SEASON 1: JOGGING MASTER (01)

JOGGING MASTER πŸ’žπŸ’ž1
(Master of LoveπŸ’—)πŸ’—πŸ’—πŸ’—πŸ’—πŸ’—πŸ’—πŸ’—πŸ’—
πŸ’—πŸ’—πŸ’—πŸ’—πŸ’—πŸ’—πŸ’—πŸ’—
Ni true story kabisaa ya maisha yangu

Huyu Jogging master bwana ni mwanaume anaefanya mazoezi ya kukimbia, yeye kila asbh na jion anapiga zake tizi akiwa na bukta yake Kali , raba Kali pamoja na singlend, huku begani kaweka kitaulo cheupe na pods masikion ,she is too handsome lol πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ …..huyo ndo yeye sasa πŸ˜‚πŸ˜‚ nadhan mshapata picha yake ………hahha
sasa unaweza kupitia shida ila ukaja kukutana na king of your heart alafu moyo ukatulia tuliiiiii na ukasahau kila kitu ….

Huyu ndo Mimi sasa na Mr Jarred A.k.a Jogging πŸƒ master aliniokoa kutoka shimoni 🀣🀣 nika shine like a ⭐…..

Baada ya kumaliza form six matokeo yalitoka na nilikuwa na division one Kali ,mnaijua one Kali nyieπŸ˜‚ yaani ile A,A,A…..one ya 9….

alooh Baba na mama weweeeeee vibe kama lote pale nyumbani ,yaani walinibeba juu juu baba kanishika mikono mama kashika miguu naning’inia kama nyau πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Walinichinjia mbuzi mzima Tena mbuzi mwenye mimba πŸ˜‚πŸ˜‚ oya Kijiji kizima kilijaa pale uwanjani kwetu Yan uwanja ukawa hautoshi mpaka watu wakawa wanaparamia mahindi huko pembeni mwa nyumba yetu 🀣🀣πŸ”₯ chezea ubwabwa wa Bure wewe πŸ™Œ

Ilikuwa bonge ya Sherehe baada ya msoto mzito wa miaka saba ya primary jumlisha minne ya olevel plus miwili ya advance aloo shkamoo elimu sirudii kusoma tenaaa πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚….

Basi katika application Mungu mkubwa nikachaguliwa kujiunga na chuo kikuu flani hapo mjini daslam… aah nilifurahi nilichagua zangu course ya ualimu ☺️ naupenda mno jamni yaan upo kwenye damu …..

Tukafanya application za mikopo majibu yakachelewa kutoka , mwezi wa 11 huu hapa ukafika …..mpaka muda wa kwenda chuo unafika Bado majina ya waliopata mkopo yalikuwa hatajatoka ……

hofu tele moyoni ila nikajipa moyo ,Nina vigezo vyote siwezi kukosaaa

“Anyways tunamwamini Mungu na tunajua utapata asilimia mia moja ,wewe jiandae kesho unasafiri kwenda Dar utafikia hostel na taratibu zingine zitafuata ……
yalikuwa ni maneno ya baba yangu kipenzi mtumishi wa MUNGU mwinjilisti wa vitabu vya Mungu 😒 nampenda sana baba yangu

Ulikuwa ni Mwezi wa kumi na moja huo na kesho ilikuwa ndo siku yenyewe ya kwenda zangu dar kutokea Namtumbo …….
Nilipanga vitu vyangu vya muhimu ,lkin hakukuwa na chamaana zaidi ya vyeti vyangu tu maana ukiongelea kuhusu nguo nilikuwa na nguo tatu tu nazo zimechoka vibaya mno daah so sad 😒 maisha haya acheni tu

Mama alisema hawezi kukubali niondoke kizembe alinichemshia mahindi pamoja na magimbi humohumo akachanganya akanijazia na maziwa kwenye dumu la lita Tano akavipack humohumo kwenye mfuko wangu wa salfeti niliowekea nguo 😒😒

ni kawaida mno kwa sisi maskini Tena watu wa vijijini kubebea nguo kwenye masalfeti hiyo ni kawaida mnoooooo haya ndo maisha yetu na hatuwezi kuyakataa huku ndiko tulikotoka na tumelelewa huko kwahyo mpaka kufikia umri huu tumekuzwa na maisha haya na tunaona ni kawaida tu…….yaani fresh tu ….

Asbh na mapema kabla hata sijaamka baba ,mama ,bamdogo na familia yake …..kule shangazi na watoto wake….huku mamdogo mjme wake na watoto wake …pale majirani woote, yaan mtaa mzima walikuja nyumbani kwaajili ya kunisindikiza stend πŸ˜‚πŸ˜‚,

Raha ya vijijini ukiwa unasafiri watakuja ukoo mzima na marafiki zao kukutakia Kila lakheri πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Walinisindikiza mpaka stend kabisa ya mabasi na nilipanda bas huku mama akilia machozi na kuniombea baraka tele huko niendako kwamaana sikuwa na ndugu wala jamaa huko Mimi ni mgeni kabisa …..

Baba aliniombea maombi mazito mno ndugu zangu wengine waliishia kushika matama yao tu huku wakinipungia mkono 😭😭

Ilikuwa ni huzuni sana nililia sana moyo ulikuwa unauma sana kuiacha jamii yangu niliyoizoea na kwenda mbali nao sikuzoea kabisa maisha Yale hata shule nilizosoma zilikuwa karibu kabisa na Kijijini kwetu

Naitwa Fanikiwa , kwa kifupi kila mtu ananiita Fani ….Nina umri wa miaka 21 tu katika ukuaji wangu wote niliyachukia mno maisha yetu maisha ya wazazi wangu na ndugu zangu wote kiujumla yalikuwa yananipa hasira nyingi mno kutokana na umasikini uliovuka mipaka

Hivi nikisema umasikini umevuka mipaka mnanielewa kweli 😒😒 ?

Umasikini uliopita kiwango Cha kawaida yaan kulala chini kwenye mifuko ni kawaida …..kukaa chini,yaan sebuleni hakuna viti ni chini kwenye vumbi ilikuwa kawaida na kuvaa mavazi chakavu yaliyochokaaa πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œ daah nilikuwa naumia sana ……

Baba yangu alikuwa na mifugo michache tu ambayo hakutaka kabisa kuichezea aliniahidi atanisomesha kwa gharama yoyote ile kwa kuuza mifugo michache aloyonayo …….alisema nitasoma tu hata iwe kwa kuuza mavazi yake yote atafanya hivyo 😒😒😒 dah what a Father πŸ™ŒπŸ™Œ
itaendelea dears

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

SIMULIZI YA INGIZA FULL

BIKIRA YA BIBI HARUSI FULL

BIOLOGY TEACHER FULL