CHAGUO LA MOYO (14)

Sehemu ya 14

Kesho yake asubuhi mama aliniita chumbani kwake nikaenda
“Abee mama”niliitika baada ya kufika

“Sonia nimekuita hapa kwasababu Nina maongezi na wewe “

(Mungu wangu nafukuzwa kazi au nn maana hya mambo ya kuitana chumbani inaonekana kuwa ni kitu Cha muhimu sana )niliwaza hivyo

“Ndio mama”
” Okay nimetaka kuongea na wewe kuhusu uwepo wako humu ndani aaa nilikuwa naona nikuhamishe sehemu nyingine maana hapa naona fujo zitakuwa nyingi na sehemu yenyewe ni huku huku lakin kwa jilani yangu hapo alafu nitatafuta mtu mwingine”

(😓 Nilijua tu)

“Mama kwani kunakitu nimekosea mbona kazi zangu nafanya vizuri”

“Sonia naomba nielewe binti yangu sio kwamba nataka kukutoa hapa kwasababu hufanyi kazi vizuri hapana ila kwasababu naona wazi kuwa ukikaa humu ndani itakuwa shida maana najua Berat hakupendi hata kidogo na kama sio mm kung’ang’ania wewe kupaki hapa basi ungeshaondoka mda sana pili naona Rahul anakupenda na hilo ndio tatizo kubwa maana hata weza kukaa kimya pale Berat atakapo kuwa ana kugombeza au kufanya chochote Cha tofauti hivyo lazima kutakuwepo na mpishano kwa watoto wangu kitu ambacho sitaki kukiona kinatokea “

“Sawa mama ” niliongea huku chozi likinitoka maana nilikuwa nimeshapazoea kuhusu Berat huyo niliona kuwa ndio changamoto yangu ambayo nilitakiwa kuikabili na sio kuikimbia sasa hii habari ya kuhama tena imeniumiza mno

“Usihofu Sonia najua umemzoea Rahul atkuwa anakuja kukuona Wala siwez kukataa wewe na yeye kuwa karibu ila tu kuwa makini sawa, alafu huko unakoenda Hana shida kabisa maana namfahamu vizuri hivyo kuwa na amani “

“Haya mama Asante sana “
Niliinuka na kutoka chumbani sasa ile natoka nikakutana na Berat huyu hapa aisee nilimkata jicho hilo Kisha nikampita fyaaa

Nilifika chumbani kwangu nikapang nguo zangu kwenye begi na kukaa tayar kuondoka

Mida ya saa kumi hivi ndio nilitakiwa kuondoka hivyo nikaburuta begi langu hadi seblen wote walikuwepo na waliponiona na begi wakashangaa

“We vp mbona uko n begi unaend wapi”aliuliza Nicole

“Anaondoka ‘mam alimjibu Nicole

“Anaondoka? Kwenda wapi?’

“Ataend kukaa kwa mama Abby”

“Heee kwann”Nicole na Rahul waliuliza mda huo mr kauzu yuko bz na sm yake yaani Kama hasikii vile

“Sitaki maswali we juma msaidie Sonia kubeba begi “
Juma alikuja akachukua begi langu n kutoka nalo nje

Mama aliinuka tukaanza kwenda mm sikuwa hata na nguvu ya kuongea ila moyoni mwangu nilitamani sana kusikia Berat akisema kitu lakin alikuwa bz

“Mama please naomba asiondoke kama kunakosa kafanya Niko tayar kubeba hiyo adhabu ila sio aondoke”

“Hapana hawezi kukaa humu ndani tena “
Walimbembeleza sana mama yao lakin wapi alisimamia msimamo ule ule
Alinishika mkono na tukatembea hadi na tunafika mlangoni Berat Bado yuko bz na sm yake nyie roho iliuma sijui kwann nilitamani kumfata nimwambie kwaiyo uko tayar mm kuondoka si ndio ila ningeanzia wapi

Ile tunatoka ndani tu nikasika sauti wait mom
Moyo ulicheza kiduku 😅 hembu subiri ni Berat kaongea au naota

Mwamba alisimama na kuja tulipo “anaweza kukaa tu’
Heee niliposikia hivyo meno 42 yote nje ona nimechakanyikia hadi nachanganya mambo meno 32 sio 42 msinipopoe jamani ni furaha imezidi

Sasa nikawa nawaza atkuwa kaja kunishika mkono anirudishe ndni kama kwenye season za kihindi vile ila mwamba akapit shwaaa moja kwa moja kwenye gari kpanda. Na kutoka nduki
“Heee huyu mtu vip tena”niliwaza

Mama aliningalia akatabasamu na kusem haya unaweza kurudi nilichotaka kujua nimeshakijua so karibu

🤔 Huyu mama vip alitaka kujua nn mara Nicole alikuja kunikumbatia na kusema waoo my wiso nilikuwa na hofu ila now nifuraha

“Acha kuzingua basi mimi ni wiso wako,? “

“Naisi hivyo siunaona Rahul alivyokuwa nataka kubeba madhambi yako yote 😅jamaa kadata”

Yaani wakati huo nilikuwa nipo pale kimwili tu ila akili na moyo vilikuwa mbali sana nilikuwa nawaza kama Berat hapendi mm kuwa humu ndani kwann amezuia nisiondoke na huyu mama ni bala Yani wengine wameongea wee Wala hakusikiliza ila huyu kauli moja tu kanirudiamsha ndani

Juma alirudisha begi langu chumbani mm na Nicole tukaenda chumbani kwake “ila leo ndio nimejua kuwa Rahul anakupenda kweli na siku ile nilikosea kukwambia kuwa uwe wifi yangu kwa Berat, hapana Bora uwe na Rahul mwanaume amabae anaweza kukutetea na kusimama na ww pia anajitoa sana kwaajili yako ila sio huyu kauzu yuko kama anagawa pumzi zawatu vile ‘
“Kwaiyo sasaiv unataka nitoke na Rahul ?”
“No usiingie kwenye mahusiano nae eti kisa nimesema no angalia moyo wako “
“Haya”
Mda huo huo akaja Rahul
Alipofika tu Nicole aliinuka na kuondoka
Tukabaki wawili

Rahul alinifata na kunikumbatia kwa hisia sana huku moyo wake ukienda mbio hatari

Mimi mda huo nimetulia tu kwenye kumbato wala sikuhisi tofauti yoyote

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

BINTI MDUNGUAJI FULL

BIKIRA YA BIBI HARUSI FULL

BIOLOGY TEACHER FULL

JOGGING MASTER FULL

error: Content is protected !!