KIAPO CHA MASIKINI (90)

EHEMU YA 90

ILIPOISHIA SEHEMU YA THEMANINI NA TISA: “afande za jioni ni salama, lakini siyo salama sana, maana jioni hii, imepigwa simu kuwa askari wa doria wanaitajika kwa RCO, na alie piga simu inasemekana ni RPC mwenywe sijajuwa kuna inshu gani” alisema afisa wa zamu, wa polisi wilaya, “unasema awajasema kuna inshu gani?” aliuliza OCD, kwa sauti ya mshtuko, huku analitazama gari la Kalonga ambalo sasa lilikuwa limesha potea kwenye upeo wa macho yake.. …..…..Endelea…

“afande awajasema wanaelekea wapi, kufanya nini, nilizania unafahamu lolote” alisema afisa wa zamu ambae kikawaida anakuwa na nyota moja au mbili mabegani mwake, hapo OCD ambae alianza kuona pombe inamtoka kichwani, alikatuliza kidogo hakili kdogo, akijaribu kuwaza juu ya jukumu jipya ambalo RPC anawaitia askari wote wadoria, tena bila yeye kujulishwa.

Lakini wakati anawaza huku simu hipo hewani, afisa wa zamu akaonekana kukumbuka jambo, “ila afande kuna tetesi ya kutoweka kwa mume wa yule mwanamke wa #Mbogo_land sonara, maana insdemekana alichukuliwa na polisi nyumbani kwake, lakini ajulikani amepelekwa kituo gani cha polisi” alisema afisa wazamu, na hapo OCD alikataka simu bila ata kuuliza swali jingine, na kuanza kupekuwa kitabu cha majina kwenye simu yake, akiwa na lengo la kupiga kwa RPC iliaweze kuuliza kama ni kweli wanamsaka Peter, na kama kweli wanasaka Peter, je watakuwa wamegundua yupo wapi, “lakini sidhani kama wamesha gundua kama wapo TRM, lazima wanataka kuanza msako” aliwaza Mwanauta, huku anaendelea kuitafuta namba ya afande wake.

Lakini alipoipata ile namba ya simu ya RPC, akasita kidogo kumpigia RPC, maana kunaswali lilimjia kichwani, “kwanini ajajulishwa juu ya tukio ilo, inamaana wanamzunguka ili kumchunguza, na vipi akiga simu nakuulizwa anajuwa nini juu ya tukio la kukamatwa kwa Peter, na kwanini alikaa kimya.

Hapo Mwanauta akaona nivyema kama ata wai haraka, eneo la tukio, yani TRM, wakamalize kilakitu na kupoteza ushaidi kwa kumuuwa Peter kabla awajampata, maana mpaka sasa Peter lazima atakuwa anajuwa mengi juu yao.

Lakini sasa, ile anataka kunyaga mafuta, mala akona mwanga wagari, inakuja tokea mjini, hivyo akatulia na kutazama upande wamjini yani nyuma yake kwa kutumia side mirro, akaona kuna magari kama matano yanakuja kwa mwendo wa kasi sana, na ata walipo mkaribia gari la mbele lilipiga honi ya tahadhari, kwanguvu sana, huku yanapita kwa speed ya hatari.

Nahapo ndipo Mwanauta alipo pata nafasi ya kuyatazama na kuyatambua vizuri yale magari, ambayo kati yake yalikuwa magari matatu ya polisi, yaliyo sheheni askari wenye bunduki zao za kivita, pia alitambua gari binafsi, la RPC, pia alitambua gari la Careen, yani land rover dicover toleo la kisasa kabisa, gari la mwisho akulitambua mwanzo ila alilitambua baada ya kutazama namba za usajili za gari ilo, ambazo zilililitambulisha kuwa ni gari la ubarozi wa #mbogo_land, yote yalikuwa katika peed kali sana, kuelekea mashariki mwa mji wa songea.

Hapo haraka sana Mwanauta alie ghairi kuondoa gari pale aliposimama, alitoa simu yake na kuipiga namba ya Kalonga, ambayo akuwa na aja ya kuitafuta, kutokana nakwamba, ile namba ilikuwa juu kabisa, katika orodha ya namba alizopiga au kupigiwa.

Lakini siku ya kufanyani, miti yote imepakwa mafuta, yani aikamatiki, kwamaana Mwanauta ailipoipiga namba ya Kalonga akambiwa kuwa namba unayopiga kwa aipatikani kwasasa, “kum..make huyu anawezaje kuzima simu wakati kama huu” alijisemea Mwanauta huku anakata simu na kuipiga namba ya Panga, ambayo pia ilikuwa pale juu ya kioo, kati ya nama alizozipiga muda mfupi uliopita, akaipiga nayo ikaanza kuita…**

Yap! Sada akiwa juu ya kitanda chake anajaribu kusaka usingizi bila mafanikio, maana sasa njaa ilizidi kumchonyota, akuwa na shilingi ata moja, “Emma siku hizi amebadirika sana, yani siku hizi ata ajuwi nime kula nini, yeye anaondoka tu aachi ela yoyote, na wakati mwingine arudi kabisa, kama amenichoka aniambie tu, ata mimi nina mwanaume wangu, na ananipenda sana” alijiwazia Sada au Queen, ambae alikuwa anajiugeuza geuza pale kitandani.

“Sijuwi nita lalaje, nahii njaa?” alijiuliza Sada, huku akisiliza ngurumo kwenye tumbo lake, kitu ambacho utokea endapo mtu anakuwa na njaa, “hapana uwezi kuninyasanyasa hivi wakati ulinikuta na maisha yangu” alijisema Sada, huku anainuka na kuchukuwa ndoo ya maji, na kuelekea bafuni, ambako akuchukuwa muda mrefu kuoga, na alipotoka bafuni akajiandaa kwa kujiweka sawa na mwisho akavaa nguo zake, ambazo kiukweli ukizona lazima ungejuwa anaeleka wapi, ilikuwa ni kijishati kifupi mpaka usawa wa kitovu, na chini alivaa kitaght cheusi, chepesi kupita kiasi, ambacho kilionyesha mpaka rangi ya chupi yake nyekundu aliyo ivaa ndani, kisha akafungua mlango na kutoka nje, “moja kwa moja Lipupuma” alisema Sada, wakati anafunga mlango kwa funguo, akilitaja jina la bar moja maarufu sana, kwa wanawake wengi wanao jilahisi kwa wanaume.***

Naam !!!!tukio lilikuwa hivi, wakina Emma, walifika pale TRM na kusimamisha gari lao, kisha wakashuka na kuingia ndani ya jengo ambalo, walimuacha Dullah anamtazama Peter, ambako mwanzo walimwona, mtu amelala, na wao wakazania kuwa alikuwa ni Peter, “Dullah yupo wapi, mbona amemwacha huyu jamaa peke yake amesha muuwa” alisema Emma, kwa sauti ya kuchukia, “hoya wefala, unalala kwani hupo kwa mkeo hapa” alisema Emma, huku ana mbutua teke yule mtu alie lala chini, ambae yeye alizania kuwa ni Peter, ambae awakuweza kumtambua kutokana na giza lililokuwa lime tanda mle ndani ya jengo lile chakavu.

Lakini wawili awa, yani Janja na Emma, walishangaa kuona kuwa, licha ya teke lile zito, lakini mtu huyu akushtuka, au kujitikisa kwa maumivu, “mh! Emma huyu jamaa kafa au” aliongea Janja huku ana ingiza mkono mfukoni, na kutoa simu yake, “kwanza yupo wapi huyu mshenzi?” ali uliza Emma, huku anatazama ushoto na kulia pasipo kuona mtu wala dalili ya mtu.

Naam baada ya kutoa simu yake mfukoni, Janja akawasha tochi ya simu yake ile, na kuangazia mle ndani, na hapo wote wakashtuka na kutazamana, ni baada ya kumwoa Dullah, akiwa amelala pale chini ajitambui tena, “emetoroka!!!!!” wote wawili walijikuta wanaongea neno moja, linalofanana, kisha awakakimbilia dirishani, na kuchungulia, awakuona mtu yoyote, zaidi waliona nyasi zilizo lala kuonyesha kuwa kuna mtu amekimbia na njia hiyo, “kaka huu ni msala, huyu fala ata kuwa amesha toa taarifa, na polisi wengine watakuja sasa hivi” alisema Emma huku ana anaanza kukimbia kuelekea nje ya jengo yani ni upande ule walio ingilia, “Pengine Boss alikupigia ili akuambie hii inshu, na alipoona upokei akaamua kuzima simu na kwaajili ya huu msala” alisema Janja ambae alikuwa anamfwata Emma, na ile wanaibukia nje tu, wakaona mwanga wa taa za gari unakuja upande wa majengo yale ya TRM, likitokea upande wa kulia wa eneo lile, yani ambako kuna barabara ya kuelekea Luhila stend.

Mwanzo walihisi kuwa, ni gari la boss wao, ni kutokana na mng’ao wa taa za gari lile, lakini kilicho wa shtua ni gari jingine lililoonekana ghafla nyuma ya gali ilo, na kufanya idadi ya magari kuwa mawili, tena ili la mbele likiwa katika mwendo wa kasi sana, “hoya wajomba haoooo” alisema Emma, kwa mshtuko mkubwa, wakihisi kuwa ni polisi, tayari wameshapata taarifa za kutekwa na Peter.

Naam hapo akuna alie ambiwa cha kufanya, wote wakageukia, upande wa kushoto wa jengo lile, kuanza kutimua mbio, kuelekea upande wa kushoto wa jengo lile, ambako kulikuwa kuna chochoro wa watembea kwa miguu, ulio tandwa na nyasi ndefu pembeni, lakini wao walikimbia kama wapo kwenye barabara ya mwendo kasi, awakujari gari na vitu vilivyo ndani ya gari ilo.***

Mida hii Sada ndiyo alikuwa anaingia Lipupuma Bar and Guest house, ambapo palikuwa pamejaa watu wengi sana, ungesema kuwa nib ado mapema, walionekana wanaume kwa wanawake, wapo waliokaa peke yao na wapo waliokaa wawili wawili, yani wake kwa waume, au wanau watu na wegne wanaume watupu.

Bahati ilikuwa upande wa Sada , ambae alikuwa amesimama anatazama pakuanzi, mala akashtuka akishikwa kalio toka nyuma, Sada aligeuka kwa hasira huku amesha andaa mkono kwaajili ya kuantupa kofi, lakini macho yake yakakutana na mwanaume mtu mzima alie onekana kulewa sana, “vipi mrembo, tunaweza….. tunaweza kwenda kukaa kwenye meza yangu” aliuliza yule mwanaume mtu mzima, hakika tabasamu alilolitoa Sada, ni lile la fisi mwenye njaa alieona mfupa, “wewe tu mepenzi, mimi sina neno” alisema Sada huku anamshika mkono yule mwanaume, ambae aliongoza kwenye meza yake

“mrembo agiza unacho taka ela hipo” alisema yule mzee mala tu baada ya kukaa kwenye viti vyao, na hapo ungeliona tabasamu la pili usoni kwa Sada, ambae alisuniri mhudumu na alipofika alimwagiza chakula kingi ambacho ungezania wanakula watu wawili, akuishia hapo akaagiza pombe kali chupa moja, na kuanza kuifakamia akujwa fika kuwa baada ya hapa lazima akalipie, kitu ambachi hakikuwa tatizo kwake, kitu ambacho alisha kizowea.**

Yap! Kalonga alisimamisha gari pembeni ya gari la kijana wake Emma, yani Toyota ist, na kushuka toka ndani ya gari, wakati huo gari kubwa la polisi lilikuwa lina simama nyuma ya gari lake, akulishangaa wala kuliogopa maana alijuwa kuwa ndio lilikuwa linaingia na mzigo wake wa bangi, toka kijijini Linjumbwi.

Wakina Panga wakashuka toka kwenye gari kubwa, na kuungana na Kalonga, huku wakiamini kuwa wakina Emma wapo ndani ya lile jengo, walilomwacha Peter, “Mwanauta ameishia wapi, alikuwa nyuma yangu?” aliza Kalonga huku wanatazama kule walikotokea, na waote wakashangaa kuona mwanga wagari una kuja kwa speed ya ajabu, “huyoooo anakuja” alisema Mwanauta, huku anachukuwa mlango wa gari lake na kutoa chupa ya pombe, huku wakati huo simu ya Panga ikianza kuita, na alipoitazama akaona kuwa mpigaji alikuwa ni OCD, hapo aka shtuka kidogo, na kutazama kule walikoona mwanga wa taa za gari, akaona ni zaidi ya gari moja, tena yalikuwa yame karibia sana, ni kama mita hamsini, “tumekwisha” alisema Panga kwa sauti ya chini, huku simu yake ikiendelea kuita, na wote wakatazama yake magari, ambayo sasa yalikuwa yamesha ingia mahali pale, huku magari matatu ya polisi yakisimama kwa kuwazunguka, huku askari waliokuwa kwenye magari yale wakishuka wka haraka, na kuzunguka huku wakiwa na silaha zao mikononi, “Panga nini kinaendelea inamaana Mwanauta amenizunguka?” aliuliza Kalonga kwa sauti ya kushangaa na mshtuko. …..…..

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata