JOGGING MASTER (09)

JOGGING MASTER πŸ’žπŸ’ž9
(Master of loveπŸ’—)
πŸ’—πŸ’—πŸ’—πŸ’—πŸ’—πŸ’—πŸ’—πŸ’—

Tulipita pale barabarani wala hata sikuwa na munkari Tena wa kumuona yule mkaka ,kwanza duka lilikuwa limefungwa ….pia nilishaomba na kuapa Sitaki ujinga Mimi nataka kusoma tu na kutimiza malengo yangu

“Hutaki kumuona Tena ? Maombi aliniuliza

“Nani”nilimuuliza pia

“Wa siku zote” akimaanisha yule mkaka

“Sina shida na mtu yeyote Mimi “

“Kweli ? Aliuliza lkn sikumjibu nilikuwa na stress sana siku hiyo

Tulifika kazini tukaanza kazi lakini utendaji wangu haukuwa mzuri kabisa ,nilikuwa off mood kabisa 😒😒,akili iliwaza kama sitasoma nitafanya nn sasa Mimi ? Nitarudi kijijini nikaolewe ama?

Wanaume wengi sana walikuja kujaribu kumlaghai baba yangu Ili aniozeshe lakini Baba alisimamia msimamo wake ya kuwa Mimi ninasoma na hataki ujinga ,vipi kama nitashindwa kusoma 😒😒

Nilianza kulia Tena kwa kwikwi siku ilikuwa mbaya sana kwangu ….Maombi alinikumbatia na kuniomba nisilie tutashea kila kitakachopatikana na nisijali sisi ni wapambanaji na ana uhakika hata nikikosa mkopo ni lazima nitasoma tu hakuna kurudi kijijini ………nilishawaambia huyu dada anaakili kuliko Mimi tulieni msome muone πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œ….

Tulifanya kazi na jion tukapewa buku jero maana kazi haikuridhisha kabisaaa

Tulishika njia kurudi hostel ….. Tulipita pale dukani na duka lilikuwa closed kama asbh tulipita zetu bila kumjali mtu ……

“Umepata asilimia ngapi ? Nilimuuliza Maombi

“Mia moja ,hata wewe pia utapata asilimia mia” kila neno alilotoa ni lazima lingenihusisha na Mimi na kunitia moyo…..

Tulifika hostels na Muda ulikuwa ushaenda tulilala na usiku huo huo batch 2 na 3 zilitoka ……

Nyie batch 2 na 3 zimetoka huku ,alisema mdada mmoja tuliyekuwa nae pale room

Niliamka haraka na kwenda kuangalia kwenye simu yake ,tulisearch lakin holaaaa hakuna Fanikiwa hakuna Ombeni Wala Mafumbo 😒😒, sikuumia sana kwa maana nilishazoea Hali ile tangu asubuhi na akili yangu niliiset kuwa litakalo kuwa basi ndo hilohilo….

Nilirudi kulala na asbh na mapema ilikuwa siku ya usajili …..Nilimsindikiza Maombi akasain boom na kusajili kozi zake Mimi nikiwa mpenzi mtazamaji tu …moyo unauma lakini Sina Cha kufanya 😩😩……

Alifanya hivyo na baada ya siku tu waliingiziwa pesa ,alilipia hostel na pesa iliyobakia ilikuwa ya kujikimu yeye ……

“Sasa hii pesa iliyobakia tutafute maarifa tufanye lolote la maana ili tupate pesa zaidi ,na pesa tutakayoipata itakuwa ni kwaajili ya ada yako tu πŸ™„πŸ™„ alisema Maombi ……

“Nilimshangaa sana Maombi ,inawezekana vipi ? Kwa biashara ipi mpaka tupate pesa na kulipia mamilion yote hayo πŸ™„

“Sikia unamwamini Mungu? aliniuliza

“Ndiyo , Tena mnooooo …… nilimjibu

“Basi msikilize Mungu tu mengine yasikuumize kichwa alisema na siku hiyo hiyo wote waliosajili waliitwa na kuambiwa kesho wanaanza vipindi kwahyo kama Kuna mtu hajalipia hostel aondoke maramoja asikutwe huko 😒😒😒

“Ninafanya utafiti juu ya fursa yoyote ile then tutaifanya na tutapata pesa usijali….. alisema Maombi asbh moja akiwa anajindaa kwenda darasani …..

Nilibakia hostel nikawaza sasa nafanya nn pale ?? Niliona ni bora niendelee kwenda kule mgahawani huku nikijikusanya kidogo kidogo kutafuta chochote kitu litakalotokea wacha litokee lakin niwe na kakitu mkononi mwangu ….

Nilishika njia kwenda zangu kulee kwa dada Ukhty…njian nilikuwa na mawazo sana stress zilikuwa nyingi mno hata sion ninakoelekea 🚢😒……

“Paaaaaa” nilijikuta nagongana na mtu barabarani bila kujua πŸ™†

“Sorry samahani sana ,nilisema nikiokota earpods na Maji yaliyokuwa yameanguka chini ,niliokota na kumpatia mtu yule

Nilipomtizama usoni 😳

My God ni yule mkaka πŸ˜‚
itaendelea dears

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata