanacheza vizuri, na kwa usalama, “dada nguo na viatu vizuri, vinamtosha huyu mwanao wakiume” alisema Sada, mala baada ya kumfikia yule dada anae wasimamia watoto, “sante dada yangu, ila mimi siyo mama yao, mimi ni yaya wa huyu mtoto” alisema yule mschana kwa sauti tulivu iliyojaa nidhamu ya hali ya juu, “lakini unaweza kumnunulia tu ebu ona si kina mfaa hiki” alisema Sada huku anachukuwa kiatu cha mguu wakulia na kukosogeza kwenye mguu wa kushoto wa Michael, kwa lengo la kupisha, “he! kiatu changu” alipiga ukulele wa mshangao yule mtoto wa kiume, ambae sauti yake ilimshtua sana Sada, kutokana na rafudhi ya mtoto yule, kuwa na chembe chembe za kindendeule.

Hapo akainua uso wake na kumtazama yule mtoto, ili kuakikisha kama yeye anaye mhisi au siyo, twaa! macho yao yaka kutana, “he! Michel” ilikuwa ni sauti ya chini iliyoambatana na mlio mmoja mrefu, kama wa bata dume, linaloitaji kitumbua, huku Sada akiwa ametoa macho kwa mshangao akimtazama Michael, kama vile ameona kitu ambacho akukitegemeea kukiona kwenye karne hii ya ishilini, “ndio weweeeee uleiba viatu vyangu, nipe huko” alipiga kelele Michael, kwa sauti yake kitoto, sauti ambayo ilimgutua Sada toka kwenye mshangao, ambae kwa macho ya akatazama kushoto na kulia, kisha akamtazama yule yaya, “umesema wewe ndie mama unaeishi nae?” aliuliza Sada, huku anacheka cheka, “hapana mimi ni yaya wake, nipo hapa kumsimamia na kumhudumia” alisema yaya kwa sauti ile ile ya upole, na kumfanya Sada azidi kushangaa kwa kuto kuamini, anacho kisikia.

Ukweli kwa kile alicho wafanyia mala ya mwisho aliamini kuwa, mpaka sasa Peter na Michael wapo kijijini, na wanahali ngumu ya kimaisha, “nimepviatu vyangu nasema nipe viatu vyangu” alilalamika Michael huku anashuka toka kwenye bembea, kwa msaada wa yaya, na kumsogelea Sada, ambae alitazama kushoto na kulia, akaona watu wanamtazama kwa macho ya udadisi, asa kijana mmoja mwenye kualia kovia pana ya duara, alie simama mita chache toka pale walipokuwepo, akiwa anawatazama.

Hapo Sada akaona isiwe shida akaweka vile vitu chini, kuanzia begi nguo na viatu, kisha akatazama kwenye lango aliloingilia, akaona kuwa lilikuwa mbali sana akatazama upande wapili, ambako kuna min pub, akaona ni mita chache sana, hivyo akageuka upande huo na kuanza kutembea kueleka huko, kwa mwendo wa haraka sana, huku akisikilizia kama angeanza kuitiwa mwizi, lakini mpaka anakaribia mlango akuwa amesikia chochote.

Wakati huo nyuma yake, yaya alie kuwa anashangaa kwa kile kilicho tokea, “Michael inamaana huyu ndie mama yako, ambae aliwaibia fedha kule hotelini?” aliuliza yaya, huku anawatazama Michael na Jasmin waliokuwa anasaidiana kuweka vitu ndani ya begi, “siyo mama yangu, yule ni mwizi” alijibu Michael, huku wakimaliza kuweka vitu kwenye begi, “aya twendeni kwa baba, tuka mweleze kilichotokea” alisema yaya, huku anawaongoza watoto kuelekea upande ule ule aliotangulia Sada, ambae sasa alikuwa anamalizikia kwenye jiuchochoro cha kutokea upande wa nje, yani kwenye pub, huku kijana Dullah, ambae muda wote alikuwa anwafatilia wakina Michael Jasmin na yaya, akianza kuwa fwata nyuma yao, huku anapiga simu kwa Sebastian, simu ambayo aikuchelewa kupokelewa, “niambie Dullah nifanye nini?” aliuliza Seba, mala baada ya kupokea simu, “washa gari tazama hapo min pub, nikitokeza tu na wewe sogeza gari, acha wazi mlango wa nyuma” alisema Dullah na kukata simu.****

Naam huku nako, wote watatu yani Julius Tindwa, Mzee Nyoni na mama Sada, walisimama mitachache toka kwenye gari aina ya Toyota IST, nilile lile la vijana wavuta bangi, “kolikoni jamani, hiisafari ni njema kweli” aliuliza Tindwa, japo alijuwa kwa taratibu za kabira lao na watu kutoka vijiji vya kwao, unapo atikana mjini, na watu toka kijijini kwenu, na akaajuwa unapoishi, basi kila mmoja atataka kufikia kwako, ale anywe, aoge alale na kukaa sikukazaa, uzuri wao uwa awachagui pa kulala, ata kama ata lala sebuleni au kibarazani, yeye kwake sawa, ila awakujari kama ndugu au wakabira lao ni mke au mume, na ata kama ni house girl ungeshangaa wanakuja kupiga hodi, (angalizo, usije ukaogopa kuoa au kuolewa na kabira ilo, la wandendeule, kwaajili hiyo, maana wegeni uja na baraka zao)

“nisafari ya wema kabisaaaa, tena afadhari tume kuona, maana mpaka sasa tumezunguka weeeee mpaka basi, lengo letu tufike nyumbani kwa Sada” alisema mzee Nyoni, na mke wake akadakia, “yani tumeuliza kila mtu eti wanasema awaijuwi nyumba ya Sada” hapo kidogo ata Tindwa alishangaa kidogo, maana kitendo cha kusema wameuliza watu, na wanasema awaijuwi nyumba ya Sada inamaana wanamaanisha Sada nyumba yake ni maarufu, na inafahamika na watu wengi, “kwani yeye Sada aliwaambia anakaa mtaa gani?” aliuliza Tindwa, na hapo wakina mzee Nyoni na mke wake wakatazamana, niwazi kila mmoja moyoni mwake alishangaa lile swali ambalo walisha ulizwa mala kadhaa, walipokuwa wanamuulizia Sada,

“baba ukweli atujuwi anakaa mtaa gani, kwani wewe ujuwi anaishi wapi?” aliuliza Mzee Nyoni, huku mke wake akifafanua zaidi, “nilahisi kupajuwa yeye sasa hivi ni tajiri sana, anagari na anaishi kwenye jumba kubwa sana la ghorofa” alisema mama Sada, na hapo Tindwa akatabasamu, maana nikama alipata jibu kuwa, Peter kijana mchapa kazi, baada ya kulima kwa juhudi na kuvuna mavuno mengi, ambayo yamemletea fedha, hivyo ameamua kuja mjini, na kununua nyumba kubwa, lakini siyo ghorofa, maana fedha ya msimu mmoja aiwezi kununua ghorofa, “kwahiyo Sada alirudiana na Sada?” aliuliza Tindwa kwa sauti ya mshangao……………..

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata