KIAPO CHA MASIKINI (88)

SEHEMU YA 88

ILIPOISHIA SEHEMU YA THEMANINI NA SABA: huku staff officer na askari wawili wenye bunduki zao, wakiingia kwenye gari aina ya Nissan safari, pamoja na RPC mwenyewe, safari ikaanza akiongoza RPC, aliekuwa anenda gari lake mwenyewe, “kaka unajuwa sijaelewa hiki kinachotokea, yani naona kama vile huyu mwanamke anauhakika na anacho kiongea” alisema RPC kwa sauti ya mashaka, “ni kweli kaka, kama kweli huyo kijana ndie alime mwokoa mjukuu wake, inakuwa iwe yeye ndie aliepanga kumteka?” aliuliza staff officer, lakini awakupata jibu. .. …..…..Endelea…

Ndani ya gari la wakina Careen safari ilikuwa kimya kimya, huku Careen akitazama simu yake mala kwamala, kama angeona ujumbe au angepokea simu ya kijana Peter, ambayo ingepigwa na polisi yoyote, ambae angeona missed call aliyopiga mwanzo, lakini akukuwa ma dalili ya simu yoyote wala sms, hakika alionekana wazi, mwenye majonzi makubwa usoni mwake, alitulia kimya huku akiwaza na kuvuta picha hali aliyokuwa nayo Peter wakati ule.

Naam baada ya kutembea kwa mwendo kidogo na wakiwa wanakaribia nyumbani kwa RCO, ndipo akapata Careen akapata wazo la yeye kupiga simu ya Peter, akaichukuwa simu yake na kupiga, nayo ikaanza kuita, “jamani mtu yoyote apokee simu” alisema Careen kwa sauti inayo karibia kulia, wenzake walibakia wanamshangaa, pasipo kumwuliza chochote, maana wanamjuwa boss wao anapokuwa katika hali kama hii uwa apendi maswali ya kipuuzi, asa wakizingatia, alishakaa miaka miwili pasipo kucheka wala kutabasamu.

Lakini simu iliita weeeee, pasipo kupokelewa kabisa, mpaka ilipo katika nyewe, ata hivyo akapiga tena, “nitapiga mpaka mtakapo ipokea” asema Careen kwa sauti yenye hasira za wazi, huku akipofya kitufe cha kuluhusu sauti ya wazi, loud speeker, maana alichoka kuweka simu sikioni, nayo ikasikika ikiita kwa wazi kabisa, na iliita mpaka ilipokatika, na sasa walikuwa wamesha fika, kwa RCO, ambae nikama alisikia ngurumo ya gari, maana alitoka nje, nao wakashuka, huku Careen anapiga tena simu ile, na kuweka sauti ya wazi.**

Ilikuwa hivi, baada ya kumpigia Simu Careen, ambae alimaliza kwa kuongea kwa hasira, Kalonga na Mwanauta, walicheka sana, “huyu mpuuzi leo lazima atoe kum.., sasa unajuwa nini Mwanauta, inabidi aongee na huyo fala wake ndipo atatia akili” alisema Kalonga huku akicheka kilevi, “hiyo itakuwa nzuri, lakini sasa itabidi tuwe makini, na kusikilizia taarifa zote za kipolisi, maana usishangae akaenda kutoa taarifa kituo cha mkoa” alisema Mwanauta, “hiyo siyo mbaya, cha msingi nikwamba, yule mjinga anauwawa usiku huu” alisema Mwanauta, huku anachukuwa sigara kwenye pakiti iliyo lala mezani, na kuiwasha, “kweli ilo ndio jambo la msingi” alisema mwanauta huku anachukuwa glass ya pombe toka mezani, na kuigugumia mafunda mwili, kisha akaiweka mezani na kuchukuwa simu, “ngoja niwasiliane na Panga, ilinijuwe wapo wapi” alisema Mwanauta huku anapiga simu, nakuiweka sikuoni, nayo ikaanza kuita.

Naam simu baada ya kuita kidogo tu ikapokelewa, “ndiyo afande niambie” aliongea Panga kwa sauti na mtindo ambao, katika hali ya kawaida angejikuta mahabusu kwa utovu wa nidhamu, “poa dogo, vipi mmesha pakia mzigo?” aliuliza Mwanauta, huku Kalonga anasikiliza kwa umakini mkubwa sana, “tumepakia kitambo sana, yani sasa tupo nusu ya safari, ndio tunarudi” alisema Panga, na hapo Mwanauta akacheka kicheko chs kufurahi, “nakuaminia Panga, fanyeni haraka neni TRM akisha malizeni yule fala, alafu njooni mjini, tuone inakuwaje, maana vijana lazima leo mjipongeze kwa kazi nzuri mliyofanya” alisema Mwanauta kisha akakata simu, “ijana karibu wanaingia mjini wakiwa na mzigo” alisema Mwanauta, huku anamimina pombe kwenye glass, “nakuamini Mwanauta, auna kazi mbovu, kilicho bakia ni kusafirisha kwenda Iringa na mikoa mingine” alisema Kalonga alie kuwa amekunja nne, huku anapuliza sigara yake.

Naam waliongea mawili matatu, kabla Kalonga ajatoa wazo lake, “hivi mwanauta unaonaje kama tukienda mjini, kuukagua mzigo” alisema Kalonga, na Mwanauta akaongezea point, nazani itakuwa vyema kama tutaenda TRM, maana huku mjini askari wengi watakuwa doria, awapaswi kutuona ata kidogo” alisema Mwanauta, na hapo wakachukuwa maamuzi ya kuondoka, “basi kama vipi tubebe vinywaji vyetu, tuelekee huko, ili wakifika pale watukute tumesha fika” alisema Kalonga, kabla awajamwita mhudumu, aje kuwa bebea vinywaji na kuwapelekea kwenye magari yao, maana kila mmoja alikuwa na gari lake.***

Naam Dullah akiwa amebakia na Peter alie kuwa amelala pale chini, huku amefungwa pingu kwa mbele, kwenye mikono yake, amejikunyata wa maumivu, huku wenzake wakina Jinja na Emma walio aga wanaenda kuchukuwa bia pale stend, wakiwa bado awaja rudi, licha ya kupita nusu saa, akaona isiwe tabu, ngoja asokote bangi yake, ili avute na kisha aendelee kumwangalia Peter, ambae kumbe, na yeye alikuwa anapiba hesabu za kumshinda huyu mmoja, ili aweze kutoroka eneo ili kabla wenzake awajarudi na kuwa wengi, kisha kumthibiti, mpaka muda waliopanga kumuuwa.

Lakini sasa wakati Dullah anasokota angi yake, mala ika sikika simu inaita, toka dirishani, Dullah akaitazama ile simu, “inamaana wale jamaa wamesahau simu yao” aliuliza Dullah, ambae akujisumbua kwenda kuitazama ile simu, ambayo iliita mpaka ilipokatika, na ikaanza kuita tena, na tena, yeye aliendelea kuunda msokoto wake, huku Peter ambae alisha juwa kuwa mpigaji wa simu ile ni Careen, akapiga mahesabu ya kuchomoka na kwenda kuichukuwa ile simu kisha kuruka dirishani na kukimbia zake, huku akipokea simu, nakuongea na Careen, amweleze kwamba, wale waliomkamata siyo polisi, ila ni majambazi, lakini kila alipo waza kufanya hivyo akaona itakuwa ngumu kuweza kumkimbia dullah, maana yeye amefungwa mikono, hivyo asingeweza kukimbia kwaspeed kubwa.

Naam hapo Peter alitulia akimtazama Dullah, alie sokota bangi yake mapaka alipo maliza na kuiwasha, alafu akaanza kuivuta taratibu, huku simu ikaanza kuita kwa mala nyingine, “kha! ukiona simu aipokelewi si unaacha kwanza bwana, alisema Dullah, huku anapiga hatua kwenda kuichukuwa, na hapo Peter akajuwa lazima Dullah angeichukuwa ile simu na kuiweka mfukoni, na akifanya hivyo ingekuwa vigumu kwake kufika mjini, bila kuwasiliana na Careen, maana akujuwa ata pale alipokuwepo ni wapi.

Hivyo basi Peter alimwesabia Dullah, hatua ya kwanza ya pili ile anakanyaga ya tatu, tayari Peter aliinuka ghafla, na ile Dullah anageuka kumtazama Peter, tayari kijana huyu mwenye kuitaji kutetea uhai wake alisha mrukia na kumkumba kwanguvu, akimsukumia ukutani, ambako alienda na kujibamiza kanguvu kwenye ukuita mgumu wa jengo lile, ambapo Dullah akupata ata anafasi ya kupiga kelele na kumkumba Dullah, maana alijibamiza kwa nguvu kwenye ukuta ule mgumu, watofari za sementi, kisha aka enda chini kama mzigo, usingeweza kuamini pale ambapo aliilalia bangi yake iliyo mdondoka toka mkononi, pasipo kusikia maumivu yoyote, sababu alikuwa amesha poteza fahamu zake.

Hapo haraka sana, yani haaka bila kuchelewa, Peter akaichukuwa simu yake, huku mikono yake ikiwa ime fungwa pingu kwa mbele, kisha akarukia dirishani na kujaribu kurukia nje, lakini akajikuta akianguka na kudondokea upande wa nje, nikukufikia kwenye kichaka cha nyasi, zilizojaa mebezi ya nyumba ile chakavu, kisha akajiinua haraka na simu yake mkononi, hapo pasipo kujari nyasi nyingi zilizo jaa mbele yake, yeye akaanza kukimbia kuelekea upande ambao akujuwa anaelekea wapi, ilo alikuwa jambo muhimu kwake, yeye alicho jari ni kwamba anaondoka sehemu ile na kufika sehemu salama, japo vichaka vile vilikuwa ni kubwa na virefu, kiasi cha kumzidi kimo.

Lakini Peter alikimbia pasipo kujari hatari ya kukutana na wadudu wadogo dogo wanao tambaa au kutembea, kama vile nyoka na wengineo, alipenya kwenye vichaka huku simu yake mkononi ikiendelea kuita, Peter ambae akuwa na uwezo wa kuikata sauti, ambayo inge weza kumuumbua, poa alitamani kuipokea ili aweze kueleza kilicho mkuta, na kuomba msaada, lakini akuweza kufanya hivyo, maana aliitaji kuondoka kwanza eneo lile, kabla wale wengine awarudi huko walikoenda.

Naam baada ya kumbia kama umbali wa mita hamasini au stini, Peter akajikuta ametokea kwenye jengo jingine kama lile alilotokea, akajiuliza ala mbili, akaakapanda kwenye dirisha, ambalo pia lilikuwa kama la nyumba ile aliyotoka, safari hii alikuwa makini sana sana, alirukia ndani na kutua salama kabisa, japo mguu mmoja ulikuwa unamaumivu, ni sababu ya kipigo toka kwa wakina Emma, na wale polisi,

Peter akuitaji kuendelea kukaa hapa nivyema akitafuta njia ya kuondokea hapa, lakini sasa atapitia njia gani kuondokea hapa, sehemu ambayo inafanana na NYAKASELO, ikulu ya Uganda zama za IDD AMIN, maana ilikuwa ikiingia na kutoka salama, lazima ukafanye sherehe kubwa, na kutambika kwa mizimu ya kwenu.

Hapo Peter akatazama nje upande wa kushoto kwake, kupitia dirishani, kuona kama kuna njia salama ya kuondokea eneo lile, hapo akaona eneo la wazi, na hakukuwa na vichaka kama zilivyo pande nyingine za lile gofu, kule kulikuwa na vichaka vifupi vifupi, na magari, chakavu na ile mitambo ya kutengenezea barabara (greder) iliyo aribika, akujisumbua kujiuliza yupo wapi, maana hapa songea mjini, hakuwa anafahamu sehemu nyinge yoyote zaidi mfaranyaki kule alikowai kuishi Sada, pia nyumbani kwa Careen, ofisini kwake, na kule mtini pub, pengine ni pale NPF, na stend ya kupanda magari ya kwenda kwao, Peter akaitazama simu yake ambayo sasa alikuwa imesha katika, akaona itakuwa vyema kama yeye ndie akipiga simu, pasipo kusubiri apigiwe, lakii wakati anataka aipige nayo ikaanza kuita, na kwabahati mbaya akaikata.****

Naaam dakika kadhaa zilizo pita, RCO Mlashani akiwa na mke wake ndani, anatafakali nia nazumuni la ujio wa RPC usiku ule, aliwaza mengi sana, na kujiuliza kama kunasehemu alikosea, au anakuja kumpa talifa ya kukamatwa kwa Peter, mtu alie panga utekwaji wa mjukuu wake, na kama kuna tatizo ni lipi, lakini akukumbuka chochote zaidi ya hisia, hivyo akabakia ametandwa na nusu wasi wasi, nusu akiwaza kama kuna jukumu muhimu anakuja kupewa, lakini kwanini iwe nyumbani kwake na siyo ofisini.

Lichaya kuwaza sana na kukosa jibu, Mlashani akaamua kutoka nje, maana akutaka mke wake asikie mambo ya kikazi, mala nyingi uwa hivyo, asa pale mkeo anapokuwa mdadisi sana.

RCO Mlashani baada ya kutoka, akukaa sana akaona mianga ya magari ina kuja upande wa nyumbani kwake, “huyoooo anakuja sijuwi kuna nini usiku huu” aliwaza Mlashani, ambae kwa upande flani alikuwa anahisi pengine ni kuhusu Peter, lakini baada ya sekunde kama tatu mbele akagunduwa kuwa, gari alikuwa moja, yalikuwa ni magari matatu, na yote ni yakiraia, akazania kuwa magari yale ayakuhusiana na ujio wa RPC, hiyo anatakiwa kuendelea kusubiri.

Lakini hisia zake azikuwa za kweli, aligundua hilo, mala baada ya kuona gari lililo tangulia liki kata kona kuingia kwake, akilitambua kwa haraka lile la mbele, kuwa ni gari binafsi la RPC, huku yale mengine mawili na mengine mawili yakifwata, na yote yakaja kusimama mbele ya nyumba yake.

Naam hapo ndipo Mlashani alipo shtuka, na kuanza kukumbuka maneno ya mke wake, maana licha ya kulitambua gari la mkubwa wake wakazi, lakini pia aliyatambua magari mawili yaliyo ongozana na gari lile la RPC, kwanza kabisa ni gari la Careen, ambalo lilikuwa lina julikana na kila mmoja, maana lilikuwa peke yake pale mjini songea, na pengine mkoa wa ruvuma kwa ujumla, hiyo ilikuwa wazi kuwa ujio ule ni kwaajili ya ukamatwaji wa kijana Peter, ambae mpaka sasa anashutumiwa. …..….

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!