CHAGUO LA MOYO (12)

SEHEMU YA 12

Natamani uwe wifi yangu Ila kwa Berat
“Eee😳”
“Ndio unajua pamoja na kwamba Berat ni kauzu Ila akipenda anapenda kweli na Hana kauli mbili sio Kama Hawa wengine wana manenoa elfu vitendo zero”
“Naona umenichoka wewe “
“Kweli Sonia au unampenda Rahul”
“Hapana “.
“Basi mpenda Berat kaka yangu nae apate mrembo”
“Kwamba hana”
“Kwajinsi unavyomuona unadhani anae”
Niliinuka maana naona huyu anaongea vitu vya ajabu ajabu tu eti nimpende Berat katika watu wakupendwa alendwe yule mtu mwenyewe yuko Kama Askari wa motoni 😏 siwezi mm Bora nikampenda Rahul kwanza anajali mcheshi na ana upendo Ila huyu Hana hata kimoja

Basi nilivaa na kwenda kunywa chai Ile nafika tu Johari huyu hapa “malkia Kama malkia aka miss kilaza naona ulikuwa umeshikiliwa na Berat eee yaaani kitoto kimalaya hata mwezi bado unaanza kuwachanganya wakaka wawatu puuee “
“Shida yako nn Kama unataka kagawe na we siunacho au ulitaka akushike wewe 🥴”
“Alafu hiyo jeuri ya kunijibu hivyo nitakuja nikupige na huo weupe Kama papai lililo Iva ukawe wa nyanya”
“Sawa thubutu unipige uone Kama huo weusi Kama kwapa na la nyani mjane nitauongeza mara mbili”
“Unasemaje wew “aliongea nakutaka kunivamia Ila akaa kimya huku akiwa amesimama nilisikia harufu ya marashi ya Berat nikageuka nyuma kweli bhn alikuwa amesimama huku mikono iko mifukoni uongo mbaya alipendeza Sana nikama vile alitusikia hivyo akaondoka bila kusema kitu
“Huyu ndio mwanaume Nicole anataka niwe nae kuongea tu anahesabu maneno 😏”niliongea kwa sauti ya chini
“Una bahati”aliongea Johari
“Sema Nina bahati sio unahabati “
Nilichukua chai na kunywa huku Johari akiwa ananiangalia tu

Ulipofika mchana tulitoka familia yote na kwenda sehemu kula nyie huyu kaka anatisha yaani haongei wala kucheka yukoje sijui maana hata mizimu inaongea Ila yeye hapana ………….walileta menu Rahul alikuwa amekaa karibu yangu hivyo akaniambia “utakula nn “
“Chochote “
“Okay “akanichagulia pale tukaa Kama dakk 20 chakula kikaletwa tulikula Kisha tukazunguka maeneno mbali mbali na usiku pia tukala huku hivyo tukarudi nyumban
“Sonia tunaweza kuongea”
Rahul aliniuliza
“Bila shaka”
“Asantee tunaweza kwenda kuongelea kwenye bustani”
“Sawa”.
“Njoo chumbani kwangu sasaiv”. Ilikuwa saut ya Berat niliangalia juu alikokuwa nikaitika “sawa, Rahul tangulia nakuja”
“Okay”
Nilipanda ngazi nakuingia chumbani kwa Berat
“Abee”
“Nifuate” aliongea na mm nikamfuata tulienda hadi kwenye kile chumba ambacho kuna njia ya kwenda kule chini …………..alifika na kunigeukia Kisha akaniangalia kwa sekunde kadhaa ….(huyu anataka kunijinja au mbona ananipeleka huku usiku huu)niliwaza
“Funga macho yako”alisema bila hata kuuliza nikafunga …………nilisisimka baada ya kushikwa mkono haraka nikafungua macho “nimekwambia funga macho”aliniambia baada ya kuona nimefungua macho ……….. niliangalia mkono alikokuwa amenishika Kisha nikafunga macho mda huo moyo unakimbia balaa……….”unaweza kufungua”aliongea na nikafungua tulishuka ngazi najiuliza huyu anataka kunifanya nn

“Kaa hapo”
“Ee”aliniangalia hilo jicho nikaaa chap alikaa na kupiga kinanda mm mda huo nimekaa tu ………….alipiga kinanda kwa mda mrefu bila hata kusema kitu Sasa kanileta hapa ili nione anavyopiga kinanda au nn maana haongei wala hajanipa kazi yoyote………Kuna mda nilitamani niinuke ili niondoke Ila ningeanzaje hivyo nikaona nitulie tu………..nilikaa wee mwishoni nikapitiwa na usingizi nilikuja kuamka nikiwa kitandani chakwanza nikasikia harufu yake nikakurupuka Kama vile nimemwagiwa maji ya baridi kuangalia hakuwepo na chumba nilicholala hakikuwa changu ilikuwa kule kule chini nikaamka fasta Ile natoka tu nakutananae mlangoni akasogea
“Shikamoo”nilisamia Ila hakuitika huyo nikataka kukimbia nilivutwa Kama kawaida naagukiaga kifua tu🙈 nilitoa macho Kama vile mjusi aliyebanwa na mlango moyo nao hauchelewi kila Mara huyu jamaa akiwa karibu yangu unakuwaga unataka kuniacha maana sio kwa kwenda mbio huku sasa sijui unataka kwenda wapi………..
“Umeamkaje”aliuliza kwa sauti flani hivi nzito
“Mhu”
“Unajisikiaje”..huyu atakuwa anataka kunitoa kafara sio bure kwanzia nili akataka kujua nimeakaje………” salama” nilivyomjibu tu akaniachia “unaweza kwenda”

Sijufanya kosa nilitoka ndukiii hadi juu Sasa ile natoka like chumbani Nicole huyu hapa

Enheee nimeshikwa sijui nitasema nimelala wap
“VP mbona unakimbia asubuhi yote hiii”.
“Hapanaa nilikuwa na”kabla sijajibu Rahul alitupita bila kusema kitu kwanza alikuwa kanuna balaaa

Sote tulibaki tunamshangaa maana sio kawaida yake…….Ila niliwaza atakuwa amenuna Jana sikutokea

Nilitoka na kuenda chumbani nikaingia bafuni nikapiga mswaki na kwenda kuanza kazi

Hadi unafika mda wa chai Rahul hakuja mezani

“Huyu Rahul leo ananini Hadi saiz hajaja kunywa chai”aliulza mama
“Naona leo ya uhindini yameamka “

Baada ya chai niliona nikaongee na Rahul maana nilihisi kuwa atakuwa amekasirika sababu yangu

Ngo ngo ngo niligonga mlango “ingia”
“Mamboo”nilisamia baada ya kuingia
“Kwann ulinidanganya”
“Rahul sikuwa na Nia ya kukudanganya ila “
“Ukaona haina umuhimu na lala wapi’?
Nilijikuta nakaa kimya baada ya kuulizwa hilo swali
“Ulilala wapi Jana”aliuliza tena
“Nililala nae mm kuna tatizo”
Ilisikika sauti nyuma yangu hakuwa mwingine zaid ya Nicole
“Alilala na mm na kuhusu jutokuja garden mm ndio nilimzuia so kama nikasirikie mm sio yye “
Baada ya kuongea hivyo niliona tabasamu la Rahul likirudi
“Sorry nilikukasirikia bure”
“Haina shida”nikijibu kwa wasi wasi huku nikimuangalia Nicole ambae alikikonyeza kwaishara nitulie”huyu anataka kufanya nn mbona kaongea uongo Kwan jana sialikuwa ameshall au alikuja chumbani kwangu akakuta sipo na mbona wakati tunaonana hakuniambia”nilijiuliza
“Nikakuketee chai”nilimuuliza Rahul
“Hapana nitaenda kunywa mezani”.
“Haya bye”
“Asantee kwa kujali”
Niliinuka na kuondoka Nicole nae akanifuata ………

“Mbona umemdanganya Rahul”
“Ulitaka nimwambie ukweli alafu akununie”
“Hapana kwanza Umejuaje kama sikulala chumbani kwangu”.
“Mwenyewe sijui labda nikuulize ulilala wapi “.
“Acha kunichota basi kama hujui kwann ukasema nililala kwako”
“Nilisema kwasababu nilisikia akisema kuwa hukulala chumbani kwako hivyo nikaisi utakuwa ulikuwa mahari labda kwa shem minitajuaje “
“Kwa Shem?”
“Ndio kwani wewe sister hadi usiwe na mtu, kwaiyo niambie ulikuwa wapi “.
Nilishusha pumzi Kisha nikasema” nililala huku chini”
“Chini? Chini wapi”
“Huku chini “
“Acha utani Umejuaje kama huku chini kuna nyumba wakati sijakwambia wala sidhani ka Rahul ameshakwambia pili huko chini hakuna mtu anae ingia zaid ya Berat tena na yeye hajaingia huko mwaka wa 3 huu Sasa wewe unasema umelala huku umefikaje na umejuaje?”
“Berat ndio alinipeleka “
“Weeee😳 Berat huyu kaka yangu au mwingine”
“Huyu huyu kaka yako”.
“Ilikiwaje”
Kwakuwa ni shositito wangu nikamwambia kila kitu
“Ulichanjwa au kabla ya kuja huku ulipitia bahari ya Hindi ukatoa mikosi au ulivunja nazi maana hakuna msichana yeyote aliwahi kuingia huko na si kuingia tu hata kujua walikuja hadi wakaondoka bila kujua hatae huyo Johari hajui Sasa ilikuwaje wew akakupeleka tena ukalal huko huko”
“Sijui “
“Mimi naona atakuwa amekupenda sio bure”
“😂😂nicheke kwanza wakunipenda awe yule’

“Ndio kwasababu haijawahi kutokea kabisaa”.
“Bwanaee tuachane nayo ngoja nikamalizie kazi zangu”
“Haya leo nitakuja kulala kwako tuongee vizur”

Tuliishia hapo kisha nikaenda kufanya kazi zangu

Usiku Nicole alikuja kulala chumbani kwangu tuliongea maengi Sana hadi tukalala

Kesho yake mchana nikiwa nimekaa alikuja Rahul na kusema
“Mamboo “
“Poa mzima”
“Yeah”.
“Mbona umewahi kutoka kazini”
“Nimekuja ili nikufundishe kusoma,”
“Alisema na kutoa vitabu akaviweka mezani

Nilimwangalia nikajikuta natoa machozi

“Sonia kimetokea nn mbona unalia au nimekukwaza”
Nilitikisa kichwa kuashilia hapana kisha nikamkumbatia na kusema
“Asantee kwakunijali “
Alitabasamu na kunikumbatia vizur Kisha akasema “niwajibu wangu kukujali so usilie”

“Mda huo huo akaingia mama uwiii nilikurupuka na kumsukumia pembeni Rahul mama alibaki amesimama kwa mshangao

Itaendelea

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata