
KIAPO CHA MASIKINI (77)

SEHEMU YA 77
ILIPOISHIA SEHEMU YA SABINI NA SITA: Wakati anawaza hayo ndipo alipokumbuka kuwasiliana na Peter iliaweze kumwalika katika chakula cha jioni, kitu ambacho kinge saidia kuweka ukaribu zaidi kati yao, na yeye kuweza kumfahami vyema Peter, na pengine kung’amua ukweli juu ya kijana huyu, ambae endapo angekuwa maaarufu au mfanya biasharaflani, lazima angekuwa anamfahamu, au angesha wai kukutana nae ata mala moja.….ENDELEA…..
Leo Sada akusumbuliwa sana na kiu au njaa, maana alikuwa na hakiba ya fedha ile aliyo ipata jana, baada ya kudanga kule bomba mbili, hivyo aliitumia akiwa na uhakika kuwa endapo ata kutana na Peter, atapata fedha nyingi sana, “mpuuzi yani sisi tunatafuta ela hapa mjini, alafu yeye anachezea na wanawake wazake” aliwaza Sada ambae sasa alikuwa anatembea kwa haraka kutoka upande wa kanisa la Roma, kuelekea mwisho wa lami, ikiwa ndiyo mtaa ambao mala ya mwisho alimwona anaelekea upande huu, yani siku ile aliyomtukana ale mtini pub.
Leo Sada licha kuwa na uhakika wa mlo mmoja wa mchana, ambao tayari alisha ufakamia, na maji ya vifuko, lakini hakuwa na uhakika wa kutumia usafiri wa pikipiki hivyo alitembea kwa miguu, na sifa moja wao ya mji wa songea ni vumbi, asa kama una tembea kwa buruza sendo zako, hiyo ilimtokea Sada ambae sasa alikuwa amechoka kupita kiasi, maana kumbuka kuwa ilikuwa ni kutoka saa mbili za asubuhi mpaka saa nane za mchana, bado alikuwa ana puyanga mitaani, minguu imechafuka vumbi vibaya sana, “yani mimi nasumbuka hivi alafu eti aniletee za kuleta, yani simwachii ata senti tano, alafu kale ka panya ndio nimezidi kukachukia, siyo kwa kuniumbua vile, eti alchukuwa viatu vyangu” aliwaza Sada, huku anaendelea kutembea, na kukaribia mwisho wa lami.
Naam ukweli Sada akuwa na mpango wa kupitia kwa kadara, na wala akuwa na mpango wa kuonana nae, na alimini kuwa Kadara ambae alikuwa amesafari, kwenda mwanamonga, atakuwa amerudi leo asubuhi, hivyo mida hii lazima atakuwa dukani kwake, alichofanya Sada, ni kukwepa ile nyumba, kwa kupita nyuma, kisha akaenda kuibukia kwa mbele na kuendelea na safari yake.
Lakini usilo lipenda siku zote ndilo ambatishi, yani ile Sada anaibuka tu barabarani, anakutana na boda boda, ambayo ilikuwa inatokea upande wa mjini, kupitia mtini pub, “simama simama” Sada alisikia kelele toka kwa habaria wa ile boda boda, “ayaaaa! kum…make, nimeruka mkojo nikanyaga mav..” alisema Sada kwa sauti ya kuchini, huku nasimama na kutazama ile boda boda, akamwona Kachiki anashuka toka kwenye pikipiki, “yani da Queen leo nimeamini ukimuwaza sana mtu, karibu unakutana nae” alisema Kadara huku anatoa fedha na kumlipa yule boda boda, kisha akamwabia akashushe mzigo wa mazaga zaga aliotoka nao kijijini, pale kwenye nyumba yenye duka nje, na boda boda akaelekea kule nyumbani kama alivyo ambiwa, huku yeye akibakia na Sada, ambae kiukweli aliona kama anapotezewa muda tu.
Yani dada Queen, mwenzio Peter ameacha gumzo huko kijijini” alisema Kadara ambae siyo tu kufahamu habari za Peter kupeleka vitu kule kijijini, ikiwa pamoja na TV, kwa wazazi wake, “gumzo la nini tena?” aliuliza Sada akionekana kuvutiwa na habari zile, “twende basi pale nyumbani nikakusimulie maana siyo habari ndogo” alisema Kadara na Sada ambae aliitaji kusikia umbea huo alikubari.**
Naam ili lilikuwa ni jambo jipya kwa RCO Mlashani, ambae moja kwa moja alipiga simu kwa mkuu wake, yani staff officer, ambae alimweleza kuwa alikuwa njiani anaelekea nyumbani kwake, “vipi Mlashani, kuna jipya lolote?” aliuliza staff officer, “afande hakuna jipya kubwa sana, ila nilitaka kufahamu kama ulisha sikia taarifa yoyote ya jaribio au kuvamiwa kwa yule mwanamke mmiliki wa mbogo land sonara?” aliuliza RCO Mlashani, kisha akatulia akisubiria jibu toka kwa bosi wake, “he! limetokea saa ngapi ni mchana huu, vipi yupo salama kweli?” aliuliza staff officer, kwa sauti ya mshtuko, na mshangao, “hapana afande siyo tukio jipya, ila nilitaka kusikia toka kwako, kama ulisha wai kusikia hapo siku za nyuma” alisema Mlashani, na hapo akasikia mkuu wake akishusha pumzi nzito, “dah! nilishtuka sana, nilizania baada ya tukio la jana, sasa wameenda kulipiza kisasi, ukweli sijawai kupata hiyo report ata siku moja, sijuwi RPC, ila na yeye angekuwa ameipata ngekuwa amesha nijulisha, ngoja nita muuliza, alafu nitakupatia jibu” alisema staff officer, ambae pia alimwuliza RCO, kama amesikia habari ya operation ambayo itaendeshwa usiku wa sikuile, kumkamata mshukiwa wa uingizaji na muuzaji wa dawa za kulevya, hapa mkoani Ruvuma,
“nilisikia toka asubuhi afande” alijibu Mlashani, ambae pia alikuwa anashangaa taarifa zile ambazo zilikuwa ni siri kumfikia staff officer, “sasa kwanini huku tujulisha?” aliuliza staff officer, ni kama lilikuwa swali la mtego maana ata sisi tunafahamu kuwa staff officer nae alifahamu swala ili toka asubuhi, “afande nikosa langu kuamini kuwa, operation hii ni ya siri, kama nilivyoelezwa ni OCD songea mjini” alijibu Mlashani, na hapo staff officer ni kama alitoa mguno mdogo wa ung’amuzi, yani kama vile ume ambiwa kitu cha kukufunua ufahamu wako, “eti hen, nikweli ata sisi tuliambiwa kuwa operation ni yasiri, ndio maana atukuliambia jopo” alisema staff officer, “ila afande wacha tungoje tuone, pengine kunamtu amelegwa asijulishwe juu ya swala ili, kwa kuofia kufichuwa siri” alisema Mlashani na staff officer akakuariana nae.
Hapo wakaagana na kukata simu, sasa Mlashani, akusubiri akaona nivyema akianzia chini, kutafuta ukweli juu ya matukio ya kuvamiwa kwa Careen, na kisha kusaidiwa na Peter.***
Yap Kadara alimsilia Sada kila kitu juu ya safari na mapokezi ya Peter na mwanamke wake kule kijijini, na jinsi walivyo funga umeme waja nyumbani kwa mzee Jacob, na kuwawekea TV na baadhi ya vitu vya ndani, “yani siku hizi watu wote usiku, wanajazana nyumbani kwa kina Peter” alisimulia Kadara ambae alificha yale ya aibu, yani kuhusu tuhuma za Sada kumwibia Peter, na pia tuhuma, za kuwakana wazazi wake, “alafu jana mama na baba yako walikuja huku mjini, vipi ulikutana nao?” aliuliza Kadara ikiwa ni kama swali la mtego, toka kwa Kadara ambae alikuwa anataka kusikia toka kwa Sada, kama sema kwa kinywa chake yale aliyofwanyia wazazi wake, “he! walikuja huku mjini, mbona sikukutana nao walikuja kufanya nini?” aliuliza Sada kwa sauti ya kushangaa, kama ungemwona mida hii, ungesema ni kweli akukutana nao, kwamaana yale wanayosema wakina mzee Nyoni, wanamsingizia, “basi wamerudi na mivitu kibao, naela kama zote, wanasema walipewa na Peter, ambae walikutaa nae huku mjini” hakika Kadara ni mpambe.
ukiachia tabia ya kadara ya kupamba maneno, pia alifanya hivyo ilikumchonkonyoa Sada, ambae mpaka hapo alikuwa ameachama msomo wazi kwa mshangao, huku kichwani mwake akiona kuwa ni jambo ambalo linawezekana kabisa kwa Peter kukutana na wazazi wake asa akizingatia kuwa pale alipokutana na wazazi wake, mita chaeke nyuma alikuwa ametoka kukutana na Michael, “hivi Peter anatoa wapi ela zote hizo” japo aliuliza kwa sauti ya wazi, lakini nikama Sada alikuwa anajiuliza mwenyewe, “mh! hivi umemwona Peter siku hizi, mbona unamsahau, ebu muone jinsi alivyo” alisema Kadara kama ambae alikuwa anasubiri sababu ya kuonyesha ile video, toka kwenye simu yake ambayo aliipakuwa toka kwenye mtandao wa kijamii, maana atoa simu yake haraka na kuanza kuipekuwa, “kwani na wewe ulikutana nae mpaka ukampiga picha?” aliuliza Sada huku anasogealea karibu kabisa pale alipokuwepo Kadara kwa lengo la kutazama anachotaka kumwonyesha, kwenye simu yake, “kwani ujuwi mwenzio Peter amekuwa maarufu siku hizi, ukiatazama tu face book unamwona” alisema Kadara ambae sasa alikuwa amesha ipata ile video na kuiweka, huku Sada aambae nikama alishindwa kuelewa anachomaanisha Kadara akiwa amekodolea macho kwenye simu ile………..….……..

