
CHAGUO LA MOYO (11)

SEHEMU YA 11
Nilienda mezani kunywa chai nikamkuta Nicole yuko bz na simu yake aliponiona akaweka pembeni
“Pole dear”.
“Asantee”.
“Ila kuwa makini maana usije ukadhani mama amekutetea leo atakutetea na kesho kiufupi Berat ndii roho ya mama unaweza kushangaa akaenda huko chumbani akajifikilia Kisha akaja kukwambia ondoka so usimwamini hata kidogo pia hakikisha haumkwazi Berat tena maana inaonesha wazi hakupendi kuhusu Lee yule ni chawa tu kila anachofanya Berat anafagilia so akili yako iweke kwa Berat sawa dear”
“Haya asantee “
“Poa baadae mm naenda kazini “
“Haya byee”
Aliinuka na kuondoka baada ya dakika 3 akashuka Lee na Kaka mr kauzu…..nikipowaona nilihisi kutetemeka balaa niliinuka haraka na kutaka kuondoka Ila sauti nzitu ya Berat ilinistisha”subiri”……uwiii nimeishaa
“Nifuate”haraka hata bila kuuliza nilimfuata nyuma tunaenda kwenye chumba kimoja hivi akafika akaniambia
“Unga macho”
“Eee “
“Hujasikia au kiburi”
Nikaona isiwe tabu nikafumba baada ya sekunde kadhaa akasema “unaweza kufungua”
😳Nilitoa macho baada ya kuona pale chini kumefunguka na kuonesha ngazi zinazoshuka chini niligeuka nyuma kuangalia Kama niko humu ndani au nyumba nyingine ilikuwa ni nyumba hii hii nilitamani kuuliza imekuwaje hapa chini kumefunguka na hapaoneshi kuwa kunaweza kufunguka maana nadeki karibu kila siku
“Mbona umesimama nifate”
“Huko chini”
“Hapana huko juu”aliongea na kunivuta mkono tulishuka chini zaidi nilishangaa kuona kuna nyumba nyingine huko Ila kulikuwa kuchafu sana
“Nahitaji ufanye usafi humu ndani ya saa moja ukichelewa kunajifunga na hakuna mtu anaweza kukufungulia zaidi yangu na mm naondok…….
“Boss humu ndani nipachafu sana kwa huo mda hautotosha “
“Hiyo ni shida yako sio yangu”alijibu na kuondoka nikabaki na dua tu nisielewe kuwa nianzie wap niishie wap….. Nilizunguka kuangalia sehemu zote nyie kulikuwa kuchafu haswa kiasi ambacho ningetakiwa kutumia siku nzima ili pakae sawa Sasa hili lisaa nitafanya nn
Mwishoni niliamua kuanda huku nikijiongelesha mwenyewe……kutoka na kuwa ni chini nilishindwa kujua mda umeenda au bado maan hata jua nilikuwa silioni taa tu ndio ilikuwa on …… Nilifanya usafi kila mahari na nikajikuta nasahau kuwa nilipewa aaa moja tu baada ya kumaliza nilipanda ngazi kwenda juu ili nitoke kweli Kama alivyosema nilikuta kumefungwa “Mungu wang nitatokaje humu ndani”niliongea mwenyewe nikaona nigonge niligonga lakin wapi nikaita wapi mda ulizidi kwenda njaa nayo haikuwa mbali nilihisi njaa hatari…….nilikaa Sana bila mtu kuja nikaona Bora nichukue daftal na penseli nikaanza kuchora moja kati ya vitu alivyonibariki Mungu ni kuchora …… sijawahi kufundiswa na yoyote Ila nipe kazi nikufanyie hutaamini Kama ni mimi …. kwaiyo picha ya kwanza nilimchora Mr kauzu sijui kwann ila sura yake ilikuja machoni mwangu hivyo nikamchora yeye kwanza alafu nikachora na vingine…….nilitumia mda mwingi hadi nikachoka ila bado hakukuwa na dalili ya mtu kuja nilikaa mwisho nikapitiwa na usingizi ……….nilikuja kushituka na kujikuta nimelala kitandani kwangu haraka nikakurupuka ” hee vp unaota”ilikuwa ni Nicole naona alikuwa amekaa pembeni yangu “hapana nimefika je hapa”
“Umefikaje hapa kwani ulikuwa wapi?
“Nilikuwa kule c”kabla sijaongea alikuja mr kauzu na kumuita Nicole aliamka haraka nakwenda “imekuwaje niko hapa nani alinileta na mbona sikusikia🤔”nilijiuliza swali ambalo sikuwa na jibu nalo …….niliamka na kwenda sebleni hakukuwa na mtu niliangalia saa ilikuwa saa tano usiku…..😳heee inamana nilikaa kule Hadi usiku au nimelala Sana………
Nikaenda jikon nakukuta chakula kwenye sufuria nikakifakamia chap Sasa wakati nikiwa natafuna sinikamuona mr kauzu kasimama ananiangalia aisee nilipaliwa kidogo nife Sasa jinsi alivyo katili hakunipa hata maji badala yake aliondoka
Nilimaliza kula na kwenda chumbani kwangu kulala asubuhi niliamka na kwenda jikon nikakuta johari yuko bz anapika “za asubuhi”
“Salama,anhe jana ulienda wapi maana had tunaenda kulala ulikuwa haupo au ndio ushapata mwabwana huko”
“Hayakuhusu nilimjibu na kuondoka”
“Ha ha ha amakweli masikini akipata mata* hulia bwata leo hii unanguvu za kujibizana na Mimi”
Sikumjibu tena zaid niliondoka zangu nikaanza kufanya kazi nilifanya usafi kote ikabaki kwa Berat niliwaza namna ya kuingia nikawa nimesimama
Mara akaja Rahul”Sonia unaendeleaje”
“Niko poa vp wew”
“Safi mbona umesimama hapa badala upimzike sio vizur kufanya kazi ukiwa unaumwa”
“Nani anaumwa”
“Si wew au haumwi”
“Ndio mimi siumwi’
“Kwaiyo Berat alitudanganya maana wakati tunarudia alituambia kuwa unaumwa”
Mmmm huyu sialisema hapendi uongo sasa mbona kadanganya niliwaza”ndio nilikuwa naumwa Ila Sasa niko poa “
“Kweli “
“Ndio”
“Haya basi
Aliondoka nikabaki nawaza namna ya kuingia humo chumbani Ila naogopa nini so Niko kazin nikagonga hakujibu nikaingia ” za asubuhi”nilimsalimia Ila hakuitika nikaona utajiju kikubwa nimeshakusalimia nikaanza usafi yeye huyo………… nilifanya usafi nikamaliza nikaoga na kisha nikaona nilale zangu ……….zilipita siku mbili nikiwa na amani moyoni nikaamini kuwa maisha niliyokuwa nikiishi nyuma hayatajitokeza tena ………… Siku ya j mos niliambiwa kuwa kutakuwa na jumiya pale nyumban hivyo nilitakiwa kuandaa mazingira vizur baasi nikaanda kila kitu na mda ulipofika watu wakaja na sis sote tukatoka nje…………ibada ilianza Sasa mda wa kusoma neno Berat akanipa biblia ili nisome neno kwakuwa sijui kusoma nilitikisa kichwa kuashilia hapana Ila alinikazia jicho kuwa nichukue 😓nikapokea Sasa kipengele kinakuja naanzia wapi naishia wapi niliganda Kama sanamu “wewe siusome mbona unatugandisha hapa”aliongea Lee basi kinyonge huku mapigo ya moyo yakienda Kasi nilianza n e e m a y a m u n g u….. watu wote waligeuka na kuniangalia maana nilikuwa nasoma herufi moja moja Kama vile mtoto anaeanza kujifunza kuongea haraka Rohit/Rahul alikuja na kuning’anganya na kusoma yeye Mimi mda huo niliinamisha kichwa chini kwa aibu kulikuwa na watu wengi balaa ……..baada ya ibada kuisha tulirudi ndani mda huo niliamua kuonesha tabasamu Kama vile hakijatokea kitu “Sonia haujui kusoma”ilikuwa ni kauli ya kwanza mama aliuliza mara tu tulipoingia ndani.. …..”ndio” nilijibu Kama nikitu kizuri vile “Sasa Kama ulijua hujui kusoma ulikubari kuchukua biblia ya nn siungekataa kuliko kujidhalilisha vile”
“Huyu anakuwaga na kihalehele Sana anajiona anaweza kila kitu”alijibu Lee hatakabla sijamjibu mama
“Unaringa na uzuri kumbe kichwani zero brain mh makubwa “aliongea Johari huku akinipandisha na kunishusha”
“Inatosha kwani kipi Cha ajabu ” aliongea Nicole ……
“Naomba msahama kwakua nimewaaibisha”niliongea
“Sonia hina haja ya kuomba msamaha kwani haujakosea kitu”alinijibu Rahul huku akionesha kukosa furaha
Berat aliinuka na kuondoka bila kusema chochote Lee nae akafuata …… nikaona niondoke zangu
Nilitoka sebleni nikaenda chumbani kwangu nikafungua mlango na kuingia bafuni Kisha nikafungulia maji kisha nikasimama huku maji yakitiririka nilikuwa na maumivu makali 😓 japo sikutaka kuyaonesha kwa mtu yoyote …….hivyo niliona nibora nikalilie bafuni
…….. nililia huku maji yote yakinishukia na nguo zangu nililia kwa uchungu Sana
Baada ya kulia kwa mda mrefu nilinyamanza na kutoka bafuni ……….Ile nafungua mlango tu nilishtuka kumuona Rahul akiwa amekaa mlangoni ……….aliponiona tu alinikumbatia huku machozi yakimtoka ……..nilijiuliza kaingiaje wakati nilifunga mlango mda huo nilikuwa nimejufunga taulo tu
“I’m sorry kwakuruhusu macho yako kutokwa na machozi Ile hali nilikuahidi kuwa nitakurinda na kukupa furaha”aliongea kwa hisia Sana huku akiwa amenikumbatia kwa nguvu
“Rahul haujani”
“No Sonia nimekukosea nilitakiwa kuirinda furaha yako na sio kuiondoa”
“Laki”kabla sijamaliza Rahul alinikatisha kwa kuniwekea kidole mdomoni 🤫 nilikaa kimyana kubaki nikimuangalia tu alionekana Amelia mda Sana maana alikuwa mwekundu Kama nyanya vile 😁
Alinyoosha mikono yake na kunishika usoni na kusema “umenisamehe”
“Ndio”nilijibu hivyo ili asiendelee kuongea badala yake alinisogelea zaidi na kunikiss kwenye paji la uso. ……..Mara mlango ukafunguliwa nilishtuka nikataka kugeuka lakin Rahul alinivuta na kunikumbatia tena …………..”usiogope niko nawewe”alisema huku akiwa amenikumbatia………huyu annitakia nn Mimi
“Rahul”ilikuwa ni sauti ya Berat tena alionekana kukasirika Rahul baada ya kusikia sauti ya kaka yake aliniachia harka na kugeuka mlango ulipo ……..Mimi hapo nilitamani kukimbia Ila ningekimbilia wapi wakati mzee kasimama mlangoni
“Ni upuuzi gani huu unafanya”
“Brother huu sio puuzi Ila”
“Ila nn hujui huyu ni nani”
“Najua na ndio maana nafanya hivi “Rahul aliongea na kunishika mkono akanisogeza kwake mm hapo mkojo ulikuwa umeshabana niliona kuwa mda wangu wa kukaa humu ndani umeisha na sijui nitaenda wapi …….hivi kwann nisingekataa alivyonikumbatia badala yake nikasimama tu Kama mjinga ona Sasa nimeshaharibu 🙍♀️ nilimuangalia Rahul kwa jicho la niachie ila hakusikia
Berat alikuja na kunivuta kutoka kwenye mikono ya Rahul navile nilikuwa kembamba nilijikuta naangukia kifuani mwake aliniangalia kwa jicho kali huku akiwa amenishika kiunoni …………
“Mara watu wote wakaingia chumbani kwangu wakakuta Berat bado kanishika Nicole alivyoona alibaki😮
“Nini kinaendelea hapa mbona nasikia mizozo na mbona “kabla hajamaliza Berat aliniachia na kunitupia kitandani huyoo akaondoka bahati yangu taulo nililojifunga lilikuwa ndefu kidogo kwaiyo mapaja yangu hayakuonekana Ila alivyonirusha vile taulo lilitaka kudondoka nusura nibaki uchi Ila niliwahi kilishika Rahul alipoona hivyo na yeye katoka akiwa kafura hasira 😡
Kina mama wakabaki wananishangaa tu Mimi mda huo nimeinamisha kichwa chini
“Mnafanya nn ondokeni “mama aliwaguekia vijana wake na kuwaambia ……… wakaondoka akabaki yeye na Nicole wakiangaliana mama alikuwa nikama anajiuliza kimetokea nn hapa Ila akaondoka
Nicole alisogea karibu yangu nakusema
“Wewe ni Nini kinaendelea mbona nimeona Berat kakushika kiunoni tena uko na taulo tu”
Kwakuwa nilimzoea Nicole nikamwambia kila kitu
“Heee makubwa tangu lini Berat akaingia chumbani kwa mdada au kuingilia Mambo yasio muhusu hii ya leo Kali vp lakin Rahul alipokukumbatia umejisikiaje “aliniuliza huku akitabamu
“Sijasikia chochote”
“Na alipokukiss je”
“Sijahisi chochote”
Bwna mim nawewe ni marafiki so hauna haja ya kunificha kwanza natamani uwe wifi yangu lakina kwa

