CHAGUO LA MOYO (02)

SEHEMU YA 02

Baada ya kumjibu aliniambia sawa unaweza kwenda
Niliinuka na kurudi jikon

Wiki iliisha nikiwa nashinda nyumban

Siku moja alikuja mmama hivi akagonga nikaenda kumfungulia, aliingia ndani na kukaa Mimi nae huyo ni kaenda kumuita mamdogo

“Mamdogo Kuna mtu amekuja yuko sebleni”

“Mtu gani”

“Simjui

Okay nakuja.
Nilirudi na kummwambia amesema anakuja”

“Sawa binti”

Nilitoka na kwenda kwa wenzangu ambao walikuwa chumbani,kabla sijafika chumbani dada aliniita nakunipa nimpelekee mgeni mimi huyo nikapeleka na kumkuta mamdogo ameshafika

“Hee Martha kumbe umtoto mzuri hivi jamani,unajua sikuwahi kujua Kama umeolewa na mtu mweupe”

“Hapana huyu sio mtoto wangu ni wa marehemu dada yangu”

“🥺🥺ooo!jamani kumbe mama yake amefariki duh kanatia huruma bado mdogo Sana, Ila dada ako alizaa bwana khaa mtoto mzuri Kama nn ona unywele ona sura yake🥰aki nimempenda bure dada yako alikuwa ameolewa na mahindi au mwarabu maana sura yake ilivyo Kama muhindi alochanganya na mwarabu vile au nakosea” Sasa bwana nilivyokuwa kihele hele nikaropoka

“Hapana baba yangu sio mwarabu ni muhindi”weee niliona mamdogo kanikata jicho Hilo balaa mwenyewe nikageuza na kuondoka,
Sasa Yule mama Hadi anaondoka alikuwa akinisifia.

Baada ya kuondoka mamdogo aliniita na kuniambia

“Wewe ninani aliye kwambia nikiwa nimakaa na mgeni wewe unakaa au kuongea kitu,hiyo tabia ikome kwanzia leo sawaee

“Sawa “nilijibu na kuondoka baada ya kuambiwa niende,

Sasa watu walifululiza kuja pale nyumban naona no kumfariji kwa msiba,Sasa kila aliye kuwa akija alikuwa ananisifia kuwa ni mzuri sana jambo ambalo halikumpendeza mamdogo.

Baada ya watu kupunguza kuja nyumban,siku hiyo aliniita na kuniambia

“Kwanzia leo huruhisiwi kutoka/kuja sebleni mgeni yoyote akiwepo unanisikia ?”

“Ndio mamdogo”

Basi ilipofika jioni mamadogo akaniita na kuniambia niende nje kwa kaka was getini aninyoe nywele,yaani nilijihisi moyo 💔 vile napenda nywele zangu sikutaka kunyoa Ila sikuwa na jinsi basi kinyonge nikaenda kwa kaka wa getini 🥺

Nifika nakukaa alichukua wembe kutaka kuninyoa Mimi nikamstopisha. Kwa kusema mjomba siunatumia mkasi maana unazipunguza tu akajibu

Hapana mama yako kasema nikunyoe kipara………..😭woii jamani 💔 nikanyolewa bhna baada ya kumaliza niliingia ndani ukweli sikuwa nimependa
Mamdogo alivyoniona tu akasema enhe…… unatakiwa kuwa hivyo na huo ndio utakao kuwamuonekano wako siku zote utakazo kuwa humu ndani. Sawa ………

Sawa 😭😭

Unalia Nini kuna mtu kakupiga au
Aliuliza kwa ukali nikajibu

“Hapana”
“Sasa kinachokuliza ni kitu gani
Nitakupiga sitaki mideko ya ajabu hapa kwangu Mimi sio bibi yako sawaee

“😭Ndio” nikajibu huku nikifuta machozi
“Haya toka mbele yangu”
Nilitoka na kuingia chumbani nilikokuwa na lala na Dada nikajiangalia kwenye kioo kichwa kilikuwa kinawaka bonge la upala nililia pale Hadi nikalala

Sijui ni kitu gani kilitokea Ila mama yangu mdogo alibadilika Sana tena saana allikuwa akinikaripia bila hata sababu yamsingi nilifanya kosa dogo napigwa kipigo Cha paka mwizi
Nilikaa miezi na miezi bila kupelekwa shule kwajinsi alivyokuwa mkali kwangu niliogopa hata kumuuliza

Baada ya mwaka mmoja alimuondoa dada wa kazi kwakusema Hana sababu ya kuajili mtu wakati Mimi nipo,😓
Kumbuka hata shule hajanipeleka.
hivyo nikawa mtu was kazi tu nakumbuka wakati nakuja pale hawakuwa wamelima mboga mboga Ila baada ya dada kuondoka aliniambia natakiwa kulima mboga mboga na kila. Nywele zikikuwa kidogo tu napigwa kipala ……..😭😭

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!