CHAGUO LA MOYO (03)

SEHEMU YA 03

Maisha yalikuwa magumu upande wangu so kwasababu ya kufanya kazi no Bali matusi navipigo vya mara kwa mara,

Nilikuwa napika chakula lakin sikuruhusiwa kula hadi wao washibe so mara nyingi niliishia kushinda bila kula nilitamani niwe basi na kula jikon wakati napika Ila sikuweza maana aliweka. Camera hadi jikon Sasa ole wako akuone utaomba mbingu zifunguke

Nilimkumbuka Sana Bibi yangu na kumwambia Mungu kwann ulimchukua Bibi yangu 😭😭

Kila siku ilikiwa bora Jana yaani Kama nisipopigwa basi ujue nitatukanwa au sitokula siku hiyo

Chaajabu hata watoto wake nao walinibadilikia wakawa wakirudi shule wanavuruga vitu makusudi mda mwingine kama nimepika chakula nikatoka kumwagilia mboga nje wao wanakuja na kujaza chumvi Sasa mama yao akirudi😭ni matusi na kipigo juu

Hakuna kitu kilikuwa kikiniuma Kama alipokuwa alisema kuwa mama yangu alikuwa Malaya akajiona mzuri na kumpanulia miguu boss wake akidhani atamuoa mwisho aliishia kupata ukimwi 😭

Wakati huo alipokuwa anaongea maneno hayo nilikuwa na miaka 12 tu Mara ooo utakuwa Malaya Kama mama yako na utakufa na ukimwi mbwa wewe ,

Yaani alikuwa akikasirika anichagulii tusi linalomjia ndio Hilo anatoa

Niliendelea kuishi hivyo Hadi nilipofikisha miaka 20

Wakati huo moyo wangu ulikuwa unavuja damu yaani nilitama kuokolewa katika Yale maisha Ila wapi Nani aniokoe Sasa wakati huo nilikuwa nimeshakuwa binti na bado niliendelea kupigwa kipala tu nguo nilizokuwa navaa ukiniona unaweza 😭 nilikuwa nimezishona Shona Sana bila kusahau vilaka vilikuwa vyakutosha nilitolewa kwenye nyumba kubwa n kuhamishwa nyumba ndogo ambayo alikuwa analala mlinzi nyumba yenyewe ilikuwa ya chumba kimoja hivyo mm ndio nililala sebleni kwenye mkeka na shuka liliochakaa Sana huku mlinzi alikuwa analala kwenye godolo tena zuri

Lakini pamoja nashida zote hizo nilikuwa mzuri bhna 🥰 nakipala changu nikatunukiwa shepu ya mama weee nilikuwa mwembamba ndio Ila Kama nimecholwa vile 😁 sio kwamba najisifia hapana bwana ndivyo nilivyo

Basi nilikuwa navaa minguo mipanaa hatari

Nilikuwa kila siku namuomba MUNGU anitoe katika yale maisha Ila Hadi nafika miaka 22 sikuona mwanga au dalili ya kutoka nje 😓 nilikata TAMAA hata ya kuomba tena maana sikuona umuhimu wa maombi maisha yangu yalikuwa ya maumivu kiasi ambacho nilikuwa najiuliza kwann nilizaliwa kwann mimba isinge haribika tu kuliko kuja dunian kuteseka hivi nilivaa nguo ambazo zilikuwa zimeisha yaani nilikuwa naweka vilaka vya kutosha sikuwa hata na nguo ya ndani ,😓 (nadhani utakuwa unapicha ya maisha yangu Kama mtoto wakike kukaa bila nguo ya ndani inakuwaje hasa kipindi cha siku za hedhi)

siku zilienda hatimae ikafika siku ambayo Joyce alikuwa anasheherekea kuhitumu chuo kikuu………ilikuwa siku ambayo kila mmoja kwenye familia alikuwa na furaha ya kipeke yake nakumbuka niliambiwa nipike chakula Cha watu 100 watakuja kwenye sherehe sikuwa na pingamizi nilipewa vitu vya kupika na kikapewa mda kuwa wakitoka kanisani wakute chakula tayari …….basi niliamka saa kumi nakuanza kuandaa vitu ….mida ya saa moja alikuja mmama moja hivi alikuwa ni rafiki yake mamdogo

“Shikamoo mama Anethi”
“Marahabaa hujambo?”
“Sijambo “
“Nani yupo nyumban”
“Nipo mwenyewe’
“Sasa nisikilize nimekuja kukutorosha kwahiyo vaa hii nguo tuondoke”….😳kutoroka tukikamatwa je sinitauliwa mm

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata