KIAPO CHA MASIKINI (81)

SEHEMU YA 81

ILIPOISHIA SEHEMU YA THEMANINI : Hapo akatoa macho kwa mshangao, na viulizo, siyo kwaajili ya namba ngeni, ila namba ilikuwa ni ya nje ya nchi, tena toka, na aliitambua kilahisi sana, kuwa ni kutoka #mbogo_land, maana ata mwanae Johnson, uwa anampigia kwa mba zinazo fanana na code namba hizo….……..Endelea…

Mlashani alihisi mapigo yake ya moyo yanaenda mbio, “nani huyu” alijiuliza Mlashani, maana alikuwa na uhakika kuwa aliepiga siyo Johnson, sababu Johnson mida hii awezi kupiga simu, kutokana utaratibu wa chuo chao ni kwamba, mida hii uwa wanakuwa wamelala, na awatakiwi kuongea na simu, wala kufanya kazi yoyote, na japo hakujuwa mpigaji ni nani, yeye ata akaipokea simu yake, na kuweka sikioni, “hallow Mlashani hapa, RCO Ruvuma nikusaidie tafadhari” aliongea Mlashani kwa tahadhari, hapo akakutana na sauti tamu ya kike iliyojaa utulivu, “salaam mheshimiwa” hao RCO Mlashani, moja kwa moja akahisi kuwa ata kuwa ni Careen, na kwamba ata kuwa anampigia simu, kueleza kilichotokea nyumbani kwake, Careen Martin wa mbogo land sonara, naongea toka jiji la Treanch Town nchini #mbogo_land” ilisikika sauti ile ya kike tamu na tulivu, ambayo toka mwanzo alisha itambua kuwa ni ya mwanadada mrembo mwenye #mbogo_land yake.

Mpaka hapo RCO SP Mlashan alishtuka kidogo, maana kuna kitu kilicheza akili mwake, japo alishaambiwa hapo mwanzo kuwa mwanadada huyu amesafiri kwenda nchini kwao, akiambatana na mume wake, yani Peter Jacob, lakini sasa kilicho mshtua Mlashani, ni ile kuambiwa kuwa vijana wake wakazi, walienda kumkamata Peter, na kwamba akuwa amesafiri, ila alikuwa na mpango wa kuingiza dawa za kulevya usiku huu, “hoooo! Careen ni wewe nilikuwa nashangaa hii namba, vipi mbona usiku” alisema RCO Mlashani, akijitadi kuficha mshangao wake, “nime pigiwa simu mala mbili leo, toka Tanzania, moja ilieleza juu ya simu yako, ulikuwa una muulizia Peter, naamini hukuamini jibu ulilopewa, kuwa amesafiri, nasema hivyo sababu ya simu ya pili niliyopigiwa, ambayo imeeleza ujio wa polisi kuja kukagua nyumbani kwangu na kumkamata mume wangu, je kuna tatizo lolote mheshimiwa?” aliuliza Careen kwa sauti ile ile tulivu.

Sawali lilikuwa gumu kidogo kwa mlashani, maana akieleza ukweli ni sawa na kutoa habari kwa mwalifu, na kumfanya azidi kujiweka sawa na kuficha ushaidi, ilikuepuka kukamatwa na ushiadi huo, na akisema ajuwi lolote, ata ulizwa kwa nini alipiga simu mapema kuulizia juu ya Peter, “hiyo taarifa mbona sina, kwani walikuja kumkamata kwa kosa gani?” aliuliza Mlashani ilikumtega Careen ajieleze mwenyewe, “ukweli kwenye hati ya kukamatwa kwa Peter, awakueleza wanamkamata kwa sababu gani” alijibu Careen.

RCO kaona amekwama kidogo, ila kwa ujanja wa hali ya juu, akapata swali la ushawishi, “ho! kumbe awakuwa na sababu ya kumkamata Peter, ila wewe mwenyewe Careen unazani kwanini Polisi waje kumkamata mumeo?” aliuliza RCO Mlashani kama mtego ili asike jinsi Careen anavyo jichanganya, katika kujibu, “hakika sijuwi” alisema Careen, na hapo Mlashani akaona kuwa Careen siyo mtu sahihi, wakumuuliza maswali yote hayo, na kitu cha msingi ni kuhakikisha kama kweli Peter yupo na Careen, huko Mbogo Land, “samahani Careen naweza kuongea na Peter?” aliuliza Mlashani, na Careen akuwa na pingamizi, “Peter ongea na yule mzee ulie msaidia kumwokoa mjukuu wake jana” RCO alisikia Careen akiongea, “hallow shikamoo mzee” ilikuwa sauti iliyochangamka ya kijana alie ongea nae jana pale NPF kids coner.

Kwamaana hiyo RCO alitambua moja kwa moja kuwa Peter alikuwa amesafiri nje ya nchi, “marahaba bwana Peter hanari za huko #mbogo_land?” alisalimia Mlashani, “mzee asikuambie mtu, huko kumekucha kweli kweli, yani nikuzuri, muda wote nikama mchana, yani ulaya ulaya, yani mpaka sasa bado naona tumbo kama ina pwaya, nikikaa hivi najihisi nipo kwenye bembea, maana nege siyo mchezo” alisema Peter akisifia kwa sauti iliyo changamka, kiasi kwamba RCO akajizuwia kucheka, lakini wakati huo huo akamsikia vicheko toka upande wapili wa simu, niwazi Peter alionekana mgeni sana, kwa matembezi ya mjini, “haaaa! Peter unaniangusha bwana, kwani ndio mala yako ya kwanza kufika huko?” aliuliza Mlashani, kwa lengo la kupata jibu, litakalo mlahisishia kumtambua Peter vizuri, “unauliza kufika huku, ata songea mjini yenyewe nime fika hii karibuni” alisema Peter akimalizia kwa kucheka kidogo.

Ukweli majibu ya Peter aya kuwa maigizo, ila nikweli ni kwamba Peter ameishi muda mwingi kijijini, “sasa Peter ebu niambia kwanza polisi leo wamekuja kukusaka nyumbani kwako, je unahisi umefanya kosa gani?” aliuliza Mlashani, kwa sauti iliyojaa urafiki mkubwa, “mh! mzee yani hapa nimeambiwa na Careen mpaka nimeshangaa, alafu wewe si polisi, kwani uko kazini kwako wanasema nimefanya nini, lakini ata kupagana nilimpiga yule jamaa kwasabu, alikuwa ni mwalifu, au nimejichukulia sheria mkononi? ata hivyo nazani utanitetea wasiniweke lupango” alisema Peter, kwa sauti iliyopoa ghafla, kiasi kwamba Mlashani aliingiwa na simanzi flani, kwa ona kama hisia zake hazikuwa sahihi.

“Ok! bwana Peter, ngoja nifwatilie nitakupa jibu” alisema bwana Mlashani na kukata simu, kisha akatulia akiwaza jinsi mambo yanavyo kwenda, “hivi awa wanauhakika na wanacho kisema, au wamechanganya kuwa Peter ndiyo amefwata ayo madawa, na kwamba atakaporudi ndiyo atakapo arudi nayo?” alijiuliza mzee Mlashani, ambae kiukweli imani yake kwa Peter bado ilikuwa ndogo, maana kuwai kuonamtu anajitolea namna hii, kumwoka mtoto, wa mtu asie mjuwa, “lakini Mwanauta anasema kuwa amewatoroka, inakuwaje awatoroke mtu ambae kwa sasa yupo nje ya nchi?” alijiuliza Mlashani, ambae sasa alikuwa anafunga mlango, na kisha akaelekea chumbani kwake, huku maswali mengi sana yakiwa kichwani mwake, ni kwanini wamemlenga mtu ambae kwa sasa yupo nje ya nchi, na wao wamesema mtu huyo amewatoroka, “hapana inabidi nifanye uchunguzi, tena ni uchunguzi binafsi” aliwaza Mlashani ***

Naam mambo yalikuwa ni mpwito mpwito, maana siku ya pili Sada aliamka na kujikuta akiwa peke yake kitandani, inamaana Emma akuwa amerudi, hii ilisha wai kutokea mala kadhaa, asa Emma anapokuwa na kazi za ziada, kama vile kuingiza mizigo yao haramu, au pale anapokuwa na mwanamke wa kulala nae, mida ya saa mbili Sada alitoka nyumbani, na kuelekea moja kwa moja mtaa wa Zanzibar.

Njia nzima Sada alikuwa anawaza kwa machungu makubwa sana, juu ya kile ambacho Peter amekifanya, na mbaya zaidi kila dakika zilivyosonga, alikuwa anazidi kupata machungu kwa kuona Peter amejifanya mjanja na kumsaliti, ukweli kwa hakiri ya sada mida hii, kama ungemwuliza kwanini anawaza hayo, kwakweli labda ange kuambia kuwa, ni mume wake, na ungemwuliza akimpata Peter ata mwambia nini, sijuwi kama angekupa jibu la kueleweka, japo moyoni mwake Sada, alijikuta anaumia sana kumwona Peter akiwa na mwanamke mwingine, tena mrembo na tajiri kweli kweli,

Naam, safari ya Sada iliishia mbele ya jengo kubwa la #mbogo_land, ambapo mida hii ndiyo lilikuwa limetoka kufunguliwa, na kwa siku za kazi kama leo jumanne, mida hii akukuwa na wateja wengi, hivyo ilikuwa lahisi kwake, kuingia ndani na kupata anacho kitaka.

Sada aliingia moja kwa moja na kwenda kusimama dirisha moja, kati ya mengi yaliyopo mle ndani, ambayo usimama wasimamizi wa malipo, ambae alikuwa ni mwana dada mrembo, “habari za asubuhi, nikusaidie tafadhari” alisema yule mhudumu, ambae kwa mharaka haraka, alimtazama Sada na kuona akuwa na kitu chochote cha kufanyia malipo, “naomba kuonana na yule boss wenu mwanamke” alisema Sada huku anajizuwia kuonyesha hasira zake, “ulikuwa unamwitaji kwa mambo binafsi au ya kibiashara” aliuliza yule mwanamke, muuzaji wa moja duka pale mbogo Land sonara, “mbona maswali mengi, kwani lazima ujuwe, we niambie nampata wapi” aliuliza Sada kwa sauti kavu ambayo sasa alishindwa kuzuwia hasira zake.

Hapo yule mwanamke mhudumu, wa duka akamtazama Sada kwa tahadhari, “nime kuuliza hivyo sababu, unae mwitaji hayupo” alisema yule mwanamke kwa sauti tulivu ya upole yenye nidhamu, “sasa kama hayupo, siunieleze nitapata wapi, kama ni nyumbani kwake, au wapi nijuwe, lazima leo nimpate” mpaka hapo yule mhudumu alikuwa amesha mtambua Sada ni mtu wa aina gani, hivyo aka chukuwa kipande cha karatasi, na kuanza kuandika, alipomaliza akamtazama Sada, “anuani ya sehemu ambayo anapatika sasa ni hii hapa” alisema yule mwanamke huku anainua mkono kumpatia Sada kile kipande cha karatasi, lakini kabla ajampatia vizuri Sada akakikwapua, kisha akaanza kutembea kuelekea nje ya duka.***

Mida hii tayari RCO alikuwa na makamanda wengine, ndani ya ofisi ya RPC katika kikao chao cha asubuhi, ambacho mpaka kina karibia kuisha saa tatu kasoro, akukuwa na mtu ambae alizungumzia operation ya siri, ambayo iliendeshwa jana usiku, ya kumkamata muuzaji na msambazaji wa dawa za kulevya, muda wote wakikao RCO alitamani kuliza juu ya operation hii lakini akujuwa ataanzia wapi, akichelea kuwa anaweza kuonekana ametoa siri ya operation ya siri, ambayo bado aijakamilika, na pia ukichukulia alimua kufanya uchunguzi binafsi.

Hivyo akabakia na duku duku lake, mpaka alipo maliza kikao, na kurudi ofisini kwake, akampigia simu kwa OCD Songea mjini, yani bwana Alphonce Mwanauta, ambae kiukweli akuchelewa kupokea simu yake, “jambo afande, alisikika mwanauta akisalimia, “jambo OCD, habari za kazi” alisema Mlashani, kwa sauti tulivu, “salama tu afande tunashukuru tunaendelea vizuri” alijibu Mwanauta, “ok! sasa ebu nieleze kuhusu awa watu, waliojaribu kumvamia huyu mwanamke mmiliki wa Mbogo Land Sonara” alisema Mlashani, kama vile anauhakika wa kile anacho kisema,

“hooo! afande umezungumzia jambo la muda mrefu sana, ni kama mwaka sasa upita, tena alikuwa ameshuku, siyo kwamba alivamiwa” alisema OCD, kama ambae alitaka kubabaika kidogo, “lakini OCD inasemekana kuwa siyo mala moja, na mala mbili kati ya hizo alizo vamiwa alisaidiwa na yule kijana alie msaidia mjukuu wangu” alisema Mlashani, akionyesha shaka na jibu la Mwanauta, “mh! afande kwakweli taarifa hipo moja tu, kuna siku aliingia hapa kituoni, akasema kuwa kuna gari limekuwa likimfwata kwa muda mrefu, askari aliowakuta waliangalia ilo gari, awakuliona na wakamluuhusu aondoke baada ya kuhakikisha akukuwa na mtu anae mfwata, baada ya hapo akukuwa na tarifa nyingine yoyote, labda kama alilipoti huko mkoani” alisema mwanauta.

Hapo Mlashani akashusha pumzi ndefu, kisha akatulia kama sekunde tano hivi, anatafuta swali la kuuliza, maana aliona kuna utofauti mkubwa wa jinsi hadithi yenyewe ilivyo, ukichukulia kuwa, yule mwanamke jana alimweleza kuwa amevamiwa mala mbili, na zote ameokolewa na Peter, na hiyo ni baada ya kuacha kutoa taarifa kituoni, kwakuona kuwa polisi hawakuwa na msaada wowote kwake, “OCD nivyema kama utakuwa unasema kile unacho kiamini, kuwa unauhakika nacho, vinginevyo nakushauri utafute jibu, maana hii ni kashfa kwa jeshi la polisi na wizara nzima ya mambo yandani, kwakushindwa kusimamia usalama wa raia, tena wakigeni” alisema RCO……….. itaendelea

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata