KIAPO CHA MASIKINI (80)

SEHEMU YA 80

ILIPOISHIA SEHEMU YA SABINI NA TISA: Jasmin akatazamana na Alpha, wakabasamuliana, kabla Alpha ajamtazama yule askari, “afisa nivyema ukianza tena mwanzo kufwata utaratibu, huo nilio kueleza, ila kunajambo unatakiwa kulizingatia, nikwamba unaemwitaji yupo nchini Mbogo Land, na anatarajia kutumia week moja huko Mbogo Land” alisema Alpha, na hapo yule askari kiongozi akatoa simu yake na kusogea pembeni, huku anabofya simu na kuipiga kisha akaweka simu sikioni, sekunde chache wakaanza kumsikia akiongea….Endelea……

Pasipo kusikia upande wapili wa simu unaongea nini, “afande zoezi limefeli….. jamaa amesafiri leo saa nne asubuhi kwenda #mbogo_land,….. ndiyo afande amesafiri na Careen…… ndiyo afande” alimaliza yule askari, kisha akakata simu, na kuwageukia wenzake, “ingieni kwenyegari” alisema yule askari, kwa suti ya kuamrisha, huku yeye akisogelea gari lile la polisi, na kufungua mlango wa mbele, upande wa abiria.

Pasipo kuaga wala kuongea chochote, askari wote wakaingia ndani ya gari na kuondika zao, wakiwaacha wakina Jasmin, na waafanyakazi wengine wakiangua kicheko, “Jasmin, nazani itakuwa vyema ukiwasiliana na Careen” alisema Alpha huku anaondoka zake kuelekea upande wa nyumba za wafanyakazi, “tena nampigia asa hivi” alisema Jasmin huku anaweka sawa simu yake na kuanza kubofya bofya, na kisha akaiweka sikioni, ambapo sekunde chache baadae akaanza kuongea na simu ile.***

Naam kijijini mwanamonga mambo yalikuwa bado ayapoa, watu walikuwa wanaendelea kuburudika wka pombe na nyama za kuku na mifugo mingine kama ng’ombe au mbuzi, huku taarifa za kitendo cha Sada kuwakataa wazazi wake zikiendelea kusambaa, sambamba na kuongelewa kwa habari za maisha mapya ya Peter, na mwanamke wake mzuri kupitiliaza.
Mida hii ya saa tatu, watu wengi walikuwa nyumbani kwa mzee Jacob wakitazama video, huku watu wazima wakiwa wamekaa pembeni kidogo, yani wazee makamo wake kwa waume, wakiendelea kunywa pombe, ambazo walizianza mida ya saa kumi na moja ya jioni, huku wakiongea na kubadirishana mawazo.

kati yawazee walikiwepo hapo, alikuwepo mzee Nyoni, ambae tayari alikuwa amesha lipa fedha ya mzee Kabwenga, na pia sasa walikuwa wamependeza kwa nguo mpya walizonunua mjini, muda wote awakuisha kumsifia Peter na mke wake, kwajinsi walivyo wakarimu, na wenye upendo, pia awakumsahau binti ya kwa kile ambacho aliwafanyia.***

Yap! OC Mwanauta, akiwa Kuchile Motel, pamoja na Kalonga, aliweka simu yake mezani, ni baada ya kumaliza kuongea na simu toka PC Sokoro, ambae alimpatia jukumu la kuhakikisha anamkamata Peter. kisha wanatimiaza leongo lao la kumbambika pakiti kadhaa za dawa ya kulevya, alafu, wamamshikilia kwa siku kadhaa kaya kudunga sindano ya sumu kwa lengo la kumuuwa, kwa kisingizia chamba amekufa kwaajili ya kutaa kula.

“huyu mshenzi ameondokaje nchini, pasipo sisi kuwa na taarifa yoyote, mpaka tumejivesha mkenge” aling’aka Mwanauta, ambae alikuwa amekaa kwenye kochi zuri la kisasa, nyuma ya meza ndogo, yenye chupa kubwa ya pombe kali, na grass mbili zenye pombe hiyo hiyo, “inamaana ameenda sehemu ambayo atuwezi kuifikia?” aliuliza Kalonga, ambae alikuwa amekaa kwenye kochi kama Mwanauta, huku amekunja nne, na sigara yake mkononi, “anasema ameenda Mbogo Land, na yule demu wake” alisema Mwanauta na hapo Kalolonga akashtuka kidogo, “weeee! yani wamefikia hatua hiyo?” aliuliza kwa mshangao Kalonga, “au amepiga juju mtoto wawatu, unazani yule fala anauwezo gani wa kummiliki mtoto kama yule” alisema Kalonga akionyesha kuto kuwa na imani juu ya penzi la Careen na Peter.

Hapo Mwanauta akujibu chochote, zaidi alitulia kama vile anawaza jambo flani, “sikia Kalonga hapa atuna muda wakupoteza kuwaza mapenzi yapo, cha msingi ni kufanya kitu ambacho kitatuwezesha kunmanasa Peter haraka sana pale atakapo ingia nchini” alisema Mwanauta, “unawazo lolote ambalo, linaweza kusaidia?” aliuliza Kalonga, na hapo Mwanauta akachukuwa grass na kusogeza mdomoni, ambapo alipiga funda moja, kisha akairudisha mezani, “tega watu wako kila kona, ili akirudi tu, tumuwai kabla ajafika nyumbani kwake” alisema Mwanauta, na hapo Kalonga akaitikia kwa kichwa kukubariana na mpango wa Mwanauta, huku Kalonga anachukuwa simu yake na kuipiga kwa Emma.***

Careen akiwa bado amekaa na wazazi wake na mpenzi wake Peter, wakijadiri kuhusu maisha kwa ujumla, huku wakipunga upepo, mala Careen akasikia simu yake inaita, akaichukuwa na kutazama mpigaji, “jasmine” alinong’ona Careen akitazama jina lililoandika kwenya kioo, sijuwi kwanini akili, yake ilimtuma kuwa nyumbani kwake kule Tanzania akukuwa salama.

Hapo Careen akaipokea simu mala moja, “Jasmin niambie mbona usiku sana?” aliuliza Careen, kwa sauti ya mshangao na uoga, na hapo kila mmoja yani Peter baba na mama Careen, wakamtazama Careen ambae alionekana wazi kuwa na hofu, “walikuwa wanamtaka wanini, mbona leo wamemuandama sana?” aliuliza Careen kwa sauti ya malalamiko, kisha akatulia na kusikiliza, kisha akasema, “wacha nimpigie yule mzee, maana yeye ndie alie anza kupiga simu mchana” alisema Careen, na kukata simu.

Naam wote waki wakiwa wanasubiri Careen awaambie kilicho tokea huko Tanzania, wakamwona Careen ana geuka na kumwita mmoja kati ya wafanyakazi wake, “nenda kaniletee ile simu kubwa, pale mezani” alisema Careen akimaanisha kuwa aletewe simu ambayo kwa sasa ilikuwa imezimwa, sababu ina namba ya mitandao ya Tanzania, ambayo kwa kule ilikuwa aifanyi kazi, “Careen kuna nini mbona unatuacha njia panda?” aliuliza mama Careen, “mama ukweli nashindwa kuelewa, yani jana Peter amemsaidia mjukuu wa mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai kule Songea, leo anaanza kupiga simu kuuliza maswali mengi juu ya Peter, kama aitoshi usiku huu, wamekuja kumkamata” alisema Careen kwa sauti ya kuchukia, “Careen kama unaona usalama wako ni mdogo huko Tanzania, unaweza kurudi uishi huku na mume wako” alisema mama Careen, kwa msisitizo, “hapana mama, najuwa Peter anaitaji kuwaangalia wazazi wake kwa ukaribu, pia tunaingiza fedha nyingi tanzania, itasaidia sana kwa mimi na Peter kufungua kampuni kubwa ya uandaaji na uuzaji wa vyakula, ambavyo pia tunaweza kuja kuuza hapa nchi kwetu” alisema Careen, kwa msisitizo

Nikweli Careen akukosea, maana nchi hii licha ya kuwa ni tajiri kwa madini na fedha, na vivutio vya utarii, lakini ilikuwa na maeneo machache ya kilimo, hivyo vyakula kama unga wa ngano wamaindi na mchele, pia mbaazi maaragwe na kunde, walikuwa wanategemeatoka nchi za jilani, “ni wazo zuri, lakini sasa ili swala inabidi ulikomeshe mapema, nitakusaidia kufanya hivyo, wacha kesho nikamwone mfalme” alisema mama Careen, lakini Careen akapingana na wazo ilo, “sipendi Elvis ajuwe matatizo yangu” alisema Careen, “inamaana bado tu unaugomi na Elvis ata baada ya kupata mumeo?” aliuliza mama Careen kwa mshangao, “wala sina ugomvi nae, kwanini iwe hivyo, Peter ni mwanaume bora, kuliko Elvis, amenifanya niwe na furaha, kubwa kuliko ile aliyo ipoteza Elvis” alisema Careen kwa sauti ya kujidekeza.

Wakati huo akaja yule mhudumu wao, akiwa na simu aliyo agizwa, mkono mwake, na kumpatia Careena ambae aliiwasha, tayari kuchukuwa namba za simu alizo ziitaji.***

Naam Ema akiwa na kijana wake Husseni, yani Janja, walikuwa pale msogeze pub, wanaendelea kupata vinywaji huku, kila mmoja akiwa na mwanamke, pembeni yake, ambao pia walikuwa wanapata vinywaji yao, yani pombe pia, “sasa mwanangu, leo wapi, siunajuwa siwezi kwenda gheto?” aliuliza Emma, huku anachukuwa glass ya bia na kuipeleka mdomoni, “kaka kwani kuna shida tukienda ghetoni kwangu, si unajuwa mimi naishi kisela” alisema Janja, na Emma akaunga mkono, “tena itakuwa bomba sana mwanangu, kwama kwenye video” alisema Emma na wote wane wakacheka.

Kabla ata kicheko akija katika, wakashtuliwa na mvumo wa simu, ya Emma, ambae ilikuwa mezani, wote wakaitazama, nikweli ilikuwa yenyewe, maana ilionyesha alama ya mwanga, huku kisota kwa mvumo wa mtetemo wake, inamaana ilikuwa kwenye vibration, Emma akaichukuwa haraka na kutazama jina la mpigaji, akaona kuwa ni, Kalonga, “hoya boss huyo sijuwi ananini” alisema Emma kabla ya kuipokea simu na kuiweka sikioni, “shikamoo boss” alisamia Emma, ambae baada ya hapo akusikika akiongea chochote, zaidi ya kuitikia tu, “ndiyo …… sawa boss…… najuwa boss, ndiyo boss” ilikuwa hivyo mpaka karibu na mwisho wa maongezi, “sawa boss, nitazingatia, na kuhakikisha safari hii atuzingui” alisema Emma kisha akatoa simu sikioni, ikionyesha imesha katwa, “hoya janja, kumbe yule fala alienda #mbogo_land, hivyo boss amesema kuwa tuhakikiche siku anayo ingia tuna kuwa nae sambamba, huku tuna mpa taarifa, wazee kazi wamdandie watuletee machinjoni” alisema Emma ambae safari hii aliweka simu yake mfukoni.****

Naam kama kuna usiku ambao ulitaka kumfanya Mlashani ajisikie furaha basi ni usiku huu, kwa kuamini kuwa akipata Peter ambae anaweza kuwa ni mshiriki wa Kalonga, basi itakuwa lahisi kwake, kumfanya Peter aeleze ukweli juu ya Kalonga, ambae alimini kuwa ni mshiriki wake.

Tayari alikuwa amesha liona gari la polisi, likiwa linarudi mjini, hapo Mlashani aka toa simu yake na kumpigia OCD Mwanauta, ili kupata uhakika wa mafanikio ya kazi, simu iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa, ata ikakatika, akaipiga tena, safari hii aliisikiza huku anaelekea nyumbani kwake, na bahati nzuri aikuita sana ikapokelewa, “hallow Mwanauta, nipe taarifa ya huko, mmesha kamata huyu mpuuzi?” aliuliza Mlashani kwa sauti iliyojaa shahuku, pasipo kusubiri salamu ya OCD “afande taarifa mbaya, mtuhumiwa ameweza kutukwepa, atuja mkuta eneo la tukio, na sasa tunaendelea kumtafuta” alijibu Mwanauta, na hapo, Mlashani akajikuta mwili ukipwaya, “uzembe gani tena Mwanauta, yani mmempoteza tena huyu mshenzi, tutapataje nafasi ya kumkamata na ushaidi?” aliuliza Mlashani, kwa sauti ya ukali, “afande nakuhakikishia safari ijayo awezi tena kutukimbia, tuta mtia nguvuni, na ushahidi wa nguvu kabisa” alisema Mwanauta, kwa sauti ya kujiamini, “ok! naomba taarifa ya kila kitachokuwa kinaendelea” alisema Mlashani, abla ya kukata simu, na kuingia ndani, ya nyumba yake.

Naam lakini kabla Mlashani ajafunga mlango wa nyumba yake, mala simu yake ikaanza kuita tena, moyo wake ukalipuka kwa shahuku, akizania kuwa Mwanauta anapiga tena kumpa taarifa mpya, aka tazama simu kutazama jina la mpigaji.

Hapo akatoa macho kwa mshangao, na viulizo, siyo kwaajili ya namba ngeni, ila namba ilikuwa ni ya nje ya nchi, tena toka, na aliitambua kilahisi sana, kuwa ni kutoka #mbogo_land, maana ata mwanae Johnson, uwa anampigia kwa mba zinazo fanana na code namba hizo….……..

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!